oh samahani mkuu.Sikuona hili swali.
zipo sababu mbalimbali zinazoweza kufanya mche/miche isilete matokeo yaliyotarajiwa.Sababu hizo zimegawanyika katika makundi tofauti
1.Mabadiliko ya tabia nchi
2.Magonjwa
3.kutokufuata mashrti na muongozo uliopewa na mtaalamu
4.Uchaguzi usio sahihi wa aina ya miche kulingana na eneo/hali ya hewa husika
5. Mkulima kushindwa kuupa mche/miche mahitaji unaostahili kwa wakati n.k
6.
Mtaalamu kushindwa kufanya uchaguzi sahihi wa aina nzuri ya mche husika kwa ajili grafting au budding n.k
Sababu zote hizo nilizozitaja(na nyinginezo) kwa sehemu kubwa zinamlenga mkulima.Isipokuwa sababu ya 6.
Hivyo ni wajibu wako mkulima kufanya uhakiki wa eneo lako kabla ya kuanza kilimo. Kama unalima kibiashara nikimaanisha utapanda miche mingi ni bora ufanye treatment ya udongo kabla,kupima PH etc.
Uwe tayari kukabiliana na mabadiliko ya tabia inchi pindi yatakapotokea katikati ya safari yako.
Hudumia miche yako kwa kuipa mahitaji na matunzo yote muhimu ,pamoja na kusafisha shamba lako kila wakati.
Fuata maelekezo yote utakayopewa na mtoa huduma pindi tu utakaponunua miche Hasa miche iliyofanyiwa gratting na budding.Hii ni point muhimu sana,Hapa ndipo wateja wengi wanapokosea.
Nina amini ukifuata hayo yote lazima utapata matokeo mazuri.