Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Manchester United are crying out for a player like Spurs' Luka Modric

The elusive little Croatian showed the artful touches and nimble footwork that Sir Alex Ferguson's side are lacking


  • Luka-Modric--Nani-Tottenh-007.jpg
    Even in a cramped midfield against Manchester United the quality of Luka Modric shone through. Photograph: Matthew Peters/Manchester Utd via Getty Images Sir Alex Ferguson always wanted to know one thing from Harry Redknapp when his old friend was in charge at West Ham United. "How's Joe?" the Manchester United manager would ask. As in Joe Cole, who, at the time, was the hottest young talent in English football. Ferguson was not the only one to inquire about Cole and Redknapp used to enjoy throwing a protective arm around the prodigy.
    It is not difficult to imagine what Ferguson asks Redknapp about these days. He went on record before this visit to Tottenham Hotspur to admit that Gareth Bale was the one that had got away from him. Ferguson made what he described as a "good offer" to Southampton four years ago only to be rebuffed. Tottenham's capture of the Welsh flier looks a sounder investment with each passing week.
    Yet Bale is not the only Tottenham player who Ferguson might close his eyes and imagine in a red shirt. Luka Modric looked every inch the United player here, from the sureness of his touch to the way that he sought to impose his class upon proceedings. Redknapp's pre-match comment reverberated. "We have a few players here that Alex would love to have in his team," he said.
    In a helter-skelter first half, Modric produced a fistful of moments that cut through the tumult to advertise his quality. There was nothing better than the sharpness of his turn in the ninth minute, his low centre of gravity seeming to give him magnetic properties, and the subsequent ball out to Alan Hutton, whose cross might have been tucked away by Peter Crouch. The home crowd chorused Modric's name.
    Although this was not a game for the creative talents – witness Wayne Rooney's perspiration, rather than inspiration – Modric consistently demanded the ball. The intelligence of his darting runs and the smoothness of his technique were so easy on the eye and he did not need Wilson Palacios, all heavy touches and misplaced passes alongside him, to look good.
    The Croat can make opponents seem foolish with a drop of his shoulder. Darren Fletcher might attest to that after Modric left him trailing along the byline following a short corner routine, yet he is no mere jinking trickster. Despite his small frame he has plenty of strength and is not easily knocked off the ball. His intuitive grasp of the angles of a game and where to position his body ensures he rarely loses possession.
    Modric has settled into the role of the deep-lying playmaker since Rafael van der Vaart's arrival at Spurs and the position feels tailor-made for his vision, the clever weight of his pass and his ability to set the tempo. As Tottenham stepped on to the front foot in the second half, particularly after Rafael da Silva's sending-off, it was Modric who waved the baton. He did not neglect his defensive duties, though, as one timely interception from a Rooney cross on 67 minutes showed.
    United's supporters have wondered this season whether there is sufficient creativity in the centre of their midfield and Ferguson would surely relish the opportunity to work with Modric. There was interest expressed from Old Trafford at the end of last season but, happily for Tottenham, Modric, who signed a new six‑year contract in the summer, feels a debt of loyalty to them.
    He is grateful that they took such an expensive chance on a player from the Croatian league and, with Chelsea having also shot covetous glances at him, has simply put his head down and channelled all of his energies into repaying Tottenham. This was the latest instalment. Nemanja Vidic might have had an argument and, frankly, nobody would choose to argue with the United captain, a totem in central defence, but Modric deserved the man-of-the-match champagne.
    Tottenham had entered the game full of confidence that they could end a winless streak against United that had stretched 10 years and 23 matches in all competitions. Certainly, they fear nobody on their own turf. But United kept them largely at arm's length – it was hard to recall Edwin van der Sar making a save – and, after a pulsating start, the game gradually took on the characteristics of a stalemate.
    Tottenham remain in fifth and their grand statement of intent did not materialise. They had to content themselves with an individual one from the little man with the No14 on his back.
 
Kuwaona Yanga, Wabrazil 5,000/-


Na Elizabeth Mayemba

WAANDAAJI wa mechi za kirafiki za kimataifa kati ya timu ya Atletico Paranaence ya Brazil na Yanga, wametangaza viingilio kwamba vitakuwa sh. 200,000 kwa VIP A na cha chini sh. 5,000.Viingilio hivyo ambavyo viliwahi
kutumika katika mechi ya kirafiki kati ya Taifa Stars na timu ya taifa ya Brazil, pia vitatumika keshokutwa kati ya Simba na Wabrazil hao.

Akitangaza viingilio hivyo jana, Mkurugenzi Mtendaji wa Klabu ya African Lyon ambayo ndiyo waliyoileta timu hiyo, Nabil Alkharous alisema viingilio vingine kwa jukwaa la VIP B ni sh. 100,000, VIP C sh. 50,000, orange sh. 20,000, nyuma ya magoli sh. 10,000 na viti vya bluu sh.5,000.

"Tunaimani viingilio hivyo vimeendana na mechi yenyewe na pia kila shabiki atapata nafasi ya kufika uwanjani kwa kuwa kiingilio cha chini kabisa tumeweka sh. 5,000 ambacho mashabiki wengi watamudu," alisema Alkharous.

Akizungumzia mchezo wa leo Kocha Mkuu wa Yanga, Kostadin Papic alisema wamejiandaa vizuri japo kuwa timu yake inakabiliwa na majeruhi wengi.

"Pamoja na kwamba kikosi changu kinamajeruhi wengi, nitaingiza timu yangu uwanjani kwa kuwa mchezo huu ni muhimu kwa sisi tunaojiandaa na michuano ya kimataifa," alisema Papic.

Alisema endapo wachezaji wake waliopo kwenye timu ya taifa 'Taifa Stars' waliopo Misri kwenye michuano ya Bonde la Mto Nile watawahi kurudi nchini wataungana na wenzao.

Naye kocha wa Simba, Patrick Phiri aliwapongeza waliodhamini ziara ya timu hiyo na kwamba wachezaji wake watatumia mchezo huo kupata uzoefu katika michuano inayowakabili."Ni kipimo kizuri kwetu na tunawapongeza sana wenzetu wa African Lyon, kutuletea timu hii ambayo itatusaidia katika maandalizi ya michuano inayotukabili," alisema Phiri.

Timu hiyo iliwasili nchini mwishoni mwa wiki kwa ziara ya michezo miwili ya kirafiki.
 
Kocha Micho aichambua Taifa Stars


Na Mwandishi Wetu, Cairo

KOCHA wa zamani wa Yanga, Sredojevic Milutin 'Micho', amesema ni vyema Watanzania wakampa muda Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Jan Poulsen ili aijenge timu, kwani namna alivyoiona kuna kazi kubwa inahitajika ili ilete
matunda mazuri.

Alisema ni vigumu kuamini namna Taifa Stars, inavyocheza kama ilikuwa na kocha mmoja kwa miaka minne, badala yake inaonekana ni timu mpya na yenye kocha anayeanza moja kufundisha, hivyo matunda yake yatachelewa kuonekana.

Alitoa kauli hiyo juzi mjini hapa, baada ya kumalizika mchezo wa kuwania nafasi ya tano kati ya Taifa Stars na Sudani katika michuano ya soka Nchi za Bonde la Mto Nile, Uwanja wa Al Salam na Stars kulala mabao 2-0 yote yakifungwa kipindi cha pili.

Micho ambaye kwa sasa ni Kocha Mkuu wa El Hilal ya Sudan, hakumtaja kwa jina lakini kocha aliyekuwa kabla ya Poulsen ni Mbrazil Marcio Maximo, aliyefika Tanzania Julai 2006 na kuondoka Julai 2010 na Poulsen raia wa Denmark alirithi mikoba Agosti mwaka jana na amesaini mkataba wa miaka miwili.

Desemba mwaka jana Poulsen, aliiongoza timu ya taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' kutwaa Kombe la Chalenji.

"Niwe mkweli katika hili, Tanzania ina safari ndefu sana kufikia kwenye mafanikio, Watanzania ni marafiki zangu, nimeishi nao vizuri, mpaka kesho nikienda wananipokea vizuri, lakini timu yao inahitaji muda sana kujengwa, wampe muda mwalimu ni kocha mzuri na ana uzoefu wa kutosha atawasaidia," alisema.

Alisema Stars sasa ndiyo inaanza kujengwa upya, inaonekana si timu ya ushindani na haioneshi kama kweli ilikuwa na kocha mmoja kwa miaka minne mfululizo, badala yake kinachoonekana ni timu mpya na kocha mpya anaanza kuijenga.

Micho yupo mjini Cairo na El Hilal iliyoweka kambi kujiandaa na michuano ya kimataifa na alisisitiza hasemi kocha aliyekuwepo Stars kabla ya Poulsen ni mbaya, lakini Stars haionekani kama ilikuwa ikinolewa na kocha mmoja kwa miaka minne.

Michuano ya soka Nchi za Bonde za Bonde la Mto Nile ilitarajiwa kumalizika jana usiku kwa mchezo wa fainali kati ya wenyeji Misri na Uganda, ambapo Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) zenyewe zilicheza kuwania mshindi wa tatu. Burundi imeshika nafasi ya saba kati ya timu saba.

Wakati huo huo, Poulsen akizungumza juzi baada ya vijana wake kufungwa mabao 2-0 alisema kuna makosa waliyafanya sehemu ya ulinzi na ndiyo yaliiangusha timu yake na kuruhusu mabao kipindi cha pili.

Hata hivyo alisema soka ndivyo lilivyo, lakini hakuwa tayari kuzungumzia kwa ujumla kufanya vibaya kwa timu katika michuano hiyo, au kitu gani ilichopata kiufundi na kusema atafanya hivyo akishafika Dar es Salaam na kujipanga vizuri.

Timu itaondoka Cairo leo saa tano usiku na inatarajiwa kufika Dar es Salaam saa 11 jioni, ikiwa imeshika nafasi ya sita kati ya timu saba zilizoshiriki michuano hiyo, ambayo bingwa amejinyakulia zaidi ya sh. milioni 200 za Tanzania, wa pili zaidi ya sh.
milioni 170 za Tanzania na wa tatu zaidi ya sh. milioni 130 za Tanzania.
 
Tenga kupasua jipu la waamuzi wa FIFA


Na Zahoro Mlanzi

RAIS wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodegar Tenga leo anatarajia kukata mzizi wa fitina kwa kuelezea kilichojiri katika sakata la waamuzi waliopewa beji za Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA), kinyume na
taratibu.

Shirikisho hilo liliingia katika kashfa hiyo, baada ya kudaiwa kupeleka majina ya waamuzi tofauti na yale yaliyowasilishwa na Kamati ya Waamuzi nchini huku yaliyostahili yakikatwa.

Waamuzi wanaodaiwa kuingizwa na TFF kinyemela ni Oden Mbaga, Hamis Chang'walu, Jesse Erasmo na Israel Nkongo.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa shirikisho hilo, Boniface Wambura wakati akitangaza waamuzi watakaocheza michuano ya Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho, alisema Rais Tenga atalitolea ufafanuzi suala hilo leo.

"Siwezi kulizungumzia suala hilo ila hilo ni moja ya ajenda ya Rais Tenga atakapozungumza na vyombo vya habari kesho (leo), kila kitu kitakuwa wazi lakini CAF (Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika) ndiyo waliowachagua si sisi," alisema Wambura.

Wambura aliwataja waamuzi watakaochezesha michuano hiyo kuwa Waziri Sheha, Kombo Ali na Samuel Mpenzu ambao watachezesha mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya SOFAPAKA ya Kenya dhidi ya AS Aviacao ya Angola, utakaopigwa kati ya Februali 11, 12 na 13 nchini Kenya.

Alisema Waamuzi Mbaga, Chang'walu na John Kanyenye watachezesha mechi ya Klabu Bingwa Afrika kati ya Young Buffaloes ya Swaziland na St. Michael United ya Shelisheli na Hafidh Ali ameteuliwa kuwa Kamishna wa mechi ya Klabu Bingwa Afrika kati ya ZESCO United ya Zambia na Desportiva Muculmana ya Msumbiji.

Wambura aliongeza kuwa waamuzi Ramadhan Kibo na Nkongo wameteuliwa kuwa waamuzi wa akiba kwenye mechi ya Kombe la Shirikisho kati ya KMKM ya Zanzibar na DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC).
 
Mtemvu aipiga 'tafu' KEMWADEFO


Na Mwandishi Wetu

MBUNGE wa Jimbo wa Temeke, Abbas Mtemvu ametoa sh. 500,000 kwa ajili ya taasisi ya Keko Mwanga Development Foundation (KEMWADEFO), zitakazotumika kuendesha mashindano ya kumuenzi muasisi wa michezo katika
Kata ya Keko, Dar es Salaam Miraji Salum 'Kizoka'.

Akizungumza katika uzinduzi wa mashindano hayo kwenye viwanja vya Sigara, Dar es Salaam juzi, Mtemvu alisema michezo ndiyo njia ya pekee ya kuwafanya vijana kuepuka vishawishi na kujenga miili yao.

Katika uzinduzi wa mashindano hayo ambayo yatashirikisha timu 10 za Keko Mwanga, timu ya Veterani ya KEMWADEFO ilifungwa mabao 4-0 na timu ya Waandishi wa habari za Michezo (TASWA).

Mbali ya jitihada za mabeki wa KEMWADEFO, Francis Julius, Henry Nindi na Rashid Kamanyola kujitahidi kuwalinda washambuliaji wa TASWA ilijikuta inafungwa la kwanza na Mohamed Akida, dakika ya tisa baada ya kupokea pasi ndefu ya Sultani Sikilo.

Bao la pili la TASWA, lilifungwa na Julius Kihamba dakika ya 23 aliyeunganisha pasi ya Majuto Omari na bao la tatu lilifungwa na Kihampa tena kabla ya Majuto kufunga bao la nne dakika ya 54.

Mechi ya kwanza ya ufunguzi wa mashindano hayo, ilizikutanisha timu za Eleven Fighter na Bad Boys katika pambano kali lililokuwa kivutio kwa mashabiki wa soka waliohudhuria.

Pamoja ya ufundi wa kusakata soka ulioneshwa na timu hizo, Eleven Fighter ilishinda mabao 2-0 huku bao la kwanza likifungwa na Dini Dadi dakika ya 26 kwa mpira wa adhabu na bao la pili lilifungwa na Salum Taratibu dakika ya 70 aliyeunganisha pasi ya Januari Augustino.

 
Everton yakubali Pienaar kwenda Chelsea


LONDON, England

KOCHA wa Everton, David Moyes amesema kuwa wamepokea ofa kutoka kwa Chelsea kuhusu kiungo wao, Steven Pienaar ikiwa ni baada ya kukataa ofa kutoka kwa Tottenham.Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28, raia wa
Afrika Kusini alikuwa nje ya kikosi kilichotoka sare ya mabao 2-2 na Liverpool Jumapili iliyopita na Moyes, alikaririwa akisema kichwa chake kilikuwa si kizuri kwa kucheza.

Pienaar anatarajiwa kuwa nje ya mkataba mwishoni mwa msimu huu na Chelsea inasadikika kurusha ndoana ya pauni milioni 3, ili kumnasa mchezaji huyo.

Mchezaji huyo wa zamani wa Ajax alijiunga na Everton mwaka 2007 akitokea Borussia Dortmund kwa kitita cha pauni milioni 2.

"Pienaar bado hajafikia makubaliano na Chelsea," alisema Moyes. "Ila tumeshamkabidhi mwakilishi wa kufanya mazungumzo na Chelsea. "Ila hatukumruhusu kufanya mazungumzo na Tottenham kwa sababu hawakutoa kiasi cha fedha kama hicho," aliongeza na akasema endapo Tottenham watatia kiasi kama hicho, wanaweza kubadili msimamo vinginevyo wataingia makubaliano na Chelsea.

Hata hivyo akizungumza baada ya timu yake kutoka sare ya mabao 2-2 na Manchester United, kocha wa Spurs, Harry Redknapp alieleza kuwa klabu hiyo ya White Hart Lane inavyoelekea haina mpango wa kutoa kiasi kama cha Chelsea kwa ajili ya nyota huyo wa Afrika Kusini.

Msimu uliopita, Pienaar alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa klabu lakini msimu huu hakuweza kufikia kwenye kiwango kama cha mwaka jana na mapema msimu huu, Moyes alisema kuwa mchezaji huyo amekataa kusaini mkataba mpya.

 
Kuziona Yanga, Atletico Shs.200,000-50000
Monday, 17 January 2011 20:02

phiri%20and%20papic.jpg
Vicky Kimaro
KWA mara ya kwanza katika historia mashabiki wa klabu za Yanga na Simba watalazimika kulipa shilingi 200,000 ili kuzishudia timu hizo zikicheza na Atletico Paranaense ya Brazil kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Miamba hiyo ya Brazil itaanza ziara yake leo kwa kucheza dhidi ya Yanga mchezo utakaochezwa majira ya saa kumi na moja jioni kabla ya kupimana na Simba keshokutwa Januari 20 kwenye uwanja huo.

Akitangaza viiingilio hivyo Mkurugenzi wa African Lyon wenyeji wa Atletico, Nabil Al Kharoos alisema VIP A kingilio ni shilingi 200,000 wakati VIP B kingilio ni shilingi 100,000 huku VIP C kingilio kikipangwa shilingi 50,000.

Kwa upande wa viti vya rangi ya Machungwa kingilio ni shilingi 20,000 wakati viti vya kijani shilingi 10,000 na kwa viti vya juu kabisa ya uwanja shilingi 5,000.

Viingilio hivyo vinafananishwa na vile ambavyo TFF ilitangaza kwenye mchezo wa kirafiki baina ya Taifa Stars dhidi ya Brazil iliyojaa nyota wengi kama Kaka, Robinho na wengine wengi mwezi Juni mwaka jana, lakini mashabiki walijitokeza wachache.

Na kusababisha mjadara mzito wa shutuma kwa TFF kwamba haiwajali mashabiki wa soka na walipanga kuwanyima kutazama mchezo huo wa kihistoria dhidi ya Brazil. Ni ajabu, sijui kwa sababu ni Brazil, kiasi hicho cha kiingilio hakijawahi kutokea nchini kinatukatisha tamaa mashabiki tuliokuwa na hamu ya kutazama mchezo huo.

Wakizungumza kwenye mkutano huo kocha wa Yanga, Kostadin Papic alisema "Nawashukuru wadhamini wa mechi, imekuja wakati muafaka tukiwa tunahitaji timu imara ya kupimana nazo kabla ya mashindano yetu, Atletico nahifahamu ni timu nzuri."

"Kikosi changu kina majeruhi wengi, lakini nitaingiza timu na ninaamini nitafanya vizuri, sahauni kuhusu Kombe la Mapinduzi,"alisema Papic

Naye kocha wa Simba, Patrick Phiri aliwashukuru waratibu wa mchezo huo na kusema "Kila mtu anajua mpira ulivyo na ulipoanzia, tunachoangalia ni mechi yetu ya keshokutwa, nafurahi wachezaji wangu kupata nafasi ya kucheza na timu kutoka Brazil, ni timu nzuri naamini itasaidia kutupa uzoefu zaidi," alisema Phiri.

Atletico Paranaense inashika nafasi ya tano kwenye Ligi Kuu ya Brazil.
Mbali na mechi hizo pia kutakuwa na mchezo wa bahati nasibu kwa wale ambao watanunua tiketi kipindi cha mapumziko itachezeshwa droo maalum na zawadi kama Pikipiki, Friji na vitu vingine zitatolewa kwa washindi ikiwa ni pamoja na burudani kutoka kwa wasanii ambao hata hivyo hawakuwaweka hadharani.
 
Makocha walia uteuzi Poulsen Monday, 17 January 2011 19:55 Jessca Nangawe
BAADA ya Taifa Stars kufanya vibaya kwenye michuano ya Bonde la Mto Nile makocha wazalendo wametupia lawama Mdenmark Jan Poulsen kwa kushindwa kuteua vijana kwa ajili ya michuano hiyo.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti makocha hao walisema kitendo cha kocha huyo kuendelea kutumia wachezaji 'profesheno' na kuwaacha wale chipukizi kunaendelea kuua soka la Tanzania, sasa wakati umefika wa kufanya mabadiliko kama ilivyo kwa nchi za wenzetu.

Kocha msaidizi wa Yanga, Felix Minziro alisema Poulsen hakuwa na haja ya kuwaita wachezaji wa kulipwa na badala yake angewatumia wachezaji vijana walionyesha uwezo mkubwa katika michuano ya Chalenji pamoja na Ligi Kuu.

"Mchezaji kama Said Maulid hakuwa na sababu ya kuitwa amerudi hapa nyumbani muda mrefu kwa ajili ya mapumziko hivyo hakuwa na mazoezi yoyote," alisema Minziro na kuongeza iweje waachwe kina Mwinyi Kazimoto na wengine ambao bado wachanga huku anaendelea kutumia wachezaji wale wale tuliowazoea? sidhani kama ni sahihi sana."

Naye mchezaji wa zamani wa Yanga na kocha wa Polisi Dodoma, Sekilojo Chambua alisema kufanya vibaya pia kunachangiwa na misingi duni na utayarishaji mbovu wa timu sambamba na kutowapa nafasi wachezaji chipukizi kwa kiasi kikubwa inachangia kushindwa kwa timu.

"Wachezaji wetu wamekuwa na tatizo moja kubwa la kujisahau, wakifanya vizuri kidogo wanaona wamefika, lakini baya zaidi sisi wenyewe ndio wachawi katika hili hatuna misingi imara, vijana wengi wazuri naamini wangefanya vizuri zaidi, angalia wenzetu wamekuwa wakiwapa nafasi wachezaji chipukizi ndio sababu wanafika mbali."

Kwa upande wa kocha wa timu ya Taifa ya wanawake, Bonifase Mkwasa alisisitiza kwa tatizo kubwa ni kuendelea kutumia wachezaji wakongwe na kutowaamini vijana.

Alisema kocha anapaswa kutazama kwa mapana wachezaji na kuangali vijana kutoka katika klabu za ligi kuu wenye uwezo na kuachana na kasumba ya kuendelea kutumia wachezaji ambao wamekua wakishiriki kila mwaka bila manufaa yoyote.
 
Tisa bora Tanga
Monday, 17 January 2011 19:54

Salome Milinga
SHIRIKISHO la Soka nchini TFF, limeuteua jiji la Tanga kuwa kituo cha fainali za hatua yaTisa Bora ya Ligi Daraja la Kwanza Tanzania bara zinazotarajia kuanza kutimua vumbi Januari 30.

Akizungumza na wanahabari kwenye ofisi za shirikisho hilo jana jijini Dar es Salaam afisa habari wa TFF, Boniface Wambura alisema baada ya TFF kutangaza mkoa ambao ungependa kuandaa fainali hizo lazima uwe na kiasi cha Sh 20 milioni na kushindikana ndipo kamati ya utendaji ikaamua kukutana jana na kujadili ajenda mbalimbali zilizowakilishwa nbele yake ikiwemo ya fainali hizo.

"Kamati ya utendaji ya mashindano ya TFF iliyokaa jana chini ya uenyekiti wa Rais Leodegar Tenga ili fanya uamuzi wake kuwa fainali za Ligi Daraja la Kwanza hatua ya Tisa Bora zitafanyika kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga," alisema Wambura.

Timu zilizofuzu kucheza hatua hiyo ni Tanzania Prisons ( Mbeya), Coastal Union (Tanga), Morani FC (Manyara), Rhino Rangers (Tabora), Polisi Morogoro(Morogoro), JKT Oljoro (Arusha), Villa Squad, Temeke United na Moro United zote za jijini Dar es Salaam.

Wakati huo huo; Wambura alisema kuwa mkutano wa mwaka wa TFF umepangwa kufanyika Machi 26 na 27 jijini Dar es Salaam.

"Taarifa za mkutano huu kwa wanachama zinaandaliwa, wajumbe wa mkutano huo ni vyama vya mkoa, vyama shirikishi na klabu 12 za Ligi Kuu ya Vodacom," alisema Wambura.
 
Uchafu Uwanja wa Ndani Taifa: Maisha ya wachezaji, mashabiki wa RBA hatarini Monday, 17 January 2011 19:53

Sosthenes Nyoni
WACHEZAJI na wapenzi wa mpira wa kikapu wanaohudhuria michuano ya ligi ya mkoa wa Dar es Salaam (RBA) inayochezwa Uwanja wa Ndani wa Taifa wapo hatarini kupata magonjwa ya kuambukizwa kama kipindupindu na kifua kikuu endapo mamlaka inayohusika haitafanyia ukarabati miundombinu ya uwanja huo haraka.

Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kuwa uwanja huo mkongwe hauna hewa ya kutosha, mfumo wa maji umekufa na pia hakuna umeme hali inahatarisha afya za wachezaji na wapenzi wanaohudhuria hapo.

Pia, mbali ya kukosa maji na umeme, vyoo vilivyoko uwanjani hapo vimefurika kinyesi na mikojo huku vingine vikionekana kufungwa na hivyo kusababisha baadhi ya wachezaji na wapenzi wanaofika hapo kutoka nje kwenda kujisaidia vichakani.

Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti baadhi ya wachezaji walisema kuwa wamelalamikia suala hilo siku nyingine, lakini hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.

"Tumelalamika wee hakuna anayekusikiliza imefikia wakati tumeacha tu ni bora ufungwe tu hii ni hatari, tumeshasahau kitu kinachoitwa maji hapa, umeme nao ndio hivyo hakuna pia joto ndio usiseme tunaomba wahusika warekebishe hali hii haraka,"alisema Frank Augustine mchezaji wa timu ya ABC.

Naye mchezaji Nina Mliga wa timu ya Lady Lioness alisema kuwa ni dhairi afya zao ziko hatarini kutokana na kukithiri kwa uchafu kunakotokana na duni katika uwanja huo.

Juhudi za Mwanachi kumtafuta mkurugenzi wa michezo Leonard Thadeo ili azungumzie suala hilo hazikuzaa matunda, lakini chanzo cha habari cha kuaminika kutoka ndani ya Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo ambacho hakikutaka kutajwa jina kwa madai si msemaji kililiambia Mwananchi kuwa uwanja huo hauwezi kufanyiwa ukarabati badala yake utavunjwa na kujengwa mwingine wa kisasa ukiwa ni sehemu wa mradi wa eneo Changamani.
 
SPUTANZA waanzisha mfuko wa wagonjwa Monday, 17 January 2011 19:52

Sweetbert Lukonge
UONGOZI wa Chama cha Wachezaji Soka Tanzania (Suptanza) umeanza kutekeleza mkakati wake kuhakikisha unakuwa na mfuko maalum utakaokuwa ukikisaidia chama hicho kukabiliana na matatizo mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwasaidia wanachama wake wagonjwa.

Akizungumza na Mwananchi jana, Katibu Msaidizi wa chama hicho, Abeid Kasabalala alisema kuwa ili mkakati huo uweze kufanikiwa kwa kiwango kikubwa wanachama wote wa chama hicho watakakiwa kushirikiana kwa karibu zaidi ikiwa ni pamoja na kulipa ada ya uanachama katika muda muhafaka.

"Tupo katika mchakato huo kwani kuna mambo mengi ambayo kwa hakika tumekuwa tukishindwa kuyataekereza kutokana na kutokuwa na sehemu ya kukimbilia.

"Hivyo kutoka na hali hiyo imetubidi kuhakikisha tunaanza mara moja mchakato wa kutekeleza mikakati yetu ya mwaka 2011 ikiwa ni pamoja na zoezi hilo kuimarisha mfuko wetu ili tuweze kukabiliana na matatizo mbalimbali yanatukabili," alisema Kasabalala.

Alisema kutokana na hali ya ukata ndani ya chama hicho wameshindwa hata kuwa na kutoa fungu maalu kwa ajili ya kuwasidia wanachama wake ambao wanasumbuliwa na maradhi mbalimbali zaidi ya kuanza tena kuandaa utaratibu wa kuwaomba wadau na wapenzi wa michezo nchini ili kuwasaidia.
 
DRFA yaonja jeuri ya Yanga
Monday, 17 January 2011 12:24

Sosthenes Nyoni
TIMU ya Yanga jana ilirejesha historia yake ya kugoma kucheza mechi katika dakika za mwisho baada ya kukataa kuwavaa mabingwa wa Zambia, Zesco mchezo ulipangwa kufanyika jana kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Zesco ambayo iliwasili wiki iliyopita nchini kwa ziara maalumu ya kimichezo kwa mwaliko wa Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam(DRFA), ilitarajia kucheza mpambano huo ikiwa ni siku moja baada kuichabanga Simba mabao 2-1 kwenye uwanja wa Uhuru.

Hata hivyo Yanga ambayo mwaka 2008 iligomea mechi ya kutafuta mshindi wa tatu ya Kombe la Michuano ya Kagame dhidi ya Simba baada ya kuingia mitini dakika za mwisho kwa kisingizo cha kushindwa kuelewana na Cecafa juu ya malipo yao yatayotokana na viingilio.

Haikuweza kucheza mpambano wao dhidi ya Zesco kwa madai kocha wa timu hiyo Kostadin Papic alikataa kupeleka kikosi chake uwanjani baada ya baadhi ya wachezaji wake kuwa majeruhi.

Mratibu wa ziara ya timu hiyo, George Wakuganda alisema jana kuwa wamesikitishwa sana na kitendo cha Yanga kukataa kucheza mchezo huo dakika za mwisho.

"Tumesikitishwa sana huu sio ustaarabu kabisa tumeshawatangazia mashabiki kuhusu mechi hii halafu wao wakatae ghafla,"alisema Wakuganda.

Alisema, "Wametumbia kocha wao Papic amekataa eti ana majeruhi wengi hiki ni kisingizio tu, ukweli ni kwamba wameamua tu kwa sababu hata katika mechi dhidi ya FC Leopard walitaka kutufanyia hivi hivi, hebu fikiria tulishakaa na kukubaliana vizuri tu kati yetu, wao, TFF na DRFA halafu ghafla wanatuambia mambo haya,huu sio uanamichezo,"alilalama Wakuganda.

Mwananchi lilimtafuta msemaji wa Yanga Louis Sendeu azungumzie suala hilo na lilipompata alisema,"Ni kweli hatuchezi leo kwa sababu baadhi ya wachezaji ni majeruhi kama Chacha Marwa wakati Razack Khalfan na Nsa Job wamefiwa."

Jitihada za gazeti hili lilifanikiwa kumpata Nsa Job ambaye alisema,"Aaah ni kweli ilikuwa ni family Friend tu (rafiki wa karibu wa familia."
 
Majimaji:TFF inatuhujumu kwa Mwakingwe Monday, 17 January 2011 12:23

Sosthenes Nyoni na Clara Alphonce
KLABU ya Majimaji ya Songea imelilalamikia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa kuwanyima leseni ya winga Ulimboka Mwakingwe aliyejiunga nao katika msimu wa usajili wa dirisha dogo.

Wengine waliojiunga na Majimaji msimu wa usajili wa dirisha dogoni ni mchezaji wa zamani wa klabu hiyo Patrick Betwel, Mohamed Kijuso, Yahya Shaaban na Kasimu Kiungo.

Akizungumza kwa simu kutoka Songea jana msemaji wa Majimaji, Andrew Chatwanga alisema wanashangazwa na kitendo cha TFF kutoa leseni za wachezaji wanne pekee iliowasajili na kuacha ya Mwakingwe ambaye pia shirikisho hilo lilikwishamtangaza kuwa mmoja wa waliosajiliwa.

Chatwanga alisema kuwa wamefuatilia suala hilo, lakini hadi sasa hawajafanikiwa na walipomuuliza mtunza takwimu wa TFF, Sad Kawemba aliwajibu hayo ni maagizo ya wakubwa wake.

Alisema kuwa baada ya kulifuatilia zaidi ndani ya TFF walijibiwa kuwa leseni hiyo haijatolewa kwa sababu mchezaji huyo ana tuhuma za rushwa.

"Ndugu yangu hii sasa mizengwe tumeshindwa kumtumia Ulimboka kwa sababu tumekosa leseni yake, tulimuuliza Sad akasema ni maagizo ya wakubwa.

"Hatuwaelewi kabisa TFF unajua baada ya kuwasumbua sana walituambia ana tuhuma za rushwa, sasa huyu mtu hajathibitika na na hili suala haliko polisi wala Takukuru kwa nini watubanie?,"alisema Changwanga.

Jitihada za Mwananchi kuwasaka watendaji wa TFF ili watoe ufafanuzi wa sakata hilo hazikufanikiwa kwani muda mwingi simu zao hazikupatikana.

Afisa Mipango wa Majimaji John Nchimbi alisema kuwa TFF, wamewakataza kumtumia mchezaji huyo kwa sababu bado ana kesi ya kutoa rushwa mahakamani kitu ambacho wameona kuwa ni cha kuwahujumu kwa kuwa mtuhumiwa mwenzie Shaban Kado anacheza.

Ulimboka alihusishwa na kosa la kutoa rushwa ya Shilingi 400,000 kwa mchezaji wa Mtibwa, Shaban Kado ilia achie magoli wakati wakicheza na Simba katika mechi ya ligi kuu Tanzania bara mzunguko wa kwanza.

"Tunajua kuwa TFF, wamepanga kuihujumu timu yetu, haiwezekani wamkatalie Ulimboka kucheza katika timu yetu halafu wamruhusu Kado kucheza tena hata kwenye timu ya taifa kaitwa wakati wote wana kesi mahakamani," alisema.

Ulimboka aliachwa na Simba na msimu huu alisajiliwa na Majimaji katika usajili wa dirisha dogo mwaka jana kwa ajili ya kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya timu hiyo
 
Mashindano ya ngumi Taifa, mikoa yathibitisha
Monday, 17 January 2011 12:25

Imani Makongoro
MIKOA ya Pwani, Mtwara, Iringa na Bukoba, imethibitisha kushiriki mashindano ya Taifa ya Ngumi za ridhaa yatakayoanza kutimua vumbi Februari 26 hadi Machi 3 jijini Dar es Salaam.

Mabondia wa mikoa hiyo wataungana na wenzao kutoka mikoa kumi na tano ya Tanzania Bara ambayo tayari imekwisha thibitisha kushiriki mashindano hayo makubwa.

Lengo la mashindano hayo ni kupata timu ya taifa ya ngumi za ridhaa ambayo itaiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa kama ya Olimpiki jijini London Uingereza na yale ya All Africa mjini Maputo, Msumbiji, mapema mwaka huu.

Katibu Mkuu wa BFT, Makore Mashaga, aliiambia Mwananchi kuwa baada ya mikoa hiyo kuthibitisha kushiriki mashindano hayo inatakiwa kulipia ada ya ushiriki Sh 50,000.

"Baadhi ya mikoa ambayo ilithibitisha kushiriki mashindano ya taifa mapema imekwisha ingiza fedha hizo kwenye akaunti ya BFT ingawa baadhi bado, mbali na ada hiyo kila mkoa utajigharamia Chakula na Malazi kwa muda wote ambao watakuwa kwenye mashindano.

"Endapo tukipata mfadhili basi gharama hizo zitakuwa juu ya BFT, kwani katika bajeti yetu vitu hivyo vipo ingawa tuliiandikia mikoa barua kuwasiliana na viongozi wao wa mikoa kwa ajili kuwagharamia chakula na malazi kwa kipindi chote ambacho watakuwa katika mashindano," alisema Makore.

Mikoa mingine ambayo imethibitisha kushiriki mashindano hayo ni Mwanza, Mara, Mbeya,Tanga, Arusha, Tabora, Polisi JKT, Ngome,Shinyanga, Singida, Kinondoni, Ilala, Temeke.
 
Yanga kunafukuta

Monday, 17 January 2011 19:46 administrator



* Wanachama kuamua hatima ya Nchunga, Davis
* Ni baada ya viongozi hao kuvutana

NA SOPHIA ASHERY
MTAFARUKU unaofukuta katika klabu ya Yanga, utawekwa hadharani Alhamisi wiki hii, ambapo kutafanyika mkutano wa wanachama uliotishwa na uongozi wa matawi ya klabu hiyo. Mkutano huo utajadili kwa kina mivutano ndani ya klabu hiyo, hasa kati ya mwenyekiti wake, Llyod Nchunga na makamu wake, Davis Mosha, ambao wamekuwa hawaelewani kwa muda sasa jambo linalodaiwa kuugawa uongozi wa klabu hiyo uliochaguliwa mwaka jana.

Mwenyekiti wa Matawi la Klabu hiyo, Mohammed Msumi, alieleza kufanyika mkutano huo, alisema jana utafanyika makao makuu ya
Yanga yalioko makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Kariakoo, Dar es Salaam, kuanzia saa nne asubuhi.

Alisema mkutano huo wa dharura utawapa nafasi wanachama kujadili na kutoa maamuzi juu ya mgogoro unaoila na kuitikisa klabu
wa mwenyekiti na makamu wake kushindwa kufanyakazi pamoja, na kusababisha mambo katika klabu hiyo kwenda ovyo kutokana na
mgawanyiko wa uongozi.

Alisema wanachama wanataka kuona maendeleo ya klabu na si mgogoro ambao viongozi wameuanzisha, unaoonekana ni wa mslahi
binafsi na kuiacha klabu ikitetereka.

Alisema mbali ya kuwajadili viongozi hao, mkutano huo pia utajadili uteuzi wa Abbas Mtemvu kuwa mdhamini wa klabu hiyo, jambo ambalo limeibua mjadala mkubwa miongoni mwa wanachama.
Msumi alisema wanachama wanataka kujua vigezo gani vilivyotumiwa na uongozi katika kumpa wadhifa huo Mtemvu ambaye hana sifa za kuwa kiongozi katika klabu hiyo.
Alisema tayari taratibu za mkutano za kuitishwa mkutano huo zimekwishaanza kufanywa, ambapo barua za kuuitisha zimeshasambazwa katika matawi yote nchini.
Ili kufuata taratibu za amani na utulivu alisema, wameliandikia pia barua Jeshi la Polisi kuliarifu juu ya kuwepo mkutano huo ambao una lengo la kutafuta haki na amani katika klabu hiyo inayoaminika kuwa na wafuasi wengi zaidi nchini.
 
Yanga yaikimbia Zesco

Monday, 17 January 2011 08:13 newsroom



NA SOPHIA ASHERY

YANGA jana iliingia mitini kucheza na mabingwa wa soka wa Zambia, ZESCO katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa, uliokuwa uchezwe Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam. Kocha wa timu hiyo, Kostadin

Papic, alisema asingeweza kukubali kuingiza timu uwanjani, kwa sababu wachezaji wake wengi ni majeruhi. Papic alisema wachezaji wake wengi ni majeruhi, wakati wengine wamefiwa na hana timu ya ushindi, baada ya wachezaji wake muhimu wako na timu ya taifa nchini Misri. Aliwataja wachezaji waliofiwa kuwa ni Nsa Job na Razack Khalfan, wakati majeruhi ni Chacha Marwa na Idd Mbaga, ambao wote ni wachezaji muhimu katika kikosi chake. Kocha huyo alisema katika mazingira hayo, si rahisi kupeleka timu uwanjani na kwenda kuaibika, na kusema licha ya kuwa anahitaji kucheza michezo ya kirafiki ya kimataifa, hana timu ya kucheza michezo hiyo kwa sasa. Alisema wachezaji wake wagonjwa wanapata matibabu, huku wengine wakiendelea na mazoezi ili kujiweka sawa kwa ajili ya michezo mingine. Alisema timu yake itawakabili mabingwa wa zamani wa Brazil, Atletico, ambao nao wametua nchini kwa michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa, ambapo kesho wamepangwa kucheza na timu yake.
Wakati Papic akisema hayo, waandaaji wa mchezo dhidi ya ZESCO, wamepata mshituko mkubwa kufuatia uamuzi huo wa Yanga kukataa kucheza mechi hiyo, na kujikuta wakichanganyikiwa baada ya mchezo huo kuyeyuka. Akizungumzia hali hiyo, mmoja wa waandaaji hao, George Wakuganda, alisema wamepata hasara kubwa ambayo hawakuitarajia, na kusema hasara hiyo imemsababisha kupata presha, na kuongezewa maji ya kuongeza nguvu kufuatia mshituko wa habari za kufa pambano hilo. Alisema wamepata hasara ya zaidi ya sh. milioni 10 na kusema hasara hiyo hawajui wataiziba vipi, na wanatarajia kuuandikia barua uongozi wa Yanga ili kudai fedha hizo. Alisema ni lazima Yanga walipe fedha hizo kwa sababu walithibitisha kwa maandishi kucheza mchezo huo, na kitendo cha kubadilika katika siku ya mwisho ya mchezo wanashangaa kimetoka wapi. Zesco juzi ilicheza na Simba na kuifunga mabao 2-1, katika mchezo uliofanyika katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam
 
Stars yaambulia patupu Misri

Monday, 17 January 2011 08:09 newsroom


Na Mwandishi Maalum, Cairo
TAIFA Stars, timu ya taifa ya Tanzania imeshindwa kuambulia hata nafasi ya tano katika michuano ya kuwania Kombe la Nile, inayomalizika mjini hapa, leo. Stars ambayo nafasi hiyo ndio ilikuwa ya mwisho

kwake baada ya kutolewa kwenye michuano hiyo, iliipoteza jana baada ya kuchapwa
mabao 2-0 na Sudan, ambayo imeipoka nafasi hiyo. Kwa kupoteza ushindi katika mchezo huo, Stars imekosa pia kitita cha sh. milioni 40 ambazo ni zawadi kwa timu inayoshika nafasi hiyo,
ambazo zimechukuliwa na Sudan. Mchezo wa fainali wa kuwania kombe hilo utachezwa leo kwa kuzikutanisha wenyeji wa michuano hiyo Misri, na Uganda, utakaopigwa mjini Ismailia. Timu itakayotwaa kombe hilo atazawadiwa pia kitita cha dola za Marekani 176,000 (sh. milioni 264), mshindi wa pili ataondoka na dola 125,000 (sh. milioni 187.5) na timu itakayoshika nafasi ya tatu itatuzwa dola 100,000 (sh. milioni 150).
 
TFF isiruhusu uzembe mzunguko wa pili wa ligi kuu Tanzania Bara

Monday, 17 January 2011 07:44 newsroom



MZUNGUKO wa lala salama wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ulianza mwishoni mwa wiki, ukiashiria kibarua kigumu inazozikabili timu zote 12 zinazoshiriki ligi hiyo. Kibarua hicho kinakuwa kigumu kutokana
na ukweli kwamba ni katika ngwe hii ya mwisho ya ligi, kila timu hujipanga kwa kila
hali kuhakikisha inafanya vizuri kwa kushinda mechi zake zote au nyingi kadiri inavyowezekana, ili kutwaa ubingwa au kubaki katika nafasi za juu. Ni katika mzunguko huo wa pili ambapo kila timu, hata zilizo katika nafasi za chini, hujitutumia kukwepa janga la kushuka daraja, hivyo hujipanga kwa hali na mali kuhakikisha inakusanya pointi nyingi kadiri itakazoweza kuzipata. Kwa maneno mengine kila timu
hukaza buti isifungwe, na hilo ndilo linaloifanya hatua hii ya mwisho ya ligi kuwa ngumu kwa kila timu.

Lakini wakati kila timu inayoshiriki ligi hiyo ikijizatiti kufanya vyema kwenye hatua hiyo, ni wajibu wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), kuwa makini katika uendeshaji wa michuano hiyo na kuhakikisha sheria za soka zinafuatwa kikamilifu, ili bingwa atakaepatikana awe bingwa mwenye uwezo na anayestahili. Tunasema TFF iwe makini kwa sababu baadhi ya timu katika kipindi hiki, hutumia kila mbinu kuhakikisha zinapata ushindi, hata kama ushindi huo zitaupata kwa njia zilizo nje ya kanuni za soka. Waamuzi ni miongoni mwa wanaotajwa kuchangia upindishaji sheria uwanjani, na huko nyuma mechi kadhaa zimeshawahi kuvurugika kutokana na kasoro zinazowagusa waamuzi katika uchezeshaji, ambapo hudaiwa kuwa ama wanachezesha kwa upendeleo wa makusudi, au kwa kutojua sheria za soka.
Hatutarajii kuwa miongoni mwa waamuzi walioteuliwa kuchezesha ligi kuu, ambayo ni ligi ya juu kabisa nchini inayotoa bingwa wa Bara na mshindi wa pili ambao wataiwakilisha nchi katika mashindano ya kimataifa barani Afrika msimu ujao, watakuwemo waamuzi wa aina hiyo. Kinachotoa faraja ni kwamba TFF katika mzunguko wa kwanza, ilishaanza kuwamulika waamuzi wa aina hiyo na kuachukulia hatua,
ambapo baadhi wameshaondolewa kwenye orodha ya kuchezesha michezo ya ligi kuu baada ya kuvurunda katika michezo walioichezesha. Matumaini ni kwamba kama ilivyokuwa makini katika ngwe ya kwanza, TFF itaendelea na umakini huo huo na kuwa wepesi zaidi katika kuchukua hatua, itakapotokea waamuzi au wasimamizi wa mechi kuvurunda, iwe kwa bahati mbaya au kwa makusudi ili kulinda hadhi na heshima ya ligi hiyo. Wakati tukiitarajia TFF kuwa makini na kali kwa waamuzi wazembe, vivyo hivyo isiruhusu timu zinazoshiriki ligi hiyo kufanya vitendo visivyoendana na 'fair play' iwe kwa wachezaji au viongozi, na wote watakaokiuka kanuni na sheria za soka wachukuliwe hatua bila
kuangaliana usoni, ili ligi kuu iwe ligi yenye hadhi, heshima na utulivu utakaotoa bingwa ataeheshimika ndani na nje ya Tanzania.
 
Mbinu chafu ziepukwe ngwe ya mwisho

Monday, 17 January 2011 07:42 newsroom



Mhariri,
MICHUANO ya Ligi Kuu ya Soka ya Vodacom Tanzania Bara, imeanza mzunguko wa lala salama wakati timu 12 zinazocheza ligi hiyo zitaanza hekaheka za michezo yao ya raundi ya pili zikiwa mbioni kumaliza
ligi hiyo. Wakati ligi ikifikia katika hatua hiyo, timu zimekwishajipanga kuendelea na kampeni zao za kutwaa ubingwa, baada ya kutafakari zilivyocheza mechi zao za mzunguko wa kwanza, kila moja ikiwa imeshapata muelekeo wa nafasi itayoweza kujiweka katika msimamo wa ligi hiyo itakapofikia tamati. Kuna klabu zinazopigana kutwaa ubingwa, ziko zinazocheza kupigana zibaki kati, lakini ziko ambazo zitapigana kuepuka kushuka daraja.
Timu zinazotaka ubingwa na zitazokwepa kushuka daraja, ndizo zitakazokuwa na hekaheka zaidi katika ngwe hiyo, na si ajabu katika hatua hiyo mambo yasiyopendeza katika soka yakatokea, mradi kila timu ikitaka kufikia lengo lake. Nalikumbushia mapema Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), ambalo linabeba jukumu la kusimamia ligi na soka kwa jumla, kujiweka tayari kukabiliana na aina zote za mbinu chafu zinazoweza kutumiwa na timu hizo katika harakati zake za kusaka ushindi.
Ziko aina nyingine za mbinu chafu ikiwemo hata ya utoaji wa hongo, ambazo zinaweza zikatumiwa na klabu zinazowania ubingwa na zile zinazokwepa kushuka daraja. TFF ambayo imepata baadhi ya watendaji wapya akiwemo mtendaji mkuu, ina wajibu wa kuhakikisha inajipanga kikamilifu kupambana na mbinu zote chafu zinazoweza kutumiwa na timu zinazocheza ligi katika kusaka ushindi.
Udhibiti mzuri wa mbinu chafu katika mechi zilizosalia, ndio utaoweza kuifanya ligi hiyo imalizike vizuri kwa kuhakikisha inatoa bingwa anayestahili kuwa bingwa, atakaepatikana kutokana na matokeo ya uwanjani. Natahadharisha hilo mapema kwa sababu kumpata bingwa anayestahili kwa kushinda kihalali uwanjani, ndiko kutakoweza kuipatia Tanzania Bara mwakilishi mwenye uwezo wa kuiwakilisha vizuri kwenye michuano ya kimataifa, ambaye ataleta ushindani badala ya kuwa mshiriki tu.
Ramadhani Mohammed,
Mwananyamala Kisiwani,
DAR ES SALAAM.
 
Micho amsikitikia Poulsen
• Adai utafikiri Maximo hakuweko, ataka apewe muda zaidi

na Mwandishi wetu, Cairo


amka2.gif
KOCHA wa zamani wa Yanga, Mserbia Sredojevic Milutin 'Micho', amewataka Watanzania kuendelea kumpa muda zaidi Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars', Mdenish Jan Poulsen, ili aijenge timu, kwani namna alivyoiona kuna kazi kubwa inahitajika ili ilete matunda mazuri.
Alisema, ni vigumu kuamini namna Taifa Stars inavyocheza kama ilikuwa na kocha mmoja kwa miaka minne, badala yake inaonekana ni timu mpya na yenye kocha anayeanza moja kufundisha, hivyo matunda yake yatachelewa kuonekana.
Micho alitoa kauli hiyo juzi mjini hapa, baada ya kumalizika mchezo wa kuwania nafasi ya tano kati ya timu ya Taifa Stars na Sudan katika michuano ya Nchi za Bonde la Mto Nile, Uwanja wa Al Salam na Stars kulala mabao 2-0 yote yakifungwa kipindi cha pili.
Micho ambaye kwa sasa ni Kocha Mkuu wa El Hilal ya Sudan, hakumtaja kwa jina, lakini kocha aliyekuwa kabla ya Poulsen ni Mbrazil Marcio Maximo, aliyefika Tanzania Julai 2006 na kuondoka Julai 2010 na Poulsen kurithi mikoba Agosti mwaka jana, ambapo amesaini mkataba wa miaka miwili.
Desemba mwaka jana, Poulsen aliiongoza timu ya Taifa ya Tanzania Bara 'Kilimanjaro Stars' kutwaa Kombe la Chalenji kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati, wakati Maximo Januari mwaka juzi aliiongoza Taifa Stars kucheza fainali za Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN), zilizofanyika Ivory Coast na kuishia hatua ya makundi.
"Niwe mkweli katika hili, Tanzania ina safari ndefu sana kufikia kwenye mafanikio, Watanzania ni marafiki zangu, nimeishi nao vizuri, mpaka kesho nikienda wananipokea vizuri, lakini timu yao inahitaji muda sana kujengwa, wampe muda mwalimu, ni kocha mzuri na ana uzoefu wa kutosha atawasaidia," alisema.
Micho yuko mjini Cairo na El Hilal iliyoweka kambi kujiandaa na michuano ya kimataifa na alisisitiza, hasemi kocha aliyekuwepo Stars kabla ya Poulsen ni mbaya, lakini Stars haionekani kama ilikuwa ikinolewa na kocha mmoja kwa miaka minne.
Michuano ya soka Nchi za Bonde za Bonde la Mto Nile ilitarajiwa kumalizika jana usiku kwa mchezo wa fainali kati ya wenyeji Misri na Uganda, ambako Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), zenyewe zilicheza kuwania mshindi wa tatu. Burundi imeshika nafasi ya saba kati ya timu saba.
Wakati huo huo, Poulsen akizungumza juzi baada ya vijana wake kufungwa mabao 2-0, alisema kuna makosa waliyafanya sehemu ya ulinzi na ndiyo yaliiangusha timu yake na kuruhusu mabao kipindi cha pili.
Hata hivyo alisema, soka ndivyo lilivyo, lakini hakuwa tayari kuzungumzia kwa ujumla kufanya vibaya kwa timu katika michuano hiyo au kitu ilichopata kiufundi na kusema atafanya hivyo akishafika Dar es Salaam na kujipanga vizuri.
Timu itaondoka Cairo leo saa 5:00 usiku na inatarajiwa kufika Dar es Salaam saa 11 ikiwa imeshika nafasi ya sita kati ya timu saba zilizoshiriki michuano hiyo, ambayo bingwa amejinyakulia zaidi ya sh. milioni 200 za Tanzania, wa pili zaidi ya sh milioni 170 na wa tatu zaidi ya sh.milioni 130.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom