Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Msechu apinga BSS kushirikisha wageni


na Shabani Matutu


amka2.gif
MSANII wa muziki wa kizazi kipya, Peter Msechu, ambaye ni mshindi wa pili wa shindano la Tusker Project Fame amekosoa uamuzi wa Bongo Star Search (BSS), kumshirikisha Joseph Payne kwenye shindano hilo lililojizolea umaarufu hapa nchini na nchi za jirani.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi hivi karibuni, Msechu alikwenda mbali na kudau kuwa kwa kufanya hivyo kunaondoa uhalisia wa shindano hilo, ambalo ni maalumu kwa kuinua vipaji vya Watanzania na wala si shindano la kimataifa ambalo hushirikisha wasanii wa mataifa mbalimbali.
"Kwa maoni yangu kumshirikisha Payne haikuleta maana, kwani hata Marekani katika mashindano yao ya American Idol huwa hawashirikishi watu wa mataifa mengine zaidi ya raia wao wa Marekani, hivyo ningependa kuwashauri kutorudia kosa hilo" alisema.
Akizungumzia kuhusu masuala yake ya muziki, msanii huyo alisema kwamba hivi sasa ameachia wimbo wake mpya katika studio za MJ Records chini ya Marco Chali unaojulikana kama 'Majaribu' akiwa amemshirikisha Godzillah.
Alibainisha kuwa, hivi sasa yupo katika harakati za kutengeneza video ya wimbo huo nchini Kenya na anatarajia kutoa taarifa za Kampuni ambayo atafanya nayo kazi hiyo baada ya mambo kuwa tayari.
 
THT wapagawisha ZIFF


na Andrew Chale, Zanzibar


amka2.gif
WANAMUZIKI wa kizazi kipya Marlow, Amini na Barnaba juzi walitambulisha nyimbo zao mpya katika tamasha la ufunguzi wa filamu la Zanzibar International Film Festival (ZIFF) lililofanyika Ngome Kongwe mjini Zanzibar.
Tamasha hilo ambalo lilihudhuriwa na wadau wa burudani kutoka nchi mbalimbali limeandaliwa mahususi kwa ajili ya kuonyeshwa filamu za Kitanzania, ambapo mbili zitachaguliwa leo kwa ajili ya kuwakilisha nchi katika tamasha kubwa la Afrika litakalofanyika nchini Burkina Faso.
Mbali na wasanii hao kunogesha tamasha hilo kwa kupiga nyimbo zao mpya, pia kundi zima la Tanzania House of Talent (THT), kupitia bendi yao na madansa, waliweza kukonga nyoyo za mashabiki waliohudhuria.
Akizungumza katika ufunguzi wa tamasha hilo, Mkurugenzi wa ZIFF, Martine Mhando alisema, tamasha hilo ni maandalizi ya tamasha kubwa la ZIFF linalofanyika Julai kila mwaka, ambalo uhusisha filamu kutoka nchi mbalimbali za majahazi."Huu ni mwanzo wa maandalizi ya tamasha kubwa la ZIFF litakalofanyika mwezi Julai na leo hii mmeweza kushuhudia filamu ya 'This is it' ya Steven Kanumba na nimeona mashabiki wengi wameifurahia pia filamu ya 'Huba', na hizi ni miongoni mwa filamu nane zitakazoshindania tuzo ndogo ya ZIFF itakayotolewa siku ya Jumapili" alisema Mhando.
Filamu zilizoonyeshwa jana katika ukumbi wa Ngome Kongwe ni 'Divorce' iliyotayarishwa na Vicent Kigosi ' Ray', 'Don't Cry' na 'Black Sunday' iliyoongozwa na Yvone Cherly 'Monalisa' ambako leo ndio tuzo ya 'Mini Festival' itatolewa kwa filamu bora itakayoibuka kidedea.
 
Usaili mwingine vipaji vya dansi leo


na Makuburi Ally


amka2.gif
KAMPUNI ya Makukwe Entertainment leo inakamilisha hatua ya tatu ya usaili wa kusaka vipaji vya muziki wa dansi kwa vijana, unaotarajiwa kufanyika katika ukumbi wa New Msasani Club jijiniDar es Salaam.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Makukwe, Suleiman Mathew, alisema, Desemba 20 na 21 usaili ulifanyika katika ukumbi wa Afri Centre Ilala jijini Dar es Salaam, huku hatua ya tatu ikifanyika leo.
Mathew alisema, baada ya usaili huo, fainali za kuanza kumsaka mshindi wa shindano hilo zitaanza Januari 16, ambapo kabla ya fainali hizo, watakaofanya vizuri wataingia kambini katika Hoteli ya Giraffe Ocean View kupata elimu zaidi ya muziki.
Fainali za mashindano hayo zitakoma Machi 6 katika ukumbi wa Club Bilicanas jijini Dar es Salaam.
Majaji watakaofanikisha shindano hilo ni pamoja na Nyota Waziri, Tshimanga Kalala Asosa, Abdul Salvador 'Father Kidevu' na Ally Choki.
 
Yanga vichwa chini tena
• Yapigwa 3-1, Mwape akosa penalti Uhuru

na Chile Kasoga


amka2.gif
KWA mara nyingine tena mashabiki wa timu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam jana walitoka vichwa chini Uwanja wa Uhuru baada ya kushuhudia wakipigishwa 'ligwaride' na Maafande wa JKT Ruvu na kulala kwa mabao 3-1.
Katika mechi hiyo ya kirafiki maalumu kwa ajili ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara na michuano ya kimataifa, Yanga ndiyo iliyoanza kuzisalimia nyavu za JKT kwa bao la Omega Seme dakika ya 19.
JKT Ruvu wanaonolewa na Charles Kilinda, walitulia na kufanikiwa kuchomoa mfungaji akiwa Haruna Adolf.
Kipindi cha pili JKT ilizidisha mashambulizi na kufanikiwa kupata bao la pili dakika ya 58 mfungaji akiwa Hussein Bunu, kabla ya George Minja kupachika la tatu kwa kichwa dakika ya 71.
Katika mechi ya jana, mchezaji wa kimataifa wa Yanga, Davies Mwape, alikosa penalti baada ya kufanyiwa madhambi na Stanley Nkomola.
Hiyo ni mechi ya tatu kwa Yanga, ambako ilipoteza kwa Azam FC kabla ya kuishinda AFC Leopards 1-0 na kuangukia kipigo cha jana dhidi ya maafande hao.
Yanga inatarajiwa kuondoka jijini leo alfarjiri kwa boti kwenda Zanzibar kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Kwa upande wake, Kocha wa Yanga, Mserbia Kostadin Papic alielezea kusikitishwa kwake na kuwakosa nyota wake ambao wako Stars.
Yanga: Nelson Kimathi, Fred Mbuna, Ernest Boakye, Isaack Boakye, Ibrahim Job, Nsa Job, Davis Mwape, Juma Seif, Abuu Ubwa, Godfrey Boni na Omega Seme.
JKT: Shabani Dihile, Kessy Napande, Stanley Nkomola, Shaibu Nayopa, George Minja, Mwinyi Kazimoto, Bakari Kondo, Pius Kisambale, Haruna Adolf, Nashon Naftal na Damas Makwaya.
 
NMB yamwaga vifaa Stars
• Kocha Marsh atamba kufanya kweli Misri

na Makuburi Ally


amka2.gif
WADHAMINI wa timu ya Taifa ya Soka Tanzania 'Taifa Stars' benki ya NMB jana ilikabidhi vifaa mbalimbali vya michezo kwa timu hiyo vyenye thamani ya sh milioni 20 kwa ajili ya michuano ya Nile Basin, kuanzia Januari 5-17 jijini Cairo Misri.
Akikabidhi vifaa hivyo jana, Meneja Masoko wa NMB, Shilla Senkoro, alisema, vifaa hivyo vitafanikisha ufanisi wa timu hiyo katika mashindano hayo.
Senkoro alisema, kutokana na kuwa wadhamini wa timu hiyo, ndio sababu iliyowafanya watoe vifaa hivyo ikiwa ni sehemu ya udhamini wake.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na jezi za nyumbani na ugenini, viatu, suti za michezo na jezi za mazoezi.
Naye nahodha wa Stars, Shadrack Nsajigwa, aliishukuru NMB kwa vifaa hivyo ambavyo vitafanikisha ushindi katika mashindano hayo.
Kwa upande wake, Kocha Msaidizi wa Stars, Marsh Sylvester, aliahidi kufanya makubwa katika mashindano hayo, kutokana na maandalizi bora aliyowapa wachezaji wake.
Marsh alisema, watatumia mifumo ambayo ilitumika katika mashindano ya Chalenji yaliyomalizika mwaka jana katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam.
Marsh alisema, timu yake inatarajia kuondoka kesho alfajiri kuelekea Misri katika michuano hiyo ikiwa na wachezaji baada ya viongozi kutangulia tangu jana.
Wachezaji wanaounda Stars ni pamoja na Juma Kaseja, Shaaban Kado na Said Mohamed ambao ni makipa.
Mabeki ni Shadrack Nsajigwa, Stephano Mwasika, Aggrey Mourice, Kelvin Yondan, Juma Nyoso na Nadir Haroub 'Cannavaro'.
Viungo ni Idrissa Rajab, Nurdin Bakari, Shaaban Nditi, Henry Joseph, Jabir Aziz na Abdi Kassim 'Babi', wakati washambuliaji Godfrey Taita, Mrisho Ngassa, Nizar Khalfan, Athuman Machupa, Jerryson Tegete, Ally Ahmed Shiboli na Said Maulid 'SMG'.
 
Hatma mwenyeji Daraja la Kwanza bado


na Makuburi Ally


amka2.gif
WAKATI Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara, inatarajiwa kuanza Januari 15, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema hatma ya mkoa utakaokuwa mwenyeji katika hatua ya tisa bora iko chini ya Kamati ya Mashindano.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam jana, Kaimu Katibu Mkuu wa TFF, Sunday Kayuni, alisema awali walitoa nafasi kwa mkoa unaohitaji kuandaa hatua hiyo ya lala salama daraja la kwanza, uwe na sh milioni 20 ambazo ni sehemu ya kuendeshea hatua hiyo.
Kayuni alisema, kamati hiyo inatarajiwa kutolea ufafanuzi wa mashindano hayo hivi karibuni.
"Suala hilo kwa sasa liko katika kamati ya mashindano, hivyo tuwaachie watalitolea ufafanuzi wao" alisema Kayuni.
Ligi imepangwa kwa makundi, ambapo A lina timu za Villa Squad, Temeke Utd na Moro Utd wakati B ni Prisons, Coastal Union na Morani FC na kundi C ni Mwanza Utd, Polisi Morogoro na Rhino Rangers.
 
Makungu amkataa rais wake ZFA


na Mohamed Said Abdullah, Pemba


amka2.gif
MAKAMU wa Rais mteule wa Chama cha Soka Zanzibar (ZFA), Amani Ibrahim Makungu amekataa kuyapokea matokeo ya Urais wa chama hicho, kwa madai ya kuwashirikisha wajumbe ambao hawakuwa na sifa za kikatiba kushiriki sambamba na baadhi ya watendaji wakuu kufanya kampeni chafu na kufanikisha Rais wa zamani kurejea tena madarakani.
Akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kutangazwa matokeo ambayo alisusia baada ya kuvuja kabla ya kutangazwa rasmi, Makungu alisema kuna wajumbe watatu hawakuwa na sifa za kupiga kura.
Wajumbe hao wanadaiwa kutofanya uchaguzi kupitia vyama vyao vinavyowapa nafasi kuwa wajumbe wa mkutano mkuu, kitendo ambacho ni kinyume na katiba ya ZFA, kwa vile walijiwakilisha wao binafsi bila ya kuwa na baraka za wanachama wao.
Alifahamisha kuwa, hali hiyo ilijitokeza wakati mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi, Ali Suleiman Ali alipokuwa akitangaza orodha ya wajumbe wa mkutano mkuu, ambapo aliita majina ya wajumbe ambao walianguka katika uchaguzi wa wilaya na kamati za uwakilishi, hatua aliyoileza kuwa ni ushahidi tosha ZFA haikuhakiki wapiga kura kabla ya uchaguzi mkuu.
Kuhusu kampeni chafu, Makungu alisema kwamba, Katibu wa ZFA, Mzee Zam Ali ambaye ni muajiriwa wa Serikali, pamoja na msaidizi wake Masoud Atai walikuwa wakifanya kazi ya kuwakusanya wajumbe katika vikao vya faragha na kumuendeshea kampeni Rais mteule Ali Ferej Tamim, wakati sura ya kwanza ibara ya 4(ii) inakataza vitendo vya rushwa kutumika katika michezo.
"Mimi sikubaliani na ushindi wa Ali Ferej Tamim, kwa sababu kwanza hakuwasilisha cheti cha kumaliza kidato cha nne, hivyo alikosa sifa ya kuwa mgombea, kamati ya uchaguzi ilimuamini kwa maneno aliyayaeleza bila ya kuonesha uthibitisho, wakati hayana nguvu za kisheria, ikiwemo barua ya Polisi ya kuthibitisha maelezo yake kuwa cheti chake kiliungua moto" alilalamika Makungu na kuongeza.
"Nawahakikishia Wazanzibar kuwa, timu yangu ya Zanzibar Ocean View haitoshiriki mashindano ya klabu bingwa ya Afrika, hadi tuumalize huu mzozo, matokeo hayakuwa halali, kwa nini kamati ilimtoa mgombea wa makamu wa Urais Ali Dai kwa kushindwa kuwasilisha cheti cha kidato cha nne, ikamkubali Ali Ferej, ambaye hakutoa ushahidi wowote kuonyesha kuwa kweli alimaliza kidato cha nne na alikuwa na cheti, wakati wote rangi zao zinafanana" alisema Makungu.
Wakati bundi akianza kuingia taratibu, wajumbe wa mkutano mkuu walisema maandalizi ya mkutano huo yalikuwa ya ubabaishaji, hasa baada ya kulipwa shilingi 10,000 kwa kila mjumbe kwa siku mbili, kulazwa wajumbe wawili kwa kila chumba katika nyumba za kukodi badala ya hoteli, pamoja na kulishwa chakula duni kilichopikwa kwa kutumia mchele wa mapembe.
Hata hivyo katibu msaidizi wa ZFA Masoud Atai, alisema wajumbe hao walilipwa shilingi 10,000 kwa siku mbili kutokana na chama hicho kukabiliwa na hali mbaya ya kifedha, lakini alishukuru uchaguzi umekwisha salama na viongozi wamepatikana.
Katika uchaguzi huo, Ali Ferej Tamim alirejea tena madarakani baada ya kuzoa kura 32 na kufuatiwa na Suleiman Mahmoud Jabir kura 20, huku mwandishi mwandamizi wa Channel Ten, Munir Zakaria akiambulia kura 2 kati ya kura 54 zilizopigwa.
Katika nafasi ya Makamu wa Rais Unguja, Amani Ibrahim Makungu alifanikiwa kumuangusha Haji Ameir ,Bosi Mpakia' aliyekuwa akiitetea nafasi yake kwa kupata kura 32 dhidi ya 22 za Mpakia.
 
TFF yaunda chama Simiyu


na Samwel Mwanga, Maswa


amka2.gif
SHIRIKISHO la Soka la Tanzania (TFF), limeridhia kuundwa kwa Chama cha Soka Mkoa wa Simiyu ili kurahisisha shughuli za mchezo huo mkoani humo.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa TFF, Athuman Nyamlani, aliyasema hayo hivi karibuni mjini hapa, katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Greenbeach Hotel na kuwashirikisha viongozi wa vyama vya soka kutoka Wilaya za Maswa, Bariadi na Meatu.
Alisema, ni jukumu la shirikisho hilo kuhamasisha uundwaji wa vyama kwa mikoa yote ya kiserikali na kuhakikisha vinakuwa imara sambamba na kukuza kiwango cha mpira wa miguu hapa nchini.
"Sisi shirikisho la mpira wa miguu tunajukumu la kuhamasisha uundwaji wa vyama vya mpira wa miguu hasa katika maeneo ya mikoani, kama mnakumbuka kuwa, hivi karibuni Rais Jakaya Kikwete ametangaza kuanzishwa kwa mikoa mipya na mkoa wenu wa Simiyu ni miongoni hivyo ni wajibu wetu kuwasimamia na kuhakikisha chama hiki kinaanzishwa" alisema.
Naye Mkurugenzi wa Fedha na Utawala wa TFF, Mtemi Ramadhani, aliwaomba wajumbe hao kuchagua jina na nembo ambazo zitatumika katika kuutambulisha Mkoa huo kimichezo.
Wajumbe hao, kwa kauli moja walikubaliana kuwa, jina la chama hicho liwe Simiyu Football Assoction (SIFA), na nembo yake itakuwa na mpira, viatu na alama ya mto.
Aidha, Mtemi aliwataka viongozi hao kuhamasisha kuundwa timu nyingi za soka katika Wilaya zote zinazounda Mkoa huo, ambazo ni Maswa, Bariadi, Meatu, Itilima na Busega.
 
Cheka extends unbeaten record
Sunday, 02 January 2011 21:33

By Majuto Omary
The Citizen Reporter
Dar es Salaam. Francis Cheka proved his invincibility on Saturday following a point victory over Mada Maugo in the eight-round middleweight bout at PTA Hall here.
The Morogoro-based boxer, who is also the Universal Boxing Organisation (UBO), International Circuit Boxing (ICB) and World Boxing Commission (WBC) middleweight inter-continental champion, managed to extend his longstanding unbeaten streak at the expense of the outspoken boxer.

Cheka scored 79-78, 79-78, 79-79 from the judging trio of Ibrahim Kamwe, Abdallah Mpemba and Omari Yazidu respectively.
The bout, which was graced by the Dar es Salaam Special Zone Police Commander, Suleiman Kova, saw hundreds of boxing fans throng the venue.
Cheered by hordes of home fans, Maugo embarked on the fight imposingly, forcing the fancied opponent to the ropes severally.

Maugo cornered the Morogoro-born pugilist with vicious punches in the second round to the delight of his fans, but the latter refused to go down.

The first two rounds signalled that Maugo would have ended Cheka's domination in the ring, but the winner of multiple titles regained his poise in the third round.
Maugo, seemingly overconfident in the third round, saw his brilliant start snapped as Cheka came into the fight, unleashing power-packed punches that earned him undisputable points.

The fifth round was even worse for the boxer who started the fight on a high note, as Cheka picked from where he left to batter Maugo mercilessly.
Cheka could have registered a knockout win in the same round, but failed to release killer punches, thus giving Maugo a chance to reorganise.

The Mara-born boxer got the sixth round underway strongly, employing uppercuts to hit tired Cheka.
His resurgence made the fight look unpredictable. However, Cheka was too clinical after most of his punches in the remaining rounds earned him points.
After being announced the winner, Cheka, who was all smiles, boasted that his action always describes the kind of a boxer he is.

He said: "I don't talk too much the way others do, but my action in the ring speaks.
"I'm delighted to win this bout, it was a tough one, but eventually I proved that I'm unbeatable in the country." Asked whether he would meet Japhet Kaseba in March, Cheka belittled the kick boxer saying he was not of his calibre.

"Kaseba is an ordinary boxer, he can't help improve my game, so at present I am focusing on winning more international bouts," he said.

Cheka was aiming at grabbing coveted titles like the World Boxing Council (WBC), World Boxing Association (WBA) and International Boxing Federation (BF.
Speaking after the bout, Maugo claimed that the judges ruled in favour of Cheka.
"Cheka fought well in the fifth round only, I wonder where he got all these points... the judges have demoralised me," Maugo said.
 
Chelsea's poor League form continues draw against Villa
Sunday, 02 January 2011 21:31 London. Chelsea's amazing late fightback was in vain as Aston Villa scored a stoppage-time equaliser to leave the champions' Premier League title defence in considerable doubt.

Didier Drogba and John Terry looked to have snatched victory from the jaws of defeat with goals in the final six minutes at Stamford Bridge but the hosts' poor defending cost them when Ciaran Clark nodded home a late equaliser.
The result left Chelsea marooned in fifth place, six points behind Manchester United having played a game more, and crucially outside the Champions League places.

That will place manager Carlo Ancelotti's position under fresh scrutiny, while opposite number Gerard Houllier may enjoy some respite after ending a run of six defeats in seven games.

Chelsea began the match buoyed from ending their worst set of results for 11 years in Wednesday night's ugly 1-0 win over Bolton.

But for all their early possession, they once again lacked any real penetration.
Jeffrey Bruma - making his full Premier League debut - saw a header from a corner blocked but the better chances all fell to Villa, with Gabriel Agbonlahor, Ashley Young and Stewart Downing all going close.

But a sudden loss of discipline cost them dear, captain Stiliyan Petrov booked for a stupid lunge on Florent Malouda moments before James Collins climbed all over the Frenchman to concede a penalty.

Malouda did throw himself to the floor, and Brad Friedel and Collins were both cautioned for protesting, but it was a definite foul and Lampard stepped up to convert his first goal since August.

Villa's frustration got the better of them and they were penalised for more than one late tackle, while Reo-Coker, Agbonlahor and Clark were all booked before half-time.

Ramires was booked for clipping Petrov's heels and Villa's pressure finally told when Essien's clumsy tackle on Reo-Coker handed them a penalty four minutes before the break. Young made no mistake from the spot.

And Heskey put them ahead just two minutes in when he climbed above young Bruma to power home Downing's excellent right-wing cross.
Lampard, Drogba and Ramires all saw shots blocked before the latter drilled just wide after the ball broke to him in the box.
 
Yanga coach remains optimistic despite defeat Sunday, 02 January 2011 21:30

Doris Malyaga
The Citizen Correspondent
Dar es Salaam. Young Africans head coach, Kostadin Papic insists his team can develop into an outfit capable of challenging the continent's top sides despite their dispiriting defeat to less fancied JKT Ruvu in a friendly match at the weekend.

The Serbian has slightly fallen from grace just months after being hailed as a hero for guiding his team to a 1-0 win over their arch-rivals Simba in a Premier League match.
Spectators at the Uhuru Stadium in the city looked on in disbelief as Papic's star-studded team crashed to a 3-1 defeat to the army team.

But Papic, whose main challenge now is to guide Yanga in the Africa Confederation Cup, remained optimistic, describing the defeat as a slip up.
"I expect to rectify the weaknesses I noted during our friendly against JKT Ruvu before we launch our campaign in the Confederation Cup," the Serbian said.

The preliminary round of the eight Orange Confederation Cup seems kinder to Yanga as they are drawn against, Dedebit, a little known side from Ethiopia.

But they face a difficult path in their pursuit of taking their football reputation to the next level with fancied Haras El Hodoud of Egypt standing on their way.
 
Kenyan wraps up 2010 with superb win
Sunday, 02 January 2011 21:29

Sao Paulo. Running in warm and pleasant conditions, Brazilian Marílson Gomes dos Santos and Kenyan Alice Timbilil won the 86th edition of the traditional 15 kilometre in São Paulo, Brazil, on the New Year's Eve.

It was the third victory at the classic race (a record for a Brazilian runner since 1945, the year the race became open for international athletes) for the 33-year-old dos Santos, who also won twice the New York City Marathon (2006, 2008).
He previously won in São Paulo in 2003 and 2005, the last year he ran the race. His winning time on Friday was 44:07.
The 27-year-old Timbilil repeated her victory from 2009.
Her winning time was 50:19, a course record that improves the 17-year-old previous best of fellow Kenyan Hellen Kimayo (50:26).

The men's race started at 16:45 local time, in front of the MASP (Museum of Modern Arts of São Paulo).
The first part of the race was dominated by the rabbits at a pace of 2:50-2:55 per km.

He crossed the line with a 200m gap over the runner-up Barnabas Kosgei from Kenya who clocked 44:49.
Dos Santos ends the year with a fine victory at home, after obtaining good results over the Marathon distance: 6th in London with a SB of 2:08:46, and 7th in New York
"It was a tough victory. I left the field a little bit too early, and I almost paid the price at the hill of the Brigadeiro Luiz Antônio, which is very hard for your legs.

"I almost had forgotten how hard it was", Dos Santos said with a smile.
The pacemakers did their job at the initial parts of the women's race, which started 15 minutes before the men's.
The first attack was thrown by Ecuadorian Diana Landi at the end of the Rua da Consolação (2nd km).
Landi ended up being caught back by the field at the 4th km (Avenida São João).(AFP)
 
Dar ace golfers to miss Mexico tournament
Sunday, 02 January 2011 21:27

By Suleiman Jongo
The Citizen Reporter

Dar es Salaam. The Tanzania Ladies Golf Union (TGLU) will not field a team in the invitational tournament planned to tee off in Mexico on Thursday owing to lack of funds.

The team was to leave for Mexico yesterday, but last minute efforts by the union to raise the cash hit the wall, according to TLGU president Mbonile Burton.
Burton disclosed that Hawa Wanyeche and Madina Iddi were lined up for the tournament, but the union could not get the money for processing their visas in Nairobi.
"We have no Mexico embassy here, so we could not afford to process their visas in Nairobi because of our limited budget," she said.

Burton added: "It's embarrassing not to honour the invitation, but there is nothing we can do now to enable them to participate.
According to her, the union has already notified their Mexican counterparts about the failure to field the team.

The golfers will be inactive for the rest of this month due to being in the off season.
"Golf tournaments will resume next month, therefore our golfers will be out of action for the whole month," she said.

The duo, who represented the country in last year's African Championship held in Nigeria, managed to finish the year on a high note after claiming the second spot.

Burton voiced optimism that the TLGU would have yet another year of success given the mushrooming brilliant golfers.
 
Stars trip hangs in the balance
Saturday, 01 January 2011 10:55

juma%20kaseja2.jpg
Taifa Stars Goalkeepers,Juma Kaseja

By Majuto Omary
The Citizen Reporter
Dar es Salaam. The national soccer team, Taifa Stars' trip to Cairo, Egypt for the inaugural Nile Basin championship hangs in the balance, it has been revealed.

As of yesterday evening, Tanzania Football Federation (TFF) was yet to receive air tickets for the Cairo-bound squad for the six-team tournament opening on Wednesday.
TFF acting secretary general, Sunday Kayuni confirmed yesterday that they were still on the dark over the team's departure.
"As of now, we are yet to secure air tickets from the Egypt football authorities. We have tried to contact them several times but to no avail," Kayuni said.

"The Nile Basin championship organizing committee told us that we are required to be in Cairo on Monday. Hopefully, we will get the tickets before that day," he added.

The team's first batch is expected to jet off tomorrow, according to the TFF official. He said the first batch will comprise eight players. But he fell short of naming them.

It is understood that TFF vice-president Athuman Nyamlani will the head of the delegation. Referees Oden Mbaga and John Kanyenye will also make part of the country's contingent to Egypt.

Taifa Stars stand-in head coach Sylvester Marsh said yesterday that his players were in high spirits, looking forward to making their presence felt in the championship.

"My players are physically, tactically and psychologically fit for the Cairo championship, I am optimistic we'll make a mark in the event," Marsh said.

The players expected to make the trip are goalkeepers Juma Kaseja, Shaban Kado and Said Mohamed.
Also in the list are defenders Shadrack Nsajigwa, Stephano Mwasika, Kelvin Yondani, Juma Nyoso, Aggrey Morris, Nadir Haroub.

Others are midfielders Shaaban Nditi, Nurdin Bakari, Abdi Kassim, Idrissa Rajab, Rashid Gumbo, Nizar Khalfan, Jabir Aziz, Taita and Machaku Salum, and strikers Mrisho Ngassa, Jerry Tegete, Said Maulid and Athumani Machupa.
 
Babi auzwa rasmi Sunday, 02 January 2011 20:49

Clara Alphonce
KLABU ya Dong Tam Long An ya Vietnam wamekubali kumnunua kiungo wa Yanga, Abdi Kassim 'Babi' kwa gharama ya dola za Kimarekani elfu 40 na anatarajia kuondoka nchini wiki hii.

Katika mazungumzo ya awali klabu hiyo ilitaka kumnunua mchezaji huyo kwa dola elfu 35, lakini Yanga waligoma na kutaka walipwe dola hizo 40 elfu ili waweze kumwachia mchezaji huyo.

Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako alisema kuwa tayari wameshakubaliana na klabu hiyo na sasa bado kukamilika kwa mambo madogo madogo.

Alisema kuanzia leo watakuwa wakipeana mikataba ya pande zote mbili ili kila mmoja aweze kuisoma na kuielewa, lakini mambo yote yameisha na wameishatuma barua TFF ya kutaka watoe kibari chake cha kimataifa- ITC.

Alisema kuhusu maandalizi ya safari ya mchezaji huyo yamekamilika na viza ameshapata na wiki hii muda wowote anaondoka tayari kwa kuanza kazi katika timu yake mpya.
 
Dk Riki azishauri Simba,Yanga Sunday, 02 January 2011 20:45

Sosthenes Nyoni

MCHAMBUZI maarufu wa soka nchini, Riki Abdallah 'Dokta Riki' amezishauri klabu za Simba na Yanga kufanya maandazili ya vitendo badala ya mdomo ili ziweze kufanya vizuri katika michuano ya kimataifa.

Simba itaiwakilisha Tanzania katika michuano ya klabu bingwa Afrika ambapo imepangwa kuanza kampeni yake kwa kuikabili Elan C. de Mitsoudje ya Comoro wakati wapinzani wao Yanga yenyewe itashiriki michuano ya kombe la washindi ikiwa imepangwa kuanza kibarua chake kwa kuikabili Dedebit ya Ethiopia.

Akizungumza na kituo kimoja cha televisheni, Dokta Riki alisema kuwa michuano hiyo ni migumu hivyo ili klabu hizo ziweze kufanya vizuri zinahitaji maandalizi ya uhakika.

"Napenda kuzishuri Simba na Yanga zifanye maandazi mapema na kwa vitendo sio maneno tu michuano watakayoshiriki ni migumu,ile sio ligi ya hapa kwetu ambayo ina mambo yake.

"Ukiangalia kwa haraka haraka unaona mechi zao za kwanza wanaweza wakashinda na wakapita ingawa pia hawatakiwi kujipa matumaini makubwa, lakini mechi zitakazofuata ni ngumu kila mmoja anafahamu rekodi ya TP Mazembe na El Hodood si timu rahisi,"alisema Dokta Riki.

Katika hatua nyingine Dokta Riki alitoa wito kwa wachezaji mbalimbali wa zamani kuomba uongozi katika klabu na vyama vya soka ili kutumia uzoefu wao kuleta maendeleo ya mchezo huo hapa nchini.

Alisema kuwa kwa uzoefu wake nchi zilizoendelea kama Ujerumani na Uingereza zimekuwa zikiwatumia wachezaji kuongoza klabu na vyama badala ya watu wasiojua chochote kuhusu soka.

 

Apania kuweka filamu za Tanzania kimataifa

Imeandikwa na Mwandishi Wetu, Zanzibar; Tarehe: 3rd January 2011 @ 07:34

MKURUGENZI wa tamasha la kimataifa la filamu la Zanzibar, Dk. Martin Mhando amesema kwamba ushiriki wa sinema za hapa nyumbani katika tamasha hilo kama kategori inayojitegemea ni mwanzo wa kuiweka Tanzania katika ramani sahihi ya tasnia ya filamu duniani.

Katika mahojiano maalumu na mwandishi wa gazeti hili, kwenye ofisi za asasi hiyo ya hiari, Ngome Kongwe, Zanzibar, Dk. Mhando alisema kama wasipowashirikisha watengenezaji sinema wa hapa nyumbani, kiwango chao hakitakua.

"Kwa sasa najua udhaifu wake, najua pia kwamba katika mfumo wa sasa hatuwezi kusogea mbele katika soko la kimataifa, lakini tukiwaacha kwa sababu hawajakidhi viwango hawatakua," alisema Dk. Martin.

Dk. Martin alisema katika matamasha ya kimataifa hakuna sinema inayoruhusiwa ya part 1 na 2 kwani hakuna muda wa kutazama saa tatu na kwa sasa sinema nyingi za Tanzania zipo hivyo na pia hazina lugha za maandishi ili wageni waweze kuelewa.

Alisema ZIFF imeamua kwa makusudi kuanzisha Bongo Movie ili kuandaa Watanzania kwenda nafasi ya juu kwa kuwasogeza na wataalamu wa kimataifa ili kuwawezesha kutengeneza sinema kwa ajili ya dunia nzima.

"Soko la Tanzania ni DVD, watengenezaji wamefanya hivyo kwa kuwa wanunuzi wao ni wa majumbani, Watanzania wengi hawaendi sinema na katika hili wamefanikiwa sasa tunataka tuwajenge kimataifa katika misingi kamili na matamasha madogo kama haya yanasaidia sana," alisema Dk. Martin.

Katika tamasha dogo la ZIFF ambapo sinema nane zinagombania nafasi mbili ya kupelekwa Fespaco kwenye tamasha la kimataifa kampuni za Steps, RJ na Pilipili zimeingiza filamu kwa ajili ya mashindano.

Hata hivyo katika mazungumzo Dk. Martin alikiri kwamba kama filamu isiyokuwa na maelezo ya Kiingereza imeshinda au inahitaji part 2 imeshinda itamuwia vigumu kuipatia uwakilishi Fespaco.

"Nitaipeleka lakini sijui kama wataikubali, wana mambo ya kimataifa na hili hatuwezi kukwepa," alisema Dk. Martin.

Nyingi ya filamu zilizoletwa zinakosa kitu kimoja au kingine. Ama ina sehemu mbili au haina lugha nyingine zaidi ya Kiswahili.

Wakati huo huo Dk. Martin alisema kwamba anatarajia kutoa mhadhara mkubwa kuhusu sinema za hapa nchini Januari 14 mwaka huu katika Ukumbi wa Utamaduni wa Ubalozi wa Ufaransa nchini.

Alisema katika mhadhara huo atazungumzia ukuaji wa sinema za Kitanzania, matatizo yake na kupendekeza njia bora ya kuimarisha tasnia hiyo.

Alisema kwamba anatarajia watu wengi wanaopenda sinema watahudhuria mdahalo huo ambao utakuwa na maana kubwa kwa tasnia ya filamu katika siku zijazo.

Dk. Martin pamoja na kuwa Mkurugenzi wa ZIFF ni mtengenezaji wa sinema na pia ni mwalimu wa masuala ya sinema katika Chuo Kikuu cha Murdoch, Australia.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom