Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Italian Serie A Roundup, Jan. 9






PRINT
RSS


19 comments »

Updated Jan 9, 2011 2:53 PM ET
Zlatan Ibrahimovic scored an injury-time equalizer for Serie A leader AC Milan to draw 4-4 with Udinese in a wild match at the San Siro on Sunday.
Milan fell behind 3-1 following two goals from Udinese's Antonio Di Natale, who raised his league-leading total to 13, but an own goal from Mehdi Benatia and Alexandre Pato's second goal in the 82nd minute drew Milan level at 3-3.
Argentine forward German Denis put Udinese back in front in the 84th, and Ibrahimovic equalized in the third minute of added time after collecting a pass inside the area from Antonio Cassano, who has now set up two goals in his first two matches with Milan.


"We're not taking advantage of the chances to pull away," said Milan midfielder Gennaro Gattuso. "We've got to do more. If Inter wins the two games it has to make up they'll be back within five points, and that's what worries me."
Five-time defending champion Inter Milan also struggled before winning 2-1 at Catania.
Alejandro Gomez gave the Sicilian club the lead in the 71st before Esteban Cambiasso hit back in the 75th and 79th minutes to hand new Inter coach Leonardo his second consecutive win since replacing Rafa Benitez.
On a day in which all of the top teams looked in trouble at some point, Lazio lost 2-1 at home to Lecce and Brazil defender Juan made two costly errors as Sampdoria rallied to beat 10-man AS Roma 2-1.
Lazio goalkeeper Fernando Muslera scored an own goal in the 39th, Stefano Mauri equalized for the hosts in the 47th but Carlos Grossmuller put Lecce back ahead in the 72nd.
Milan led with 40 points, six in front of Lazio. Napoli is next with 33 points, Roma has 32 and Juventus and Palermo 31 each.
Inter, which has two games to make up, is seventh with 29 points.


"We made some mistakes, but it was another show of character on everyone's part," said Leonardo. "These two games give us security and enthusiasm moving forward. ... It's difficult to read the standings now. We've just got to keep moving forward on our own road little by little, game by game, like today."
Napoli was set to host Juventus later.
Also, it was: Bari 0, Bologna 2; Cesena 0, Genoa 0; Chievo Verona 0, Palermo 0; Fiorentina 3, Brescia 2; and Parma 1, Cagliari 2.
In the new lunchtime fixture, Mirko Vucinic put Roma ahead in the 18th after taking advantage of a stagnant defense. But in the 55th, Juan gifted the ball to Angelo Palombo and Roma goalkeeper Julio Sergio tripped the Sampdoria captain, receiving a red card and giving away a penalty that was converted by Nicola Pozzi.
Stefano Guberti then scored the winner in the 83rd when Juan was unable to clear.
"They were two errors, but two errors from a great champion and that can happen over the course of a career," said Roma coach Claudio Ranieri.
Sampdoria ended the match with nine men after Stefano Lucchini and Daniele Guastaldello picked up their second yellow cards in the final five minutes.
Having joined on a six-month loan from Manchester United, Federico Macheda made his Sampdoria debut in the final 13 minutes and wasted an excellent scoring chance by heading wide a minute before Guberti's winner.
 
Inter comeback cheers Leonardo


RivalsDM



PRINT
RSS


0 comments »

Updated Jan 9, 2011 2:52 PM ET
Inter Milan coach Leonardo showered his players with praise after they came from behind to beat Catania on Sunday afternoon.
Trailing 1-0 with 19 minutes remaining, Esteban Cambiasso's two goals fired Inter to a 2-1 success in Sicily.


Leonardo said: "There has been a great display of character and determination from all of my players. This is a fantastic comeback."
The result allowed Inter to close the gap on Serie A leaders AC Milan to 11 points after their city rivals were held to a 4-4 draw by Udinese on Sunday.
Inter have two games in hand and Leonardo is convinced his team will catch the Rossoneri in the standings.
He said: "I believe the idea of being among the teams that are battling for the scudetto has always been present.
"The race is a long one and we are in it. We will continue on this path.
"There is the right spirit in the team. "My players know how to battle and sacrifice themselves to get the win."
 
Italian Football Results






PRINT
RSS




Updated Jan 9, 2011 4:42 PM ET
ROME (AP)

Results in the Serie A, the Italian first-division football league (home teams listed first):
Sunday's GamesSampdoria 2, AS Roma 1
Bari 0, Bologna 2
Catania 1, Inter Milan 2
Cesena 0, Genoa 0
Chievo Verona 0, Palermo 0
Fiorentina 3, Brescia 2
Lazio 1, Lecce 2
AC Milan 4, Udinese 4
Parma 1, Cagliari 2
Napoli 3, Juventus 0
Saturday, Jan. 15:Napoli vs. Fiorentina
Inter Milan vs. Bologna
Sunday, Jan. 16:Cagliari vs. Palermo
Brescia vs. Parma
Catania vs. Chievo Verona
Cesena vs. AS Roma
Genoa vs. Udinese
Juventus vs. Bari
Lazio vs. Sampdoria
Lecce vs. AC Milan
 

U-20 iwe chachu kuwekeza soka la vijana Tanzania


MASHINDANO ya vijana chini ya miaka 20, ‘Uhai Cup' yanafikia tamati leo kwa timu za JKT Ruvu na wenzao wa Ruvu Shooting kuvaana, katika mchezo wa fainali, utakaopigwa katika Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam ulio katika ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
JKT Ruvu waliingia hatua hiyo baada ya kuitandika Polisi Tanzania bao 1-0 na ndugu zao Ruvu Shooting wakiwaondosha katika mashindano AFC ya Arusha baada ya kuwafunga mabao 2-0.
Fainali ya leo ni ya tatu tangu kuanzishwa kwa mashindano hayo yenye lengo la kusaka vipaji vya soka ambavyo ni msingi wa maendeleo stahili ya soka letu la kesho.
Fainali ya leo inatarajiwa kuwa na ushindani wa hali juu kutokana na kiwango cha timu zote mbili ambacho zilikuwa zikikionyesha tangu mwanzo wa mashindano kiasi cha kufikia hatua hiyo, huku mabingwa watetezi wa kombe hilo Azam FC na timu za Simba na Yanga wakiaga mapema.
Mashindano hayo ambayo yalianza Desemba 27 mwaka jana yanafanyika kwa mara ya tatu, yakiwa yanashirikisha timu za vikosi vya pili kwa timu za Ligi Kuu Tanzania Bara, kwa lengo la kusaka vipaji.
Tayari mashindano hayo yameshuhudiwa yakiibua vipaji vya wachezaji mbalimbali ambao baadhi yao wameanza kuwika na timu kubwa ikiwemo timu ya taifa ‘Taifa Stars' ambao ni Thomas Ulimwengu, Himid Mao, Kabali Faraji, Abuu Ubwa na wengineo.
Sisi Tanzania Daima kwa kuzingatia umuhimu wa kuimarisha msingi wa soka ambao ni vijana, tunatoa wito kwa wadau na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kulitilia mkazo kwa kuendeleza zaidi soka la vijana hasa ukizingatia vijana hao ndio hazina ya kesho.
Soka la vijana ndio dira ya soka sehemu yoyote, na kwa kuzingatia Tanzania hatuna msingi imara katika hilo, tunashauri ligi hii ya U-20 iwe chachu katika kubuni nyingine ya U-17 na hata U-10.
Kiukweli bila soka la vijana tutakuwa tukitwanga maji kwenye kinu, jambo ambalo linatakiwa lifanyiwe kazi na wadau wa soka Tanzania na si TFF pekee yake.
TFF waongeze kasi ya kusaka wadau zaidi, ili mashindano hayo yawe chachu ya kupatikana vijana ambao watasaidia timu za Ligi Kuu Tanzania Bara.
Wito zaidi kwa mashirika na wadau wengine wenye mapenzi na soka letu, kuonyesha kujali vipaji vya Tanzania kwa kuongeza nguvu pale walipoanzisha Uhai ili kufanikisha dhamira halisi ya kuleta mapinduzi ya maendeleo ya soka.
Tujifunze kwa wenzetu ambao wameendelea katika soka, iko wazi waliwekeza kwenye soka la vijana muda mrefu na sasa wanakula matunda kila kukicha.
Ingawa tulipata mwangaza kutoka kwa aliyekuwa kocha Mkuu wa Stars, Mbrazil Marcio Maximo, ambaye mara alipowasili alianzisha na kukazania programu ya vijana, ikiwamo kuwachukua katika kikosi chake mara kwa mara ili kupata uzoefu na baadhi ya vipaji vichache vinaonekana sasa.
Wito kwa wadau na TFF, Uhai Cup ya mwaka huu iwe chachu katika kuwekeza katika soka la vijana kwa manufaa ya kesho.
 
Wachezaji na wasanii shule ni muhimu kwenu

Zainab Mlimbila

KADIRI siku zinavyozidi kwenda na teknolojia pia inakua; hii inahitaji watu pia kuyamudu mazingira haya ya sayansi na teknolojia.
Nchi zinazoendelea hapa duniani huenda sambamba na kukua kwa sayansi na teknolojia ambayo ndiyo inayofanya dunia kuwa kijiji.
Kukua huku kwa sayansi na teknolojia hapa Tanzania kumeleta mambo hasi na chanya kwa wananchi ambapo kwa watu wenye uelewa finyu huyafanya mambo kuwa hasi.
Katika mtazamo wangu wa leo ningependa kuzungumzia wachezaji wa mpira wa miguu na wasanii wa fani mbalimbali ambao wamekwishapata majina lakini sasa shule wameamua kuipa kisogo kwa maana ya kujiendeleza kitaaluma na kujikita zaidi katika kucheza mpira na kuigiza.
Pengine nianzie na baadhi ya wachezaji wa soka ambao wameshapata majina kupitia timu mbalimbali za Ligi Kuu ambao wanakipiga wakiwa wametwaliwa katika shule za michezo (sports academies) ambazo zilikuwa zikiwapa elimu ya soka na taaluma nyingine kwa lengo la kuwa na fani nyingi ili kukabiliana na tatizo la ajira nchini.
Hoja yangu ni kuwa wachezaji hao baada ya kupata majina wamejisahau kujiendeleza kielimu na badala yake wamekalia kucheza soka lakini wakisahau mpira una kupanda na kushuka jambo linaloweza kuwagharimu baadaye kama ilivyowahi kutokea kwa baadhi ya wachezaji.
Nayasema haya nikiwa nimeshuhudia wachezaji hao wakiwa katika hali ngumu za maisha huku namna ya kujiendeleza kielimu ikiwa imefikia ukomo kwa maana ya uwezo wa kujilipia karo huku timu walizokuwa wakizichezea zikiwa zimewaacha na kosa jingine kubwa ambalo hulifanya ni kujisahau kuweka akiba wakiamini nyota yao itaendelea kung’ara milele.
Siyo kwamba wachezaji wote hawana elimu lakini ni wengi wao ambao wana kiwango cha chini cha elimu na wamekuwa wakipata nafasi ya kucheza mpira kutokana na vipaji vyao lakini baada ya kiwango kushuka hujikuta wakitaabika na kuwa ombaomba wakiwa wametelekezwa na klabu zao.
Kwa mtazamo wangu ni wakati wa wachezaji wa Tanzania iwe wametoka katika shule za michezo au hawakupitia huko kucheza soka huku wakijipambanua na elimu ili kukabiliana na mizengwe ya soka ya Tanzania ambapo wachezaji kuachwa ni suala la kulala na kuamka.
Wachezaji hao hawapaswi kujisahau na kujikita katika soka zaidi badala yake watambue bado wanatakiwa kujipa nafasi ya kusoma ikiwezekana pale wanaposaini mikataba yao na klabu husika kuweka kipengele cha kupata fursa ya kusoma ili kujitengenezea mazingira ya baadaye hata baada ya kustaafu soka.
Lakini hali hii haiwagusi wachezaji peke yake hata wasanii wa fani mbalimbali ikiwemo ya uigizaji ambayo imekuwa na mashiko kwa jamii katika miaka ya hivi karibuni kujisahau kwao na kulewa na ustaaa waliokwishaupata badala ya kusoma.
Nasema hivi kwa sababu kuna baadhi ya wasanii iwe wa muziki au filamu baada ya kupata majina kupitia kazi zao za sanaa wameamua kuikacha shule na kujikita katika usanii zaidi.
Lakini leo hii kuna hao walioitosa shule na kuona haina umuhimu wamepotea kabisa kwenye ulimwengu wa sanaa na kukosa vyote kwa wakati mmoja.
Ni muhimu kwa wasanii wetu kujifunza kutoka kwa wasanii wa ughaibuni na siyo kuishia kuiga mambo ya laana tu na kuacha vitu vya muhimu ambavyo wasanii wa majuu wanavifanya, hususan katika masuala ya elimu.
Nina uhakika kuna baadhi ya wasanii wa Kibongo wanakosa mikataba yenye fedha kutoka nchi za mbali kutokana na kutokuwa na elimu ya kutosha katika masuala ya sanaa.
Binafsi nimefurahishwa sana na hatua ya meneja wa TipTop connection Babu Tale kuamua kumpeleka Dogo Janja shule, kwa kumlipia gharama zote za shule na mahitaji mengine.
Ni mameneja wachache sana ambao huamua kuwapeleka wasanii wao shule, hii imekaa vizuri sana kwa upande wa babu Tale na ni funzo kwa mameneja wengine.
Dunia ya sasa lazima ikimbizane na watu wenye elimu ili kuweza kuyakabili mazingira ni aibu kwa wasanii kukacha shule.
Nasisitiza hili kwa sababu taifa limekuwa likikosa vitu muhimu kama tuzo au makombe kutoka kwa wasanii ambao wanakuwa wameshiriki mambo mbalimbali katika nchi za wenzetu.
Kinachowafanya wasanii kushindwa kumudu ushindani ni kukosa elimu ya ile sanaa na wapo pia ambao hushindwa kutokana na lugha mbovu ya Kiingereza.
Kikubwa kinachowafanya wasanii kukacha elimu ni kulewa sifa ambazo ni za musimu tu, lakini wapo pia ambao wanastahili kupongezwa kutokana na juhudi zao za kujiendeleza kielimu iwe ni kwenye sanaa au mambo mengine.
Nasema hivi kwa sababu kuna wasanii kama Mr. Blue ambao walipopata majina makubwa wakalewa sifa na kuona shule haina umuhimu, ona sasa wako wapi? Wakiulizwa utasikia bado najipanga ndio majibu yao.
Najua kwa sasa atakuwa anajutia uamuzi wake wa kuitosa shule, kwani kwenye muziki havumi tena kwa sasa angekuwa na taaluma nyingine si angeitumia kujipatia kipato na kumrudishia heshima?
Tuache wivu na chuki, kiukweli Ally Kiba anastahili pongezi kwa kuipeperusha bendera ya Tanzania vyema kimataifa kutokana na wimbo wa ‘Hands Across the World’ uliotungwa na Robert Kelly au R Kelly.
Katika hili wasanii wanapaswa kujifunza na kuchukua hatua, najua wapo wenye viroho vya wivu lakini kimsingi wanatakiwa kuwa na wivu wa maendeleo na si vinginevyo.
Kwa mtazamo wangu nawaomba wachezaji na wasanii waweze kujiendeleza kielimu kwani inawanyima fursa ya kushiriki kwenye matamasha ya kimataifa na hivyo kujikosesha tuzo na heshima ambazo zingeweza kuitangaza Tanzania katika medani ya kimataifa.
 
Confusion over Beckham's proposed Tottenham loan






PRINT
RSS


0 comments »

Updated Jan 9, 2011 3:24 PM ET
LONDON (AP)

David Beckham will begin training with Tottenham on Monday and the club hopes a loan deal with the Los Angeles Galaxy can still be completed.
Beckham wanted to play for Spurs for two months during the Major League Soccer offseason, despite the Galaxy's reluctance to allow its star to risk another injury.
The former England captain injured his Achilles' tendon while at AC Milan last March and was out until September.
Tottenham manager Harry Redknapp said Sunday morning that a loan was not possible after it became ''all too complicated with the insurance issues'' and a statement stated that Beckham would instead only train with the club.
But Redknapp later backtracked by indicating that a deal could still be reached that would allow the midfielder to play in the Premier League for the first time since 2003, when he left Manchester United for Real Madrid.
''Hopefully it could still happen. The situation is ongoing,'' Redknapp said after Tottenham beat Charlton 3-0 in the FA Cup. ''I was led to believe that insurance was a problem, but apparently that's not the case.''
Beckham's announcement in December that he was seeking another loan to Europe took the Galaxy by surprise.
The team issued a statement through the AP within hours of Beckham's comments emerging in December saying that it expected him back in training more than a month before the March 15 season opener at the Seattle Sounders.
On Sunday, Redknapp reflected that by saying: ''They wanted him back in early February so that made it difficult to do a playing deal on the basis of three weeks.''
Even if Beckham doesn't play, Redknapp said the midfielder can still help his squad as it prepares for a Champions League knockout matchup with Beckham's former club AC Milan and continues its push for a second straight top-four finish in the Premier League.
''He will be a great influence around the place and I am sure we will all benefit from his winning mentality,'' Redknapp said. ''I think everyone will enjoy having him here. We'd love to have him here for longer but respect his commitments to LA Galaxy.''
In a statement, Beckham thanked the Galaxy for allowing him to train with Spurs.
''It's important that I maintain a high level of fitness during the MLS offseason,'' said Beckham, who also trained with Arsenal three years ago. ''I look forward to getting to work as soon as possible.''
The former Manchester United and Real Madrid player is still hopeful of being recalled to the England team by manager Fabio Capello, having made 115 appearances - the most by any non-goalie.
Beckham also announced Sunday that his wife, Victoria, is expecting their fourth child later this year.
 
Wajumbe uchaguzi ZFA, hadi juisi za mabungo!

Mwandishi wetu

NI Jumatatu nyingine tena tunakutana katika safu hii ya Uwanja wa Kuchonga iwajiayo kila siku kama ya leo, lengo likiwa ni kupeana changamoto za kispoti ili kuleta maendeleo katika sekta hii nyeti.
Bila shaka mu wazima wa afya na mnaendelea na majukumu ya kila siku ya ujenzi wa Taifa, ila kwa wale afya zao si shwari tunawaombea nafuu.
Leo uwanjani tunatiririka na soka la Zanzibar ambalo hivi sasa mustakabali wake unakwenda hali jojo baada ya uchaguzi wake mkuu uliofanyika Desemba 31 mwaka jana kutenguliwa kutokana na kutokufuata taratibu, ikiwamo kuchakachuliwa kwa kuingizwa wajumbe wasiokuwa na sifa.
Matokeo katika uchaguzi huo ambao ulikuwa ukitarajiwa kuleta mapinduzi makubwa ya uongozi hasa ukizingatia kinara wake, Rais wa chama hicho, Ali Ferej Tamim yuko madarakani zaidi ya miaka 15 huku hamasa ya soka visiwani humo ikizidi kufifia kila kukicha.
Zile hamasa za Small Simba, Malindi, Mlandege, Kikwajuni na nyinginezo sasa hivi zimebaki hadithi na hamasa zote za wapenda soka zimeamia ligi za Ulaya.
Lakini katika hali ambayo haikutarajiwa wajumbe wakamrejesha tena Ali Ferej Tamim kuwa Rais wa ZFA, kwa kupata kura 32 na kufuatiwa na Suleiman Mahmoud Jabir kura 20 na Munir Zakaria kura mbili kati ya 54 zilizopigwa na wajumbe wa mkutano mkuu.
Lakini siku chache baada ya kupatikana kwa washindi hao, Suleiman Mahmoud Jabir akakata rufaa kupinga matokeo hayo kwa madai ya ukiukwaji wa sheria, ikiwemo wajumbe kutoka kamati tano za Waamuzi, Wanawake, Central, kamati ya ufundi na watu wenye ulemavu hawakuwa wapiga kura halali kutokana na kutoteuliwa na kamati hizo na kuthibitishwa na kamati ya utendaji ya ZFA Taifa, huku pia Tamim akidaiwa kushindwa kuwasilisha cheti cha kumaliza kidato cha nne, kama ambavyo katiba ya ZFA inavyosema.
Katika pingamizi hilo, lilikubaliwa mia kwa mia na hivyo kutenguliwa na Kamati ya Uchaguzi ya Chama hicho na kuagizwa urejewe ndani ya wiki mbili, huku kamati zenye utata zikitakiwa kufanya hivyo ndani ya wiki moja.
Lakini baada ya hukumu hiyo, ZFA imeibuka na kudai haina fedha za kuitisha uchaguzi mwingine, lakini ikabainisha endapo kampuni, taasisi au serikali itakubali kugharamia mkutano mkuu haitakuwa na pingamizi kuitisha uchaguzi wa marudio ili kupata safu mpya ya uongozi ambayo itasaidia kuleta mabadiliko na maendeleo ya mchezo wa soka, ili kurudisha hamasa ya mashabiki waliokata tamaa na mchezo huo kwa upande wa visiwani.
Uwanja wa Kuchonga hautajikita zaidi katika hayo, bali hali halisi ya mustakabali wa soka la Zanzibar, ambayo imebebwa na wajumbe hao 54 sambamba na Kamati hiyo ya uchaguzi inayosimamia uchaguzi huo.
Inasikitisha kuona watu wanapewa dhamana kubwa ya kuongoza chombo nyeti kama hicho cha kusimamia uchaguzi, kushindwa kutekeleza jambo hilo kwa umakini na kuhakikisha haki inatendeka na washindi wanapatikana kihalali.
Hivi kweli, Kamati tano zinaingiza wajumbe wasio sahihi na wasimamizi wako hapo hapo, huku ikiwaondosha wagombea waliokosa sifa ikiwamo kushindwa kuwasilisha vyeti vya kuhitimu kidato cha nne, huu ni udhaifu ambao leo unaigharimu ZFA.
Hayo tisa, kumi ni pale uchaguzi huo kutawaliwa na vitendo vya matumizi yasiyo sahihi ya fedha, kwa lugha nyepesi rushwa kama vile hakuna vyombo vya kudhibiti hali hiyo, au kam vile vitendo hivyo vimebarikiwa.
Habari za wajumbe ambao wamepewa dhamana na Wazanzibar wapenda soka kuwawakilisha, wanakubali kufanya maamuzi kwa shinikizo la rushwa hakika roho zenu zitawahukumu kama amekwenda kinyume cha wale waliowatumeni hapo.
Fununu za kispoti za ‘Kiintelejensia' zilikuwa zikimwaga wajumbe kushawisha kwa fedha kuanzia 20,000, wengine 50,000 wengine 100,000 mara pilau hadi juisi ya mabungo! Inasikitisha juisi ya mabungo inawasukuma kupindisha kura zenu, hakika inasikitisha na kama hali ndio hiyo basi safari ya soka la Zanzibar bado iko mbali sana.
Wajumbe wa mkutano mkuu wa ZFA, hebu dhamira zenu ziwasute, wachagulieni Wazanzibar viongozi kutokana na matakwa ya wadau na wapenda michezo kwa ujumla si kwa ajili ya kundi la watu wachache.
Tambueni kama dhamana ya kulifufua au kuzidi kulizamisha soka la Zanzibar iko mikononi mwenu, wakati ndio huu, mkicheza kama ambavyo inadaiwa mlicheza kwa shinikizo hakika mtazidi kuwajutisha Wazanzibar wapenda soka.
Mwisho ni kwa Kamati ya Uchaguzi, simameni katika katiba ya ZFA na wala kusuwepo kubebana bali haki itendekea ili kutorejesha sintafahamu kama hizi zilizojitokeza na kuigharimu hivi sasa ZFA.
Mungu Ibariki ZFA, Mungu libariki soka Zanzibar. Tukutane wiki ijayo.
 
Wadau sasa wamewachoka makocha wa Kibongo

Mwandishi wetu

KARIBUNI tena wapenzi wasomaji wa gazeti letu la Tanzania Daima na hasa katika Kona ya Mwaisabula; ni matumaini yangu sasa tumefikia mwisho wa kupeana zile salaam za kheri ya mwaka mpya au kheri ya X-mass, sasa tunaangalia mambo mengine ndani ya mwaka huu, yaani 2011.
Makala yangu ya leo inahoji, wadau wa soka nchini kuwachoka makocha wazawa. Na sasa wameamua kusema hadharani.
Kazi kwao makocha kusuka au kunyoa.
Nilikuwa miongoni mwa waalikwa katika kipindi cha ITV kinachorushwa kila Jumapili usiku, kuanzia saa 3.15 cha Kizaazaa, kilichokuwa kikiongozwa na mwandishi mahili hapa nchini, Salehe Ally, akishirikiana na Ezekiel Kamwaga au maarufu kama ‘Mzee wa Liverpool'.
Lakini mwaliko wa kuhudhuria kipindi hicho niliutumia na aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela. Kipindi kilikuwa ni kizuri mno na kilikuwa na mada nyingi tu, mojawapo ya mada iliyonifanya niandike makala hii ni inayozungumzia nafasi ya makocha wazawa nchini dhidi ya makocha wa kigeni.
Utamu wa kipindi kile, kilijumuisha wadau wengi na maarufu wa soka nchini, wakiongozwa na mwenyekiti aliyepita wa Simba, Hassan Dalali, wakala wa kuuza wachezaji nchini, Saidi Tully, wachezaji wakongwe kama Abdul Kipenge, Abeid Mziba, Katibu Mwenezi wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam, Simba Gadafi, na wengineo wengi tu.
Mada ilipoanza, ilichangiwa na wengi mno na hadi ilipokwisha, mimi nikiwa na kocha mwenzangu Joseph Kanakamfumu iliniweka katika wakati mgumu mno na kuona nina sababu gani ya kuendelea kuwa kocha ndani ya nchi hii, kama thamani yangu na mchango wangu kwa taifa langu hauthaminiwi na haukubaliki kabisa.
Pamoja na kutoa tathmini ya mataji yote yaliyotua nchini kwetu, ukiondoa hili la juzi la Babu Poulsen, yote yaliletwa na wazawa kina Marijan Shabaan, Sunday Kayuni, Syllersaid Mziray, Paul West Gwivaha, Abdallah Kibaden, Tito Mwaluvanda, Joel Bendera, Mohamed Msomali, Elijah Kategile na Salum Madadi bado wadau hawakukubali na wana zidi kukunyooshea vidole kuwa hufai.
Wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Simba Sports Club, Godfrey Nyange ‘Kaburu', waliwaponda makocha wa Kitanzania hadi unasikia uchungu, moja ya matatizo ya makocha wazawa ni kwanza hawajaenda shule na aliyesoma ni mmoja tu na bahati mbaya kafariki mwishoni mwa mwaka jana, yaani Super Coach Mziray, wengine wote ni wababaishaji tu, mna vikozi vidogo vidogo tu vya miezi isiyozidi miwili na wengi wao hawajui lugha mbalimbali za kimataifa, ingawa lugha yetu ya taifa tunaijua.
Makocha wa hapa nchini hawajiamini wanapokuwa wakifanya kazi zao, listi wanapangiwa na viongozi wa klabu zao tofauti na wageni, viongozi wanapanga wachezaji wanaowataka na makocha wa Kibongo wako kimya tu, kwa sababu wengi wao wana njaa na hawajiamini.
Binafsi kama kocha, nilitumia muda mwingi kujenga hoja za kupinga hizo hoja hapo juu bila mafanikio na nilikuwa siamini, kwa kuwa mimi hayajawahi kunitokea kupangiwa timu na kiongozi yeyote.
Mbali ya kufundisha timu nyingi hapa nchini, pia nimewahi kufundisha moja ya klabu kongwe hapa nchini, yaani Yanga nikiwa chini ya Francis Kifukwe na Katibu Mkuu ambaye yeye mbali ya kuwa ni mtendaji mkuu, lakini ndiye aliyekuwa karibu mno na timu: Jamal Malinzi, kamwe hakuwahi hata siku moja kuingilia benchi letu la ufundi.
Malinzi, ambaye kwa kushirikiana na viongozi wenzake wakati timu ikiwa haina mfadhili hata mmoja, walihakikisha timu inakaa mahali pazuri, inakula vizuri, inasafiri kwenda popote kwa usafiri ulio bora, posho na mishahara ya wachezaji inapatikana kwa wakati, makocha walipewa kila walichohitaji bila kujali huyu ni mzawa au mgeni, mwisho wa siku wenyewe walikaa jukwaani kusubiri matokeo ya uwanjani na wala sio kupanga timu, hao ndio walikuwa viongozi wa mpira na wala si wababaishaji, wanajua utawala wa soka.
Ndio maana, nilipata taabu siku ile katika kipindi kile cha Kizaazaa Spoti, kwa sababu mimi hayajawahi kunitokea katika maisha yangu yote ya ukocha na ninaamini siku yangetokea kwangu, huyo kiongozi maji angeyaita ‘mma'.
Kama kweli, leo makocha tunapangiwa timu na hao viongozi wa klabu zetu, basi ni bora tuachane na kazi ya ukocha tutafute kazi nyingine tufanye.
Kwa sababu, wakishakupangieni listi, pembeni wanawasema kwamba hamna ujanja, yaani tu waoga na hatujiamini ni kashfa kubwa mno kwetu.
Kama kweli elimu yetu ni ndogo kiasi hicho kinachosemwa na wadau cha kuhudhuria tu hivi visemina vya kozi ya awali, kati na pevu, basi hatufai kufundisha mpira, tuachane nao twendeni darasani tukasome tupate ujuzi zaidi, maana hatuwezi kufundisha kwa mafanikio makubwa.
Ingawa mmoja kati ya wadau Abeid Mziba au Tekero, alikiri mafanikio yake yote ya soka kayapata kutoka kwa makocha wazawa, alisisitiza kwamba leo hatuna elimu, waoga, hatujiamini na mbaya zaidi hatujiheshimu.
Wadau wale waliendelea kutuponda kuwa haiwezekani ukawa kocha halafu una kitambi au unafanya biashara ya magari na kwamba makocha sisi hatuko makini na kazi zetu; ingawa hao waliowasema kuwa na vitambi na biashara ya magari ni asilimia 2 tu ya makocha, wengine wote wamejikita katika kazi ya ukocha, lakini bado wanakosa heshima.
Nadhani ni jukumu sasa la Chama cha Makocha Tanzania (TAFCA), chini ya mwenyekiti wake, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Sunday Kayuni, na Katibu wake, Eugene Mwasasmaki, kuhakikisha wanawapeleka wanachama wake zile kozi ndefu za miaka miwili na kuendelea, kama kweli wote hawana elimu hiyo na kama wanayo, basi kazi kwenu kuwaelimisha wadau kuwa tupo tuliosoma elimu hizo.
Mchezo wa mpira sehemu yoyote husika, ili upate mafanikio ni lazima waamuzi, makocha, madaktari wa michezo, viongozi wa TFF, viongozi wa klabu na wadau wote kwa ujumla, wafanye kazi kwa umoja na kuaminiana zaidi, lakini kama kuna kundi la watu ambalo linaonekana ni mzigo (makocha), basi tusitegemee miujiza katika kuendeleza soka.
Sasa kama makundi yote hayo yanatamka hadharani na katika moja ya TV kubwa nchini, inayoangaliwa sehemu nyingi za dunia, kuwa nchi hii hakuna makocha kuna wasimamizi wa mazoezi tu, hiyo ni hatari kweli kweli; inanifanya mimi nifikirie mara mbilimbili kuendelea na kazi hii iliyokosa kabisa thamani ndani ya ardhi yetu au la.
Kipindi kile cha ‘Kizazaa', ambacho kilikuwa ni cha pili tangu kilipoanza, kilibaini kuwa mbali ya kuwa makocha hawajasoma, hata wale waliosoma elimu nzuri, hawakubaliki katika chama chao cha makocha baada ya Kocha Joseph Kanakamfumu kutamka kuwa yeye ni mmoja wa makocha waliosoma kwa upeo mkubwa, lakini kila nafasi zikitoka za mtu mwenye sifa yake Mwenyekiti wa TAFCA hataki ashiriki, ni hatari kweli kweli, je kweli tutafika!?
Najifikiria mara mbili mbili, kwa hali hii ukocha una faida gani? Niache au nizame tu, au bora nikauze nyanya wateja wangu wataniheshimu kwa biashara yangu?!
 

Nahisi Poulsen anashikiwa masikio

Ojuku Abraham

UTEUZI wa kwanza tu wa wachezaji wa Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars' Jan Poulsen kutoka Denmark, ulinipa taabu kama kweli ulitoka kwake binafsi. Mashaka yangu hata hivyo, yalitoka baada ya kubaini kwamba katika kabati la benchi la ufundi ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kulikuwa na orodha ndefu ya wachezaji wengi waliowahi kuchaguliwa kuichezea timu hiyo.
Hata hivyo, uteuzi wa baadhi ya wachezaji, ulinipa shaka kama kweli ulitokana na matakwa yake au kushinikizwa, kwa sababu kwa namna yoyote, hakukuwa na sababu za kutosha za kuwajumuisha kikosini hata kama mechi yake ya kwanza akiwa na timu hiyo ilikuwa ni ya kirafiki.
Kama awali nilikuwa na shaka juu ya uteuzi wa wachezaji wa kikosi hicho hapo awali, basi nilithibitisha katika uteuzi wa safari hii katika michuano inayoendelea ya nchi za ukanda wa Bonde la Mto Nile, yanayoendelea kule Cairo, Misri.
Ni kweli, kama nilivyosema awali kwamba katika kabati la benchi la ufundi pale TFF, ipo orodha ya majina ya wachezaji ambao ama waliwahi kuichezea timu hiyo, au wako katika mipango ya baadaye ya kikosi hicho.
Hata hivyo, kitendo cha kuitwa kwa wachezaji Athuman Machupa na Saidi Maulid ‘SMG', kimenipa hofu kama ni kweli huo ni utashi wa kocha aliyepewa dhamana hii.
Kwa nini ninahisi hivi ni kwa sababu Poulsen hakuwahi kuwaona wachezaji hawa wakicheza, hata kama wana rekodi nzuri. Machupa anacheza soka Sweden na Maulid yuko Angola.
Kipindi ambacho Poulsen amekuja, wachezaji hawa wote wamemaliza ligi za nchi walikokuwa wakicheza.
Ni wazi, kwa maana hiyo, kwamba ama wasaidizi wake au baadhi ya maofisa ndani ya TFF ndiyo waliotoa wazo la kujumuishwa kwa wachezaji hawa kikosini.
Sina tatizo na kuitwa kwa wachezaji hawa, kwa sababu nafahamu uwezo wao, shida yangu iko juu ya jinsi walivyoteuliwa.
Najaribu kuamini kuwa Poulsen pengine tofauti na Maximo, ameamua kuwapa uhuru zaidi wasaidizi wake au ameamua kuwa mtu wa kutekeleza kila ushauri anaousikia. Kama hivi ndivyo, kwangu ni tatizo.
Mimi ni shabiki wa makocha wa kigeni, nadhani wanastahili zaidi kuifundisha timu yetu ya taifa kuliko wazawa kwa sababu zilizo wazi kabisa. Moja ya sababu ya kutotaka makocha wa nyumbani kupewa nafasi ya kuifundisha timu hii wakiwa ni makocha wakuu, ni kitendo chao cha kuteua wachezaji kwa kujuana, kuogopana na mbaya zaidi, kulipa fadhila.
Katika uteuzi wa timu ya kwenda Cairo, kulikuwa na ninaouona dhahiri ulifanywa kwa misingi hiyo niliyoitaja hapo juu. Sijui mtazamo wa TFF na wadau wengine katika michuano hii ya Mto Nile, lakini kwangu, sioni tofauti yake na Bonanza.
Si mashindano ambayo yatatusaidia chochote katika ulingo wa kimataifa, zaidi ya kutupa mazoezi. Na kwa sababu hiyo, sikuona sababu ya kuwaita katika kikosi wachezaji wanaocheza nje.
Wachezaji kama Henry Joseph, Nizar Khalfan, Said Maulid na Athuman Machupa hawakuwa na sababu ya kuitwa. Hawa tayari ndo ‘professional' wetu, tayari wana uzoefu wa michezo ya kimataifa. Kuwaita katika bonanza kama hili ni ama kuwadhalilisha ama kutaka kujikosha.
Hii ilikuwa ni michuano ya kuwachukua wachezaji kama Mbwana Samatta, Himid Mao, Kiggi Makassy, Zahoro Pazi, Thomas Ulimwengu, Mwinyi Kazimoto na chipukizi wengine wa aina hii. Hawa ni wachezaji ambao wangekwenda kupata uzoefu wa kucheza michezo ya kimataifa, ili kuwajengea uwezo wa kuweza kucheza michezo ijayo ya Taifa Stars pasipo na woga.
Na wachezaji hawa wa kulipwa, kwa vyovyote wameitwa kwa shinikizo la ama kutoka kwa makocha wazawa waliokuwa wanaiandaa timu wakati Poulsen akiwa kwao, ama maofisa ndani ya TFF.
Wamewaita kwa sababu wanajuana, wanawaogopa ama kutaka kujikosha. Hili, kila mara ndilo limekuwa kosa letu. Hatuamini katika kuandaa na kukuza kizazi kipya. Bado tunaamini kuwa tunao wachezaji wakongwe wenye uwezo wa kutupatia mataji na ushindi katika mashindano makubwa ya leo.
Hatutaki kujenga timu ya kesho kwa kutumia mabonanza ya leo. Tunawapeleka wakongwe hawa kwenye bonanza, tutawahitaji tena kwenye CAN, halafu Kombe la Dunia na baadeye Chalenji, hivi chipukizi wetu watapata wapi nafasi ya kuonyesha uwezo wao?
Poulsen amekutana na watu wenye hofu juu ya uwezo wao wa kufanya kazi. Amekutana na watu wanaosoma mawazo hasi ya mashabiki wa Tanzania.
Wao wanajua ni wapi Maximo alikosea. Wanapitia katika kivuli chake ili kujihalalishia. Sio ajabu wamemwambia moja ya sababu ya kuchukiwa kwa Maximo ni kutosikiliza ushauri na kwa sababu hiyo, ili apendwe, anatakiwa kukubali kila anachoambiwa. Ni hapa ndipo anapotajiwa majina na kwa jinsi Poulsen anavyoonekana, hataki makuu.
Lakini nina hofu na watu hawa. Ni kwa sababu wao ndiyo watakuwa wanaiongoza Stars, muda siyo mrefu wataanza lawama kwa ‘Babu' huyu.
Lawama zitakuja baada ya kuona majina wanayomtajia kocha hayafundishiki, wataanza kumwona hafai.
Kwa timu kama yetu, kocha pekee anayetufaa ni mwenye kariba ya Maximo, kichwa ngumu, haambiliki na asiyetaka kusikiliza ‘ushauri'. Hii ni kwa sababu kila shabiki wa Tanzania ni mshauri.
Nadhani watu hawa wanaomshikia masikio Poulsen, wangemsaidia sana kocha huyu kama wangempeleka kuwaona wachezaji, popote walipo ili aamue mwenyewe, kuliko kuanza kumtajia majina.
 
Papic, mawingu ni dalili za mvua

Mwandishi wetu

NINAPOMTAZAMA Kocha Mserbia wa Yanga, Kostadin Papic, mwenyewe akitaka afananishwe na rais wa zamani wa Marekani, Bill Clinton, ananikumbusha wenzake wengine wawili waliokuwepo Jangwani kabla yake. Hawa ni Milutin Sredojevic ‘Micho' na Dusan Kondic. Niliwahi kufanya kazi na makocha wote wawili wa awali, ingawa niliiva zaidi na Micho.
Kitu kimoja nilichokigundua kwa makocha hawa wote watatu, ni kujisifu. Jamaa wanajisifu sio kitoto.
Kwa mfano, Micho alikuwa na kawaida ya kunieleza kwamba ni yeye ndiye aliyekuza kipaji cha beki mahiri wa Manchester United, Nemanja Vidic hadi akawa kama unavyomuona sasa.
Alinieleza kuwa alimfundisha mchezaji huyo, ambaye pia ni Mserbia katika kikosi cha timu ya taifa ya Serbia ya vijana chini ya miaka 17.
Vidic alizaliwa Oktoba 21, 1981.
Milutin "Micho" Sredojević alizaliwa Septemba 1, 1969 hii ikiwa na maana kuwa wamepishana miaka 12 na beki huyo anayechukuliwa kuwa mmoja wa mabeki bora zaidi kwa sasa duniani.
Lakini ukitazama historia ya Vidic, haionyeshi ni lini alichezea timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17 na hata historia ya Micho mwenyewe, haionyeshi kama amewahi kuwa kocha wa timu hiyo, ingawa unasoma kuwa amewahi kufundisha klabu za Afrika, zikiwemo St George, Orlando Pirates, SC Villa na Yanga.
Kondic naye si haba kwa majisifu. Unakumbuka wasifu wake wakati akija nchini? Alikuwepo katika benchi la ufundi la timu ya taifa ya Angola ambayo ilifanikiwa kucheza fainali za kombe la dunia mwaka 2006 nchini Ujerumani!
> Wapo waliodiriki hata kumpa cheo cha uprofesa!
> Alikuja kwa mkwara na moja ya kauli mbiu yake ilikuwa ni kuiendesha Yanga kibiashara, kwamba angenunua na kuuza wachezaji kama zinavyofanya klabu za Ulaya.
Mfadhili Mkuu wa Yanga, Yussuf Manji, akaingia mkenge. Akaipeleka timu Mwanza na baadaye Afrika Kusini ambako tunaambiwa ilicheza mechi za kirafiki na wafanyakazi wa hoteli. Alisajili wachezaji wengi kutoka DRC na Kenya lakini mwisho wa siku, hawakuisaidia chochote Yanga, zaidi ni kuwapa hasara tu. Pamoja na kwamba ilichukua ubingwa, lakini ulikuwa wa mbinde!
> Ndio maana nadhani hata alipoondoka bila kulipwa sehemu ya mshahara wake hakujali kwa sababu alisaidia sana kuiingizia klabu hiyo hasara!
> Na kuhusu Papic, usiseme. Huyu jamaa ana sifa ya kufundisha klabu nyingi zaidi barani Afrika kuliko wenzake wote. Lakini kama umejaribu kufuatilia kwa karibu, wote watatu, licha ya kufanana kwa majisifu, pia wana nyongeza ni walalamishi!
> Alianza kulalamika Micho, enzi hizo Yanga ikiwa chini ya Francis Kifukwe. Kwamba wachezaji waliosajiliwa hakuridhika nao na hivyo akataka msimu unaofuata yeye ndiye apewe nafasi.
Alifanya hivyo makusudi ili kutafuta sababu kwa kuwa anafahamu fika kuwa katika Afrika, usajili hufanywa na viongozi na si makocha.
Akafuata kulalamika Kondic, akilalamikia maisha magumu na kutolipwa mshahara kwa wakati. Yanga walimtoa kutoka hoteli ya New Africa alikoishi kwa kipindi kirefu na kumpeleka uswahini Kariakoo. Maisha yalivyozidi kuwa magumu, akaishia zake.
Sasa ni zamu ya Papic. Wenzake wote wawili waliondoka pasipo maelewano mazuri na uongozi na hakuna dalili kama huyu anaweza kuondoka kwa kheri.
Licha ya kulalamika kila mara hadharani kuhusu mshahara wake, hivi karibuni amesema wazi kuwa anafundisha klabu hiyo kama ‘deiwaka' tu, kwa sababu mkataba wake umekwisha.
Na Yanga katika kuthibitisha kwamba haina mkataba na kocha huyo, imeingia mkataba na mchezaji wake mahiri wa zamani, Fred Felix Minziro kuwa msaidizi wa Mserbia huyo.
Lakini Papic amepinga kitendo hicho, akidai haiwezekani kutafutiwa msaidizi bila yeye kushirikishwa. Anadai kwamba msaidizi wake alipaswa kutafutwa kwa yeye kushirikishwa.
Ni kweli, lakini mambo ya kitaaluma kama haya, inapotokea yanapindishwa makusudi, ishara ni moja tu, hutakiwi!
> Sisi waswahili tunajua. Unapokuwa hutakiwi mahali, utaona tu mambo yanakuwa ndivyo sivyo. Kwa wenye akili zao, hung'amua mapema na kuamua kujiweka kando, lakini kwa wale ambao ubongo wao upo kama ulivyo, hung'ang'ania.
Yanga haihitaji tena huduma ya Papic, maana kama kweli inamhitaji, isingeweza kumuajiri kocha msaidizi bila kupata baraka zake. Baraka haimaanishi kukubali tu, bali hata kumtaarifu tu katika hali ya kawaida ya kibinadam.
Lingekuwa jambo jema sasa kwa Papic kuanza kutafuta timu nyingine, hasa kutokana na uzoefu wake kwa soka la Afrika.
Kwa kipindi chote ambacho Yanga imekuwa chini ya makocha wa kigeni, haijaweza kuwa na soka maridadi mfululizo. Inacheza kwa vipindi kutegemeana na mchezo.
Ni vigumu kutofautisha soka ya Yanga chini ya Micho, Kondic au Papic na ile ya Kenny Mwaisabula ‘Mzazi' au Minziro.

Imeandikwa na Ojuku Abraham
 

Huu ni mzaha viongozi kukwepa majukumu

Mwandishi wetu

WAKATI tukisherehekea kuanza kwa mwaka mpya, kila mmoja kwa wakati na nafasi yake anapanga yale ambayo atayafanya, kwa miezi 12 ya mwaka huo.
Watu hujipangia kuanza masuala kadhaa au kuendeleza mipango, ambayo waliianza katika mwaka uliopita, dhamira ikiwa kufikisha hatima yake ya kimaendeleo.
Mipango hiyo, haiwi kwa mtu mmoja mmoja pekee, lakini pia hupaswa kuwa ni kwa taasisi, vyama au mashirikisho ya michezo mbalimbali.
Hata hivyo, inasikitisha kuona kwamba, viongozi wa mashirikisho au vyama vya michezo mbalimbali nchini kuwa wakikwepa majukumu na wajibu wao.
Viongozi wa vyama kadhaa, huacha kusaka fedha kwa ajili ya kuendeshea ofisi, kuzigharamia timu za taifa zinapojiandaa na mashindano au mechi za kimataifa na mambo mengineyo.
Ni bahati mbaya sana kwamba, viongozi wengi wa vyama vya michezo wamejijengea tabia ya kuuhadaa umma, wakijitahidi kadiri wa wawezavyo kuaminisha kwamba, wajibu na jukumu la kuzigharamia timu hizo ni wa serikali.
Kwa hakika hilo sio, wajibu wa serikali ni kuandaa mazingira ya michezo kuchezwa kwa amani, lakini suala la maandalizi linabaki kwa vyama au taasisi husika.
Kwa kweli, kwa staili hii ya ‘usanii usanii' hatutafika katika mafanikio ya kweli ya kimichezo, kama viongozi wataendelea na mtindo wa kukwepa majukumu.
Ni lazima wajue kuwa, wanapaswa kujipanga tangu Januari Mosi ya kila mwaka, kwa kujua watakapozipata fedha za kuendesha chama kwa ujumla wake kwa mwaka mzima ulio mbele yao.
Wanapaswa kujiandaa kugharamia mashindano ya kitaifa na kimataifa kama watapewa uenyeji na pia kuhakikisha timu za taifa ama wawakilishi wao katika michuano ya kimataifa, hawakwami kushiriki kwa sababu yoyote ile.
Ninajiuliza, kama kiongozi amegombea uongozi wa chama cha michezo, huku akijua kuwa chama hakina chanzo au vyanzo vya mapato, kipi kinachomshinda kuanzisha vyanzo hivyo?
Ninawasihi viongozi wetu waache ubabaishaji, wawajibike wasitake sifa na kuona fahari tu kuongoza vyama, huku wakishindwa kuleta ufanisi katika nyanja za kimataifa.
Tumezoea kuwasikia viongozi wakijinadi kwa ahadi kem kem za kuleta mabadiliko na maendeleo katika mchezo huu au ule, pale wanapowania uongozi, lakini wanapopata hujifanya kusahau kila kitu.
Tumekuwa tukiwashuhudia viongozi wa michezo mbalimbali hapa nchini, wakizungumza mchana kutwa kwenye vyombo vya habari nchini wakiilaumu serikali kuwatekeleza kila wanapokabiliwa na mashindano.
Viongozi hao, huanza kuhangaika kupita pita kuomba fedha kwa serikali au wadhamini unapobaki mwezi mmoja au wiki chache kabla ya kufanyika mashindano.
Huwa mafundi wa kulaumu serikali, kampuni na mashirika kwamba wamewatelekeza, lakini wao hawajafanya chochote katika kufanikisha upatikanaji wa fedha hizo.
Wanaposhindwa kushiriki ama wakishiriki na kufanya vibaya, kitu cha kwanza wanachokisema ni kuwa hawakuungwa mkono katika maandalizi.
Nawakumbusha viongozi wa vyama mbalimbali vya michezo nchini kwamba, wanapaswa kuanza maandalizi sasa kwa ajili ya mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kwa mwaka 2011 kama wanataka ufanisi.
Kusubiri ubaki mwezi mmoja ndipo waanze kuinyooshea serikali kidole ni mchezo usiopendeza, Watanzania tuna vipaji vya hali ya juu katika kila mchezo, lakini kinachotuangusha ni maandalizi duni hivyo.
Ili kuondokana na hilo, ni wajibu wa kiongozi wa kila chama, shirikisho au taasisi ya kimechezo, kuhakikisha wanajiwekea miradi au mitego ya vyanzo vya mapato na sio kusubiri mashindano yafike waanze kulalamikia ukata, kwa staili hii hatutafika.
 
Huu ni mzaha viongozi kukwepa majukumu

Mwandishi wetu

WAKATI tukisherehekea kuanza kwa mwaka mpya, kila mmoja kwa wakati na nafasi yake anapanga yale ambayo atayafanya, kwa miezi 12 ya mwaka huo.
Watu hujipangia kuanza masuala kadhaa au kuendeleza mipango, ambayo waliianza katika mwaka uliopita, dhamira ikiwa kufikisha hatima yake ya kimaendeleo.
Mipango hiyo, haiwi kwa mtu mmoja mmoja pekee, lakini pia hupaswa kuwa ni kwa taasisi, vyama au mashirikisho ya michezo mbalimbali.
Hata hivyo, inasikitisha kuona kwamba, viongozi wa mashirikisho au vyama vya michezo mbalimbali nchini kuwa wakikwepa majukumu na wajibu wao.
Viongozi wa vyama kadhaa, huacha kusaka fedha kwa ajili ya kuendeshea ofisi, kuzigharamia timu za taifa zinapojiandaa na mashindano au mechi za kimataifa na mambo mengineyo.
Ni bahati mbaya sana kwamba, viongozi wengi wa vyama vya michezo wamejijengea tabia ya kuuhadaa umma, wakijitahidi kadiri wa wawezavyo kuaminisha kwamba, wajibu na jukumu la kuzigharamia timu hizo ni wa serikali.
Kwa hakika hilo sio, wajibu wa serikali ni kuandaa mazingira ya michezo kuchezwa kwa amani, lakini suala la maandalizi linabaki kwa vyama au taasisi husika.
Kwa kweli, kwa staili hii ya ‘usanii usanii' hatutafika katika mafanikio ya kweli ya kimichezo, kama viongozi wataendelea na mtindo wa kukwepa majukumu.
Ni lazima wajue kuwa, wanapaswa kujipanga tangu Januari Mosi ya kila mwaka, kwa kujua watakapozipata fedha za kuendesha chama kwa ujumla wake kwa mwaka mzima ulio mbele yao.
Wanapaswa kujiandaa kugharamia mashindano ya kitaifa na kimataifa kama watapewa uenyeji na pia kuhakikisha timu za taifa ama wawakilishi wao katika michuano ya kimataifa, hawakwami kushiriki kwa sababu yoyote ile.
Ninajiuliza, kama kiongozi amegombea uongozi wa chama cha michezo, huku akijua kuwa chama hakina chanzo au vyanzo vya mapato, kipi kinachomshinda kuanzisha vyanzo hivyo?
Ninawasihi viongozi wetu waache ubabaishaji, wawajibike wasitake sifa na kuona fahari tu kuongoza vyama, huku wakishindwa kuleta ufanisi katika nyanja za kimataifa.
Tumezoea kuwasikia viongozi wakijinadi kwa ahadi kem kem za kuleta mabadiliko na maendeleo katika mchezo huu au ule, pale wanapowania uongozi, lakini wanapopata hujifanya kusahau kila kitu.
Tumekuwa tukiwashuhudia viongozi wa michezo mbalimbali hapa nchini, wakizungumza mchana kutwa kwenye vyombo vya habari nchini wakiilaumu serikali kuwatekeleza kila wanapokabiliwa na mashindano.
Viongozi hao, huanza kuhangaika kupita pita kuomba fedha kwa serikali au wadhamini unapobaki mwezi mmoja au wiki chache kabla ya kufanyika mashindano.
Huwa mafundi wa kulaumu serikali, kampuni na mashirika kwamba wamewatelekeza, lakini wao hawajafanya chochote katika kufanikisha upatikanaji wa fedha hizo.
Wanaposhindwa kushiriki ama wakishiriki na kufanya vibaya, kitu cha kwanza wanachokisema ni kuwa hawakuungwa mkono katika maandalizi.
Nawakumbusha viongozi wa vyama mbalimbali vya michezo nchini kwamba, wanapaswa kuanza maandalizi sasa kwa ajili ya mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa kwa mwaka 2011 kama wanataka ufanisi.
Kusubiri ubaki mwezi mmoja ndipo waanze kuinyooshea serikali kidole ni mchezo usiopendeza, Watanzania tuna vipaji vya hali ya juu katika kila mchezo, lakini kinachotuangusha ni maandalizi duni hivyo.
Ili kuondokana na hilo, ni wajibu wa kiongozi wa kila chama, shirikisho au taasisi ya kimechezo, kuhakikisha wanajiwekea miradi au mitego ya vyanzo vya mapato na sio kusubiri mashindano yafike waanze kulalamikia ukata, kwa staili hii hatutafika.




 
Kalala alalama uchelewaji wa kesi ya Kituo cha Sanaa Shekilango


na Makuburi Ally


MWANAMUZIKI nguli wa muziki wa dansi Tanzania, Komandoo Hamza Kalala ‘Ngozi ya Kitimoto' ametoa wito kwa mahakama Kuu ya Ardhi Tanzania kufanikisha kwa haraka kesi zinazokikabili Chuo cha Sanaa Shekilango jijini Dar es Salaam kilichoasisiwa na aliyekuwa gwiji la muziki Tanzania marehem John Ondolo Chacha zilizoanza tangu mwaka 2007.
Akizungumza na Tanzania Daima juzi, Kalala alisema uchelewaji wa kesi hizo unachelewesha mipangilio iliyoachwa na Chacha ambayo ilikuwa ni kwa ajili ya wasanii Tanzania ikiwa ni dhamira yake wakati akiwa ni mtumishi wa Serikali ya Tanzania katika masuala mbalimbali yanayoihusu nchi hii ikiwemo sanaa.
Kalala alisema marehemu Chacha alipanga kujenga studio za kisasa za filamu na ya kurekodi muziki sambamba na waangalizi wa kazi za sanaa, masuala ambayo yanakwamishwa na muendelezo wa kesi hizo mahakamani ambazo zinakwenda katika mtindo wa kinyonga ambapo ameshapatikana mfadhili wa kuliendeleza eneo hilo katika nyanja ya sanaa ikiwa familia ya marehemu ina taratibu zote za kulimiliki eneo hilo kihalali kutoka serikalini lakini kuna baadhi ya wajanja wachache wanataka kulivamia eneo hilo.
Aidha Kalala alisema asilimia kubwa ya vijana wa sasa hivi hawawaogopi wakubwa katika maamuzi sababu inayopoteza maendeleo stahili kwa jamii kwa sababu wangemfaham Ondolo Chacha katika nyanja ya maendeleo ya nchi hii, wasingefikia hatua ya kiubabaishaji inayotaka kuvuruga mipangilio bora ya maendeleo ya nchi.
Kalala alisema kwa ubabaishaji unaofanywa na baadhi ya wadau, Tanzania itafikia mahali itapigiwa vifaa vya muziki na wageni kutoka nje kwa sababu ya kutozingatia maendeleo yaliyoanzishwa na wasanii nguli waliopita kama Ondolo Chacha.
"Wanamuziki wa sasa hivi hawatumii vifaa husika na badala yake wanaimba tu, hali ambayo inapoteza mwelekeo wa muziki wa dansi, Chacha alituachia muongozo wa kuendeleza kituo cha Sanaa Shekilango ambacho kingefua vijana katika tasnia ya sanaa kwa ujumla lakini wenye uchu wanataka kuvamia eneo lake ni hatari," alisema Kalala.
Alisema vigogo wa muziki kila uchao wanakufa na fani zao, kuna wasiwasi baadaye vipaji vyote vikaondoka kutokana na kutozingatiwa kwa maendeleo kama ya Chuo cha Sanaa Shekilango na kutoa wito kwa serikali kuzingatia maendeleo yanayoasisiwa na wadau husika ili kutoipa mzigo.
Naye Chacha ambaye ni mtoto wa marehemu ametoa wito kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwasaidia kudhibiti matapeli wanaowanyanyasa kila uchao ambao wanawatishia kuwanyanyasa nyumbani kwao.
Chacha alisema hivi sasa wanasubiri haki yao Mahakama Kuu ya Ardhi jijini Dar es Salaam ambako kesi ya kwanza itatajwa Februari 3 dhidi ya Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na nyingine itatajwa Februari 7 dhidi ya Manispaa ya Kinondoni.
 
Washiriki Music Dance kuendelea kupigwa msasa


na Mwandishi wetu


WASHIRIKI 55 wa kusaka mwimbaji bora wa muziki wa dansi Tanzania katika zoezi la kusaka vipaji vya muziki wa dansi, Alhamisi ijayo wanatarajia kupatia elimu zaidi ya muziki dansi kutoka kwa wataalamu wa muziki hapa nchini.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, katika ukumbi wa Msasani Club, Mkurugenzi wa Makukwe Entetainment, Suleiman Mathew, alisema hatua ya kutoa elimu kwa mara ya pili imetokana na baadhi ya washiriki kuwa na kiwango duni cha muziki kuelekea fainali za shindano hilo.
Mathew alisema fainali za kusaka vipaji vya muziki wa dansi zinatarajia kuanza Januari 14 huku fainali za mwisho zinatarajia kufanyika Machi 6 katika ukumbi wa klabu Bilicanas jijini Dar es Salaam.
Aidha Mathew alisema vijana hao wananolewa na mwanamuziki Mkongwe, Abdul Salvador na Carola Kinasha, ambao wanawafunza kuimba muziki wakisindikizwa na vyombo.
“Tunataka vijana wakianza kuingia katika fainali wawe wameiva, jambo ambalo tunahitaji majaji wafanye kazi ya ziada kung’amua mshindi katika kinyang’anyiro hicho,” alisema Mathew.
Naye mwalimu wa vijana hao, Abdul Salvador, alisema vijana wameiva kiasi katika tasnia ya muziki kinachotakiwa ni kuwapiga msasa wa mwisho ambao utafanikisha kufanya vizuri katika shindano hilo.
Salvador alisema asilimia kubwa wanafanya vizuri, wachache ndio wanawafanyia marekebisho madogo ambayo yatawaweka vizuri katika shindano hilo.
Majaji watamtangaza mshindi wa muziki wa dansi ni pamoja na Tshimanga Kalala Assosa, Nyota Waziri, Ally Choki, Salvador na Kinasha.




 
Washiriki Music Dance kuendelea kupigwa msasa


na Mwandishi wetu


WASHIRIKI 55 wa kusaka mwimbaji bora wa muziki wa dansi Tanzania katika zoezi la kusaka vipaji vya muziki wa dansi, Alhamisi ijayo wanatarajia kupatia elimu zaidi ya muziki dansi kutoka kwa wataalamu wa muziki hapa nchini.
Akizungumza na Tanzania Daima jana, katika ukumbi wa Msasani Club, Mkurugenzi wa Makukwe Entetainment, Suleiman Mathew, alisema hatua ya kutoa elimu kwa mara ya pili imetokana na baadhi ya washiriki kuwa na kiwango duni cha muziki kuelekea fainali za shindano hilo.
Mathew alisema fainali za kusaka vipaji vya muziki wa dansi zinatarajia kuanza Januari 14 huku fainali za mwisho zinatarajia kufanyika Machi 6 katika ukumbi wa klabu Bilicanas jijini Dar es Salaam.
Aidha Mathew alisema vijana hao wananolewa na mwanamuziki Mkongwe, Abdul Salvador na Carola Kinasha, ambao wanawafunza kuimba muziki wakisindikizwa na vyombo.
"Tunataka vijana wakianza kuingia katika fainali wawe wameiva, jambo ambalo tunahitaji majaji wafanye kazi ya ziada kung'amua mshindi katika kinyang'anyiro hicho," alisema Mathew.
Naye mwalimu wa vijana hao, Abdul Salvador, alisema vijana wameiva kiasi katika tasnia ya muziki kinachotakiwa ni kuwapiga msasa wa mwisho ambao utafanikisha kufanya vizuri katika shindano hilo.
Salvador alisema asilimia kubwa wanafanya vizuri, wachache ndio wanawafanyia marekebisho madogo ambayo yatawaweka vizuri katika shindano hilo.
Majaji watamtangaza mshindi wa muziki wa dansi ni pamoja na Tshimanga Kalala Assosa, Nyota Waziri, Ally Choki, Salvador na Kinasha.
 
Wanamuziki waunda umoja wa kufa na kuzikana


na Tutindaga Mwakalonge


KUFUATIA vifo vilivyofuatana vya wanamuziki wa dansi hapa nchini jijini Dar es Salaam, wanamuziki wa bendi mbalimbali wamekutana na kuamua kuunda umoja wao lengo likiwa ni kusaidiana katika shida mbalimbali zitakazowakabili.
Wazo hilo la kuunda umoja wa wanamuziki nchini limetolewa kufuatia vifo vya wanamuziki watatu ambao ni Dr. Remmy Ongala aliyekuwa Super Matimila kabla ya kuamua kuokoka na kuingia katika muziki wa Injili; na Abuu Semhando aliyekuwa katika kundi la The African Stars ‘Twanga Pepeta'; pamoja na Charles James Ngosha aliyekuwa katika bendi ya Mlimani Park Orchestra.
Wanamuziki hao walikutana baada ya mazishi ya mwanamuziki Chales Ngosha yaliyofanyika Tandale Popobawa na kuamua kuunda umoja huo utakaowasaidia sambamba na kuwahusisha wanamuziki kutoka bendi mbalimbali ambapo umoja huo utakuwa na maalum katika kusaidiana katika matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na msiba na ugonjwa.
Aidha akizungumza na Tanzania Daima Jimmy Chika ambaye ni mmoja wa Wana Kamati ya usimamizi wa maandalizi ya umoja huo alisema umoja huo hautahusisha matatizo pekee bali uongozi na wajumbe wa kamati hiyo watakuwa wakikutana kwa lengo la kupeana mawazo ya jinsi ya kukuza muziki wa Kitanzania na utasaidia kukuza uhusiano bora kati ya wanamuziki.
Katika hatua za awali viongozi waliochaguliwa ni Cosmas Chidumule pamoja na kiongozi wa bendi ya Kilimanjaro ‘Wana Njenje' Waziri Ally ambao hadi sasa wapo katika mchakato wa kutafuta ofisi ya uratibu na utendaji wa shughuli zote zitakazohusisha umoja huo.
Mkutano uliofanyika Tandale Popobawa ulihusisha wanamuziki mbalimbali ambao baadhi yao ni Kikumbi Mwanza Mbang'o (King Kiki), Ali Adinani wa shikamoo jazz, Maliki Star, Hassan Rehani Bitchuka, Ramadhan Mapesa, Ally Choki, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone' na wengineo.
 
JKT Ruvu, Ruvu Shooting fainali Uhai Cup leo


na Juma Kasesa


MASHINDANO ya vijana chini ya miaka 20, ‘Uhai Cup' yanafikia tamati leo kwa timu za JKT Ruvu na maafande wenzao wa Ruvu Shooting kuvaana, katika mchezo wa fainali, utakaopigwa katika Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
JKT Ruvu walitinga hatua hiyo juzi baada ya kuitandika Polisi Tanzania bao 1-0, huku ndugu zao Ruvu Shooting wakiwaondosha katika mashindano AFC ya Arusha baada ya kuitandika mabao 2-0.
Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa na ushindani wa hali juu kutokana kiwango cha timu zote mbili ambacho zilikionyesha tangu mwanzo wa mashindano kiasi cha kufikia hatua hiyo huku mabingwa watetezi wa kombe hilo Azam FC na timu za Simba na Yanga wakiaga mapema.
Mashindano haya ambayo yalianza kutimua Desemba 27 mwaka jana yanafanyika kwa mara ya tatu yakiwa yanashirikisha timu za vikosi vya pili kwa timu za Ligi Kuu Tanzania Bara kwa lengo la kusaka vipaji yakidhaminiwa na Maji ya Uhai ambayo hutengenezwa na mfanyabiashara bilionea Saidi Salim Bakhresa.
Tayari mashindano hayo yameshuhudiwa yakiibua vipaji vya wachezaji mbalimbali ambao baadhi yao wameanza kuwika na timu kubwa ikiwemo timu ya taifa ‘Taifa Stars' ambao ni Thomas Ulimwengu , Himid Mao, Kabali Faraji na Abuu Ubwa.
 
Ruvu Shooting yajichimbia Zanzibar


na Dina Ismail


KATIKA kujiandaa na mzunguko wa pili wa Ligi Kuu bara timu ya soka ya Ruvu Shooting ya mkoani Pwani, imeamua kujichimbia Visiwani Zanzibar, imefahamika.
Chini ya kocha wake mpya Charles Boniface Mkwasa, timu hiyo inatarajiwa kucheza mechi moja ya kujipima nguvu kabla ya kurejea jijini Dar es Salaam tayari kuanza safari ya kuelekea mjini Morogoro.
Ofisa habari wa timu hiyo Masau Bwire aliiambia Tanzania Daima juzi kwamba wameamua kuipeka timu hiyo visiwani humo kutokana na utulivu ulioko hivyo kufanya wachezaji watulize akili katika maandalizi yao.
Bwire alisema timu yao iko katika hali nzuri kwa sasa na hasa ikizingatiwa kuwa kocha waliyenaye pia ana uzoefu katika ufundishaji hivyo wana uhakika wa kufanya vema katika duru hilo.
"Wadau wasiwe na wasiwasi na timu yao kwani kocha tuliyenaye ni mzuri na ushirikiano mzuri tutakaompa ndio utakaomuwezesha kuifikisha pazuri timu yetu," aliongeza Bwire.
Katika mzunguko wa kwanza wa ligi hiyo Ruvu Shooting ililala bao 1-0 likifungwa na mshambuliaji wa Kagera Sugar, Gaudance Mwaikimba.
 
Mji Mkongwe wasikitishwa na uvamizi wa viwanja


na Mohamed Said Abdullah, Zanzibar


VIONGOZI katika jimbo la Mji Mkongwe Zanzibar wamesikitishwa na vitendo vya baadhi ya wavamizi wa viwanja vya michezo na kujenga majengo ya biashara wakati maeneo hayo yana umuhimu wa kuinua michezo na kutumika kwa shughuli za kijamii.
Wakizungumza katika hafla ya kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu 25 za jimbo hilo, Mwakilishi wa Mji Mkongwe Ismail Jussa, alisema viwanja vya michezo vina umuhimu mkubwa katika kukuza vipaji vya vijana ndio maana uongozi wa jimbo hilo umeanza kushughulikia tatizo hilo na kuwataka wanamichezo kuwa na subira.
Msaada huo wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh mil 5, umetolewa kwa ushirikiano kati ya Mbunge Mohamed Ibrahim Sanya na Mwakilishi Ismail Jussa ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya uchaguzi ambapo kila timu imepata seti moja ya jezi pamoja na mipira miwili wakati timu za Malindi, Shangani na Vikokotoni zilizopatiwa mipira mitatu kwa kila timu.
Jussa alisema jambo la kushangaza mji mkongwe ni miongoni mwa miji iliyomo katika urithi wa kimataifa chini ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kushughulikia elimu (UNESCO) lakini baadhi ya watu wameanza kuvamia maeneo ya wazi na kujenga majengo ya biashara na kutoa mfano katika Uwanja wa Malindi ambako kunajengwa maduka na kupoteza sura ya Mji Mkongwe.
Jussa alifika mbali zaidi kwa kuwalaumu wanaosimamia ramani za mipango miji katika mamlaka ya Mji Mkongwe wa Zanzibar kuruhusu ujenzi wa majengo yenye urefu wa zaidi ya ghorofa tano kinyume na sheria ya mamlaka ya mji mkongwe ambapo nyumba zote zinatakiwa kuwa na urefu wa ghorofa tatu.
Akizungumza kabla ya kukabidhi vifaa hivyo, mbunge wa jimbo hilo, Mohamad Ibrahim Sanya, alisema programu ya maendeleo katika jimbo hilo imeshatayarishwa ikihusisha michezo, elimu na vikundi vya wajasiriamali vinavyotarajiwa kukabidhiwa boti na mashine zake.
Sanya alisema katika programu hiyo, wanatarajia kukabidhi vifaa kwa timu za mpira wa kikapu ili kukuza mchezo huo sambamba na kuandaa mashindano maalum ya soka ya kugombea Kombe la Mbunge na Mwakilishi yatakayofanyika mara mbili kwa mwaka hatua itakayosaidia kuibua vipaji vya vijana.
Kwa upande wake mratibu wa hafla hiyo Seif Mussa 'Ferguson' alilalamikia matumizi mabaya ya uwanja wa Malindi ikiwemo vyombo vya moto kukatisha katikati ya uwanja sambamba na ukosefu wa uzio jambo ambalo linasababisha uwanja huo kugeuka sehemu ya malisho na umwagaji wa vifusi vya ujenzi.
 
Nsajigwa, Kaseja waahidi kuiua Uganda
Sunday, 09 January 2011 21:14

kipa wa Taifa Stars,Juma Kaseja(kushoto) na nahodha wa timu hiyo, Shadrack Nsajigwa.

Mwandishi Maalum, Cairo
WACHEZAJI wa timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' na Kocha Jan Poulsen wameahidi kufanya vizuri kwenye mchezo wao wa kesho dhidi ya Uganda ili kufuzu kwa nusu fainali ya michuano ya Bonde la Mto Nile.

Stars juzi iliendelea kufanya vibaya kwenye michuano hiyo baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 na Burundi kwenye Uwanja wa Polisi Abbassiya mjini hapa.

"Nasikitika kwamba tumeshindwa kuifunga Burundi, tumecheza kadri ya uwezo wetu, lakini tumeshindwa kuzitumia nafasi tulizopata, yatupasa kubadilika, naamini vijana wameona na watabadilika," alisema Poulsen jana.

"Najua Uganda nayo itacheza kwa nguvu, lakini tutabadilika sana, haitakuwa kama tulivyocheza na Burundi. Sijui nini kimetokea, lakini dakika 20 za mwisho ndiyo tulizinduka.

"Tunahitaji kubadilika sana, mashindano ni magumu, kila timu inacheza kwa nguvu sana," alisema Poulsen.

Pia, kipa Juma Kaseja naye alizungumzia mechi hiyo na kusema Waganda wataipata kwani wameshaona uchezaji wao, ingawa wenzao waliibana Misri na kufungwa bao 1-0, wakati Stars ilifungwa mabao 5-1.

Kocha wa Burundi, Amas Niyongabo alisema baada ya mchezo kuwa Taifa Stars haifanyi vizuri kutokana na wachezaji kuvimba vichwa baada ya kutwaa ubingwa wa Chalenji mwezi uliopita jijini Dar es Salaam.

"Sioni ambacho Tanzania imecheza, si kama ile timu ya Dar es Salaam, naona wamejisahau na ubingwa, wanaona tayari wamepata mafanikio makubwa.

"Wale vijana hatari wote hawaonekani, ni kama timu mpya, hata bao la penalti ni zawadi wamepewa haikuwa penalti halali," alisema kocha huyo na kuwapongeza vijana wake kwa kucheza vizuri, licha ya kutoibuka na ushindi.

Lakini nahodha wa Stars, Shadrack Nsajigwa alipinga madai hayo kwamba wamebweteka na kusema soka ndivyo linavyokuwa kuna kushinda, kufungwa na sare, lakini pia kutwaa kwao ubingwa wa Chalenji kumezifanya baadhi ya timu ziwakamie.

Stars imepata matumaini ya kufuzu nusu fainali baada ya juzi Misri kuifunga Uganda bao 1-0, lililofungwa dakika ya 90 na Haji Gedo kwenye mchezo uliofanyika Uwanja wa Arab Contractors.

Matokeo hayo yanaifanya Misri kutinga nusu fainali kwani imefikisha pointi sita, ambapo hata kama itafungwa mchezo wake wa mwisho kesho dhidi ya Burundi haitaathirika.

Ili Stars ifuzu nusu fainali itabidi iifunge Uganda kesho, kisha iombee Misri iifunge Burundi ama itoke nayo sare, vinginevyo kama Burundi itashinda basi itabidi timu hizo ziangalie uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Mpaka sasa Stars imefungwa mabao sita na imefunga mawili, hivyo ina deni la mabao manne, wakati Burundi imefungwa manne na imefunga mawili huku nayo ikiwa na deni la mabao mawili.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…