Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Wigan 0-1 Newcastle




Updated Jan 2, 2011 1:57 PM ET
Shola Ameobi's first-half tap-in earned Newcastle a deserved 1-0 Premier League win over woeful Wigan at the DW Stadium on Sunday.
Ameobi, in the Magpies side as a replacement for injured top-scorer Andy Carroll, pounced in the 19th minute when Ali Al Habsi blocked Joey Barton's shot and Peter Lovenkrands's follow-up hit the upright.

Sat., Jan. 1
West Brom 1-2 Man Utd | Recap
Liverpool 2-1 Bolton | Recap
Man City 1-0 Blackpool | Recap
Stoke City 2-0 Everton | Recap
Sunderland 3-0 Blackburn | Recap
Tottenham 1-0 Fulham | Recap
West Ham 2-0 Wolves | Recap
Birmingham 0-3 Arsenal | Recap
Sun., Jan. 2
Chelsea 3-3 Aston Villa | Recap
Wigan 0-1 Newcastle | Recap
BPL Scores | Table | Fixtures

Fabricio Coloccini and Steven Taylor also both struck the woodwork for the visitors, while Gary Caldwell saw his header come back off the bar for the Latics.
It was a welcome start to 2011 for Alan Pardew as his side bounced back from two straight defeats and moved up to 10th place.
For Wigan, who are just a point and a place above the relegation zone, the situation is more concerning.
Newcastle created the first goalscoring opportunity after just two minutes as Danny Simpson swung a cross into the box from the right.
Ameobi was allowed the space to meet it but the striker was unable to find the target, heading the ball back across the face of goal.
Three minutes later Wigan went close themselves as a failed clearance from Ben Watson's free-kick fell to Tom Cleverley, whose curling shot drew a smart save out of Steve Harper. Antolin Alcaraz headed the resulting corner straight at the Magpies goalkeeper.
Cleverley was presented with another chance on the quarter-hour mark after receiving a neat pass from Mohamed Diame, but the on-loan Manchester United youngster volleyed over the bar.
It was encouraging stuff from the hosts, but within moments, they were behind after a defensive error by Steven Gohouri.
Having dispossessed the Ivorian, Barton struck an effort which Al Habsi managed to parry, but Lovenkrands hit the loose ball against a post and Ameobi was on hand to tuck away the rebound.
An unmarked Lovenkrands should have doubled his side's advantage in the 31st minute after Barton squared to him right in front of goal, but the Dane got the ball stuck under his feet and Watson rushed in to avert the danger.
At the other end Cleverley's deflected shot from the edge of the box earned Wigan a corner which was met by Caldwell. The Latics skipper saw his header bounce back off the bar and the ball came to Hugo Rodallega, who lifted his attempt over.
Newcastle were next to hit the woodwork soon after as Coloccini looped a header onto the top of the goalframe and then Al Habsi had to be alert in rushing out to halt Jonas Gutierrez's progress.
Lovenkrands nodded a good chance over from a cross by Barton, and the former Manchester City man sent a free-kick off-target just before the break.

WHAT A YEAR!

Take a pictorial look back at an incredible year in soccer with the 2010 Year in Pictures gallery.

Martinez substituted Hendry Thomas for James McArthur at half-time and Wigan made the early running after the re-start, Jordi Gomez advancing down the right side but sending his delivery into Harper's arms.
Rodallega tried his luck twice in quick succession only to shoot wide of the mark each time.
Mauro Boselli was then introduced in place of Gomez to give Rodallega fresh support in attack, but it was Newcastle who nearly scored 10 minutes later as yet another header hit the crossbar.
This time it was Taylor denied after he got on the end of Barton's free-kick.
Lovenkrands and Ameobi came off for Wayne Routledge and Leon Best as the visitors looked to close out the game.
Boselli claimed his shot had been blocked by Taylor's hand in the box, but referee Howard Webb waved play on.
The Yorkshire official, who had been made an MBE in the Queen's New Years Honours List, then booked Barton for a rash challenge on McArthur.
Newcastle might have added a second goal towards the end as first Best poked wide after finding himself through one-on-one and then Jose Enrique blasted over, but come the final whistle, they had done enough
 
Osiah, Wambura kuanika mikakati yao kesho


Na Zahoro Mlanzi

KATIBU Mkuu mpya wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Angetile Osiah na Ofisa Habari wake, Boniface Wambura, kesho wanatarajia kuanika mikakati
na malengo yao katika kuliongoza shirikisho hilo.

Viongozi hao walipata nafasi hizo baada ya kuteuliwa na Kamati ya Utendaji ya shirikisho hilo, na kuwapiku wengine 64 walioomba nafasi ya ukatibu na 44, uofisa habari.

Akizungumza ofisini kwake Dar es Salaam jana baada ya kuanza kazi rasmi, Osiah alisema anashukuru kwa kupata nafasi hiyo na pia kwa saa chache alizokaa ofisini humo, amepata ushirikiano mzuri kwani alipokelewa vizuri.

"Tumeanza kazi rasmi leo (jana) na mwenzangu (Wambura), lakini bado hatujakabidhiwa ofisi rasmi kwa maana ya makabidhiano ya document (nyaraka), kwani aliyekuwa akikaimu ameondoka," alisema Osiah.

Alisema Kayuni (Kaimu Katibu Mkuu) ,ameisindikiza timu ya Taifa 'Taifa Stars' kwenda Misri na atakaporudi atakuwa na mapumziko kwani amekuwa akikaimu nafasi hiyo kwa muda mrefu, hivyo atakaporudi, makabidhiano yatafanyika.

Alisema pamoja na hayo, kesho wataanika mikakati yao na mipango katika kuliendeleza soka la Tanzania, ambapo watatoa na taarifa nyingine na jinsi watakavyofanya kazi.

Viongozi hao wameingia madaraka baada ya aliyekuwa Katibu Mkuu, Fredrick Mwakalebela kung'atuka madarakani kwa kuamua kujiingiza katika siasa na aliyekuwa Ofisa Habari, Florian Kaijage, kusimamishwa, lakini mkataba wake ulikuwa umemalizika.

Osiah ana Shahada ya Sayansi ya Jamii kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), amehudhuria kozi nyingi katika taaluma yake ya uandishi wa habari, pia alikuwa Mhariri wa Habari wa magazeti ya Mwananchi.

Kwa upande wa Wambura, ni msomi wa Shahada ya sheria kutoka Chuo Kikuu cha Tumaini, na Stashahada ya Tasnia ya Habari, amehudhuria kozi mbalimbali za uandishi wa habari na pia alikuwa Mhariri Mkuu wa gazeti la Jambo leo.
 
Taifa Stars yaenda Misri


Na Zahoro Mlanzi

KIKOSI cha wachezaji 21 wa timu ya Taifa 'Taifa Stars', kimeondoka jana alfajiri kwenda Misri huku kikiwa na matumaini ya kufanya vizuri katika mashindano ya
Mto Nile.

Timu hiyo itapumzika leo na kesho usiku, itaanza kutupa karata yake kwa kuumana na wenyeji Misri katika mchezo utakaopigwa saa moja usiku ukitanguliwa na mchezo kati ya Kenya na Sudan.

Akizungumza kwa simu akiwa njiani jijini Nairobi, Kenya kwenda nchini huko, Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Silyvester Marsh, alisema timu yake ipo katika hali nzuri kutokana na maandalizi waliyofanya.

"Kwa sasa (jana asubuhi), ndio tumefika Nairobi kwa ndege ya Shirika na Ndege la Misri na muda si mrefu tutaanza safari ya kwenda huko, kila kitu kinakwenda vizuri na wachezaji wapo katika morali ya juu kucheza mashindano hayo," alisema Marsh.

Wachezaji walioondoka ni makipa Juma Kaseja, Shaaban Kado na Said Mohamed, mabeki ni Shadrack Nsajigwa, Stephano Mwasyika, Nadir Haroub 'Cannavaro', Aggrey Morris, Kelvin Yondan na Juma Nyosso.

Viungo ni Nurdin Bakari, Shaaban Nditi, Jabir Aziz, Rashid Gumbo na washambuliaji ni Salum Machaku, Nizar Khalfan, Godfrey Taita, Athuman Machupa, Jerry Tegete, Ali Ahmad Shiboli na Said Maulid 'SMG'.

Mashindano hayo ni maalum kwa ajili ya kudumisha uhusiano miongoni mwa nchi zinazotumia maji ya mto Nile.

Nchi za Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Ethiopia na Eritrea zitashiriki michuano hiyo.

 
Yanga kumuaga Babi Zanzibar leo


Na Elizabeth Mayemba

TIMU ya soka ya Yanga, inatarajia kumuaga rasmi mchezaji wake Abdi Kassim 'Babi', wakati wa mechi yao ya dhidi ya Mafunzo ya Zanzibar, ya kuwania Kombe la
Mapinduzi itakayochezwa kesho katika katika Uwanja wa Amaan mjini Zanzibar.

Babi alifuzu majaribio katika klabu ya Thang Long ya Vietnam, na uongozi wake, umemalizana na klabu hiyo.

Yanga, kesho itacheza mechi yake ya pili usiku kwenye Uwanja wa Aman mjini Zanzibar, mechi ya kwanza dhidi ya Ocean View, walitoka sare ya bao 1-1.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Msemaji wa klabu ya Yanga Louis Sendeu, alisema wameamua watumie mechi hiyo kwa kuwa, Babi ni mchezaji wao aliyeitumikia timu hiyo kwa uaminifu mkubwa.

''Tumeona ni vizuri tukimuaga kwa mchezo wetu wa kesho dhidi ya Mafunzo, kwani muda wowote kuanzia sasa, ataondoka,'' alisema Sendeu.

Alisema katika mchezo huo, Babi atacheza dakika 15 za mwisho, ambazo atatumia kuwaaga mashabiki wa Yanga, viongozi, wanachama na wachezaji wenzake, na tayari kocha anataarifa kuhusu suala hilo.

Sendeu alisema mchezaji huyo anatarajia kuondoka muda wowote kuanzia sasa, ndio maana alishindwa kuunga na timu ya taifa 'Taifa Stars', kwenye nchini Misri kushiriki michuano ya Nile Basin.

 
Simba yatinga robo fainali Uhai Cup


Na Addolph Bruno

TIMU ya soka Simba ya vijana wenye umri chini ya miaka 20, imemaliza vizuri hatua ya makundi na kutinga robo fainali ya Kombe la Uhai, kwa kuikung'uta African Lyon mabao
4-1.

Mchezo huo wa kundi B, uliochezwa jana asubuhi katika Uwanja wa kumbukumbu ya Karume, Dar es Salaam, Simba ilikuwa ya pili kukata tiketi ya robo fainali katika michuano hiyo, ikitanguliwa na AFC Arusha na kuongoza kundi lao kwa pointi tisa.

Wakicheza kwa kasi na kujiamini, Simba ilipata bao la kwanza dakika ya 20, kupitia kwa Kelvin Charle, baada ya kupokea pasi nzuri ya Miraji Athumani.

Bao hilo liliwafanya Lyon kuongeza kasi, lakini walijikuta wakipigwa bao la pili dakika ya 36, kupitia kwa Marcel Bonventure alipokea pasi ndefu ya Athumani.

Timu hizo zilishambuliana kwa zamu, lakini African Lyon ilipata nafasi nyingi za kufunga kupitia Hamis Thabit, mikwaju mingi ilidakwa na kipa wa Simba, Mohamed Azizi.

Dakika ya 34, Charle aliipatia Simba bao la tatu, baada ya kushirikiana vizuri na Miraji, ambaye alikuwa mpishi mkubwa wa mabao.

Chale ambaye pia alifunga bao la nne dakika ya 71, baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa wapinzani wao.

Mabeki wa Simba, walishindwa kumdhibiti Abuu Mwasekaga, aliyeifungia bao African Lyon dakika ya 89 .

Michezo ya hatua ya makundi ya inamalizika leo kwa mechi za kundi C, Mtibwa Sugar itaumana na Kagera Sugar asubuhi na jioni JKT Ruvu na Majimaji 'Wanarizombe' ya Songea.

 
Matibabu ya India yamenirudishia uhai- Uhuru Monday, 03 January 2011 18:26

Sosthenes Nyoni
NI majira ya saa 5.00 asubuhi ya Jumapili, nimeanza safari ya kuelekea Temeke kwa ajili ya kumwona na kumjulia hali Uhuru Selemani, mchezaji wa klabu ya Simba na Taifa Stars ambaye amerejea nchini kiasi cha wiki sasa akitokea India kwa matibabu ya goti.

Kichwani, ninapanga na kupangua mambo mengi hasa kuhusu jinsi ya kuifanya kazi hiyo, ingawa kwa maelekezo ya simu, Uhuru aliniambia nishukie kituo cha daladala cha Usalama (Chang'ombe).

Lakini, Uhuru ambaye ni mchangamfu alikuwa amenipa namba nyingine ya simu ambayo alinieleza kuwa ni ya mke wake, aitwaye Jamila, ili endapo nitashuka kituoni pale, nimpigie yeye (Jamila), ambaya atanipokea.

Hapo, ndipo udadisi wangu ukaanza, nikidhani pengine mwenyeji wangu alikuwa hajiwezi, kumbe haikuwa hivyo, niliposhuka nikampigia simu mwanamama huyo ambaye sikuwa namfahamu alinielekeza jinsi ya kufika nyumbani kwao.

Hivyo ndivyo nilivyofika nyumbani kwa Uhuru ambako katika mazungumzo yetu, mchezaji huyo ambaye amerejea nchini akitokea India alikoenda kwa matibabu ya goti alionekana mwenye matumaini mapya.

Katika simulizi yake iliyojaa tabasamu, mchezaji huyo akaeleza jinsi alivyopata huduma ya upasuaji ambao anaamini ni bora na wa uhakika.

Katika mahojiano hayo maalum na Mwananchi, Uhuru akasema kuwa kabla ya kwenda India alianza kukata tamaa akijua mwisho wa kipaji chake cha kucheza soka umewadia kutokana na tatizo lake kujirudia mara kwa mara.

"Kwa kweli namshukuru Mungu nimepata matibabu ya uhakika na nina matumaini mpya sasa, unajua lile tatizo lilikuwa linajirudia rudia kila wakati na kwa mazingira ya kwetu ingekuwa ngumu sana kupona.

"Lakini, pia namshukuru Mungu kwa sababu daktari aliyenihudumia aliniambia nisiwe na hofu nitarudi tena uwanjani kwani umri wangu unaruhusu, lakini kama ningekuwa na miaka zaidi ya 30 nisingeweza kupona kabisa kutokana na aina ya tatizo nililokuwa nalo,"akaeleza Uhuru ambaye aliumia wakati wa mechi ya ligi kuu dhidi ya Toto Afrika ya Mwanza.

Anaongeza kuwa faraja nyingine aliyonayo ni matokeo ya vipimo vya damu kuonyesha hana maambuziki ya virusi vya Ukimwi au ugonjwa wowote mkubwa ikiwa ni sharti mojawapo la mtu mwenye tatizo kama lake ili aweze kufanyiwa upasuaji.

"Unajua sharti jingine alilotuambia daktari kabla ya kufanyiwa upasuaji ni kwamba ni lazima damu yangu iwe safi isiyokuwa na maambukizi ya Ukimwi ambalo pia namshukuru Mungu baada ya vipimo majibu yalikuwa safi,"anasema Uhuru.

Uhuru ambaye ni baba wa mtoto mmoja aliyemtaja kwa jina la Nasri, mwenye umri wa miezi minne anasema kuwa daktari wake alimwambia ili aweze kupona kabisa itachukua miezi mitatu na mitatu mingine kuweza kucheza soka ya ushindani, kitu ambacho kitamweka nje ya dimba mzunguko wote wa pili.

Hata hivyo, hafichi shukrani zake kwa makamu mwenyekiti wa klabu yake, Godfrey Nyange'Kaburu' akisema kwa yeye ni kama baba yake kwa vile amekuwa msaada mkubwa kwake wakati wote.

"Acha nikuambie kwamba Kaburu kwangu ni baba na ni sehemu ya familia yangu ni mtu wa aina yake kwa kweli amenisaidia sana mpaka sasa.

"Siwezi kusema ni kiasi gani cha fedha kimetumika, lakini ni fedha nyingi na matibabu yake ni ghali sana, lakini yeye hakuangalia hilo zaidi ya kutaka mimi nipone,"anasema.

Uhuru pia anatoa ushauri kwa viongozi wa klabu nyingine nchini kutoyapuuzia matatizo ya wachezaji wao hasa pale wanapokuwa na matatizo kama yake akiwataka waige mfano wa wenzao wa Simba ambao hawakujali ukubwa wa gharama za matibabu yake.

"Huko India nimehudumiwa vizuri sana, wale jamaa wako mbali sana tofauti na sisi kuna vifaa vingine mimi ndiyo mara yangu ya kwanza kuviona," anaeleza.

 
Maulid tutafanya vema Misri Monday, 03 January 2011 18:20

Imani Makongoro
MSHAMBULIAJI wa zamani wa klabu ya Yanga, Said Maulid ‘SMG' amesema ana matumaini makubwa kuwa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars itafanya vyema katika mashindano ya kwanza ya Mto Nile.

Maulid alisema hayo kabla ya kuondoka nchini jana alfajiri kwenda Cairo, Misri kwa ajili ya mashindano hayo.

Alisema kuwa kitu ambacho amevutiwa nacho sana katika timu hiyo ni moyo wa kujituma na morali ya wachezaji tofauti na timu za taifa zilizokuwepo kabla ya kocha Marcio Maximo.

Kwa mujibu wa Maulid, wachezaji wameonyesha wapo tayari kupigania taifa lao na kumpa heshima kubwa kocha msaidizi, Sylvester Marsh kinyume na matarajio yake.

"Kwa kweli tumepiga hatua kubwa sana na hii tabia ya kuishi kwa lugha moja ndani ya kambi imenipa faraja kubwa na nina imani kubwa tutafanya vizuri sana huku Cairo, morali ni kubwa sana na kila mchezaji anazungumzia ushindi na ushindani kwenye michuano hiyo," alisema.

Alisema kuwa kwa kipindi cha miaka mitatu akiwa Angola, ameona mabadailiko makubwa na amesifia msingi uliowekwa na Maximo umesaidia sana kujenga nidhamu kwa timu hiyo.

Aliongeza kuwa wachezaji wote wa Taifa Stars wanatabia za wachezaji wa kulipwa , jambo ambalo limempa faraja kubwa sana.

Alisema kuwa wachezaji wanajua majukumu yao kwani wanawakilisha watu zaidi ya milioni 35 ambao wote wameelekeza masikio na macho yao huko Misri.

Maulid anayechezea klabu ya Onze Bravos ya Angola alisema kuwa watatumia mashindano hayo kama kipimo halisi kabla ya mashindamo ya kufuzu ya Mataifa ya Afrika.

Taifa Stars itafungua dimba kesho usiku kwa kupambana na wenyeji, Misri. Mchezo huo utachezwa usiku (kuanzia saa 2.00). Nchi nyingine zanazoshiriki mashindano hayo ni Burundi, Rwanda, Kenya, Sudan na Uganda.

 
Arusha waitosa AFC Monday, 03 January 2011 18:19

Calvin Kiwia
UONGOZI wa timu ya AFC ya Arusha ya U-20 iliyotinga hatua ya robo ya mashindano Kombe la Uhai, unaomba msaada kwa wadau wote wa soka nchini baada ya kutimuliwa kwenye hoteli African waliofikia iliyopo Tandika jijini Dar es Salaam.

Meneja wa timu hiyo Dennis Shemdoe aliliambia Mwananchi jana jijini Dar es Salaam kuwa wanaishukuru kampuni ya Clouds Intertainment kuguswa na kujitolea kuwagharamia timu hiyo chakula na malazi.

"Tunaishukuru sana kampuni ya Clouds Intertainment kukubali kutulipia gharama za chakula na malazi kwenye hoteli hiyo pia tunawaomba wadau wote wa soka nchini kutusaidia kwa kipindi hichi kigumu," alisema Shemdoe.

Pia alitoa shukrani zake kwa wachezaji wa timu ya Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa na Nurdin Bakari kwa kuichangia kiasi cha sh 40,000 ambazo ziliwasaidia wachezaji wa timu hiyo kupata chakula jioni.

Shendoe alisema wadhamini wa mashindano hayo walitoa kiasi cha Shs milioni moja kwa kila mshiriki, lakini wao walizitumia kwa kununua vifaa vya timu hiyo vya kufanyia mazoezi kama vile bipsi, viatu kwa baadhi ya wachezaji na mipira ambavyo viligharimu zaidi ya sh 500,000.

"Hatukupewa chochote na chama cha soka mkoa wa Arusha (ARFA) tuliondoka kama tulivyo, lakini tumewasiliana na kuwaeleza hali yetu kwa sasa na hapa ndiyo tunasubiria majibu kutoka kwao," alisisitiza.

Aliongeza kuwa amekuwa kwenye wakati ngumu kutokana na wazazi wa wachezaji wake kumpigia simu na kumtaka awaachie warudi majumbani kwao kwa ajili ya maandalizi ya shule baada ya kusikia hali iliyowakumba.

"Wengine walinifuata mpaka jijini Dar es Salaam wakiwataka watoto wao, lakini nashukuru niliwaelewesha na kunielewa japo kwa shingo upande huku wakitoa masharti kama hali hiyo itaendelea watafika kuwachukua," alisema Shemdoe.
 
Ocean View pungufu waishika Yanga
Monday, 03 January 2011 18:16

Jackson Odoyo, Zanzibar
UPEPO mbaya bado unaendelea kuiandama Yanga baada ya kukubali kulazimishwa sare ya 1-1 na wachezaji 10 wa Zanzibar Ocean View jana usiku kwenye mwendelezo wa michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Mwamuzi wa mchezo huo Makame Haji Mpoma alilazimika kusimasha pambano hilo kwa dakika 15, baada ya kukatika kwa umeme kwenye Uwanja wa Amaan.

Mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia, Davies Mwape aliifungia Yanga bao la kwanza tangu alipojiunga nayo kwa kumalizia vizuri pasi ya Iddy Mbaga.

Mbaga kabla ya kumtengenezea mfungaji alifanyaka kazi nzuri baada ya kuwazidi ujanja mabeki wa Ocean View pamoja na kipa na kumpa pasi Mzambia huyo.

Furaha ya mashabiki wa Yanga haikudumu baada ya Amour Suleiman kufunga bao la kusawazisha dakika ya 22 kwa mpira wa adhabu uliokwenda moja kwa moja wavuni na kumuacha kipa Mghana Yew Berko asijue chakufanya.

Dakika ya 62 mfungaji wa goli la Ocean View, Suleiman alitolewa nje kwa kadi nyekundi baada ya kumchezea vibaya mchezaji wa Yanga.

Zanzibar Ocea View walionekana kuwa bora zaidi kwa kucheza pasi fupi fupi ingawa washambuliaji wake walikosa umakini wa kumalizia mbele ya kipa Berko.

Wachezaji wa Yanga, Godfrey Bonny na Ernest Boake walizadiwa kadi ya njano huku Azizi Shaweji wakipatiwa kadi ya njano kwa upande wa Ocean View.

Timu hizo zilikwenda mapumziki zikiwa sare 1-1, katika kipindi cha pili Yanga walifanya mabadiliko na kumtoa Mbaga, Juma Self na Omega Seme nafasi zao kuchukuliwa na Nsa Job Mahenya, Lazaki Khalfan na Godfrey Bonny ‘Fundi'.

Hata hivyo mabadiliko hayo haya kuwasaidia wanajangwani hao ambao katika muda mwingi wa kipindi cha pili walicheza kwa kujiami zaidi kuliko kushambulia.
 
Osiah, Wambura waingia mzigoni Monday, 03 January 2011 18:16

Imani Makongoro

KATIBU mkuu mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah na Ofisa Habari, Michael Wambura, jana walikabidhiwa rasmi Ofisi sambamba na kuanza majukumu yao kama waajiliwa wapya wa Shirikisho hilo.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Osiah alisema kuwa kesho wataanza rasmi majukumu yao ya kiofisi ambapo watakutana na wandishi wa habari katika ofisi za Shirikisho hilo Karume kwa ajili ya kujitambulisha kwao na kuelezea mikakati yao.

Alisema kuwa ingawa wamekabidhiiwa ofisi, lakini wanamsubili aliyekuwa Kaimu katibu mkuu wa TFF, Sunday Kayuni kwa ajili ya makabidhiano ya mwisho kwani yeye ndiyo mambo yote.

"Kama mnavyojua Kayuni ambaye alikuwa akikaimu nafasi hii ameisindikiza timu iliyoondoka leo alfajili (jana) kwenda Cairo, Misri kwenye mashindano hivyo mara tu atakaporejea tutafanya makabidhiano ya mwisho," alisema Osiah.

Alisema kuwa wanashukuru walipofika katika ofisi hizo wamepokelewa vizuri na wafanyakazi waliowakuta ofisi hapo na kuahidi kufanya nao kazi bega kwa bega katika kuendeleza gurudumu la soka hapa nchini na kimataifa.

Osiah na Wambura walishinda nafasi hizo baada ya mchakato wa kuwapata viongozi wapya uliofanyika kwa muda wa miezi mitatu kumalizika, kufuatia aliyekuwa katibu mkuu Fredrick Mwakalebela na Ofisa habari, Florian Kaijage kumaliza muda wao.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…