Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Phiri aipa uzito Mapinduzi


Na Julius Kihampa

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Phiri, ameitaja michuano ya Mapinduzi kama moja ya kipimo sahihi kwa timu yao kwa ajili ya maandakilizi ya Ligi Kuu na Klabu Bingwa Afrika.Simba ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Bara, wakiongoza
katika msimamo msimu huu, wanatarajia kuvaana na timu ya Comoro kabla ya kuvaana na TP Mazembe, katika raundi ya kwanza ya Klabu Bingwa Afrika msimu huu.

Akizungumza kutoka visiwani Zanzibar, Phiri alisema kikosi chake hakijaathirika kwa kiasi kikubwa na kushindwa kufanya vizuri katika michuano hiyo, pamoja na kuondoka kwa baadhi ya wachezaji.

Alisema kila mchezaji aliyesajiliwa na katika timu hiyo, wameonesha kuiva na kusbiri kufanya vizuri katika michuano hiyo ambayo imeandaliwa kwa ajili ya kusherehekea kumbukumbu ya Mapinduzi ya Zanzibar.

"Kwa sasa inaweza kuonekana kama ni kwa ajili ya kujiandaa na Ligi Kuu, lakini naweza kusema ni pamoja na Klabu Bingwa, hasa kutokana na aina ya timu ambazo tutakutana nazo.

"Kuna timu kama Yanga, Azam, Zanzibar Ocean View, Mtibwa zote zina uzoefu mkubwa wa kucheza michuano ya kimataifa, hali ni nzuri kwetu na tunaamini tutafanya vizuri," alisema Phiri.

Nae, Meneja wa timu hiyo, Innocent Njovu, alisema lengo lao siyo kucheza fainali, bali kurudi na kombe hilo ili kuwahakikisha kuwa, kikosi chao kinaweza kufanya maajabu katika michuano yoyote.

"Tunataka kufika fainali, lakini lengo si kucheza tu mchezo huo, bali kurudi na heshima tunayostahili ya kunyakua kombe hili, hakuna mgonjwa mpaka sasa, na yeyote atakayepewa nafasi na mwalimu, anaweza kucheza bila wasi," alisema Njovu.

Simba itawakosa wachezaji walioko katika kikosi cha timu ya Taifa 'taifa Stars', kitakachoshiriki michuano ya Mto Nile ambao ni kipa Juma Kaseja, Kelvin Yondani, Juma Nyosso na Mohamed Banka.

 
Taifa Stars yaenda Misri

Imeandikwa na Betram Lengama; Tarehe: 3rd January 2011 @ 07:34


TIMU ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars' ilitarajiwa kuondoka leo alfajiri kwenda Misri kwa ajili ya kushiriki kwenye michuano maalumu ya soka ya Mto Nile ambayo inajumuisha mataifa tisa itakayoanza kutimua vumbi keshokutwa jijini Cairo.

Kwa mujibu wa kocha Msaidizi wa kikosi hicho cha Stars Sylvester Marsh timu hiyo ilitarajiwa kuondoka nchini leo saa 12 alfajiri kwa ndege ya Egypt Air ikiwa na kikosi cha wachezaji 23 ambao waliitwa kambini kwa ajili ya kujiandaa na michuano hiyo.

Kocha Marsh alibainisha kuwa hakuna mchezaji aliyechujwa kwenye kikosi hicho ambacho kinajumuisha wachezaji wazoefu na wasio na uzoefu mkubwa wa michuano ya kimataifa. Wachezaji ambao walitarajiwa kusafiri leo ni Makipa: Juma Kaseja (Simba), Shaaban Kado (Mtibwa) na Said Mohamed(Majimaji).

Walinzi ni Shadrack Nsajigwa (Nahodha), Stephano Mwasika , Nadir Haroub ‘Cannavaro' (Yanga), Aggrey Morris, (Azam),Kelvin Yondani, Juma Nyosso, (Simba).

Viungo: Idrissa Rajabu (Sofapaka, Kenya), Nurdin Bakari, Abdi Kassim ‘Babi', (Yanga), Shaaban Nditti (Mtibwa) ,Jabir Aziz (Azam) na Rashid Gumbo kutoka Simba aliyechukua nafasi ya Henry Joseph aliyeondolewa kwenye kikosi hicho.

Washambuliaji ni Salum Machaku (Mtibwa), Mrisho Ngassa (Azam), Nizar Khalfan, (Vancouver Whitecaps- Canada), Godfrey Taita (Kagera Sugar), Athumani Machuppa, (Vasuland IF -Sweden), Jerry Tegete, (Yanga) Said Maulid(Onze Bravos-Angola) na Ali Ahmed Shiboli (Simba).

Ratiba ya michuano hiyo inaonesha kuwa Stars itafungua pazia la michuano hiyo kwa kuumana vikali na wenyeji Misri keshokutwa usiku majira ya saa moja wakati Kenya ' Harambee Stars' itaivaa Sudan saa kumi jioni.

Awali ilitangazwa kuwa kikosi hicho cha Stars kilikuwa kiondoke jana lakini badala yake jana walitangulia viongozi na wanahabari, Kocha Mkuu wa Stars Mdenmark Jan Poulsen anatarajiwa kuungana na kikosi hicho huko Cairo akitokea kwao ambako alikuwa kwenye mapumziko ya sikukuu za mwisho wa mwaka.

Michuano hiyo ambayo ni maalumu kwa ajili ya uhamasishaji wa utunzaji wa maji wa Mto Nile kwa ajili ya kizazi cha sasa na vijavyo mbali na Tanzania inashirikisha timu kutoka nchi zilizopo kwenye Ukanda wa Ziwa Victoria na Mto Nile ambazo ni Kenya, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Eritrea, Ethiopia, Sudan na wenyeji Misri.
 
Papic aanza kusaka timu

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 3rd January 2011 @ 07:31

KOCHA Mkuu wa Yanga Kostadin Papic ameanza mchakato wa kutafuta timu atakayofundisha baada ya kumaliza mkataba wake Yanga.

Mkataba wa Yanga na Kocha huyo unatarajiwa kumalizika Oktoba mwaka huu na tayari uongozi wa Yanga ulishasema hautasaini naye tena mkataba mwingine.

Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga zilizopatikana Dar es Salaam jana, zilidai kuwa kocha huyo tayari ameshawasiliana na rafiki zake wanaoishi mataifa mbalimbali wamtafutie timu.

"Papic anaondoka, safari hii mkataba wake ukiisha sidhani kama atakubali kuongeza mwingine, maana mwenyewe anaonekana ameshachoka na Yanga,"alisema mtoa habari wetu ambaye hakutaka jina lake liandikwe gazetini.

Habari zaidi zinasema, kitu kikubwa kinachomkatisha tamaa kocha huyo ni namna ya uendeshwaji wa Yanga kwani viongozi wenyewe kwa wenyewe hawapatani.

"Hicho kinamchanganya Papic, kama viongozi hampatani timu itaendeshwa vipi?" "Lakini pia kingine ni baada ya mfadhili Yusuf Manji kuonekana kama kujiweka kando na masuala ya kifedha ndani ya Yanga, kwani siku hizi hatoi fedha kama ilivyokuwa zamani hivyo klabu inashindwa kujiendesha,"alisema.

Hivi karibuni wachezaji wa Yanga waligoma wakishinikiza uongozi kuwalipa fedha zao za usajili zilizosalia ambazo ni takriban Sh milioni 70.

Hata hivyo baadaye uongozi uliwatuliza wachezaji hao na kuwapunguzia kidogo sehemu ya madeni yao.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga Davis Mosha aliwahi kulizungumzia suala hilo katika gazeti hili na kushusha lawama kwa mfadhili wao huyo.

"Manji ndio yeye aliyekubaliana na wachezaji, sisi viongozi hatujui lolote maana tuliingia madarakani tayari wachezaji walishasajiliwa, sasa yeye ndiye alitakiwa kuwalipa," alisema Mosha.
 

Ngosha wa Sikinde afariki dunia


Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 3rd January 2011 @ 07:27
BENDI ya muziki wa dansi ya Sikinde ' Ngoma ya Ukae' imeanza mwaka mpya wa 2011 vibaya baada ya mmoja wa wanamuziki wake John Charles Ngosha kufariki dunia jana asubuhi jijini Dar es Salaam.

Ofisa Habari wa Bendi hiyo Jimmy Chika aliliambia gazeti hili jana kuwa Ngosha ambaye alikuwa mpiga gitaa la besi alifariki saa tano asubuhi akiwa nyumbani kwake Buguruni Sheli baada ya kusumbuliwa kwa muda na maradhi ya homa ya matumbo, (typhoid).

Kwa mujibu wa Chika, Ngosha alikuwa anasumbuliwa na maradhi hayo kwa kipindi cha takribani mwezi mmoja na alikuwa akipata matibabu katika hospitali mbalimbali ikiwemo Hospitali ya Wilaya ya Ilala Amana hali iliyomsababisha kutokuwepo ofisini kwa kipindi hicho chote.

Aidha Chika alibainisha kuwa kutokana na msiba huo uliotokea jana ghafla , onesho la bendi hiyo ambalo lilipangwa kufanyika katika ukumbi wa Suwata liliahirishwa kwa ajili ya kupisha msiba huo.

Ofisa habari huyo pia alibainisha kuwa taarifa zaidi kuhusiana na msiba huo zitatolewa leo baada ya kufanyika kikao na ndugu wa marehemu Ngosha nyumbani kwake ambako ndiko msiba ulioko.

Chika amebainisha kuwa msiba huo ni pigo kubwa kwa bendi hiyo kutokana na mchango wa marehemu katika kuleta maendeleo ya bendi pamoja na kuitangaza akitolea mfano pale Ngosha alipochaguliwa na mwanamuziki maarufu kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Kanda Bongoman kufanya naye ziara ya kimuziki katika mataifa mbalimbali ya Afrika jambo ambalo liliisaidia bendi kujulikana zaidi.
 
Cheka akata ngebe za Maugo

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 3rd January 2011 @ 07:27 Imesomwa na watu: 15; Jumla ya maoni: 0



Mabondia Francic Cheka (kushoto) na Mada Maugo wakichuana vikali wakati wa pambano lao la raundi nane lililofanyika kwenye Ukumbi wa PTA, Dar es Salaam juzi ambapo Cheka alishinda kwa pointi. (Na Mpigapicha Wetu).



BONDIA Francis Cheka ‘SMG' kutoka Morogoro, juzi usiku alimdunda bondia Mada Maugo ‘Mbunge wa Musoma' katika pambano lisilo la kuwania ubingwa, lililofanyika kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam.

Maugo ambaye kabla ya pambano hilo alikuwa akijinasibu katika vyombo mbalimbali vya habari kuwa atampiga vibaya Cheka, juzi alishindwa kutimiza kauli hiyo na badala yake yeye ndie alikumbana na wakati mgumu ulingoni toka raundi ya kwanza ya pambano hilo.

Maugo alishindwa mpambano huo dhidi ya Cheka kwa pointi, kwa majaji wawili kwa mmoja, lakini ni dhahiri bondia huyo alishindwa kuonesha uwezo wa kuhimili vishindo vya mpinzani wake Cheka.

Maugo aliyepigwa ngumi tatu mfululizo baada tu ya kengele ya kuwaruhusu kuanza pambano hilo kulia, alijua nini kitafuata kama hatakuwa makini, akaamua kujihami kwa kukumbatia mtindo alioutumia hadi mwisho wa pambano hilo.

Wapenzi na mashabiki wa ngumi waliofurika kwenye ukumbi huo wakiongozwa na Kamanda wa Kanda Maalum ya Polisi Dar es Salaam Suleiman Kova, walishindwa kuamini kile wanachokiona ulingoni.

Kwani hakuwa Maugo yule waliyemtarajia, kutokana na tambo zake, bondia aliyewaahidi wapenzi kumchakaza Cheka amegeuka mtu wa kujihami jukwaani, kabla hata ya uamuzi wa majaji kutolewa wapenzi na mashabiki wa ngumi walioingia ukumbini humo walijua matokeo, hivyo kuanza kutoka nje.

Kabla ya pambano hilo kulikuwa na mapambano manne ya utangulizi, la kwanza Idd Mohammed wa Dar es Salaam, alimshinda kwa pointi Juma Ramadhani ‘Afande' wa Morogoro, pambano la raundi nne uzani wa Feather.

Amos Mwamakula wa Morogoro, akalipa kisasi kwa kumchapa kwa pointi Obote Ameme wa Dar es Salaam, pambano la raundi sita uzani wa Feather.

Cosmas Cheka, ambaye ni mdogo wa Francis Cheka, akaendeleza furaha kwa watu wa Morogoro, baada ya kumshinda kwa pointi, Hussein Mbonde wa Dar es Salaam, uzani Feather, likiwa moja ya mapambano yaliyovutia usiku wa juzi.

Albert Mbena wa Morogoro, akashindwa kuendeleza wimbi hilo la ushindi kwa watu wa Morogoro, baada ya kushindwa kwa pointi na chipukizi Ramadhani Mashudu, bondia kutoka klabu ya Mabibo Dar es Salaam.
 
Watanzania watakiwa kuthamini filamu za wazawa


Na Amina Athumani, Zanzibar

WATANZANIA wameombwa kununua nakala halisi za filamu za wasanii wa ndani, ili kuwapa moyo wa kuendelea na kazi hiyo. Kauli hiyo imetolewa mjini Zanzibar jana na Meneja wa nembo halisi za filamu zinazojulikana kama
Steps Entertainment, Kambarage Ignatus, alisema kama watanzania wataendelea kununua filamu ambazo si halisi, wataua fani hiyo.

Alisema wasanii wengi wanategemea kazi zao, hivyo wakihujumiwa, watakuwa wakikatishwa tamaa. Ignatus alisema kazi nyingi za filamu zimekuwa zikihujumiwa na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakitoa nakala ambazo siyo halisi na kuziuza kwa bei nafuu.

Hali hii ikiendelea, wasanii watakata tamaa ya kuendelea kutengeneza filamu, gharama ya kutengeneza filamu ni kubwa, lakini malipo yanakuwa madogo.alisema.

Alisema wakati umefika kwa watanzania kuthamini mchango mkubwa unaotolewa na wasanii kwa kununua kazi zao ili kuwaongezea ari na mwamko wa kuipenda kazi hiyo.

Naye, Mkurugezi wa Zanzibar International Film Festival (ZIFF), ambayo ndiyo inayoandaa tamasha la filamu nchini Martin Mhando, alisema ZIFF itaendelea kuunga mkono kazi za wasanii wa Tanzania kwa kuwaandalia matamasha ili kazi zao zionekana na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchini.

Mhando alisema mwaka huu, ZIFF imejipanga katika kuzipeleka filamu za watanzania nje ya nchi, ili kushiriki katika matamasha makubwa ikiwemo tamasha la Afrika litakalofanyika nchini Burkina Faso Februari mwaka huu.

Filamu mbili zitakazoshinda leo (jana), kwenye tamasha dogo la ZIFF (Mini-Festival), zitaiwakilisha nchi kwenye tamasha la filamu la Afrika litakalofanyika Burkina Faso, tunaendelea na taratibu zitakazowezesha filamu zetu kuonekana sehemu nyingi duniani,¡± alisema.

Tamasha la ZIFF la Mini-festival lilitarajiwa kumalizika jana usiku katika ukumbi wa Ngome Kongwe mjini Zanzibar.
 
Wachezaji Toto washindwa kuingia kambini


Na Addolph Bruno

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Toto African ya Mwanza, Choki Abeid, ameshitushwa na kitendo cha baadhi ya wachezaji wake kushindwa kuripoti kambini kujiandaa na Ligi Kuu Bara hatua ya lala salama.Timu hiyo ilianza kambi baada ya
sikukuu ya Krismasi, ikiwa na wachezaji tisa waliorejea kutoka kwao, kwa ajili ya kujiandaa na mzunguko wa pili.

Akizungumza na Majira kwa simu jana, akiwa jijini Mwanza, kocha huyo alisema wachezaji walioripoti kambini ni tisa, na wengi wao wakiwa bado hawajawasili na hawajatoa taarifa yoyote.

"Mpaka sasa wachezaji wetu wengi kutoka mikoani hawajawasili, walioripoti ni wa hapa Mwanza, hatuna taarifa zao,¡± alisema.

Alisema aliamua kuliweka wazi suala hilo kwani timu inapofanya vibaya, kocha huwa wa kwanza kulaumiwa.

Alisema wachezaji ambao hawajaripoti ni kutoka Dar es Salaam na Shinyanga, wanawasubiri ili waanze programu nzima ya mazoezi.
Kocha huyo alisema wataendelea kuwasubiri mpaka timu yao ya vijana wenye miaka chini ya 20, itakaporejea jijini Mwanza ikitokea Dar es Salaam, kwenye michuano ya Kombe la Uhai.

Choki aliongeza kuwa, programu aliyoiandaa haitafaa huku akiwa na hofu wa kutofanya vizuri kwa kikosi chake katika mzunguko wa lala salama.
Alisema aliandaa programu iliyoonesha watakuwa na mechi tatu za kirafiki kujiandaa na mzunguko wa pili, lakini michezo hiyo kuna uwezekano wa kutochezwa.
 
Abramovich atumia bilioni 11 kusherehekea mwaka mpya


LONDON, Uingereza

WAKATI watu wengi wakifikiria watapataje fedha, lakini wengine kwa hilo si tatizo, kwao tatizo ni jinsi ya kutumia.Tajiri wa Kirusi, ambaye ni mmiliki wa timu ya ya soka ya Chelsea, Roman Abramovich, aliamua kutumia fedha
kufurahi yeye pamoja na watu wengine maarufu aliowaalika katika sherehe ya kuuanga mwaka 2010 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2011.

Sherehe hiyo iliyofanyika katika kisiwa vya St. Barts Carribbean, inaelezwa kuwa, ilikuwa ya kufana pengine ni sherehe nzuri zaidi kuliko zote, ambapo miongoni mwa wageni waalikwa, walikuwa ni wasanii maarufu wa Jiji la Hollywood, Marekani na bendi maarufu ambazo ziliburudisha wageni waalikwa.

Tajiri Abramovich, alionekana kama kuwa mtu wa kawaida na kujichanganya na watu wengine kucheza.

Sherehe hiyo ya mwaka mpya ilimgharimu pauni milioni 5 ambazo ni sawa na fedha za Kitanzania zaidi ya sh. bilioni 11.

Pamoja na kuwepo wasanii maarufu kama marapa wa bendi ya Black Eyed Peas, bilionea wa Russia alionekana kama ni wa kawaida tu, hakupagawa kwa furaha kama walivyokuwa watu wengine.

Abramovich alionekana kama ameboreka, lakini kulikuwa na mastaa kama Salma Hayek na Demi Moore.

Wageni waalikwa katika sherehe hizo walikuwa wamevalia mavazi ya bei mbaya, akiwemo mwanamitindo aliyegeuka kuwa, mwigizaji wa Uingereza, Rosie Huntington.

Lakini, mmiliki huyo wa Chelsea, alionekana kuwa katika hali ya utulivu, akiwa karibu na mkewe Daria Zuchova, kwa kuandaa sherehe hiyo iliyomwongezea umaarufu wake.

Mwaka 2009, alitumia pauni milioni 3, zaidi ya shilingi bilioni 6.6, kwa sherehe kama hizo za mwaka mpya, ambapo nyota kama Orlando Bloom na Kanye West walitumbuiza na Prince, Gwen Stefani na Beyonce.Abramovich inaaminika alimlipa Prince pauni 500,000, ambazo ni zaidi ya sh.bilioni 1.1.Haikujulikana mara moja kwamba, kundi la Black Eyed Peas lililipwa kiasi gani, bila shaka itakuwa ni fedha nyingi.

Abramovich mwenye miaka 44 na mkewe Zuchova mwenye miaka 29, ndiyo waliokuwa wakikaribisha wageni kwenye geti katika eneo lake alilonunua kwa pauni milioni 58, lenye ukubwa wa ekari 70, liliko karibu na Governor Beach katika kisiwa cha Caribbean.Eneo hilo lenye nyumba, mabwawa ya kuongelea na vitu vingine liko bahari, awali lilikuwa likimilikiwa na familia inayomiliki benki Marekani ya Rockefellers.

Baadhi ya wageni waliokuwepo ni panmoja na mwelekezaji wa filamu ya Star Wars, George Lucas, rapa Sean P.Diddy Combs, Ellen DeGeneres, mwimbaji Alicia Keys na Harvey Weinstein, walipelekwa katika kisiwa cha St Barts kwa helikopta kabla ya mwaka mpya.

Katika sherehe hiyo, inaaminika kuwa, Abramovich alitumia mamilioni kwa ajili ya kununua chakula na vinywaji vya wageni 2,560, aliowaalika.

Katika ufukwe kulikuwa na boti yake ya kifahari ambayo inatajwa kuwa ni ndefu kuliko zote duniani, pia ilikuwepo boti ya bilionea mwingine wa Kirusi Andrey Melnichenko, ambayo ina vyumba vya kulala, rasmi kwa wageni ambao walikuwa hawataki kulala kwenye nyumba zilizopo kwenye uzio.

Mwaka mpya wa 2011 ulipowadia, fataki zililipuliwa kutoka kwenye boti na kuwafanya wageni wafurahie. Siku moja kabla ya mwaka mpya, Roman na Daria, mama wa mtoto wake wa kiume mwenye umri wa mwaka mmoja Aaron, walionekana wakienda kwenye boti yake ya kifahari yanye urefu wa futi 543.

Boti hiyo yenye thamani ya pauni milioni 300, ina vyumba 12 na walinzi watano na sehemu ya kuangalia sinema, maktaba na mgahawa. Pia, inaelezewa kuwa, imetengenezwa katika mfumu ambao paparazzi hawawezi kupiga picha ikiwa pia haiwezi kulipuliwa.

 
Ancelotti: Title bid is not over




Updated Jan 2, 2011 12:51 PM ET
Carlo Ancelotti insisted Chelsea are still in the title race despite watching them throw away two vital points in a 3-3 draw with Aston Villa.
But the Blues boss admitted Sunday afternoon's result, which left his side outside the top four, means they must beat Manchester United in March to stand any hope of retaining the Premier League crown.

Sat., Jan. 1
West Brom 1-2 Man Utd | Recap
Liverpool 2-1 Bolton | Recap
Man City 1-0 Blackpool | Recap
Stoke City 2-0 Everton | Recap
Sunderland 3-0 Blackburn | Recap
Tottenham 1-0 Fulham | Recap
West Ham 2-0 Wolves | Recap
Birmingham 0-3 Arsenal | Recap
Sun., Jan. 2
Chelsea 3-3 Aston Villa | Recap
Wigan 0-1 Newcastle | Recap
BPL Scores | Table | Fixtures

Failure to see off Villa left Chelsea marooned in fifth place, six points behind United having played a game more.
While a slip-up from their unbeaten arch-rivals in not impossible, it is highly unlikely Manchester City, Arsenal and Tottenham will all press the self-destruct button.
Ancelotti said after Wednesday's ugly win over Bolton that Chelsea's title defence would have been over had they failed to end their worst run of league results for 11 years - but he was defiant on Sunday.
"It's not over because we are improving and I think that we can say something again this season," he said, pointing out United had to win their game in hand to go nine points clear. "First, they have to win. Second, I think that the gap is not a light gap at this moment. But everything is open again.
"Obviously, we have to beat them here, and we can say something again about the title."
Sunday's result put Ancelotti's position under fresh scrutiny after Wednesday night's ugly 1-0 win over Bolton had eased the pressure on the Italian.
At least Chelsea avoided defeat, a prospect that looked highly likely six minutes from time against a Villa side that had largely outplayed them.
Trailing 2-1 after Ashley Young's penalty and Emile Heskey's header had cancelled out Frank Lampard's spot-kick, the home side thought they had won it when Didier Drogba and John Terry found the net.
Terry's goal sparked wild celebrations as Chelsea's players mobbed Ancelotti, but the joy was short-lived as Ciaran Clark levelled in stoppage-time.
Ancelotti said: "I think that we had a fantastic reaction second half, we played very well, with a lot of energy, with a good spirit.
"And when we thought that the game was won, we lost two points at the last situation.
"For this reason, I'm disappointed because at this moment, when we needed to win, it was our fault because I think we were not able to maintain concentration until the end."
Ancelotti denied his players had paid for over-celebrating, saying: "I think that it was not over-celebration. It was a good reaction after the goal.

WHAT A YEAR!

Take a pictorial look back at an incredible year in soccer with the 2010 Year in Pictures gallery.

"The last goal, yes, it was a mistake, because we conceded an easy cross and we didn't mark in the box."
He also played down an argument between Terry and Drogba at the final whistle, saying: "Everything is okay."
Brad Friedel hailed the fighting spirit of his Villa team-mates as they twice came from behind.
The draw follows on from defeats at the hands of Tottenham and Manchester City, and Friedel hopes it can spark a move away from the drop zone.
"It's a massive point," he told Sky Sports 1. "We've been in such a bad run of form we needed something and it's great to get it at Stamford Bridge.
"We went down 3-2 and all credit to the lads. We've got over what I thought was a poor penalty decision against us at the start and we've fought back and hopefully this will kick-start our season and we can get back up the table."
Clark, Heskey and Young returned to the Villa side on Sunday, along with other recent injury victim Richard Dunne and Friedel hopes their problems in this area are finally over.
"We had a few long-term injuries back in the side today and when you're on a poor run you have to draw a line under it at some stage," he added.
"We showed today we've got a lot of fight in us and we're going to have lot of fight in us for the rest of the season.
"There was a different feel about us today. We showed a lot more determination, they brought wave after wave of attacks in the second period but all in all we're going to go away pleased with a point and hopefully now we can get a win against Sunderland."
 
Chelsea 3-3 Aston Villa




Updated Jan 2, 2011 11:10 AM ET
Ciaran Clark scored a stoppage-time equaliser as Aston Villa snatched a dramatic 3-3 draw against Chelsea at Stamford Bridge on Sunday.
Didier Drogba and John Terry looked to have snatched victory from the jaws of defeat with goals in the final six minutes - but the hosts' poor defending cost them when Clark nodded home a late equaliser.

Sat., Jan. 1
West Brom 1-2 Man Utd | Recap
Liverpool 2-1 Bolton | Recap
Man City 1-0 Blackpool | Recap
Stoke City 2-0 Everton | Recap
Sunderland 3-0 Blackburn | Recap
Tottenham 1-0 Fulham | Recap
West Ham 2-0 Wolves | Recap
Birmingham 0-3 Arsenal | Recap
Sun., Jan. 2
Chelsea 3-3 Aston Villa | Recap
Wigan 0-1 Newcastle | Recap
BPL Scores | Table | Fixtures

Both sides had held the lead in an exciting game, with Frank Lampard's penalty cancelled out by Ashley Young's spot-kick and Emile Heskey's header giving Villa the lead.
The result left Chelsea marooned in fifth place, six points behind Manchester United having played a game more, and crucially outside the Champions League places.
That will place manager Carlo Ancelotti's position under fresh scrutiny, while opposite number Gerard Houllier may enjoy some respite after ending a run of six defeats in seven games.
Chelsea began the match buoyed from ending their worst set of results for 11 years in Wednesday night's ugly 1-0 win over Bolton.
But for all their early possession, they once again lacked any real penetration.
Jeffrey Bruma - making his full Premier League debut - saw a header from a corner blocked but the better chances all fell to Villa, with Gabriel Agbonlahor, Ashley Young and Stewart Downing all going close.
But a sudden loss of discipline cost them dear, captain Stiliyan Petrov booked for a stupid lunge on Florent Malouda moments before James Collins climbed all over the Frenchman to concede a penalty.
Malouda did throw himself to the floor, and Brad Friedel and Collins were both cautioned for protesting, but it was a definite foul and Lampard stepped up to convert his first goal since August.
Villa's frustration got the better of them and they were penalised for more than one late tackle, while Reo-Coker, Agbonlahor and Clark were all booked before half-time.
Clark and the recalled Richard Dunne both missed glorious chances to level when they headed and hooked over, respectively, from close range as Chelsea's defence went to sleep.
Dunne also produced a last-gasp tackle to stop Malouda and a vital clearance to thwart Michael Essien.
Ramires was booked for clipping Petrov's heels and Villa's pressure finally told when Essien's clumsy tackle on Reo-Coker handed them a penalty four minutes before the break. Young made no mistake from the spot.

WHAT A YEAR!

Take a pictorial look back at an incredible year in soccer with the 2010 Year in Pictures gallery.

Collins nodded another half-chance too close to Petr Cech before half-time and Villa picked up where they had left off right from the restart.
And Heskey put them ahead just two minutes in when he climbed above young Bruma to power home Downing's excellent right-wing cross.
The former England player was then booked for a late tackle on Essien as Chelsea began to wake up to their predicament.
Lampard, Drogba and Ramires all saw shots blocked before the latter drilled just wide after the ball broke to him in the box.
The weakness of Ancelotti's bench was summed up when he sent on Jose Bosingwa for Paulo Ferreira.
Lampard was unlucky not to level in the 63rd minute when he sent a vicious volley straight at Friedel, who then brilliantly closed down Malouda as the forward tried to slot Lampard's ball through the keeper's legs.
Ancelotti threw on Salomon Kalou for Ramires for the final 17 minutes.
Downing drilled straight at Cech from 25 yards before Terry was carded for a lunge on Young and Ancelotti played his final card by introducing Daniel Sturridge for Nicolas Anelka.
Chelsea were denied in the final 10 minutes by some desperate Villa defending as the visiting fans began to chant, "You're getting sacked in the morning!", at Ancelotti.
But Drogba came to his manager's rescue six minutes from time with the ugliest of equalisers.
The struggling striker's miscontrol set up Kalou, whose shot was blocked back for Drogba to rifle home via Carlos Cuellar.
Drogba then nodded over Malouda's corner after Villa had brought on Marc Albrighton for an injured Agbonlahor.
With barely a minute remaining, Chelsea snatched what they thought was a winner.
Drogba's bullet header was parried by Friedel straight to Terry, who produced a superb sidefoot finish to spark wild celebrations, with Ancelotti mobbed by his own players.
But the joy was short-lived, with Clark stealing in completely unmarked at the back post to nod in Albrighton's cross.
There was still time for Drogba to volley Bosingwa's cross wide and Albrighton to mishit a volley as both sides poured forward in search of a winner.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…