Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
- #201
Castle yanogesha mashabiki Ligi England
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 10th December 2010 @ 23:20
WAPENZI wa soka nchini hasa wale wa Ligi Kuu ya England sasa wamepata uhakika wa kutazama ligi hiyo baada ya Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Castle Lager sasa imedhamini uoneshwaji wa mechi hizo na zitaonekana katika vituo vya televisheni vya TBC1 na Star TV.
Hayo yalielezwa katika taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana na TBL, ambapo ilieleza kuwa kampuni hiyo imeanzisha uhusiano na Ligi Kuu ya England (EPL) kwa kudhamini urushaji wa matangazo ya ligi hiyo maarufu zaidi dunia kupitia vituo mbalimbali vya televisheni katika mataifa 48 ya Afrika ikiwemo Tanzania.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo mechi hizo zitakuwa zikirushwa moja kwa moja kila Jumamosi kupitia vituo viwili vya TBC 1 pamoja na Star TV ambayo tayari ilikuwa imeshaanza kurusha matangazo ya moja kwa moja ya ligi hiyo tokea msimu mpya wa ligi hiyo kuanza.
Katika taarifa hiyo Mkurugenzi wa Masoko wa TBL, David Minja alieleza kuwa kampuni hiyo imefurahia kuwa sehemu ya washirika wa Ligi ya England ambayo ni moja ya ligi bora duniani.
Ligi Kuu ya England imezoa mashabiki wengi hapa nchini na Afrika kwa ujumla ambapo, kuna mashabiki wengi hasa wa timu kubwa za ligi hiyo kama Manchester United, Liverpool, Chelsea na Arsenal .