Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Sarah Harding given engagement ring similar to Princess Diana's


  • transparent.gif
  • transparent.gif
By Mirror.co.uk 12/01/2011
arah-harding-and-tom-crane-pic-splash-726016200.jpg



Pop princess Sarah Harding has been given an engagement ring similar to Princess Diana's.

The Girls Aloud singer flashed the expensive ring as she walked through Heathrow airport with fiancé DJ Tom Crane.
Advertisement - article continues below »




The ring bares similarities to Princess Diana's oval blue 18-carat sapphire and diamond ring which Prince William gave to Kate Middleton when he proposed.

Walking through Heathrow airport, a smiling Sarah, wearing shades, a grey jumpsuit and black jacket, looked refreshed following her New Year holiday in the Maldives.

Fiance Tom got down on one knee on New Year's Eve and proposed to his girlfriend of more than three years



 
Charlie Sheen's 'revolving door of porn stars' in Las Vegas Christmas bender


  • transparent.gif
  • transparent.gif
by Tom Bryant, Daily Mirror 12/01/2011
charlie-sheen-image-1-933773023.jpg

MOVIE bad-boy Charlie Sheen went wild with a stream of sex stars in Las Vegas, it was claimed yesterday.
He barely left his Sin City hotel suite from Christmas to New Year as a “revolving door” of porn queens allegedly came and went.
The Wall Street actor, 45, was first spotted slamming down vodka shots in a bar after flying in.
Then he allegedly hooked up with two girls in town for a porn convention at Palms hotel and casino.
And in one boozy session it is claimed he became “infatuated” with porn star Bree Olson, 23, whose website lists “older dominant males” as one her of likes – along with “saving animals”.
Advertisement - article continues below »



Sheen, who missed three festive family gatherings during his spree, later flew a private jet to Bree’s home town Fort Wayne, Indiana.
The Mirror told how Sheen trashed his New York hotel room last October after taking porn actress Capri Anderson, 22, to dinner with his ex-wife, former Bond girl Denise Richards, 39.
The mother of his two daughters left in disgust.
Police called to the hotel at 2am found Sheen drunk and the hooker naked amid the wreckage.
A source said: “Charlie is once more partying hard. He’s out of control and this looks like New York all over again.”
Sheen is said to have told pals in Vegas that CBS want him to take a break from TV hit comedy Two And A Half Men and enter rehab for the second time in a year.



 
Russell Brand starred in Danish TV ad before he was famous


  • transparent.gif
  • transparent.gif
by Ashleigh Rainbird, Daily Mirror 12/01/2011
image-3-for-paper-pics-12-jan-2011-gallery-959618600.jpg

A DECADE ago, a mullet sporting pre-Katy Perry Russell Brand "starred" in this Danish chewing gum ad for Stimerol Big Fresh.
The gnasher flasher, 35, plays a clubber out with a bloke wearing a vet's collar to protect people from his bad breath – cue cheesy close-up shot of Russ' pearly whites! Amazing.
The ad was shot in Havana and sources say randy Russ took full advantage. Naturally.



 
Mabingwa Zambia watua Dar


*Kuzikabili Yanga, Simba

Na Addolph Bruno
MABINGWA wa soka nchini Zambia, timu ya Zesco imetua nchini jana ikiwa na kikosi cha wachezaji 29 kwa ajili kucheza na
Simba na Yanga katika mechi za kimataifa za kirafiki.

Timu hiyo itaanzankucheza na Simba Jumamosi, kabla ya kukutana na Yanga Jumapili katika Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.

Mechi hizo ni maalumu kwa timu hizo kujiandaa na michuano ya kimataifa ambao Simba itaiwakilisha nchi katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika na Yanga itashiriki mashindano CAF.

Akizungumza mara baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam jana, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Fighton Simkonda alisema michezo hiyo itakuwa kipimo kwa timu yao kujiandaa na Ligi ya Mabingwa.

Alisema timu yake inafahamu vizuri viwango vya timu za Simba na Yanga, hivyo ni nafasi muhimu kwao kucheza kwa kuwa watapata nafasi ya kurekebisha mapungufu yao na kupeana ujuzi.

"Tumewahi kuja Tanzania zaidi ya mara 5 au 6 na tunazifahamu vizuri Simba na Yanga ni timu zenye uwezo katika soka, tumefurahi kupata bahati ya kucheza nao katika kipingi hiki cha kujiandaa na Ligi ya Mabingwa," alisema Kocha huyo.

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake nahodha wa ZESCO, Jackob Banda ambaye pia ni mlinda mlango wa timu ya taifa ya Zambia 'Chipolopolo' alisema ni michezo mizuri kwao, ambayo itawapa nafasi ya kubadilisha uzoefu ya soka tofauti na walivyocheza nyumbani kwao kwa muda mrefu.
 
Sara, Mashaka kukimbia Marathon Mali


Na Amina Athumani

WANARIADHA Sara Kavina na Mashaka Masumbuko, wanatarajia kuondoka nchini Januari 21 mwaka huu kwenda Bamalo, Mali kushiriki mbio za marathon Januari 23, mwaka huu Akizungumza Dar es Salaam juzi, Katibu Mkuu wa
Chama cha Riadha Tanzania (RT) Suleiman Nyambui, alisema wanariadha hao tayari wameanza maandalizi ya mbio hizo ambazo zitashirikisha wanariadha kutoka nchi mbalimbali.

Alisema mashindano hayo yameandaliwa na Benki Kuu ya Afrika (BOA) na yatashirikisha wanariadha kutoka nchi zote zenye matawi ya benki hiyo.

"Mashindano haya yatatambulika kwa jina la BOA na yameandaliwa na kudhaminiwa na benki hiyo, hivyo kwa upande wetu tutapeleka wanariadha wawili ambao wanatoka JKT na JWTZ na tayari wameshapata vibali kutoka kazini mwao kwa ajili ya kuiwakilisha nchi kwenye michuano hiyo," alisema Nyambui.

Alisema mashindano hayo ni ya siku moja na wanariadha hao wanatarajia kurejea nchini Januari 25, mwaka huu.
 
Wakala akana Arshavin kutimka Arsenal


LONDON, England

WAKALA wa mchezaji Andrey Arshavin, Dennis Lachter amezikana tetesi zinazomuhusisha nyota huyo wa Arsenal, kutimkia katika Klabu ya Juventus ya Italia.Mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Russia, amebakiza miaka miwili
na nusu katika Klabu hiyo ya Gunners, baada ya kuwasili katika klabu hiyo inayotumia Uwanja wa Emirates mwaka 2009, lakini kwa sasa amekuwa akiripotiwa kutaka kukimbilia kwa vinara hao wa ligi ya Serie A.

Lakini hata hivyo wakala wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29, Lachter alisema jana hakuna makubaliano yaliyofikiwa na akasisitiza kuwa Arshavin, anajisikia mwenye furaha Arsenal katika harakati za timu hiyo kuwania taji la Ligi Kuu.

"Kuna uwezekano wa Arshavin kuhamia Juventus," Lachter aliiambia tovuti ya michezo ya Russia. "Lakini kuna mambo mawili ya kuzuia mkataba huo," aliongeza.

"Kwanza Arsenal mwaka huu inaweza kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu. Medani hiyo ya dhahabu kwenye ligi ya Uingereza ndiyo ndoto ya kila mchezaji.

"Pili uwezo wa kifedha wa Juve na kiasi ambacho Arsenal, inakitaka ili kumwachia Arshavin si chini ya dola milioni 26 sawa na pauni milioni 17," aliongeza na akasema kuwa kwake yeye ni vigumu kuzungumza chochote kwa sababu mchezaji huyo bado ana mkataba wa miaka miwili na nusu na Arsenal na hakuna ofa ya kueleweka.

Alisema kwa mawazo yake anadhani ni uvumi tu na akasema kuwa Juventus ingekuwa imeshamchukua Arshavin miaka miwili na nusu iliyopita, lakini hawakuweza kufanya hivyo.

 
Dzeko aipitia filamu ya Man City


LONDON, Uingereza

MSHAMBULIAJI Edin Dzeko, amesoma filamu ya Manchester City ya masikitiko ya kutotwaa ubingwa katika miaka iliyopita na ameahidia neema kwa kwa siku zijazo kwa mashabiki wa timu hiyo.City ilimsaini mshambuliaji
huyo wa Bosnia akitokea klabu ya Ujerumani, Wolfsburg kwa ada ya pauni milioni 27 kwa matumaini kuwa anaweza kuisaidia kutwaa ubingwa baada ya kupita miaka 43.

Jumatatu Dzeko mwenye miaka 24, aliangalia filamu mpya ya timu yake 'Blue Moon Rising' kuhusu majaribu na mateso ya mashabiki wa City.

Alisema: "Niliiangalia na ilikuwa ni filamu yenye hisia sana na niliona mambo mengi yaliyotokea katika miaka ya hivi karibuni.

"Filamu pia ilionesha watu kuishi kwa ajili ya klabu ambacho ni kitu cha kusisimua.

"Wakati nilipoona kiasi gani walivyo na upendo kwa klabu na bado hawajatwaa ubingwa kwa muda mrefu, utii wao ni wa kusisimua.

"Na mimi nataka kuwafanya watu hawa kuwa na furaha. Nilitwaa ubingwa wa Ujerumani nikiwa na Wolfsburg kwa mara ya kwanza katika historia yao na sasa ningefurahi kupata mafanikio hayo hapa"

Dzeko alisema anafahamu upinzani uliopo dhidi ya Manchaster United, lakini anataka timu yao kupata mafanikio na kuwafurahisha mashabiki.

Alisema anaifikiria mechi kati yao ambayo itakuwa Februari 12 mwaka huu.
Dzeko anajua umuhimu wa kufunga katika mechi hiyo itakayochezwa kwenye Uwanja wa Old Trafford, kama alivyofanya akiwa na Wolfsburg msimu uliopita katika Ligi ya Mabingwa.

Uchezaji wake ndiyo ulimfanya akatoka kucheza soka Bosnia na kuhamia Jamhuri ya Czech na Ujerumani na kufunga mabao 123 katika michezo 236.

Akiwa na Wolfsburg alifunga mabao 26, na kusaidia 10, katika mechi 32 ambapo walitwaa ubingwa wa Bundesliga msimu wa 2008-09.

Alikuwa mfungaji bora wa Ujerumani msimu uliopita akifunga mabao 22 na alifunga magoli 17 kwenye mechi 31 katika timu ya Bosnia-Herzegovina.

Dzeko alisema: "Nataka kufanya ubora wangu kuonesha watu kwamba mimi nina thamani ya fedha hii, mimi najua ni mengi lakini nina mtu ambaye anahisi shinikizo.

Kocha wa City, Roberto Mancini awali alikuwa akimtaka mchezaji huyo kuanzia majira ya joto yaliyopita, alisema anatumaini atakuwa mchezaji muhimu sana kwa klabu kwa siku zijazo.

Alisema anatumaini mchezaji huyo anaweza kushirikiana vizuri na wachambuliaji wenzake, Carlos Tevez na Mario Balotelli.

Kocha huyo alisema ni mchezaji mwenye ubora, uzoefu na anaweza kucheza katika mfumo wowote na kumwelezea kuwa ni mmoja kati ya washambuliaji wazuri waliopo Ulaya kwa sasa.

Jumamosi City itacheza na Wolves, ambapo mashabiki wa timu hiyo wanaweza kumshuhudia kwa mara ya kwanza Dzeko akicheza.

 
Mapharao waitibulia Tanzania Fifa
Wednesday, 12 January 2011 20:42

kocha%20stars.jpg
Kocha wa Taifa Stars,Jan Poulsen

Mwandishi Wetu
KIPIGO cha mabao 5-1 ilichokipata Taifa Stars kutoka kwa timu ya taifa ya Misri, Pharaos, kimesababisha madhara makubwa katika ngazi za ubora wa viwango vinavyotolewa na shirikisho la soka la Kimataifa, FIFA.

Baada ya kufanya vizuri katika michuano ya Chalenji, Tanzania ilipanda kwa nafasi nane, kutoka 124 hadi 116 lakini kwa mujibu wa viwango vilivyotolewa jana na FIFA, Tanzania imeshuka kwa nafasi nne.

Kuporomoka huko ni matokeo mabaya ya kufungwa mabao 5-1 na Misri, sare ya 1-1 na Burundi na ile ya Uganda katika mashindano ya Bonde la Mto Nile yanayoendelea nchini Misri.

Mbali na kushuka nafasi hizo nne, Tanzania bado inashika nafasi ya pili katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati unaosimamiwa na Baraza la Vyama vya Soka ukanda huo, CECAFA chini ya Rais wake, Leodegar Tenga wa Tanzania.

Mbali na Tanzania ambao ndiyo mabingwa wa CECAFA, Uganda inaongoza kwa kushika nafasi ya 83 ikiwa imeporomoka kwa nafasi tatu.

Kenya inashika nafasi ya 125 ikiwa imeshuka kwa nafasi tano, na kuendelea kuwa ya tatu katika ukanda wa CECAFA ikifuatiwa na Rwanda katika nafasi ya 134 ambayo imeshuka kwa nafasi mbili na Burundi katika nafasi ya 140 ikiwa imeshuka kwa nafasi 12.

Nchi nyingine za CECAFA ni Ethiopia ambayo imeng'ang'ania nafasi yake ya 124 wakati Sudan iliyokuwa nafasi ya 92, imeporomoka kwa nafasi nane na sasa inashika nafasi ya 100 huku Eritrea ikiporomoka kwa nafasi moja, kutoka 177 hadi 178.

Somalia imeshuka kwa nafasi tatu kutoka 182 hadi 185 wakati Djibouti imeporomoka nafasi moja kutoka 191 hadi 192.

Orodha hiyo inaonyesha nchi za Afrika ya Magharibi na Kaskazini zimeendelea kufanya vizuri zaidi ya Afrika ya Mashariki na Kusini mwa Afrika.

Misri iliyo kaskazini, imeendelea kuongoza Afrika kwa kushika nafasi ya 10 katika viwango vya FIFA , ikifuatiwa na Ghana katika nafasi ya 16, Ivory Coast (21), Nigeria (32), Algeria (36) na Cameroon iliyo nafasi ya 38.

Mabingwa wa Dunia, Hispania wameendelea kushika namba moja katika orodha hiyo wakifuatiwa na Uholanzi na nafasi ya tatu inashikiliwa na Ujerumani wakati Brazil ipo katika nafasi ya nne.

Argentina inashika nafasi ya tano huku Papua New Guinea ikishika mkia katika nafasi ya 203.

Katika viwango vya Fifa mwaka huu, Tanzania imekuwa ikipanda na kushuka kwani mwezi Januari mwaka jana ilikuwa nafasi ya 108, Februari nafasi ya 108, Machi (109), Aprili na Mei (108), Juni (112), Julai na Agosti (111), Septemba 120, Oktoba 124, Novemba na Desemba ilimaliza nafasi ya 116. Januari 2011 imeanza na nafasi ya 120.

Mwezi Februari mwaka 1995, Tanzania ilishika nafasi ya 65 ambacho ndicho kiwango cha juu kabisa ambacho iliwahi kushika, kiwango cha chini kabisa kwake (Tanzania) kuwahi kushika ni nafasi ya 175 ambapo nafasi hiyo hiyo ilikuwa Oktoba 2005.
 
Simba: TFF inatuvurugia maandalizi Wednesday, 12 January 2011 20:37

Clara Alphonce
KLABU ya Simba imeitikia wito wa Shirikisho la soka nchini (TFF) kwa kuomba kibali cha kucheza mechi mbili za kirafiki dhidi ya Sofapaka ya Kenya na Zesco ya Zambia zinazotarajiwa kufanyika Jumamosi na Jumatatu ijayo.

Juzi, TFF kupitia kwa Katibu Mkuu wake, Angetile Osiah ilitangaza kutozitambua mechi za kimataifa za kirafiki zinazoandaliwa bila ya idhini ya TFF.

Lakini jana msemaji wa klabu ya Simba, Clifford Ndimbo alisema klabu hiyo kupitia kwa Chama cha soka cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) zitaomba kibali cha kucheza mechi hizo kwa ajili ya kujiandaa na mechi zake za kimataifa.

''Sisi tunashangaa kwa nini kauli hiyo imekuja ghafla tena wakati sisi tuna mechi za kimataifa Jumamosi dhidi ya Zesco kwa nini wasingesubiri tumalize michezo yetu ndio watoe tamko hilo kwani kufanya hivyo ni kutaka kutukwamisha tu tusifanye maandalizi ya kutosha,'' alisema Ndimbo.

Ndimbo alisema: "TFF itakuwa haiitakii mema Simba kama haitairuhusu kucheza michezo yake hiyo kwani tayari klabu hiyo imeshaingia gharama za kuzileta timu hizo mbili na kuziharisha wakati huu kungeitia hasara klabu hiyo ya Msimbazi.

''Simba ina michuano migumu mbele yao ya klabu bingwa Afrika tunatakiwa tujiandae kikamilifu na michezo hiyo ni moja ya maandalizi lakini wao tunaona wamekuwa na visababu vingi awali tuliomba watuachie wachezaji wetu waliopo Taifa Stars ambao wameenda katika michuano ya Bonde Nile Misri wakatukatalia tena wanaanza kusema tusicheze mechi za kimataifa mpaka wao watoe kibali kweli hiyo sio haki,'' alisema

Alisema kuwa tayari timu hiyo ya Zesco imeshawasili Dar es Salaam jana mchana kwa ajili ya mechi hiyo pia itakuwa na mchezo mwingine wa kirafiki dhidi ya Yanga, mechi itakayochezwa Jumapili.

 

Simba yalipa kisasi

Imeandikwa na Na Mwandishi Wetu; Tarehe: 13th January 2011 @ 08:46

SIMBA ilifanikiwa kulipa kisasi kwa hasimu wake Yanga baada ya kuichapa mabao 2-0 katika mechi ya fainali ya Kombe la Mapinduzi iliyochezwa kwenye uwanja wa Amaan Zanzibar Jumatano usiku.

Mechi hiyo ilikuwa ni ya kwanza kwa miamba hiyo ya soka nchini kukutana Zanzibar baada ya kupita miaka 19 toka zilipokutana kwenye michuano ya Kombe la Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati (sasa Kagame) na Simba kushinda kwa mabao 5-4 kwa mikwaju ya penati baada ya kumaliza dakika 120 zikiwa sare ya bao 1-1.

Wauaji wa Yanga jana walikuwa ni Mussa Hassan Mgosi aliyefunga bao la kuongoza katika dakika ya 33 kufuatia kazi nzuri ya Mganda Patick Ochan na Shija Mkina aliyefunga bao la pili katika dakika ya 71 kufuatia mpira wa krosi wa Ochan tena.

Mkina aliingia uwanjani katika dakika ya 57 kuchukua nafasi ya Hilary Echesa. Ochan, ambaye jana alionesha kipaji cha hali ya juu alimpenyezea Mgosi pasi aliyekuwa katikati ya ‘msitu' wa mabeki wa Yanga na bila ajizi Mgosi akaujaza mpira wavuni kwa ugoko.

Katika mechi ya Jumatano , Simba ilionekana kuanza vibaya huku ikicheza mpira wa taratibu, tofauti na wenzao wa Yanga walioonekana wako fiti na wenye stamina. Dakika ya 13 Simba ilikosa bao la wazi, baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Yanga lakini kipa mgumu kufungika Yaw Berko aliokoa hatari hiyo haraka.

Dakika chache Ochan alionesha jitihada na kufunga bao, lakini mwamuzi Rama Kibo alikataa akidai alikuwa ameotea. Hata hivyo, Yanga ilikuwa na nafasi nzuri ya kusawazisha bao hilo katika dakika ya 44 kupitia kwa Omega Seme aliyepiga mpira wa adhabu lakini kipa wa Simba Ally Mustapha ‘Barthez' alifanya kazi ya ziada kuokoa mpira huo.

Hali hiyo iliendelea mpaka kipindi cha pili, ambapo timu zilionekana kushambuliana kwa zamu na kucheza mpira wa kasi lakini safu ya ulinzi ya Yanga ilionekana kupwaya ambapo ilitoa nafasi kwa washambuliaji wa Simba kufika langoni wanavyotaka.

Yanga itabidi imshukuru sana kipa wake Berko, kwani alifanya kazi ya ziada kuokoa mipira ya hatari na mabao ya wazi langoni mwake. Kwa ushindi huo, Simba inakuwa imelipa kisasi kwa Yanga kwani mwaka jana ilifungwa mara mbili.

Ilifungwa Agosti kwenye mechi ya ngao ya hisani kwa mikwaju ya penati na ikafungwa bao 1-0 katika mechi ya mzunguko wa kwanza wa ligi kuu kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza Oktoba 2010.
 
Taifa Stars kuwania nafasi ya tano na sita
Wednesday, 12 January 2011 20:35

Clara Alphonce
PAMOJA na kutolewa katika michuano ya Bonde la Mto Nile juzi baada ya kutoka sare ya 1-1 dhidi ya Uganda 'The Cranes', Stars wanaendelea kutanua nchini humo kwa sababu wanatakiwa kucheza mechi ya kutafuta mshindi wa tano na sita.

Taifa Stars iliyotakiwa ishinde mchezo wake dhidi ya Uganda angalau iingie nusu fainali, ilishindwa kufanya hivyo na kulazimisha sare baada ya kujifunga bao dakika chache kabla ya mchezo kumalizika.

Timu hiyo, ilianza vibaya mashindano hayo kwa kupokea kichapo cha mabao 5-1 na wenyeji Misri na kutoka sare ya 1-1 na Burundi na baadaye Uganda.

Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, Boniface Wambura alisema jana kuwa pamoja na kutolewa lakini timu hiyo itaendelea kubaki huko kwa ajili ya mechi yao ya kumsaka mshindi wa tano na sita.

Katika kundi A ambalo ipo Stars, linaongozwa na Misri wenye pointi tisa, wakifuatiwa na Uganda ambao wana pointi nne huku Stars ikiwa na pointi mbili na Burundi pointi moja.

Katika kundi B, DR Congo wamemaliza kinara wa kundi hilo wakiwa na pointi sita wakifuatiwa na Kenya wenye pointi tatu na Sudan ambayo haina pointi.

Kutokana na matokeo hayo timu za Misri, Uganda, DR Congo na Kenya zimefuzu kucheza nusu fainali za mashindano hayo, ambapo Kenya itakutana na Misri kesho na Uganda itacheza na DR Congo.

Kabla ya mechi hizo kuchezwa Tanzania itacheza na Sudan kwa sababu Tanzania ni washindi wa tatu katika kundi A na Sudan ni washindi wa tatu katika kundi B.
 
Mizengwe ya vyeti yatawala uchaguzi MRFA
Wednesday, 12 January 2011 20:32

Juma Mtanda, Morogoro
WADAU wa soka mkoani Morogoro wameliomba Shirikisho la Soka Tanzania, TFF, kuingilia kati suala la uchaguzi mkuu wa Chama cha Soka Mkoa Morogoro, MRFA, kwa kuwa baadhi ya wa waombaji kutokuwa na sifa za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi wa chama hicho utakaofanyika keshokutwa Januari 15.

Sifa hizo kwa mujibu wa katiba ya MRFA kupitia ibara ya 29 ukurasa wa 18 kifungu cha 1 hadi 7 katika ukurasa wa 19 zimeelezwa sifa za wagombea.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hizi mjini hapa, Leonard Massawe na Ferinus Mrope walisema ka nyakati tofauti kuwa sifa za baadhi ya wagombea hazikidhi kuwania nafasi za uongozi MRFA ikiwa ni pamoja na kutokuwa na vyeti halisi vya kidato cha nne na kudaiwa kuwa baadhi yao wakiwa na vyeti vya darasa la saba.

Kwa mujibu wa katiba ya MRFA ibara ya 29, sifa za wagombea kifungu cha pili ukurasa wa 18 katika katiba hiyo inamtaka mgombea kuwa na sifa za kiwango cha elimu ya sekondari kuanzia kidato cha nne na kuendelea.

Nafasi ambazo zinatiliwa shaka na wadau katika uchaguzi huo kwa waombaji hao ni pamoja na mgombea nafasi ya mwenyekiti, katibu mkuu, mwakilishi wa klabu pamoja na wajumbe wa kamati ya utendaji.

Mmoja wa wanaowania uenyekiti, anadaiwa kutowasilisha cheti halisi katika mkutano wa usahili uliofanyika Januari Mosi mwaka huu katika ukumbi wa Masuka Village mjini hapa akiwemo pamoja na mgombea wa nafasi ya katibu mkuu na baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji ambao katika usahili huo baadhi ya wagombea hawakuwasilisha vivuli vya vyeti vyao na kudai kutokana na hilo wameingiwa shaka juu ya waombaji hao katika kuongoza MRFA.

Wadau hao walisema kuwa katika nafasi ya mgombea wa mwakilishi wa klabu kutoka wilaya ya Mahenge anadaiwa kuwa sio mwakilishi halali wa wilaya hiyo licha ya katibu mkuu wa chama cha wilaya kusita kuthibitisha kutambuzi wa mwakilishi huyo wakati akiongea kwa njia ya simu ambapo alidai kuwa taarifa zisizo rasmi alidai anawania nafasi hiyo kutoka klabu ya vijana wilayani humo.

Pia wadau hao walisema kuwa katika nafasi ya wagombea wa kamati ya utendaji, baadhi ya wajumbe hawana vyeti vya kidato cha nne huku wengine wakidaiwa kuwa na vyeti vya darasa la saba.

Wadau hao wametoa ushauri kwa katibu mkuu mpya wa TFF kuweka utaratibu wa kukagua upya vyeti halisi vya wagombea chini ya wataalam kutoka baraza la mitihani Tanzania (NECTA) siku tatu kabla ya uchaguzi na endapo shirikisho hilo hatazingatia ushauri huo wa wadau wa soka mkoani Morogoro watakwenda kuweka pingamizi uchugazi huo kwenye vyombo vya sheria kuzuia uchaguzi huo mpaka taratibu zitakapofuatwa.


 
Azam FC kubakia Mkwakwani
Wednesday, 12 January 2011 20:31

Sosthenes Nyoni
LICHA ya Shirikisho la Soka Tanzania(TFF) kutangaza kuruhusiwa kwa klabu za Dar es Salaam kutumia uwanja wa Taifa, Azam imesema kuwa itaendelea kutumia uwanja wa Mkwakwani hadi pale watakapokaa na kuamua vinginevyo.

Azam ambayo itaanza mzunguko wa pili kwa kuikabili Kagera Sugar keshokutwa, iliondoka jijini Dar es Salaam jana kwenda Tanga tayari kwa mpambano huo utakaofanyika Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Mwenyekiti wa timu hiyo, Said Mohamed alisema kuwa wamesikia kupitia kwenye vyombo vya habari kuhusu kuruhusiwa kutumia Uwanja wa Taifa lakini taarifa rasmi hawajapata hivyo wao wataendelea kutumia Uwanja wa Mkwakwani kama uwanja wao wa nyumbani.

"Labla tu nikwambie kwamba taarifa rasmi kuhusu kuruhusiwa kutumia uwanja wa taifa hatujapata na hata kama tungekuwa tumepata tusingeweza kubadili ratiba haraka haraka we' fikiria Kagera wameshaondoka kwao kwenda Tanga kwa ajili ya mchezo huo halafu ghafla uwaambie waje, Dar es Salaam haitakuwa sahihi.

Mwenyekiti huyo alisema kuwa licha ya kwamba wamegharamia ukarabati wa uwanja huo wenyewe kwao hawatakuwa wamepoteza kitu hata kama wataamu
 
Poulsen awafariji Watanzania

Imeandikwa na Amir Mhando, Cairo; Tarehe: 12th January 2011 @ 23:59 Imesomwa na watu: 201; Jumla ya maoni: 0


01_11_mr3ftz.jpg

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen





KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen amesema kutokuwa makini kuliiangusha timu yake katika michuano ya Bonde la Mto Nile na kushindwa kufuzu nusu fainali.

Lakini amewaomba Watanzania wasikatishwe tamaa na matokeo hayo, kwani bado anajenga kikosi imara kwa ajili ya michuano ya kuwania kufuzu fainali za Afrika mwakani.

Akizungumza jana mjini hapa, Poulsen alisema karibu mechi zote ilizocheza, ni makosa madogo ndiyo yaliyoigharimu timu yake na kwamba hilo watalifanyia kazi.

"Siwezi kusema timu ilicheza vibaya, hapana, tulicheza vizuri ingawa baadhi ya mechi tulicheza vizuri sana dakika za mwisho.

"Nimesikitishwa sana kushindwa kufuzu nusu fainali, lakini ndiyo soka lilivyo na jirani zetu Uganda na Kenya wao wameingia huo ndiyo mchezo ulivyo," alisema kocha huyo raia wa Denmark.

"Timu yetu ni nzuri kuna makosa madogo tukiyafanyia kazi tutafanya vizuri zaidi, naomba tusisikitike sana," alisema.

Alisema mechi ya juzi dhidi ya Uganda, Stars ilifanikiwa kuwamiliki vyema wapinzani wake, lakini tatizo la kukosa umakini hasa katika safu ya ulinzi na pia kushindwa kuzitumia nafasi za
kufunga ilizopata lilikuwa kikwazo.

Naye Nahodha wa Taifa Stars, Shadrack Nsajigwa alieleza kufadhaishwa na matokeo hayo, lakini akisema ndivyo soka lilivyo kuna kushinda, kufungwa na sare.

Stars juzi ilifungana bao 1-1 na Uganda katika mchezo wa mwisho hatua ya makundi, matokeo ambayo yaliipeleka nusu fainali Uganda ikiwa na pointi nne nyuma ya Misri yenye pointi tisa ambayo juzi iliifunga Burundi mabao 3-0.

Stars ni ya tatu ina pointi mbili na Burundi ni ya mwisho ina pointi moja iliyoipata kwa Stars.

Stars katika michuano hii ilifungwa mabao 5-1 na Misri, ikafungana bao 1-1 na Burundi na matokeo kama hayo na Uganda.

Kutokana na kushika nafasi ya tatu Kundi A, Stars kesho itacheza na Sudan ambayo ni ya tatu Kundi B kutafuta mshindi wa tano.

Burundi inabaki kuwa ya saba na timu itakayofungwa kati ya Stars na Sudan itakuwa ya sita, ambazo pia zina zawadi zake.

Nusu fainali inatarajiwa pia kufanyika kesho ambapo Misri itacheza na Kenya iliyoshika nafasi ya pili Kundi B, huku Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo iliyoongoza Kundi B baada ya juzi kuifunga Sudan mabao 2-1 itacheza na Uganda.
 
Tanzania yazidi kudoda Fifa

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 12th January 2011 @ 23:55

TANZANIA imeanza mwaka vibaya baada ya kuporomoka hadi nafasi ya 120 kwenye orodha ya viwango vya ubora vinavyotolewa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Katika orodha hiyo mpya iliyotolewa na Fifa kutoka Zurich, Uswisi jana Tanzania imeporomoka kutoka nafasi ya 116.

Baada ya kujitahidi kupanda kwa nafasi nane duniani na tatu barani Afrika katika nafasi ya 29 mwishoni mwa mwaka jana hali hiyo imebadilika.

Tanzania imepoteza pointi 13 na kujikuta ikishuka kwa nafasi nne duniani.

Kwa mujibu wa Fifa mechi ambazo zilihesabiwa kwenye pointi ni kabla ya ile ambayo Tanzania ililala kwa mabao 5-1 dhidi ya mabingwa wa Afrika Misri, sare ya bao 1-1 na Burundi na Uganda kwenye michuano inayoendelea ya Mto Nile.

Timu ya Taifa ‘Taifa Stars' imetupwa nje ya michuano hiyo kutokana na kukusanya pointi mbili katika mechi tatu.

Viwango vya ubora vya Fifa vinatengenezwa kutokana na matokeo ya mechi ndani ya miaka minne, wakati mechi za karibuni zinakuwa na nafasi zaidi, lakini timu pia zinapata pointi zaidi zinapokutana na timu kubwa na kupata matokeo mazuri.

Taifa Stars mechi inayofuata itakuwa ni ya kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Afrika ya Kati ambayo inashika nafasi ya 112 duniani.

Tanzania imedondoka chini ya nchi 100 bora duniani tangu mwaka 2009 na tangu wakati huo imeshindwa kujinasua na hali imezidi kuwa mbaya.

Katika Kanda ya Afrika Mashariki, Uganda pia imeendelea kushuka ikishika nafasi ya 83 kutoka ya 80 mwezi uliopita ingawa bado wameendelea kuwa vinara wa Kanda wakati Kenya imeshuka kwa nafasi tano hadi ya 125 duniani na 34 Afrika.

Hispania imeendelea kutamba duniani ikiongoza na kufuatiwa na Uholanzi na Ujerumani.

Mabadiliko pekee katika miamba 10 ni Croatia ambao wamepanda hadi nafasi ya 9 na Misri kushuka hadi nafasi ya 10.

China ndio timu ambayo imepanda kwa nafasi kubwa kwa nafasi nane hadi kushika nafasi ya 79 na Qatar wanashika nafasi ya 105 baada ya kupanda kwa nafasi 9.

 
Wanamuziki watakiwa kujiendeleza

Imeandikwa na Evance Ng'ingo; Tarehe: 12th January 2011 @ 23:50 Imesomwa na watu: 27; Jumla ya maoni: 0


01_11_rm19h7.jpg

Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha mafunzo ya muziki cha 'Alphabeta Music Centre', Mark Manji akielezea jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu uzinduzi wa kituo hicho kilichopo Tabata Liwiti, Dar es Salaam jana. Kituo hicho kinatarajiwa kuanza kuendesha mafunzo yake mwanzoni mwa wiki ijayo. (Picha na Fadhili Akida).



WASANII wa Bongo Flava na wanamuziki kwa ujumla wametakiwa kujiendeleza katika fani hiyo hususan katika matumizi ya ala za muziki.

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana Mkurugenzi Mtendaji wa Chuo cha Muziki cha Alphabeta Music kilichopo Tabata, Mark Manji alisema kuwa ili kufanikiwa kimataifa wasanii wanatakiwa kufahamu namna ya kutumia ala za muziki.

Alisema kuwa elimu ya kuandika na kutunga muziki nayo ni muhimu kwa wasanii hususan kipindi hiki ambacho kuna maendeleo ya teknolojia ya muziki.

" Najua kwa sasa wasanii wengi wanabebwa na maproduza ambao wanawatengenezea kila kitu katika studio na kuwapa kwenda kujaribu kuimba bila ya kupata elimu husika ya muziki wenyewe," alisema Manji.

Akizungumzia chuo hicho Manji alisema kuwa kitatoa elimu kwa miezi sita ambapo darasa lake litachukua idadi ya wanafunzi 20.

Alisema kuwa ada itakuwa ni Sh 60,000 kwa mwezi kiasi ambacho alisema kuwa ni kidogo na muombaji anaweza kumudu.

Alisema kuwa anatarajia wanafunzi watakaomaliza katika chuo hicho watatoa msaada mkubwa hususan katika kuendeleza na kuboresha muziki wa Kitanzania.
 
Uzinduzi wa sita kali za THT watia fora


na Khadija Kalili


amka2.gif
UZINDUZI wa albamu sita kali za wasanii wa Nyumba ya kusaka vipaji vya wasanii wachanga Tanzania ‘Tanzania House Of Talent' (THT), uliofanyika katika mkesha wa sikukuu ya miaka 47 ya Mapinduzi ya Zanzibar umetia fora kutokana na namna vijana walivyokonga nyoyo za mashabiki waliojitokeza katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Tanzania Daima ambayo ilikuwepo katika ukumbi huo na kushuhudia wasanii wake wakitia fora ambao ni Mwasiti, Mataluma, Barnaba, Amini, Linah na Dito wote kwa umoja wao wameonyesha jinsi walivyo mahiri na wameiva katika tasnia ya sanaa baada ya kupikwa na walimu wao.
Wasanii walioweza kuamsha hisia katika nyimbo zao ni pamoja na Mataluma aliyebamba na ngoma yake ya Kariakoo, huku Mwasiti ikivuta hisia za mashabiki kwa wimbo wa Nalivua pendo na Siyo kisa Pombe.
Ukiacha Mwasiti, naye Dito aliwashika mashabiki sambamba na Barnaba akizidi kuonogesha tukio hilo. Kama hiyo haitoshi naye mwana dada Linah alikimbiza na ngoma yake ya ‘Bora nikimbie', wimbo ambao unazungumzia kadhia ya mapenzi, ambapo katika wimbo unawakilisha kilio cha mwanamke ambaye baada ya kuoma mambo yanakuwa magumu kwa mpenziwe kutokana na vipigo, ulevi na karaha mbalimbali kutoka kwa mpenzi wake, anaona bora akimbie huku akisema: "Kama mapenzi ndiyo haya naona bora nikimbie nimechoshwa na vituko na vipigo, majeraha kila siku mpenzi wangu kwa nini hunithamini".
Aidha, Mratibu wa tamasha hilo la kihistoria, Kemmy Mutahaba, ambaye pia ni Msemaji wa THT, alitoa shukrani kwa vyombo vya habari, mashabiki na waliojitokeza kwa wingi kujionea kazi za nyumba hiyo iliyoanzishwa miaka mitano uliyopita.
Wasanii wengine walionogesha kwa kutoa burudani ni pamoja na bendi ya Odama, Banana Zorro, Marlaw, Maunda Zorro, Pipi na Wanenguaji wa THT.
 
BASATA walia na makandarasi wa JKT


na Makuburi Ally


amka2.gif
BARAZA la Sanaa la Taifa (BASATA) limewataka makandarasi wanaojenga ukumbi wa sanaa wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ulioko karibu na ofisi za baraza hilo Ilala, jijini Dar es Salaam kufanikisha ujenzi huo wa ukumbi huo kwa haraka ndani ya mwaka huu la sivyo wataingiza vifaa vyao hata kama haujamalizika.
Akizungumza katika hafla ya kuukaribisha mwaka 2011 iliyofanyika juzi katika ofisi za Basata, Katibu Mtendaji wa BASATA, Ghonche Materego, alisema wamepania mwaka huu sanaa kutamkwa katika maneno mengine tofauti na ilivyokuwa miaka iliyopita ambako sanaa ilikuwa ni kiburudisho pekee.
Materego alisema mwaka huu wasanii na wadau wakiunganisha nguvu kwa pamoja na sanaa italeta ajira, kukuza kipato cha msanii mmoja mmoja na kuongeza pato la Taifa.
Aidha, Materego alisema Basata kwa kushirikiana na Mashirikisho manne wataandaa mipango ya kuwawezesha wasanii ili wafaidike na kazi zao ambako alitoa wito kwa wasanii kupitia mashirikisho kuandaa takwimu sahihi kama wanavyofanya waandaaji wa Tamasha la Sauti za Busara, ambalo mwaka huu limeongeza pato la taifa kwa asilimia 400 kutokana na ukusanyaji wa takwimu zao.
Materego alisema wasanii na mashirikisho wakijipanga sawasawa watayashinda matamasha ya Sauti za Busara na Mwaka Mkoge yanayoandaliwa visiwani Zanzibar ambako kwa kuanzia wamejipanga kuandaa tamasha la siku ya msanii ambalo kilele chake kutakuwa na matukio mbalimbali ya kazi za sanaa.
Katika hafla hiyo, wafanyakazi wa Basata walionyesha matukio kadhaa ya sanaa ikiwemo kwaya, mazingaombwe na kucheza muziki ambako pia viongozi wa viongozi wa mashirikisho walitoa salamu zao za mwaka mpya kwa kuahidi kuwa bega kwa bega na Basata katika kusaka maendeleo ya wasanii.
 
Mpoto kuonyesha ‘Shangwe za Mwafrika' Mzalendo Pub


na Andrew Chale


amka2.gif
MSANII nguli wa kughani mashahiri ya kuteka hisia za watu wengi nchini, Mrisho Mpoto, leo anatarajia kuwasha moto na bendi yake ya Mjomba ndani ya ukumbi wa Mzalendo Pub uliopo Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mpoto alisema atafanya mambo makubwa ndani ya ukumbi huo na kutoa tamko kuwa kila Alhamisi atakuwa akifanya onyesho lake ndani ya ukumbi huo na itajulikana kama Shangwe za Mwafrika ambapo nyimbo mbalimbali zitapigwa.
Mpoto alisema wamejiandaa vya kutosha ili kutoa burudani ndani ya ukumbi huo kila Alhamisi huku kukiwa na kitu cha pekee ambacho alikipa jina la ‘Hoja ya Mlevi'.
"Nimejiandaa vya kutosha kwa wadau wa burudani watafurahia na kukonga nyoyo zao, njooni kushuhudia shangwe za Mwafrika, nikiwa na wasanii wakali wakiwamo walioshiriki Tusker Project Fame," alisema Mpoto.
Wasanii hao ni pamoja na Sabrina John, Ismail Kipira, Brian, Shaaban, Vasmo, Aneth Kushaba mshiriki wa ‘Tusker Project Fame' na wengineo ambao watalishambulia jukwaa.
Aidha, Mpoto alisema uzinduzi huo utaudhuriwa na wadau mbalimbali wa burudani wakiwemo wanamuziki na wasanii nyota wa filamu sambamba na wafanyabiashara na mabalozi huku kiingilio kikiwa sh 5,000.
Mbali ya kukonga shoo, pia alisema kutakuwa na dakika 20 za mjadala na wa wadau ambao watachangia mada kuhusu kibao cha Hoja ya mlevi.
"Hoja ya mlevi, watu watapata kuchangia masuala yanayotugusa katika jamii, hivyo ‘surprise' ya kesho (leo) tutajadili juu ya tatizo la umeme na tukio la Arusha, ambapo kisha nitayatungia mashairi na nitaimba hapo hapo kila wiki na mengine," alisema Mpoto.
Mpoto anatamba na vibao mbalimbali kikiwamo cha ‘Mjomba', ‘Nikipata nauli', ‘Adela' na vingine vingi huku vingine akiimba kwa kutumia mashairi ya papo hapo.



h.sep3.gif

 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom