Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Man Utd yashikiria ajira ya Hodgson
Friday, 07 January 2011 19:39

LONDON, ENGLAND
BAADA ya mchakamchaka ya wiki tatu ya katika Ligi Kuu vigogo wa England wiki hii watapooza kasi kwa kurudi kwenye michezo ya Kombe la FA.

Mchezo uliobeba hisia nyingi ni ule unazikutanisha Manchester United dhidi ya mahasimu wao Liverpool waliopoteza dira msimu huu.

Macho na masikio ya wengi itakuwa kujua hatima ya kocha wa Roy Hodgson ambaye hadi sasa anaoneka kuwa na nafasi finyu ya kuendelea kubaki kwenye kibarua chake baada ya mchezo huo.

Vijana wa Hodgson kwa sasa wanaonekana kupigana kutoshuka daraja kuliko kupanda ngazi mpaka kwenye klabu nne bora na kitu wasichopenda kukisikia wala kukiona mbele yao ni safari ya kupambana na mahasimu wao Manchester United, lakini hilo haliwezekani kwani timu hizo zitapimana ubavu katika mechi itakayotimua vumbi kesho.

Wapenzi wa soka wanaisubiri mechi kwa hamu lakini dalili iliyo wazi ni kuwa timu ya Roy Hodgson huenda ikaangukia pua.

Mechi kati ya Manchester United na Liverpool itakutanisha timu ambazo zimetofautiana sana msimu huu. Manchester United iliongeza kasi katika kiti cha uongozi kwenye ligi kuu wiki hii baada ya kuifunga Stoke City hivyo kujikusanyia pointi 44 huku Liverpool, ikizidi kuanguka baada ya kufungwa mabao 3-1 na Blackburn Rovers wiki hii, kipigo hicho kimeongeza wasiwasi kwa kocha Roy Hodgson, ambaye anakaribia kutimuliwa kutokana na timu kufanya vibaya kila kukicha.

Kocha wa Manchester United, Alex Fergsuon ambaye aliwakosa Rio Ferdinand, Edwin van der Sar na Wayne Rooney, ambao walikosa mechi ya Jumanne dhidi ya Stoke City watarudi uwanjani kupambana na Liverpool.

Licha ya kuwepo kwa mechi hiyo ratiba pia inaonyesha kuwaLeicester City inayoshiriki Ligi Daraja la Pili pia itakwaana na Manchester City kesho.

Kocha wa Leicester, Sven Goran Eriksson atakuwa na shauku ya kuiangusha klabu ambayo ilimtimua baada ya kuinoa kwa msimu mmoja mwaka 2008.

Arsenal nayo itaikaribisha Leeds United, ambayo ilishangaza watu kwa kuifunga Manchester United, wakati mabingwa wa kombe hilo Chelsea watakuwa nyumbani kupambana na Ipswich Town kesho.

Kwa kuwa ndoto za kupata ubingwa wa Ligi Kuu England zimeyeyuka kama moshi angani, matumani ya Chelsea sasa ni kunyakua vikombe vingine.

 
Nusu fainali Kombe la Uhai leo

Imeandikwa na Evance Ng'ingo; Tarehe: 7th January 2011 @ 23:50 Imesomwa na watu: 45; Jumla ya maoni: 0








NUSU fainali ya ligi ya Kombe la Uhai inafanyika leo kwenye Uwanja wa Karume, Dar es Salaam ambapo Ruvu Shooting itarajiwa kuumana na AFC huku Polisi Dodoma ikicheza na JKT Ruvu.

Mechi hizo zinatarajiwa kuwa na msisimko wa hali ya juu kutokana na vijana hao kuonesha soka safi.

Kivutio pekee katika timu hizo zilizoingia hatua hiyo ni AFC ambayo inakabiliwa na ukata mkubwa lakini wachezaji wake wanajitahidi kufa kupona kupata nafasi ya kucheza fainali.

Ruvu Shooting imefuzu hatua hiyo baada ya kuifunga Yanga huku AFC ikiifunga African Lyon katika hatua ya robo fainali.

Nayo JKT Ruvu imetinga hatua hiyo baada ya kuifunga Simba na Polisi ikiifunga Mtibwa Sugar.
 
Mikoa yakataa wenyeji tisa bora
Friday, 07 January 2011 19:40

Sweetbert Lukonge
HATUA ya tisa bora ya michuano ya Ligi Daraja la Kwanza inatarajia kuanza kutimua vumbi Januari 30, huku mikoa ikisuasua kujitolea kuwa wenyeji.

Kamati ya mashindano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilikutana hivi karibuni na kupanga tarehe hiyo, hata hivyo mpaka sasa mashindano hayo hayajulikani yatafanyika katika mkoa gani kufutia mikoa yote nchini kushindwa kujitokeza kuwa wenyeji wa ligi hiyo ambayo itatoa timu nne zitakazopanda Ligi Kuu msimu ujao.

Akizungumza na wanahabari jana Ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura alisema mapendekezo hayo ya kamati ya mashindano yalipelekwa kwenye kamati ya utendaji ya shirikisho hilo ili kuthibitiswa ikiwa ni pamoja na kutaja kituo kitakacho tumika kwa ajili ya mashindano hayo.

"Baada ya kamati ya utendaji ya TFF kuthibitisha mapendekezo ya kamati ya mashindano sasa hatua ya tisa bora ya Ligi Daraja la Kwanza itaanza Januari 30.

"Hata hivyo tangu TFF ilipotangaza fursa kwa mkoa ambao utakuwa tayari kuwa mwenyeji wa mashindano hayo kwa maana ya kubeba gharama za fainali hizo, mpaka sasa hakuna mkoa uliojitokeza hivyo kamati ya utendaji ya TFF itakutana tena ili kupanga ni wapi mashindano hayo yatafanyika," alisema Wambura.

Timu zilizofanikiwa kutinga katika hatua hiyo ya tisa bora ya michuano hiyo ni pamoja na Prisons, Coastal Union, Polisi Mogorogo, Moro United, Rhino Rangers, TMK United, JKT Olijoro, Morani FC pamoja na Villa Squad.
 
Tamasa la Wasanii kufufuliwa leo


na Khadija Kalili


amka2.gif
BENDI ya Tunaweza Sound ambayo inaundwa na wasanii wenye ulemavu wa viungo inatarajiwa kutoa burudani katika kuukaribisha mwaka 2011 kwa kufufua upya bonanza la wasanii lililokufa mwaka jana ambako sasa litakuwa likifanyika kila Jumamosi viwanja vya Leaders Club Dar es Salaam.
Mratibu wa bonanza hilo, Juma Mbizo, alisema mbali ya Tunaweza Sound, bendi nyingine zitakazokonga mashabiki ni Diamond Musica, Supershine Modern Taarab, Stone Mayasica sambamba na wasanii mbalimbali wanaotamba katika muziki wa miondoko ya Bongo Fleva.
Aliongeza kuwa, kadhalika wasanii wa michezo ya kuigiza, vichekesho pamoja na filamu watakuwepo katika bonanza hilo lililopangwa kuanza saa 9:00 alasiri kiingilio kikiwa ni bure.
Mbizo aliongeza kuwa, Bonanza hilo litatanguliwa na michezo ya soka, ambako Garage Stars itaumana na Mwananyamala, TZF Veteran itaivaa Kigogo huku Mburahati Queens watashebeduana na Mchangani Sisters ya Mwananyamala, ambako Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mbunge wa Kinondoni Idd Azzan huku Mkurugenzi wa Jahazi Modern Taarab Mzee Yussuf akiwa mwanamuziki mwalikwa.
Tunaweza Sound inasimamiwa na aliyekuwa mchezaji wa zamani wa timu ya soka ya Simba na timu mbalimbali zilizopo Falme za Kiarabu (UAE), Isihaka Kibene.
 
Simba vs Yanga Machi 5 Jamhuri Moro


na Samia Mussa


amka2.gif
VIGOGO vya soka nchini Simba na Yanga vinatarajiwa kukutana Machi 5 kwenye Uwanja wa Jamhuri Mji Kasoro Bahari, Morogoro, katika mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara.
Timu hizo zitakutana katika mechi ambayo itakuwa ni muhimu kwa timu zote, huku Simba ikitaka kulipa kisasi baada ya kufungwa bao 1-0 na Yanga katika mechi ya awali iliyopigwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza Oktoba 16 mwaka jana.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema, mzunguko wa pili wa ligi hiyo unatarajiwa kuanza kutimua vumbi Januari 15 na kufikia ukomo Aprili 10 mwaka huu katika viwanja tofauti nchini.
Wambura alisema kuwa ratiba hiyo imezingatia mambo mengi ikiwamo ushiriki wa Simba na Yanga katika mashindano ya kimataifa na timu ya taifa ‘Taifa Stars' ambayo inashiriki michuano ya awali kusaka tiketi ya kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika 2012 ambapo itavaana na Jamhuri ya Afrika ya Kati Machi 26 pamoja na kalenda ya mechi za kirafiki za Shirikisho la Kimataifa la Soka (FIFA).
Wakati Stars ikijiwinda na Mataifa ya Afrika, Simba itakuwa ikijiandaa na ligi ya mabingwa Afrika huku Yanga ikishiriki Kombe la Shirikisho.
Kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo iliyotangazwa jana na Wambura, inaonyesha Azam FC itafungua pazia kwa kukipiga na Kagera Sugar Uwanja Mkwakwani, Tanga, Toto Africa dhidi ya Polisi Tanzania Uwanja CCM Kirumba Mwanza, Majimaji na JKT Ruvu Uwanja wa Majimaji mjini Songea huku AFC ya Arusha ikipepetana na African Lyon Uwanja Sheikh Aman Abed.
Aidha ratiba hiyo pia inaonyesha kuwa mabingwa watetezi wa ligi hiyo Simba wataanza kampeni yake ya kutetea ubingwa Januari 21 kwa kucheza na Azam FC Uwanja wa CCM Kirumba, huku watani wao wa jadi Yanga siku hiyo wakivaana na AFC Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Wakati huohuo, Kamati ya Mashindano ya TFF, imepanga fainali ya ligi daraja la kwanza hatua ya tisa bora ianze Januari 30 mwaka huu, ambapo mapendekezo hayo yatapelekwa kwenye Kamati ya Utendaji kwa ajili ya kuthibitishwa ikiwemo kutaja kwa kituo.
Wambura alisema, awali TFF ilitoa fursa kwa mikoa ambayo itakuwa tayari kuwa ni mwenyeji, kwa maana ya kubeba gharama za fainali hizo lakini hadi hivi sasa hakuna uliojitokeza kubeba jukumu hilo.
Alizitaja timu zilizofuzu kucheza fainali hiyo ya mkondo mmoja ikiwamo Coastal Union ya Tanga, JKT Oljoro ya Arusha, Morani ya Manyara, Moro United ya Dar es Salaam, Polisi Morogoro, Rhino Rangers ya Tabora, Tanzania Prisons ya Mbeya, TMK United na Villa Squad za jijini Dar es Salaam, ambako timu nne za kwanza zitapanda ligi kuu msimu ujao.
 
Bingwa Uhai Cup kulamba mil. 1.5/-


na Samia Mussa


amka2.gif
FAINALI za mashindano ya vijana chini ya miaka 20, U-20 ‘Uhai Cup', zinatarajiwa kulindima Januari 10 katika Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam huku bingwa akijitwalia kitita cha sh milioni 1.5, kombe na medali.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura, mshindi wa pili atajitwalia sh milioni 1, huku wa tatu akiibuka na kitita cha sh 500,000, wakati mchezaji bora wa jumla atapata sh 400,000.
Wambura alifafanua kuwa mchezaji bora atapata sh 300,000 huku kipa bora naye akipata kiasi kama hicho.
Alisema, nusu fainali ya mashindano hayo inatarajiwa kuanza leo asubuhi kwa Ruvu Shooting kumenyana na maafande wenzao watoto wa JKT Ruvu, wakati jioni Polisi Tanzania itavaana na AFC ya Arusha.
 
Moro waapa kufa na ‘vihiyo' MRFA


na Joseph Malembeka, Morogoro


amka2.gif
WADAU wa soka mkoani Morogoro wameapa kuwapandisha mahakamani ‘vihiyo' wote waliojitumbukiza kuwania nafasi za uongozi wa chama cha soka mkoa (MRFA), baada ya kubainika wengi waliosajiliwa hawana sifa za kuongoza kwa mujibu wa katiba na maagizo ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na mwandishi wa habari hizi mjini hapa, wadau hao walisema lengo la kutinga mahakamani Januari 10 linatokana na kuchoshwa na vihiyo katika chama hicho, jambo linalosababisha kuendelea kushuka kwa kiwango cha soka mkoani humo.
"Unajua kuna ubabaishaji mwingi unaosababishwa na kutokuwa na elimu ya kukabiliana na ukuaji wa michezo mkoani hapa, wengi wa viongozi ni vihiyo hawana elimu angalau ya kidato cha nne kama ilivyoliona TFF na kuagiza kufuata...tunasubiri watoe majina ya waliopitishwa twende kudai vyeti vyao mahakamani," alifafanua Fenus Mrope.
Mrope aliongeza kuwa, nafasi zenye shaka na zinazowaniwa na wanaodaiwa vihiyo ni pamoja na Mwenyekiti, Katibu Mkuu na wajumbe, ambako katika nafasi ya wajumbe imebainika kuwa wengi wao hawana klabu wanazozichezea au kuziongoza.
Wadau hao waliongeza kuwa, hata usaili uliofanyika Januari 1 ulikuwa na mauza uza, ambako baadhi ya wajumbe waliokuwa wakitaka baadhi ya nafasi hawakuwepo na kwa mizengwe hiyo majina yao yanatarajiwa kurudi kama wagombea.
"Hatuwezi kutaja majina leo, tunasubiri kamati ya kusimamia uchaguzi huo iyaweke hadharani ndio tuamshe moto, sio kumkomoa mtu ila tunachotaka ni ukweli na haki kutendeka kila mtu apate kwa kanuni hiyo," alifafanua mmoja kwa niaba ya wenzake.
Majina ya waliopitishwa yalitarajiwa kutajwa jana, ambako uchaguzi wa chama hicho umekuwa ukikumbwa na mizengwe ya kila aina kila unapofikia wakati wa kufanyika, huku zikiibuliwa tuhuma mbalimbali kwa wagombea na uongozi wenyewe.
 
Kumekucha NSSF CUP 2011


na Mwandishi wetu


amka2.gif
MASHINDANO ya Kombe la NSSF kwa mwaka huu yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Machi 2 hadi Aprili 12 mwaka huu na yataendeshwa kwa mtindo wa ligi.
Akizungumza na Waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa mashindano hayo, Juma Kintu, alisema mashindano ya mwaka huu yatashirikisha timu za soka 20 na 16 za netiboli kutoka vyombo vya habari, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo (bara), Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo ya SMZ na wenyeji NSSF.
Alisema, mashindano ya NSSF, yalianza mwaka 2005 na kila mwaka yamekuwa yakizidi kuwa bora na zawadi kuongezwa kulingana na mahitaji ya wakati husika.
Alibainisha kuwa, jambo la kujivunia kwa sasa ni mashindano hayo kubadilika kutoka mfumo wa mtoano hadi ligi, ambao hutoa fursa kwa timu kushiriki mechi nyingi zaidi.
"Mwaka huu mashindano yetu yatakuwa tofauti sana, kwanza mzabuni wa vifaa tayari ameishapatikana na tunatarajia atatukabidhi vifaa mwezi ujao, pili tutatayafanya kwa mtindo wa ligi," alisema Kintu.
Naye Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Masoud Sanani alisema kuwa, usajili wa wachezaji watakaoshiriki kwenye michezo hiyo umeanza na unatarajia kufungwa mwishoni mwa mwezi huu.
Sanani alisema, wameunda kamati ya usajili na uhakiki wa majina ili kudhibiti kasoro ambazo zilikuwa zikitokea mara kwa mara huko nyuma, ikiwemo kuchezesha wachezaji wasiostahili ‘Mamluki'.
Aliwataja wajumbe walioteuliwa kuunda kamati ya usajili na majina ya vyombo wanavyotoka kwenye mabano ni Ibrahimu Bakari (Mwananchi), Chacha Maginga (TBC), Issa Katoba (Mwanahalisi), Willy Edward (Jambo Leo), na Baruan Muhuza (Star tv).
Wajumbe wa kamati ya uhakiki ni Lukman Maloto (Global Publishers), Salehe Mohamed (Free Media), Mfaume Mzee (NSSF), Juma Mmanga (Habari Zanzibar), na Mohamed Dume (IPP).
 
Mikoa yakataa wenyeji tisa bora Friday, 07 January 2011 19:40

Sweetbert Lukonge

HATUA ya tisa bora ya michuano ya Ligi Daraja la Kwanza inatarajia kuanza kutimua vumbi Januari 30, huku mikoa ikisuasua kujitolea kuwa wenyeji.

Kamati ya mashindano ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) ilikutana hivi karibuni na kupanga tarehe hiyo, hata hivyo mpaka sasa mashindano hayo hayajulikani yatafanyika katika mkoa gani kufutia mikoa yote nchini kushindwa kujitokeza kuwa wenyeji wa ligi hiyo ambayo itatoa timu nne zitakazopanda Ligi Kuu msimu ujao.

Akizungumza na wanahabari jana Ofisa habari wa TFF, Boniface Wambura alisema mapendekezo hayo ya kamati ya mashindano yalipelekwa kwenye kamati ya utendaji ya shirikisho hilo ili kuthibitiswa ikiwa ni pamoja na kutaja kituo kitakacho tumika kwa ajili ya mashindano hayo.

"Baada ya kamati ya utendaji ya TFF kuthibitisha mapendekezo ya kamati ya mashindano sasa hatua ya tisa bora ya Ligi Daraja la Kwanza itaanza Januari 30.

"Hata hivyo tangu TFF ilipotangaza fursa kwa mkoa ambao utakuwa tayari kuwa mwenyeji wa mashindano hayo kwa maana ya kubeba gharama za fainali hizo, mpaka sasa hakuna mkoa uliojitokeza hivyo kamati ya utendaji ya TFF itakutana tena ili kupanga ni wapi mashindano hayo yatafanyika," alisema Wambura.

Timu zilizofanikiwa kutinga katika hatua hiyo ya tisa bora ya michuano hiyo ni pamoja na Prisons, Coastal Union, Polisi Mogorogo, Moro United, Rhino Rangers, TMK United, JKT Olijoro, Morani FC pamoja na Villa Squad.
 
Ronaldinho ruksa kuondoka Friday, 07 January 2011 19:38

RIO DE JANEIRO, Brazil
KIUNGO Ronaldinho na klabu yake ya AC Milan wamekubaliana namna ya kuvunja mkataba baina yao, lakini bado hajaamua ni timu gani atajiunga nayo nchini Brazil.

Kiungo huyo alifanya mkutano na vyombo vya habari jijini Rio de Janeiro pamoja na wakala wake Roberto De Assis na makamu wa rais wa Milan, Adriano Galliani.

Galliani alithibisha kwamba pande hizo mbili zimekubaliana kuvunja mkataba huo.

"Viongozi wa Milan wamekubakuli ombi la Ronaldinho, lakini bado hatujavunja mawasiliano yetu na mchezaji huyu.

"Tumehamua kumsaidia kurudi hapa na kucheza Brazil, japokuwa uamuzi huu umekuwa ni pigo kubwa kwa rais Milan, Silvio Berlusconi. Sitoondoka Brazil hadi atapokuwa amepata timu nyingine ya kuchezea."

Kilichobaki sasa ni kusubili ni timu gani anayotaka kuchezea kati ya hizo zinazotajwa, alisema De Assis, "Nimezungumza na Gremio, Palmeiras, Flamengo na Corinthians, lakini ilikuwa vigumu kuishawishi Milan kumwachia moja kwa moja.
 
Vyama vya soka Ileje, Chunya vyakaliwa ‘kooni'
Imeandikwa na Joachim Nyambo, Mbeya; Tarehe: 7th January 2011 @ 23:30 Imesomwa na watu: 26; Jumla ya maoni: 0






CHAMA cha soka mkoa wa Mbeya (MREFA) kimeviandikia barua vyama vya soka katika wilaya za Chunya na Ileje kuvitaka vitoe maelezo ya kina juu ya sababu za kushindwa kuendesha ligi ya taifa ngazi za wilaya katika misimu miwili.

Akizungumza na gazeti hili makamu Mwenyekiti wa MREFA, John Mwamwaja alisema kuvilima barua vyama hivyo kulitokana na uamuzi wa kikao cha kamati ya utendaji kilichokaa hivi karibuni na kuazimia kutaka maelezo ya kina kwa vyama hivyo.

Mwamwaja alisema ni jambo la kusikitisha kwa viongozi wa vyama hivyo kushindwa kuendesha ligi hiyo kwa misimu miwili mfululizo, huku kukiwa hakuna sababu ya msingi iliyotolewa na viongozi hao.

Alisema kutoendeshwa kwa ligi hiyo kunadhoofisha kiwango cha soka katika ngazi za wilaya na mkoa kwa ujumla kwa kuwa vipaji vya soka vilivyopo kwenye wilaya hizo haviwezi kuvumbuliwa.

"Tunaendelea kudidimiza soka la mkoa kwa kuwa hatutimizi mikakati ya kuvivumbua vipaji.
Hatuendeshi ligi muhimu kama hii tena kwa misimu miwili mfululizo. Sasa wapi tutapata timu ya mkoa iliyosheheni wachezaji walio na vipaji?" alihoji Mwamwaja.

Hata hivyo, Mwamwaja alisema katika kikao hicho cha kamati tendaji baadhi ya wajumbe wanaotoka katika wilaya hizo walijaribu kujitetea kwa kutoa sababu kama kuhama kwa viongozi walio wengi kwa wilaya ya Ileje huku wilayani Chunya wakitaja jiografia mbaya ya wilaya kuwa kikwazo.

Alisema wajumbe walizitupilia mbali sababu hizo na kuwataka wajumbe hao kurejea katika
wilaya zao huku wakijipanga kujibu barua watakayotumiwa kutoka MREFA ambapo barua hizo licha ya kujibiwa kiofisi pia viongozi hao watapaswa kutoa majibu hayo kwa viongozi wa chama cha soka mkoa watakaofanya ziara kwenye wilaya hizo.

Ahadi ya viongozi wa MREFA kuvitembelea vyama vya soka katika kila wilaya kuhamasisha ushiriki wa timu katika ligi ya taifa ngazi ya wilaya si ya kwanza, mwaka jana kabla ya kuanza kwa ligi hiyo viongozi hao kupitia kwa Katibu Lawrence Mwakitalu walitoa ahadi kama hiyo lakini haikutekelezwa.
 
Waliojitokeza kumsaidi Mtagwa tunawapongeza
Friday, 07 January 2011 19:37

afyamtagwa.jpg
UONGOZI wa Chama cha Wachezaji wa Soka Tanzania (Sputanza) wanatarajia kumpeleka nahodha wa zamani wa Taifa Stars, Jellah Mtagwa mkoani Iringa kwa ajili ya kupatiwa matitabu ya ugonjwa wa Kiharusi unaomsumbua tangu mwaka 2006.

Hatua hiyo imechukuliwa siku chache baada ya gazeti hili kuandika habari kuhusu matatizo ya kiafya yanayomkabili kiungo huyo wa zamani wa Stars kiasi cha kumsababishia kushindwa kumudu gharama za matibabu ikiwa ni pamoja na kujikimu kimaisha na familia yake.

Baada ya gazeti hili kuandika habari za Mtagwa, alitokea msamaria mmoja ambaye amejitolea kumchukua mchezaji huyo wa zamani kwa ajili ya kwenda kupata matibabu mkoani humo, pia wapo waliojitokeza kumsaidia kwa kutoa fedha.

Kitendo cha wadau mbalimbali kujitokeza kumsaidia mchezaji huyu ni kitendo cha kizalendo na kinapaswa kuungwa mkono na wanamichezo wote nchini kutokana na mfumo wa michezo ulivyo nchini unaosababisha wachezaji wengi kuishi maisha magumu wakishastaafu katika michezo mbalimbali.

Tunaamini utamaduni wa kuchangia matibabu kwa wanamichezo wetu ndio tija kwa maendeleo ya taifa na michezo kuliko ule wa kusubili msiba ndipo tunajitokeza kugharamia gharama za mazishi.

Sasa wakati umefika kwa Sputanza kwa kushirikiana na TFF, klabu kuandaa utaratibu wa kukusanya fedha kwa ajili ya kuwasaidia wachezaji wakongwe nchini na kuhakikisha unakuwepo mfumo wa kuwasaidia wachezaji wanapostaafu.

Vyama hivi kwa kushirikiana na klabu kwa kuanzia vinaweza kuandaa mechi za kirafiki hapa jijini Dar es Salaam na mikoani na fedha za viingilio zikatumika kwa ajili ya kugharamia matibabu ya wachezaji.

 
ZFA chagueni viongozi makini
Friday, 07 January 2011 19:35

KAMATI ya Rufaa ya Chama cha Soka Zanzibar (ZFA) juzi ilifuta matokeo ya uchaguzi mkuu yaliyompa ushindi Ali Ferej Tamim na kumpa nafasi ya kuendelea kuwa rais wa ZFA .

Baada ya Tamim kutangazwa mshindi mpinzani wake Sulemain Mahmoud Jabir alikata rufaa kwenye kamati ya uchaguzi wa ZFA iliyokuwa chini ya mwenyekiti wake Ally Suleiman Shehata na katibu wake Mustapha Omary ambaye pia ni msajili wa vyama vya michezo visiwani Zanzibar.

Kamati hiyo baada ya kupitia rufaa hiyo ilibaini kwamba Tamim hana sifa za elimu kwa vile ameshindwa kuthibitisha kwa kupeleka vyeti vyake vya kidato cha nne kama kanuni za uchaguzi zilivyosema.

Tunaipongeza kamati hii kwa kujaribu kutafuta haki kwa kufuta matokeo hayo ya uchaguzi pamoja na kuitisha uchaguzi wa haraka katika kipindi cha wiki mbili ili kupata viongozi wenye sifa wa kuendeleza soka visiwani humo.

Tunaamini ili mchezo wa soka uendelee tunahitaji viongozi makini wenye sifa Stahiki za kuwania nafasi hizo, kwa kuwa kuchagua viongozi wasiokuwa na sifa kunarudisha sana michezo nchini.

Pamoja na uamuzi huu wa kishujaa, lakini tunaamini bado wahusika waliofanya uzembe wa makusudi wa kukubali kumpitisha mgombea ambaye hana sifa wanapaswa kuchukuliwa hatua kali.

Kwani tunafahamu kufanya uchaguzi wa aina yoyote ni gharama kwa kuanzia vifaa vya kupigia kura hadi kulipa posho za wajumbe, gharama za usafiri kwa sababu uchaguzi ulifanyikia Pemba na kupoteza muda, ni wazi kwamba watu hawa hakuwa na nia njema na soka ya visiwa hivyo.

Ni bora wahusika waliofanya uzembe wa makusudi wa kukubali kumpitisha mgombea ambaye hana sifa wenyewe wakajiuzulu kwa lengo la kulinda heshima ya ZFA na soka ya visiwa hivyo ambayo imekuwa ikidorora kila kukicha kutokana na kukosa viongozi makini.


 
Ligi ya kikapu yaanza bila mdhamini
Imeandikwa na Evance Ng'ingo; Tarehe: 7th January 2011 @ 23:10 Imesomwa na watu: 19; Jumla ya maoni: 0





Alisema kuwa suala la udhamini lilichelewesha kuanza kwa ligi hiyo ambapo alifafanua kuwa milango ipo wazi kwa kampuni itakayotaka kudhamini.

Alisema kuwa ligi hiyo ni muhimu kwa kuwa inapelekea kupatikana kwa timu itakayoshiriki michuano mbalimbali kama vile michuano ya majiji makuu pamoja na Ligi ya Muungano.

Pia ligi hiyo ndio inapelekea kuchaguliwa kwa timu ya Mkoa kwa wanawake na wanaume itakayoshiriki michuano mbalimbali.

"Ikiwa kesho (leo) ndio ligi inaanza lakini mpaka sasa mambo ni bila bila yaani hakuna mdhamini hata mmoja hivyo tunaendesha mambo kimapenzi yetu tu kwa huu mchezo," alisema Mwamboma.
 
Spurs complete Khumalo swoop


RivalsDM



PRINT RSS

6 comments »

Updated Jan 7, 2011 11:04 AM ET
Tottenham have completed the transfer of Bongani Khumalo from South African side Supersport United on a four-and-a-half year deal.
TRANSFER SPECIAL

Keep up with all the biggest moves around the globe with our 2011 January transfer gallery.

Khumalo impressed during a trial at Spurs last July and the north London club have chosen to take the 24-year-old on a permanent transfer for a fee of around £1.5million.
The centre half, who was born in Swaziland, impressed for South Africa during the World Cup where he scored the opener in the hosts' 2-1 group stage win over France.
Spurs boss Harry Redknapp already has a number of options in defence but there are still doubts over the long-term fitness of centre backs Ledley King and Jonathan Woodgate.
Khumalo could make his debut in Tottenham's FA Cup third round clash with Charlton at White Hart Lane on Sunday.
 
Carroll injured in six-hour, 30 Jagerbomb bender - Exclusive

Published 23:00 07/01/11 By Jeremy Armstrong

.jpeg



England soccer star Andy Carroll was left in agony after a drunken fall from a casino bar stool at 5am, it was claimed yesterday.
Carroll, 22, had just ordered 30 "Jagerbombs" – a potent mix of spirit Jagermeister and Red Bull energy drink – for himself and 15 pals.
Next day the £20million striker's club, Newcastle United, announced that a thigh injury would rule him out of at least three games.
The Geordie – who picked up an injury in United's match against Spurs on December 28 – was on a six-hour bender until 6.30am on December 30 at Aspers Casino in Newcastle.
p-e4m3Yko6bFYVc.gif
fp.gif


As well as FOUR Jagerbombs, 6ft 4in Carroll downed TWO pints of Fosters and around SIX bottles of Peroni.
Witnesses saw him slump down with his head in his hands after the Jagerbombs and one Peroni. Then all of a sudden he perked up, alert, "like a meerkat".
He stood up on the leg rest of the stool which tipped over. He then smashed against the floor of the bar area and was clutching his leg, shouting out in pain.
But his mates stood around laughing as Carroll lay in agony.
Shortly afterwards his female companion was seen massaging his leg at the roulette table – where he fell off another stool.
Then he limped off to a private function room, where he downed five more Peronis and sang on the karaoke machine before finally leaving alone at 6.30am. The following day, United boss Alan Pardew told journalists about an injury.
Carroll apparently reported his injury after the Spurs game. But it was decided not to make that injury public until it had been properly assessed.
That assessment was done on December 29, before Carroll went to the casino. The club doctor has examined Carroll regularly since then and a source close to the player said the doctor would dispute the injury being made worse. But gambler Simon Cook, 28, who witnessed the second fall in Aspers, said: "I could not believe his behaviour. He was absolutely hammered.
"When I went back to work my mates were telling me how he was going to sit out three games because of an injury. I couldn't believe it. I knew how it really happened."
Carroll, who has just signed a new, £27,000-a-week, five-year contract, has been a regular at Aspers this season.
Carroll was with United captain Kevin Nolan at Aspers after the Toon's 5-1 win over Sunderland in November.
He went on another huge bender on December 7 – the day after manager Chris Hughton was sacked.
Carroll is currently on a "mid season" break in Dubai and due back this week. He will take a fitness test on Thursday to see if he will be fit for next weekend's match against Sunderland.
Newcastle United declined to comment on the incident last night.


 
World champ David Haye backs Millwall for FA Cup KO

Published 23:00 07/01/11 By James Nursey

David+Haye.jpeg



Birmingham will hand starlet Jordan Mutch a chance to ignite his City career today at the New Den.
The England Under-19 midfielder has returned to St Andrews after a successful loan spell at Watford where he scored five goals in 23 games.
With Lee Bowyer suspended for three matches, Mutch is now set to make his full debut in the FA Cup this weekend. Mutch, 19, is out of contract this summer and hopes to earn a new deal at Brum.
His only previous City run out was as substitute at *Southampton in the League Cup in August 2008.

Mutch's form at Watford prompted the Republic of Ireland to try and recruit him but the star is ineligible.
World boxing champion David Haye has backed his Lions to knock out the Blues today. The WBA heavyweight king said: "I'm backing Milwall to win and lift the FA Cup this year. We got to the final in 2004 so why not again?
"I'm not taking any defeatist talk from the guys so I haven't asked them who they think will win the Cup. I just wanted to know who they're going to beat in the final."
Kenny Jackett's side are ninth in the Championship after a run of eight games without defeat in which they have conceded just twice.



 
Wenger moans a lot and sees nothing and Mourinho's a cheat - Ken Bates

Published 23:00 07/01/11 By Oliver Holt

Football-PremierLeague10-1.jpg



Ken Bates is back. Nearly.
So, the Leeds United chairman is sitting in a London restaurant, warming up. His club is on the verge of the big time again. They are pressing for a return to the Premier League and face Arsenal in a high-profile FA Cup tie today.
His voice will be heard loud and clear again soon enough so Bates is going through his repertoire, taking aim and shooting from the lip.
"I have never been a great fan of Arsene Wenger," he says. "He moans a lot and never sees anything. Having regard to those physical disabilities, though, he's a great manager."
So does he think the people who criticise Wenger for his lack of trophies and his financial prudence are right?
"Which people are they?" Bates says.
Jose Mourinho is mentioned.
"Mourinho's a cheat," Bates says. "Can you remember the laundry basket to overcome the (Uefa touchline) ban?"
He forces himself to be circumspect about his old club, Chelsea, and the way it has been run by Roman Abramovich.
"Their values are not my values," he says, "their methods aren't my methods, their attitudes aren't my attitudes. Maybe it's a different culture between east and west."
He's into his stride now, relishing the chat. The circumspection starts to fade.
He mentions how Peter Kenyon and Juan Sebastian Veron both arrived at Chelsea from Manchester United in quick succession.
"I told Eugene Tenenbaum (Abramovich's aide) that Manchester United must be laughing their bollocks off.
"He asked why and I said United had just sent them two lemons in the space of three weeks."
Nor can Bates resist the chance to offer the billionaire Chelsea owner, who favours casual attire, some sartorial advice.
"Mr Abramovich will be very welcome in the chairman's suite at Elland Road if we are in the Premier League next season," he says, "providing he's wearing a tie.
"What I'm looking forward to most about playing Chelsea again is when all my lifelong friends, who I haven't heard from for seven years, are ringing up asking for tickets.
"That will be my greatest enjoyment. We will relish being back in the Premier League when it happens."
Bates, 79, goes back to Wenger and says that, actually, he is a fan of the way Arsenal is run - the way they build, rather than buy, buy, buy in a splurge.
That gives him a neat opportunity to have a pop at his old adversary, David Dein, the former Arsenal vice-chairman.
"The only good thing David Dein did in his life was appointing Wenger," he says.
The foreign managers who have taken charge of the England team get it, too.
"Eriksson was a disaster and Capello's a nice guy but he's also been a disaster," Bates says.
Bates loves the rough and tumble of these conversations, the chance to offer forthright opinions, the refusal to dissemble or be diplomatic.
But none of it can hide the fact that he is at his most passionate not when he is criticising a foe but when he is talking about the love of his club.
He was like that at Chelsea, fighting tirelessly to safeguard its future, building it up and up, facing down everyone who tried to thwart him.
And he has been the same at Leeds, overcoming initial cynicism about his involvement and hauling the club up from rock bottom to a place where it can stare the rest of football in the eye again.
He loves Leeds. Not just the club. The city, too.
In the six years since he took over at Elland Road, he has taken to Yorkshire and, gradually, Yorkshire has taken to him.
"Leeds is a very different culture to Chelsea," he says. "My wife Susannah did say if we ever come back to England, she'd rather live in Leeds than London. I would agree with her.
"London is not the London I knew, whereas Leeds and Yorkshire is still the England I knew. Different values, proper place, local pride, whereas London is now so cosmopolitan. Leeds gives me a feeling of belonging.
"Simon Grayson, our manager, is a great manager. He's good for Leeds, because he's a Yorkshireman, which is very important.
"He started as a player at Leeds, went round the houses and now he's back in his spiritual home.
"That's a great advantage because Yorkshire people like Yorkshire people. It's a very nationalist county. They are his people.
"He knows how to deal with me, with them, and with the players. He struggled at first with me. Now he understands.
"Leeds United are being run on a proper, business-like basis. At the end of November we had made £483,000, we had a great December and, thanking God, we are going to have a great January, cash-wise anyway.
"We have no debts and we pay our bills before they are due. If you go through the 92 clubs in the Premier League and Football League, can you name me another one?
"Can we keep balancing our books if we go up to the Premier League? Of course we can."
At this stage of the FA Cup last season, of course, Leeds beat Manchester United at Old Trafford.
Before he leaves the restaurant, we ask Bates if the club misses the man who scored the winning goal that day, Jermaine Beckford, now that he has moved to Everton.
"Who?" Bates says.


 
Spurs' infamous Lasagna poisoning was exaggerated - reveals former starlet

Published 23:00 07/01/11 By Neil McLeman

Football-Divisions1-2-39-1.jpg



Johnnie Jackson will return to Tottenham tomorrow for the first time since the infamous Lasagna-gate game at Upton Park in 2006.
Jackson, now 28, made 20 appearances in seven years after coming through the youth ranks at White Hart Lane.
And he is desperate to add to his remarkable tally of 13 goals from midfield for Charlton this season.
But Jackson, who came through the Spurs ranks in the year below Ledley King and Peter Crouch, had a strange farewell to the North London club nearly five years ago.

"This is a perfect draw for me - I haven't been back there since I left," said Jackson, who scored his only Spurs goal against Charlton.
"The last time I was involved I got a call at 7am from Chris Hughton saying a few of the lads had gone down ill and I had to get myself to the ground quick and there would be a car to take me to Upton Park.
"It turned out I wasn't actually a sub but a few of the boys who had been called ended up on the bench.
"I think it was exaggerated a bit to be honest. The only one who I remember actually played the game who was struggling was Michael Carrick - I think he had to come off in the end.
"But they ended up losing it and missing out on the fourth and I think they made more of a deal of it than it actually was. There were some great stories going about like the chef was an Arsenal fan. I am not so sure about that."
He added: "I loved my time there but and I always felt eventually some big name would come in to take my spot. I am not bitter about that - the club was going forward and has continued to do so. They are genuine title contenders and will probably end up winning the cup with the year ending in one!"
After spells at Colchester and Notts County, Jackson joined Charlton on loan in February last year before signing in July. And since being pushed further forward to left midfield, he cannot stop scoring with 10 in his last 11 games, including two in the last round against Luton. Tomorrow he will look to continue that streak under new caretaker manager Keith Peacock.
"I am playing probably as well as I ever have at the moment and I have scored more this season than I ever have before," Jackson said.
"I am doing nothing different - everything is falling for me at the moment. Luck seems to be on my side. I will take a little deflection or tap-in or anything back at the Lane tomorrow."
 
Tutasahihisha makosa-Poulsen
Imeandikwa na Amir Mhando, Cairo; Tarehe: 6th January 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 485; Jumla ya maoni: 0







Tanzania ‘Taifa Stars', juzi ilikubali kipigo cha mabao 5-1 kutoka kwa Misri ‘Mafarao' katika mchezo wa Kundi A katika michuano ya nchi za Bonde la Mto Nile uliofanyika Uwanja wa Arab Contractors mjini hapa.

Bao la kwanza lilifungwa na Said Khamdi dakika ya nne, kisha dakika kumi baadaye Mohammed Aboutrika alifunga la pili kabla ya beki Nadir Haroub ‘Cannavaro' kujifunga dakika tisa baadaye.

Said Khamdi alipachika bao la nne dakika ya 57 na la tano lilifungwa na Ahmed Ally dakika ya 74, huku lile la Stars likifungwa na Rashid Gumbo dakika ya 77, ambaye aliingia kipindi cha pili akitokea benchi.

Kesho Stars itacheza na Burundi ambayo nayo juzi ilifungwa mabao 3-1 na Uganda, hivyo ili Stars iweke hai matumaini ya kufuzu nusu fainali italazimika kushinda na kusubiri mchezo wa mwisho dhidi ya Uganda.

Akizungumza baada ya mchezo huo, Poulsen alisema kipigo kimemchanganya lakini wamejifunza na watasahihisha makosa yao huku akisisitiza wamefungwa na timu bora Afrika.

Alisema Misri ipo katika 20 bora kwenye viwango vya Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) wakati Tanzania ni ya 116 hivyo kuna tofauti kubwa baina ya timu hizo.

"Misri ni timu nzuri Afrika na dunia kwa jumla, imecheza vizuri,ni mabingwa mara tatu mfululizo Afrika, lakini pia vijana wangu walipambana vilivyo ila walikutana na timu bora, naamini michezo ijayo tutaimarika, tumepata changamoto kubwa," alisema Poulsen.

Kocha huyo alieleza kuwa makosa machache waliyoyafanya wachezaji wake yalitumiwa vizuri na wapinzani wao kufunga na hiyo ilitokana na kucheza bila kuelewana dakika 20 za mwanzo.

"Watanzania tumejifunza mengi kwa mechi ya leo (juzi), faida yake itaonekana mechi zijazo," alisema Poulsen.

Alisema atatumia jana na leo kufanyia kazi dosari zilizojitokeza katika mchezo huo ili kuimarisha kikosi chake kabla ya kuivaa Burundi kesho na kisha Uganda Jumanne.

Naye Kocha Mkuu wa Misri, Hassan Shehata akizungumza baada ya mchezo huo aliisifu Stars kwamba ni timu nzuri, lakini inahitaji marekebisho kidogo na itatisha kwani ina wachezaji wengi chipukizi ambao watacheza kwa muda mrefu.

Alisema mpira ambao Stars ilicheza kipindi cha pili, kama ingecheza hivyo kipindi cha kwanza mchezo ungekuwa mgumu kwao na kusisitiza kuwa timu yake licha ya kupata ushindi mnono, lakini ilikabiliana na upinzani mkubwa.

Akizungumzia kipigo hicho, kipa Juma Kaseja alisema mchezo ulikuwa mgumu na makosa waliyoyafanya wenzao waliyatumia.

"Tuache utani Wamisri wapo vizuri, hata krosi zao wanazopiga si za mchezo, wanapiga mabomba, kwa kifupi wapo juu, lakini kama tunakutana nao mchezo mwingine tutawatuliza," alisema Kaseja ambaye mwezi uliopita aliibuka kipa bora wa michuano ya Chalenji.

Naye nahodha wa Misri, Wael Goma alisema michuano hiyo ya soka kwa nchi za Bonde la Mto Nile ni migumu na kwamba Tanzania si timu ya kubezwa, kwani ina wachezaji wenye miili midogo, lakini wana vipaji.

Michuano hiyo inashirikisha timu saba zilizogawanywa katika makundi mawili, ambapo timu mbili za juu kila kundi zitacheza nusu fainali, wakati timu zitakazoshika nafasi ya tatu kila kundi zitacheza kuwania mshindi wa tano. Bingwa wa michuano hiyo atazawadiwa zaidi ya Sh milioni 200 za Tanzania.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom