Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 57,951
- 32,619
Michelle Obama awakataza watoto wake kujichanganya na kina Beyonce
Malia na Sasha wakiwa na mama yao Michelle Sunday, February 01, 2009 7:00 AM
Mke wa rais wa Marekani Michelle Obama amewakataza watoto wake kujichanganya na 'masupastaa' wa Marekani katika njia ya kuwafanya watoto wake waishi maisha ya kawaida.
Mara ya mwisho watoto hao kujichanganya na masupastaa wa Marekani ilikuwa wakati wa sherehe za kuapishwa kwa baba yao kuwa rais wa kwanza mweusi wa Marekani mwezi uliopita.
Malia mwenye umri wa miaka 10 na Sasha mwenye umri wa miaka 7 walijivinjari na nyota kadhaa wa muziki na sinema wakati wa sherehe hizo.
Watoto hao sasa hawatakutana na "A-list" wa Marekani kama kina Beyonce ambaye walitumia muda mwingi naye wakati wa kampeni.
Watu wa karibu wa familia hiyo waliliambia Us Weekly kwamba mke wa Obama alikuwa anataka kuwafanya watoto wake waishi maisha ya kawaida baada ya kuanza maisha mapya Washington.
Baada ya kuhamia Washington kutoka Chicago Michelle Obama anafanya jitihada za kuwafanya watoto wake waendelee na masomo yao vizuri katika mazingira mapya.
"Michelle anatumia muda mwingi kuzungumza na binti zake kuhusiana na shule yao mpya na marafiki zao wapya katika shule hiyo" alisema rafiki mwingine wa familia hiyo.
Us Weekly lilisema kuwa Michelle hana mpango wa kukodisha mtu wa kuwaangalia binti zake kwa kuwa bibi yao Marian Robinson, 71, ameishahamia ikulu kusaidia kuwaangalia wajukuu zake.