Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
-
- #2,661
Man Utd yashikiria ajira ya Hodgson
Friday, 07 January 2011 19:39
LONDON, ENGLAND
BAADA ya mchakamchaka ya wiki tatu ya katika Ligi Kuu vigogo wa England wiki hii watapooza kasi kwa kurudi kwenye michezo ya Kombe la FA.
Mchezo uliobeba hisia nyingi ni ule unazikutanisha Manchester United dhidi ya mahasimu wao Liverpool waliopoteza dira msimu huu.
Macho na masikio ya wengi itakuwa kujua hatima ya kocha wa Roy Hodgson ambaye hadi sasa anaoneka kuwa na nafasi finyu ya kuendelea kubaki kwenye kibarua chake baada ya mchezo huo.
Vijana wa Hodgson kwa sasa wanaonekana kupigana kutoshuka daraja kuliko kupanda ngazi mpaka kwenye klabu nne bora na kitu wasichopenda kukisikia wala kukiona mbele yao ni safari ya kupambana na mahasimu wao Manchester United, lakini hilo haliwezekani kwani timu hizo zitapimana ubavu katika mechi itakayotimua vumbi kesho.
Wapenzi wa soka wanaisubiri mechi kwa hamu lakini dalili iliyo wazi ni kuwa timu ya Roy Hodgson huenda ikaangukia pua.
Mechi kati ya Manchester United na Liverpool itakutanisha timu ambazo zimetofautiana sana msimu huu. Manchester United iliongeza kasi katika kiti cha uongozi kwenye ligi kuu wiki hii baada ya kuifunga Stoke City hivyo kujikusanyia pointi 44 huku Liverpool, ikizidi kuanguka baada ya kufungwa mabao 3-1 na Blackburn Rovers wiki hii, kipigo hicho kimeongeza wasiwasi kwa kocha Roy Hodgson, ambaye anakaribia kutimuliwa kutokana na timu kufanya vibaya kila kukicha.
Kocha wa Manchester United, Alex Fergsuon ambaye aliwakosa Rio Ferdinand, Edwin van der Sar na Wayne Rooney, ambao walikosa mechi ya Jumanne dhidi ya Stoke City watarudi uwanjani kupambana na Liverpool.
Licha ya kuwepo kwa mechi hiyo ratiba pia inaonyesha kuwaLeicester City inayoshiriki Ligi Daraja la Pili pia itakwaana na Manchester City kesho.
Kocha wa Leicester, Sven Goran Eriksson atakuwa na shauku ya kuiangusha klabu ambayo ilimtimua baada ya kuinoa kwa msimu mmoja mwaka 2008.
Arsenal nayo itaikaribisha Leeds United, ambayo ilishangaza watu kwa kuifunga Manchester United, wakati mabingwa wa kombe hilo Chelsea watakuwa nyumbani kupambana na Ipswich Town kesho.
Kwa kuwa ndoto za kupata ubingwa wa Ligi Kuu England zimeyeyuka kama moshi angani, matumani ya Chelsea sasa ni kunyakua vikombe vingine.