Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Giggs plans to carry on playing






Updated Jan 21, 2011 9:27 AM ET
Ryan Giggs has confirmed he intends to extend his Manchester United career into another season - but 'doesn't know when it will be sorted".
The 37-year-old has been playing on season-long contracts for a number of years now, with a decision generally taken in the spring about whether he wants to carry on.
Sat., Jan. 22
Wolves vs. Liverpool
Arsenal vs. Wigan
Everton vs. West Ham
Man Utd vs. Birmingham
Newcastle vs. Tottenham
Fulham vs. Stoke City
Blackpool vs. Sunderland
Aston Villa vs. Man City
Sun., Jan. 23
Blackburn vs. West Brom
Mon., Jan. 24
Bolton vs. Chelsea
Tue., Jan. 25
Blackpool vs. Man Utd
Wigan vs. Aston Villa
Wed., Jan. 26
Liverpool vs. Fulham BPL Scores | Table | Fixtures

United boss Sir Alex Ferguson has offered high praise for Giggs' recent performances and the veteran Welshman has now revealed his desire to continue his stellar career into 2012.
"I am quite happy still playing at the moment and enjoying my football as much as ever," he said. "I said if I was still enjoying myself and still getting picked I would carry on.
"We will sit down and talk but I am really looking forward to playing next year."
No timescale has been put on the talks. But the evidence of recent seasons suggests discussions between Ferguson and chief executive David Gill with the player, who made his 600th league appearance for Manchester United in last weekend's game at Tottenham, will be concluded swiftly.
"I don't know when it will be sorted out," said Giggs. "We have been quite relaxed about it over the years but it is usually done and dusted quite quickly."
Giggs is bidding to win a record 12th league title this season to go alongside his two European Cups and the countless other trophies on his mantle piece.
All of this has been achieved under Ferguson. And although their relationship has changed down the years, the mutual respect is obvious.
"It is good to hear praise from the manager," said Giggs. "He would be the first one to tell me if I was not playing well or my form wasn't good.
"We talk a lot more and we are a lot more honest with each other.
"He tells me when I am not going to play and gives me a little bit more notice now.
"It is a great relationship and one that has been a big part of why I am still playing."
Not that Giggs necessarily needs anyone to tell him when his performances have not been up to scratch.
"When I was younger you are probably not as honest with myself as I am now," he said. "I am experienced enough to know whether I have played well or not."
 
Red Rafael escapes further ban


RivalsDM



PRINT
RSS


1 comments »

Updated Jan 21, 2011 9:35 AM ET
Manchester United defender Rafael has escaped with an £8,000 fine and a warning about his future conduct following an FA disciplinary hearing.
The hearing was into Rafael's reaction following the red card he received during Manchester United's goalless draw at Tottenham last week.
Sat., Jan. 22
Wolves vs. Liverpool
Arsenal vs. Wigan
Everton vs. West Ham
Man Utd vs. Birmingham
Newcastle vs. Tottenham
Fulham vs. Stoke City
Blackpool vs. Sunderland
Aston Villa vs. Man City
Sun., Jan. 23
Blackburn vs. West Brom
Mon., Jan. 24
Bolton vs. Chelsea
Tue., Jan. 25
Blackpool vs. Man Utd
Wigan vs. Aston Villa
Wed., Jan. 26
Liverpool vs. Fulham BPL Scores | Table | Fixtures

Referee Mike Dean gave Rafael his second caution for a foul on Benoit Assou-Ekotto 18 minutes from the end of the White Hart Lane encounter, forcing United to play out the game with only 10 men.
Rafael was fuming and remonstrated with the official before finally being ushered to the dressing rooms.
The 20-year-old subsequently apologised for his actions and pleased guilty to a misconduct charge, which could have brought a further suspension, in addition to the one-match ban he will serve by missing Saturday's encounter with Birmingham.
However, a specially convened panel, which heard evidence from both Rafael and Sir Alex Ferguson by video link, opted against lengthening the ban, leaving the player free to face Blackpool on Tuesday.
The verdict will be welcomed by Ferguson, who before the hearing outlined why he thought Dean was wrong to apply the second booking.
"Dermot Gallagher said it was the worst decision of the week," said Ferguson.
"Everyone knows it was a bad decision. It happens.
"Unfortunately, in a game of that magnitude it could have had a big impact."
 
Chelsea expect Terry to face Bolton

Published 17:13 21/01/11 By MirrorFootball




Frank Lampard and John Terry are both doubts for Chelsea's Barclays Premier League game at Bolton on Monday.
Lampard is the bigger concern with a calf injury the club had yesterday been confident would not rule him out, while Terry is expected to be available despite picking up a back problem.
Manager Carlo Ancelotti remains without Alex (knee), Yury Zhirkov (calf) and Yossi Benayoun (Achilles).
Provisional squad: Cech, Ferreira, Bosingwa, Ivanovic, Bruma, Terry, Cole, Mikel, Ramires, Kalou, Essien, Lampard, Anelka, Sturridge, Drogba, Malouda, Turnbull, Van Aanholt, McEachran, Mellis.



 

Yanga SC, malumbano hayana tija


KUMEKUWA hali ya mvutano ndani ya klabu ya Yanga kati ya Mwenyekiti Lloyd Nchunga na Makamu wake Davis Mosha na mambo mengine mengi ambayo kwa hakika kama yataachwa na kukua, mambo katika klabu hiyo, yatazidi kuharibika.
Katika kuepusha hatari hiyo, viongozi wa matawi ya klabu hiyo kongwe mkoa wa Dar es Salaam, jana waliitisha mkutano kwa lengo la kujadili mustakabali wa klabu hiyo ikiwemo ushiriki wa timu hiyo katika raundi ya pili ya Ligi Kuu na michuano ya kimataifa.
Kwa upande mmoja, kikao hiki cha jana tunasema kimekuja wakati muafaka hasa ikizingatiwa raundi ya pili ya Ligi Kuu ndiyo kwanza imeanza tangu Januari 15 ambapo Yanga iliyo nafasi ya pili katika msimamo wa ligi hiyo itakuwa ikipambana kutwaa ubingwa wa 23 tangu mwaka 1965.
Kazi iliyopo kwa viongozi wa Yanga, ni kuiandaa vizuri timu hiyo ili iweze kufanya vizuri katika ngwe ya pili ya Ligi Kuu na hatimaye kutwaa ubingwa unaoshikiliwa na mtani wake Simba, mwenye rekodi ya kuutwaa mara 17.
Aidha, Yanga inakabiliwa na michuano ya Kombe la Shirikisho la soka Afrika (CAF) ambapo kati ya Januari 28 na 30, itawakaribisha Dedebit ya Ethiopia katika mechi ya kwanza ya hatua ya awali kabla ya kurudiana wiki mbili baadaye mjini Addis Ababa.
Timu itakayovuka, itakwaana na timu ya Haras El Hadoud ya Misri ambayo msimu uliopita, iliing'oa Simba katika michuano hiyo kwa kuifunga jumla ya mabao 6-2, hivyo ni wazi kuwa hiyo si timu ya kubeza isipokuwa kupanga mikakati kabla ya kuikabili.
Pamoja na mambo mengine, kama wanachama wa Yanga watakuwa wamezika misigano iliyojitokeza kupitia mkutano wao wa jana uliofanyika makao makuu ya klabu hiyo, makutano ya mtaa wa Twiga na Jangwani, Kariakoo, jijini Dar es Salaam, watakuwa wameitendea haki klabu yao na soka ya Tanzania.
Wanachama wa Yanga wanapaswa kutambua kuwa mifarakano kamwe haijengi bali huirudisha nyuma klabu hiyo ambayo ilitaabika kwa zaidi ya miaka saba chini ya mgogoro wa Yanga-Asili na Kampuni ambao ulimalizwa Agosti, 2006.
Kwetu Tanzania Daima, tukiwa sehemu ya wadau wa michezo na maendeleo kwa ujumla wake, tunachukua nafasi hii kuwasihi wanachama wa klabu ya Yanga kuwa pamoja na mambo mengine, wajenge utamaduni wa kumaliza matatizo yao kwa njia ya vikao kama walivyofanya jana kwa lengo la kujenga sio kubomoa.
Tunasema haya pia kutokana na kuibuka kwa mvutano kuhusu kuwepo au kutokuwepo kwa mkutano huo ambapo licha ya wanachama kusisitiza kufanya mkutano huo, uongozi kwa upande wake umezuia mkutano huo kwa hoja kuwa ni batili.
Hata hivyo, wanachama wamekutana na kujadili mambo kadha wa kadha yahusuyo klabu yao ambayo tunaamini ni kwa lengo la kuirudisha kwenye mstari sahihi katika kuijenga Yanga imara kisoka na kiuchumi, hivyo yote yaliyoamuliwa, yafanyiwe kazi kwa maslahi ya klabu hiyo.
Tanzania Daima, tunakumbusha wajibu wa wanachama na viongozi wa klabu hiyo wa kuhakikisha klabu yao inakuwa yenye amani na utulivu ili hata hiyo mipango ya kimaendeleo ambayo imekuwa ikipangwa na uongozi pamoja na kamati nyingine za klabu hiyo, iweze kufanikiwa.
Chini ya malumbano ya wanachama kwa wanachama, viongozi kwa viongozi ama wanachama dhidi ya viongozi, Yanga haitakuwa kitu kimoja, hivyo hakutakuwa na mipango ambayo itapangika na kutekelezwa ipasavyo kwa manudaa yake.
Viongozi na wanachama wa Yanga, wakumbuke mashindano ya kitaifa na kimataifa ambayo yanaikabili timu yao kwa sasa maandalizi ya uhakika yanapaswa kufanywa kwa ajili ya raundi ya pili ya Ligi Kuu iliyoanza tangu Januari 15 na michuano ya kimataifa.
Mbali ya Ligi Kuu, viongozi wa klabu hiyo wanapaswa kuiandaa kikamilifu timu kwa ajili ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Dedebit FC, timu ambayo licha ya kuanzishwa mwaka 1998 na kucheza kwa mara ya kwanza michuano ya kimataifa, sio timu ya kuibeza.
Kitu muhimu kwa wana Yanga, ni kumaliza misigano yao na kushikamana wakielekeza nguvu zao katika kuiandaa timu kwa ajili ya michuano hiyo ya kimataifa ili timu hiyo iweze kufika mbali tofauti na miaka iliyotangulia ambapo Yanga imekuwa ikiaga hatua za awali kabisa.
Mshikamano tunaomaanisha hapa, ni ule wa wanachama dhidi ya viongozi wao kwa upande mmoja na viongozi kwa viongozi kwani tatizo kubwa ambalo limekuwa likiusumbua uongozi wa Nchunga, ni kuwepo kwa msigano na makamu wake, Mosha.
Tunamaliza maoni haya kwa kuwasihi wanachama wa klabu hiyo kufikia suluhu ya matatizo yao kwa njia bora ikiwemo ya kikao cha wanachama kilichofanyika jana ambapo wanachama walipata fursa ya kueleza yale ambayo wanaona hayaendi vizuri ili wahusika waweze kujirekebisha.
Tunamaliza maoni haya tukisisitiza kuwa viongozi na wanachama wa Yanga waone umuhimu wa kumaliza mitafaruku iliyojitokeza kwa njia ya suluhu kwani kwa kufanya hivyo, watakuwa wamedhihirisha
ukomavu wao kulingana na ukongwe wa klabu hiyo iliyoasisiwa tangu mwaka 1935.
 
Wasanii wa kizazi kipya jifunzeni kutumia ala za muziki

Ally Daudi

NAMSHUKURU Mungu kwa kunifikisha siku nyingine tena ili niendelee katika shughuli za kujenga taifa, hususan katika suala la burudani na michezo . Napenda kuwasalimia wadau wote kwa kusema salaam aleykum. Katika Mtazamo wangu leo napenda kuchukua fursa hii kuzungumzia suala la wanamuziki wa Bongo Fleva na matumizi ya vyombo vitokavyo moja kwa moja kwenye kompyuta, yaani muziki wa kutengeneza na siyo kwa kutumia sauti asili na vyombo vyake kama ngoma, gitaa, kinanda na vifaa vingine vya muziki.
Muziki huu wa Tanzania kwa vijana umekuwa chanzo cha ajira kwa wenye vipaji na kutokea kupendwa na wadau wengi wa muziki nchini kote na hata nje ya nchi.
Hivyo kufanya wanamuziki wa kizazi kipya almaarufu kama Bongo Fleva kama wanavyofahamika na kuwapa vijana wengi wa Kitanzania kupata mafanikio tangu ulipoanzishwa rasmi na wanamuziki kama Joseph Haule ‘Profesa Jay', marehemu James Dandu ‘Mtoto wa Dandu au Cool James', Jose Mtambo na wengine wengi.
Tangu muziki huu ulipoanzishwa umeweza kupiga hatua kubwa na kufanya wasanii wengi kusahau ama kutokuwa na mawazo ya kutumia vyombo asilia ili kutangaza muziki wao na badala yake kutumia vyombo vya kisasa kutoka kwenye teknolojia ya kompyuta .
Mtazamo wangu wa leo katika burudani hususan muziki wa kizazi kipya ni kwamba tunatakiwa kuthamini na kutunza asili yetu ili kusaidia kulitangaza taifa letu kwenye medani ya muziki wa kimataifa kama anavyofanya Wanne Star, ambaye kwa sasa amepiga hatua ya kuitangaza asili ya Tanzania.
Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wanatakiwa kubadilika ili kupata kazi za kimataifa kama wanavyofanya wasanii kutoka nchi nyingine kama vile kundi la Makhirikhiri kutoka nchini Botswana ambao wanawakilisha vizuri asili yao.
Hivyo basi kutokana na umahiri wao wa kucheza na kuimba kwa kutumia ala za muziki wa asili na kuvaa kiasili, wamefanikiwa kuvutia wengi kimataifa.
Kutokana na kutumia sauti za kutengenezwa kwenye kompyuta ambazo kwa lugha ya kitaalamu zinaitwa ‘Auto Tune' zinauharibu muziki wa Tanzania, ingawa wadau wegi wa muziki wanaupenda, ila tunaweza tusiutangaze muziki wetu kwani wapo wataalamu wengi wa kimataifa ambao wanatengeneza muziki mzuri na wanauza mpaka kwenye nchi zetu, tena kwa kasi zaidi.
Kumbuka kwamba sisi tunatakiwa kutambulisha kitu kipya kwa wenzetu hao ambacho kitakuwa kipya kwao na kufanya kupata soko la kimataifa katika medani ya muziki.
Pindi wageni watakaposikia vitu vigeni kutoka kwetu basi watakuwa wanapenda kusikiliza na hivyo kupelekea kupata mialiko mingi nchi za wenzetu.
Kutumia sauti asilia bila kubadilishwa kwenye vyombo vya kisasa inatusababishia kesho na keshokutwa kujua anayeimba sasa ni nani hata kama haujajitambulisha kwa jina kwa sababu sauti ya mtu huwa haibadiliki .
Katika mtazamo wangu leo, nasema wasanii tujitahidi kutumia sauti asilia kwani inatusaidia kufanya matamasha ya moja kwa moja bila ya kutumia ‘CD' zenye nakala ya wimbo na kuukopi ili kuonyesha kipaji cha kuimba na kuonyesha sauti yako ni nzuri kiasi gani kama wanavyofanya baadhi ya wasanii kama Banana Zoro, Barnaba kutoka Tanzania House of Talent (THT), Mrisho Mpoto (Mjomba) na wengine ambao wanapiga moja kwa moja nyimbo zao bila ya kutumia CD zenye nyimbo zao.
Wasanii wengi tunaowaona wakiwa kwenye matamasha huwa wanashindwa kuimba nyimbo zao bila ya kutumia ‘CD' na baadala yake wanafuatisha baadhi ya maneno katika wimbo, kitendo ambacho kinaweza kupunguza uwezo wa msanii katika sauti.
Wanamuziki wa kizazi kipya wa Tanzania wanapenda kurahisisha kazi kwa kuwa wanajua kutunga wimbo na fedha za kwenda kurekodi studio wanazo, basi wanakurupuka tu kwa kujua wao kazi yao ni kuingiza sauti mwisho wanachanganya sauti na biti kazi inatoka.
Siyo hivyo jamani, ili uwe msanii wa muziki unatakiwa kuwa mjuzi wa vyombo vyote vya asili pamoja na kutumia sauti bila ya virahisisha kazi.
Nasema wasanii tubadilike, kwani wenzetu sasa wanapenda kuimba kwenye matamasha moja kwa moja, hivyo tunaweza kupata nafasi ya kwenda kutumbuiza matamasha ya nje na tukashindwa kuimba laivu kwa kutumia vyombo vya bendi na hatima yake ni kuushusha muziki wa Tanzania.
Napenda kuwaambia tunapoelekea kwenye muziki huu hautaitwa Bongo fleva bali utaitwa (Ulaya Fleva).
Wasanii tujitahidi kuimba kwa sauti zetu asilia na kutumia vyombo asilia vya muziki kama zilivyo bendi zetu za zamani ikiwamo Msondo ngoma , Sikinde ngoma ya Ukae na nyingine nyingi.
Pia nawaomba wadau wa muziki wa Bongo fleva kwa kununua kazi zao hata wakitumia vyombo asilia vya muziki ili waweze kuwa na moyo wa kufanya kazi hiyo na kupata soko la kimataifa katika medani ya muziki kama wanavyopata mafanikio Wanne Star na wengine.
Wadau wengi wa muziki hapa nchini huwa wanapenda kusikiliza mdundo wa muziki na siyo ujumbe uliobebwa katika wimbo huo na ndiyo maana wasanii wengi wanapenda kukimbilia kutengeneza nyimbo zao kwenye kompyuta ili kuwaridhisha wadau na mwisho mafanikio yao ni kusifiwa na kuuza sura tu mitaani.
Vile vile napenda kuwashauri wadau wa muziki kuwapa moyo na kuwawezesha wasanii nchini kwa kazi zao wanazofanya za kuelimisha jamii na kuwaonya wale wanaoimba mambo ya kuhamasisha maovu kama vile zinaa na maovu mengine .Mwisho natoa rai yangu kwa wasanii wa Bongo fleva wajifunze namna ya kutumia ala mbalimbali za muziki , kuimba bila kutumia rekodi zao katika matamasha na kutotegemea sana kompyuta katika kuendeleza vipaji na mafanikio yao kimuziki.
 
Wasanii msiendekeze anasa

Khadija Kalili

SANAA ni kama dunia ndugu zangu kwani msanii unapokuja inakupokea, ikiwa ujio wako ni uliojaa mbwembwe inakutazama na kukuangalia mwisho wake.
Kama ilivyo hiyo dunia, sanaa nayo haiangalii sura wala jinsia ya msanii, siku zote hufanya lolote lile kwa yeyote yule kulingana na uwezo, kipaji pamoja na kujituma kwake.
Hizi ni nahau mbalimbali ambazo hutumika katika kutoa maonyo na kuelimisha jambo katika jamiii ili kuweza kuepusha na jambo fulani ambalo linaloweza kuwa na madhara kwa kundi la watu fulani.
Nimeamua kurudia ujumbe huu kutokana shinikizo la wasomaji wangu wengi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakinisihi niirudie nami bila hiyana na kuonyesha ninawajali nimeamua niirudie.
Hii ina maana kuwa msanii mwenye bidii, uwezo na kipaji ndiye swahiba kipenzi wa sanaa ambapo humlea na kumlinda katika maisha yake yote ya kisanaa kabla hajafa.
Sidhani kama kuna haja ya kutoa mfano juu ya hili kwa sababu wenye macho tunajionea bila kutumia tochi namna wasanii wetu wanavyolipwa na sanaa kwa usawa wa kile walichokipanda.
Yapo makundi mengi ya muziki wa dansi, mipasho na hata muziki reggae na mengineyo yaliyoibuka kwa kishindo na hatimaye kujikuta yakipoteza umaarufu au kufa kabisa baada ya kipindi kifupi tu.
Aidha, yapo yale mengine ambayo hadi hivi sasa yanaendelea kudunda huku yakizidi kujikusanyia mashabiki kila kunapokucha tangu yalipoanzishwa rasmi miaka kadhaa iliyopita.
Hata kwa upande wa wasanii mmoja mmoja, wapo pia wale waliozuka na kupotea huku wakiwepo wale ambao hadi leo wanaendelea kutikisa anga la sanaa hapa nchini.
Katika hili la kuwako kwa tabaka la wasanii waliopita na mpito wao na wale wanaoendelea kutikisa kwa raha zao, ndiko ninakotaka kuisimamishia mada ya leo.
Jamani, yote kwa yote lazima tukubali kuwa maisha ya kisanaa ni ya msimu, na hili hasa ni kutokana na mfumuko wa wasanii pamoja na fani mpya hizi na zile kila uchao.
Kwa hiyo, kinachopasa kwa wasanii wetu ni kuwa makini na kuacha kabisa mzaha wanapokuwa katika chati na kuonekana kuwa ni vinara katika fani zao.
Umakini ninaouzungumzia hapa ni ile hali ya msanii kuutumia vema wakati wake kwa kuhakikisha kuwa anajijenga kimaisha na kuwa mfano bora katika jamii yake inayomzunguka.
Nafikiri si jambo safi kwa msanii kuutumia wakati wake kwa kukesha kwenye klabu za usiku akiwa na lundo la marafiki na wapenzi huku akitanua na magari ya kuazima.
Sifa ya nini katika maisha ya sasa badala ya kujenga maisha yako ya hapo baadaye wakati wa uzeeni na usijutie uamuzi wako wa kuwa msanii?
Maana yake wasanii wengi waliowahi kutamba hapo nyuma na sasa kujikuta wakati umewatupa huko na wamekuwa wepesi mno wa kulalamika kuwa ni kheri wasingekuwa wasanii.
Ni wepesi wa kusema sanaa haijawafanyia chochote cha maana zaidi ya umaarufu na kupata sifa, huku wakiwa wamesahau kuwa hizo sifa ndizo zilizowaponza!
Hapa namaanisha hivi: endapo kama wangekuwa makini katika kipindi kile walipokuwa wanatamba na kusifiwa, basi leo hii wasingelalamika kwani tunayo mifano mingi ya wasanii wakongwe walioitumia vyema sanaa.
Kadhalika, tunayo pia mifano ya baadhi ya wasanii walio ‘danki danki' au kucheza makida makida ambapo leo hii wako kama watoto wadogo kutokana na kutokuwa na chumo lolote la uhakika wala maana.
Utakuta wengine eti, hivi sasa ndiyo wanakumbuka kuanza kujipanga kwa visenti vya mdondo wanavyovipata baada ya kuzembea huko nyuma walipokuwa wanatikisa hasa.
Somo langu la leo napenda liwaendee wale ambao hadi sasa bado wako kwenye chati wakiwa wanatikisa, wajihadhari mno kwani wajue kuwa hapo walipo hawatakuwapo milele.
Na maisha jinsi utakavyoyatengeneza ndivyo yatakavyo kumaliza hata Waswahili hunena mtoto umleavyo ndivyo akuavyo hii methali ina wigo mpana hivyo kaeni chonjo siyo siku zote utakuwa binti , kuna kuitwa mama na bibi inshaallah Mungu akipenda.
Sasa hofu yangu mimi isije ikawa ni jambo la aibu kwa hao wajukuu na vitukuu vyenu kuja kuona fedheha kutambulishwa mbele ya watu kwamba huyu ni mtoto ama mjukuu wa fulani yule aliyekuwa nambari wani katika filamu enzi hizo na kwa wakati huo ukiwa apeche alolo.
Macho ya Sanaa yanawaangalia wengi, wengine wakiwa ni wale chipukizi ambao bado hawajapata nafasi katika jamii, hivyo kuingia kwao kupanda kwao ni lazima waliopo sasa waporomoke.
Ni jambo la msingi kugangamala kama wanavyoonekana baadhi ya wakongwe katika muziki wa dansi, taarab, bongo fleva na miondoko mingine ya muziki hapa nchini. Acha niwape mfano mmoja wa msanii mwenye mafanikio huyu si mwingine bali ni galacha Zahir Ally Zorro; ninamfahamu vyema pia ni mfano bora kwani ana maisha mazuri licha ya umri mkubwa alionao hivyo ndiyo alivyojiwekea msingi wa maisha yake ya kisanii kwani kila mmoja ni shahidi na anaona jinsi alivyokirithisha hata kizazi chake na sasa anakula matunda ya muziki hivyo hana sababu ya kuilaani fani hiyo na usanii kwa ujumla. Wikiendi njema.
 
shikemshike wa Wanyambo Kijiji cha Makumbusho leo

Happiness Katabazi

WENYEJI wa Wilaya ya Karagwe na Kyerwa, mkoani Kagera ambao ni Wanyambo, leo wanatarajiwa kuanza tamasha la siku tatu la kuenzi utamaduni wao ikiwa ni katika kunadi mila na desturi zao.
Asili ya jina la kabila hilo imetokana na maana kuwa Mnyambo ni mtu mwenye asili ya eneo la Maziwa Makuu. Pia asili ya jina la kabila hilo imetokana na aina moja wapo ya ndizi inayofahamika kwa jina la Enyambo.
Aidha, neno ‘nyambo' linamaanisha mtu au kitu au mmea asilia pia yupo ng'ombe wa asili wilayani Karagwe ambaye anajulikana kwa jina la Enyambo, jina linalofahamika katika nchi za Uganda na Rwanda.
Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Tamasha la Wanyambo, Revelians Tuluhungwa, alipofanya mahojiano na Tanzania Daima mapema wiki hii, kuhusu uzinduzi wa tamasha la Wanyambo litakalozinduliwa leo na kumalizika Jumapili wiki hii na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal, katika Kijiji cha Makumbusho, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Anasema jumla ya Wanyambo 200 kutoka Karagwe wamekuja kuungana na Wanyambo waishio hapa jijini kusherehekea tamasha hilo la kuenzi utamaduni wao.
Anasema Wanyambo wamejiandaa kikamilifu kuonyesha na kueleza mila na desturi za kabila hilo hasa nyumba ya asili, makazi ya Mnyambo iliyojengwa kijijini hapo hivi karibuni ambayo imegharimu zaidi ya sh milioni nne, vyakula na vinywaji vyao vya asili, mavazi, nyimbo, ngoma, kazi za mikono, misemo, majigambo na malezi ya watoto.
Katika makala hii Tuluhungwa anaelezea mazingira ya himaya ya Karagwe na Wanyambo kutukuka na kufahamika duniani katika kipindi cha miaka 150 iliyopita na kutofahamika katika Tanzania ya leo sambamba na kupanda na kushuka kwa umaarufu wa kabila hilo.
Tuluhungwa anaeleza historia ya Karagwe kwa kusema himaya ya mfalme wa Karagwe ilikuwa ndiyo utawala mkubwa katika maeneo ya maziwa makuu kwa miaka kama 500 na Bweranyange, mji mkuu wa mfalme wa Karagwe ndipo alikaa Mfalme Ruhinda wa Kwanza, mwanzilishi wa himaya za Kihinda.
Anasema Ruhinda alitawala eneo lote la Karagwe, Ankole, Kihanja, Ihangiro Biharamulo Bushubi na Bugufi, kaskazini akipakana na Bunyoro na Mto Mwiruzi, kusini ya Biharamulo na Mkoa wa Kigoma.
Tulungwa ambaye ni mtumishi wa miaka mingi wa Shirila Umoja wa Mataifa la (UNICEF), anasema maeneo yote aliyoyataja hapo juu yalitawaliwa na watoto wa Mukama wa Karagwe ambao muda ulipopita walijitenga na kuanzisha tawala huru.
Himaya ya mfalme wa Karagwe hiyo ilitukuka na kuandikwa kwenye magazeti ya ulimwengu wakati wa wavumbuzi hususan Uingereza zaidi ya miaka 160 iliyopita.
"Karagwe ilikuwa ndiyo njia pekee ya kufikia utawala wa Buganda kwa wageni wote kutoka pwani na Zanzibar .
Kati ya Novemba 1861 na Februari 1862 John Hannington Speke na James Grant walikaa miezi mitatu Kafuro jirani na Bweranyange na wakaandika kwa kirefu juu ya mila na desturi za Karagwe chini ya mfalme Rumanyika Orugundu Rzinga Mchuchu wa Nkwanzi, ambalo ni jina la utani lenye maana ya shujaa mfuga nywele ndefu.
Na kwamba kwa hivi sasa kuna hifadhi ya wanyama ya Rumanyika Orugundu kuenzi mtawala huyo ambayo kwa mashariki yake katika Kijiji cha Ibamba kunapatikana mto wenye maji moto ya Mutagata," anasema Tuluhungwa.
Kupungua umaarufu wa Karagwe
Tuluhungwa anasema kufikia miaka ya 1880 na 1890 wakati wababe duniani wakishindwa kugawana Afrika huko Berlin 1884 na baadaye wakati Zanzibar na Buganda zilikuwa tawala zinazolindwa na mfamle wa Uingereza, Karagwe iliangukiwa na nuksi ambazo zilifika tawala nyingine zote kubwa katika historia kama za Alexander mkubwa utawala wa Kirumi. Ilipungua umaarufu mpaka wakoloni wa kijerumani hawakuitamani na Wamisionari pia waliipita kando na kuongeza kuwa visa vya kuipunguza Karagwe umaarufu vimeandikwa kwa kirefu na marehemu Profesa Katoke katika kitabu chake cha ‘The Making of The karagwe Kingdom'
Anasema awali ilikuwa ni vita ya wenyewe kwa wenyewe ambayo ilikuwa imeanza wakati Speke na Grant wakiwa Karagwe Novemba 1861 mpaka Desemba 1862.
Matokeo yake ilikuwa kupungua kwa amani na kuihama Karagwe upande ulioshindwa na kupunguza wingi wa watu.
Pili, ugunduzi wa njia fupi kutoka Mombasa kwenda Uganda kuliitoa Karagwe kwenye njia kuu ya biashara ya kimataifa na kupunguza umaarufu wake.
Magonjwa ya mifugo kama ng'ombe (sotoka) yalishambulia mifugo ya wakazi wa Karagwe katika kipindi hiki na kupunguza utajiri wa Karagwe. Wakoloni walikuwa hawavutiwi na nchi maskini.
Sababu za kisiasa na utawala; Karagwe ilipita kipindi ambacho wafalme walikufa wakiwa wadogo bila kuacha warithi waliokwisha kufikia umri wa kutawala, ikalazimu kutawala kwa kutumia viongozi wa muda kama vile Kakoko waliotawala kwa ukatili na kuharibu himaya.
Matokeo ya kupungua umaarufu
Ni kutopewa kipaumbele katika mipango ya wakoloni wa Kijerumani kulifanya wamisionari kutovutiwa kuweka vituo vyao Karagwe.
Kwahiyo wamisionari wa Kikatoliki wao walianzisha vituo vyao Kashozi 1892, Bunena 1905, Kagondo na Rubya 1904, Katoke, Biharamulo na kuanzisha shule sehemu zote hizo.
Misheni ya kwanza Karagwe ilianzishwa mwaka 1934 baada ya miaka 40 baada ya kumpata padri wa kwanza Mwafrika, Oscar aliyepadrishwa Bukoba 1917. Wa kwanza Karagwe ni Padri Rwakiboine aliyepadrishwa mwaka 1943, miaka 26 baadaye na shule na hospitali za misheni zilifuata.
Kupoteza umaarufu

Kama watu wote waliotawaliwa na wageni na kunyanyaswa, kutawaliwa na wageni wa Kihanja chini ya Wajerumani kuliwaathiri katika kujiheshimu na kujitambua kama Wanyambo.

Kujifunza elimu na dini kwa njia ya kuhemea katika lugha zaidi ya Kinyambo kuliathiri sana Kinyambo.
Waumini na wanafunzi walizoea kusikia makatekista na walimu wakifundisha Kinyambo kibovu kilichoathiriwa na lafudhi na misemo ya kabila la Wahaya.
Bila kutaka, wasomi walijikuta wakiathiri matumizi ya lugha yao ya Kinyambo kwa jeuri kutokana na wingi wa mashule ya dini na serikali.
Jumla ya yote ni kwamba kuanguka kwa umaarufu wa Karagwe ghafla wakati wa kuja kwa ukoloni, kulisababisha mazingira kuathiri Kinyambo mpaka Wanyambo wenyewe wakawa kama wamemezwa na Wahaya, kabila ambalo halikuwepo kabla ya ukoloni.
Leo hii tunapoadhimisha tamasha la Wanyambo, tunasimama kwa ujasiri wao kufanya tamasha hili la siku tatu kuanzia leo na kurudisha mchango wa Wanyambo wanaojiamini katika kujenga taifa la Tanzania.
Wanyambo kabila lisilojulikana
Tuluhungwa anasema athari za kutotambulika Wanyambo ni nyingi na zinazoendelea kuathiri Watanzania wa Kinyambo wengi.
Taarifa zinajitokeza kila siku wanyambo kubughudhiwa Idara ya Uhamiaji kwa sababu baadhi ya maofisa wake hawajui kwamba kabila hilo lipo. Ni maombi ya Wanyambo kupitia tamasha hili kwamba kubughudhiwa Wanyambo kwa kutowajua au kuwadhihaki wao kana kwamba kabila la Wanyambo si raia halali nchini, ni unyanyasaji usiokubalika na ukomeshwe mara moja.
Kabila la Wanyambo ni miongoni mwa makabila makubwa mkoani Kagera, mengine ni Wasubi, Washubi, Wahangaza, Wazinga na Wahaya.
Wanyambo wengi hawajitambui
Anasema inatia hofu kwamba hata Wanyambo wenyewe hasa waishio nje ya Karagwe hawana ufahamu kama wao ni Wanyambo au ni Wahaya kwa sababu baadhi yao hujitambulisha kama ni Wahaya na wanajaribu hata kuigiza lugha yao.
Historia ya Wanyambo haijatafitiwa kwa kina na hivyo hakuna machapisho ya kutosha yanayoelezea historia ya Wanyambo.
Yapo machapisho machache sana hasa ya Profesa Katoke na hadithi za wapelelezi kama Hans Mayer ambayo hayako sokoni tena na yaliyopo hayatoshelezi mahitaji.
Anasema mila na desturi za Wanyambo zilizo nje ziko hatarini kutoweka, ikiwa ni pamoja na ngoma za asili, nyimbo, misemo, majigambo, hadithi na taratibu za maisha nyingi zimetoweka na zilizobaki ziko hatarini kupotea kabisa.
Mfano mzuri ni ngoma ya Amakondere ambayo imebaki ikichezwa na kundi moja tu la wazee waishio Rwanyango, ambazo hazijarekodiwa, ambapo itakuwa vigumu kurithishwa kizazi kimoja hadi kingine.
Aidha, uwepo wa ngoma ile unategemea sana uhai wa wazee hao hata ala za muziki wa ngoma hizo (Amakondere) hazilimwi tena na huenda mmea huu umeshatoweka kabisa.
Kwa upande wa lugha ya Wanyambo (Orunyambo) imeanza kupoteza uhalisia wake kutokana na mwingiliano na kutozungumzwa mara kwa mara hivyo huenda ikapotea kabisa.
"Kwa ujumla Wanyambo wanapata usumbufu katika kujitambulisha hasa wanapohitaji baadhi ya huduma katika Wizara ya Mambo ya Ndani kwa sababu hudhaniwa jamii ya Wanyambo ni wakimbizi kutoka nchi jirani za Burundi na Rwanda," anasema.
Historia ya Wanyambo

Wanyambo ni kabila lilokuwa miongoni mwa makabila makubwa na yenye nguvu za kivita na kiuchumi. Watu wa kabila hili la Wanyambo walikuwa na ufalme ulioongozwa na wafalme (abakama) 14 kwa nyakati tofauti. Watu wake ni wakulima na wafugaji.

Historia ya kabila hili ilifahamika ukanda wote wa Ziwa Victoria pamoja na nchi za Rwanda na Burundi, kwa sababu ya uhunzi wa mapambo mengi ya kifalme ambayo yalitengenezwa na kuhifadhiwa kwenye ngome ya mfalme.
Mapambo hayo yalipendwa na mengine yalichukuliwa na Wajerumani, walipewa zawadi na Omukama Rumanyika.
Kwa ujumla ni kabila lililoheshimika hivyo Wanyambo walijivunia Unyambo wao, hali iliyoibua misemo kama, Ndyu Munyambo akala nakalenje, Omunyambo agamba echabweine.
Aidha, anasema siku ya utamaduni wa Mtanzania ni utaratibu uliobuniwa na Bodi ya Makumbusho ya Taifa chini ya Wizara ya Elimu na Utamaduni mwaka 1994 kabla ya Makumbusho ya taifa haijahamishiwa chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kama ilivyo sasa, ili kutoa fursa kwa jamii mbalimbali hapa nchini kuonyesha tamaduni zao katika Kijiji cha Makumbusho, Kijitonyama, Dar es Salaam.
Malengo ya kuwa na siku ya utamaduni wa Mtanzania
Ni kutoa nafasi kwa jamii moja baada ya nyingine miongoni mwa jamii nyingine tulizonazo kuonyesha mila, desturi na mienendo yao mbalimbali ya jadi ili jamii nyingine ziweze kuelewa na kuthamini utamaduni wa Watanzania wenzao.
Kujifunza na kufahamu aina mbali mbali za mila na desturi zinazofaa kudumishwa, kuboreshwa na kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kama utamaduni wa taifa.
Kufanya Kijiji cha Makumbusho kuwa kielelezo halisi cha maisha ya Watanzania.
Malengo ya kufanya Tamasha la Wanyambo
Ni kuonyesha mila, desturi na mienendo yao mbalimbali ili Wanyambo wenyewe na jamii nyingine ziweze kuelewa, kuheshimu na kuthamini utamaduni wa Wanyambo, hivyo kukuza uelewano wa kitaifa.
Wanyambo na jamii nyingine zitaweza kujifunza aina mbalimbali za mila na desturi za Wanyambo zinazofaa kudumishwa, kuboreshwa na kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kingine.
Hali hii itaondoa utata na kupunguza usumbufu pale wanapokuwa wanahitaji huduma muhimu kama vyeti vya kuzaliwa, hati za kusafiria, viza, vitambulisho vya kupiga kura pamoja na nyaraka nyingine muhimu, kwani wamekuwa wakipata shida kwa sababu ya kutojulikana kwa kabila lao.
Kuweka mikakati ya kufanya utafiti ili kubaini mila, desturi na tamaduni za Wanyambo zilizo njema na kuzihifadhi kwa njia ya maandishi ili ziweze kurithishwa kwa kizazi hadi kizazi na zitumike kwa manufaa ya jamii nzima. Kila la keri Wanyambo.
 
Heko Wanyambo, tamasha liwe endelevu

Juma Kasesa

AHLAN wasahlaan mpenzi msomaji wa kona hii ya Jamvi la Kulonga tukiwa tunachambua haya na yale yaliyojiri katika anga za burudani na sanaa.
Ni Iijumaa nyingine tunakutana Jamvini katika kudadavua masuala mbalimbali yaliyojiri katika anga ya sanaa na burudani ili kuongeza tija na ufanisi katika tasnia hiyo.
Hoja yetu ya leo Jamvini ni kujadili hatua iliyochokuliwa na kabila la Wanyambo nchini kuandaa tamasha maalumu litakalokuwa na lengo kuwaonyesha Watanzania kazi za utamaduni zinazohusu kabila hilo kwa lengo kujitangaza ndani na nje ya nchi.
Tamasha hili linalowakilishwa na jamii ya Wanyambo limepangwa kufanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia kesho jijini Dar es Salaam katika Kijiji cha Makumbusho likifunguliwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal.
Jamvi la Kulonga kwa kutambua mchango wa makabila mbalimbali nchini kwanza limeona lianze kwa kuwapongeza waratibu wa tamasha hilo, ambao kwa namna moja wamefungua njia kwa makabila mengine kufanya matamasha kama hayo kwa lengo la kuutangaza utamaduni wao ndani na nje nchi na kuweza kuwavutia watalii na wageni mbalimbali kutembelea na kuweza kujipatia kipato ikiwemo kukuza uchumi wa nchi.
Kwa kifupi Wanyambo ni moja wapo ya kabila kubwa na lililoandika historia ya Tanzania katika maeneo ya maziwa makuu katika miaka ya 500 ambapo ilikuwa himaya ya mfalme Ruhinda wa kwanza wa Karagwe.
Makamu Mwenyekiti wa Tamasha hilo, Daniel Rutasyamuka, anasema tamasha hilo litawahusisha wasanii wa aina mbalimbali kutoka wilaya za Karagwe na Kyerwa pamoja na wadau wengine ambapo pia kutakuwepo na maonyesho ya ngoma za wanyambo, vyakula vya asili kama ugali wa ulezi, uji wa ulezi nafaka , kunde, karanga, vinywaji vya asili kama Lubisi, Mlamba na vinginevyo vinavyotengenezwa kwa ndizi, mboga na majani.
Shughuli zingine ambazo zimepangwa kufanyika ni maonyesho ya zana za asili za wanyambo, mila na desturi kama mavazi, taratibu za harusi , kufundana, nyumba za asili, kazi za mikono ikiwa ni pamoja na maandishi, methali na fasihi za Kinyambo.
Licha ya kuvutiwa na tamasha hilo kwa ujumla, Jamvi hili pia limeguswa na uwepo wa warsha na kongamano litakalozungumzia maendeleo ya Karagwe na Kyerwa, vivutio mbalimbali vinavyopatikana humo kama maporomoko ya maji, misitu, mbuga za wanyama na hospitali za asili.
Kwa kumbukumbu ya Jamvi hili ni tamasha kubwa kufanyika ambalo linapaswa kuenziwa na Wanyambo ili liwe linafanyika kila mwaka katika kuutangaza utamaduni wao lakini pia kuvutia watalii wa ndani na nje ya nchi kwenda kuona kazi mbalimbali za kabila hilo.
Lakini hoja kubwa ni kwamba makabila mengine yanapaswa kufuata nyayo za Wanyambo kwa kuanzisha matamasha yao ambayo yanaweza kuwa ni njia mbadala ya kutangaza utamaduni wao lakini pia kujiongezea kipato kwa kuuza bidhaa mbalimbali za kijadi kwa watanzania wa makabila mengine na watalii.
Jamvi la Kulonga linalitazama tamasha hili kama kichocheo kipya katika kuuthamini na kuutukuza utamaduni wa makabila yetu nchini ambayo yanakadiriwa kufikia takriban 120, hivyo serikali inapaswa kuliunga mkono tamasha hili la Wanyammbo na la makabila mengine yatakayofanyika ili kuonyesha linaunga mkono harakati za kuendeleza mila na desturi zao.
Kwa upande mwingine Jamvi hili linaliunga mkono tamasha hili kwakuwa litawawezesha vijana waliozaliwa mjini kupata fursa ya kuona na kujifunza mila na desturi za makabila yao, kutokana na wengi katika ya vijana hao hawapati fursa ya kujifunza tamaduni zao kwa sababu ya kulowea mjini ambako kwa namna moja kumesababishwa na wazazi ama walezi wao.
Jamvi hili linamalizia kwa kuwapongeza waratibu wa tamasha hilo na kuwataka walifanye liwe endelevu ili kuitangaza jamii yao lakini ni changamoto kwa makabila mengine kuanza mikakati ya kufanya matamasha yenye sura hiyo kwa lengo la kujitangaza ndani na nje ya nchi, sambamba na kuitangaza Tanzania na kujiongezea kipato.
 
Karibu sana ‘Usiku wa Kale' lakini...

Abdallah Menssah

SALAAM aleyikum mpenzi msomaji wangu wa safu hii iliyo murua na maridadi kabisa ya Kijiwe cha Burudani ikujiayo kila wiki katika siku nzuri kama ya leo.
Sina shaka u - mzima wa afya wakati huu ulipolishikilia gazeti lako safi la Tanzania Daima ukitaradadi na kuperuzi kwa raha zako katika kurasa hizi na zile.
Uzima wako msomaji wangu ni fahari kwangu, ndio maana kila mara siachi kusema kuwa, tuwaombee ahueni wale wote ambao kwa namna moja ama nyingine hawakuamka salama.
Leo nitazungumzia kuhusu hizi taarifa za kuanzishwa kwa onyesho maalumu la ‘Usiku wa Kale', kwenye ukumbi wa Equator Grill, Mtoni kwa Azizi Ally, jijini Dar es Salaam.
Kwa faida ya wale ambao hawakubahatika kusikia, ukumbi maarufu wa burudani, Equator Grill uko katika maandalizi ya mwisho ya onyesho litakalojulikana kama ‘Usiku wa Kale'.
Tunaambiwa kuwa, onyesho hilo litakalorindima kila Jumatano, limelenga kutoa burudani kabambe kwa kuwakumbusha vijana wa zamani enzi zile za mwaka arobaini na saba.
Tena kimsisitizo, usiku huo wa Kale utakuwa ukipambwa na mkongwe Kikumbi Mwanza Mpango akiwa na bendi yake moto wa kuotea mbali ya La Capital.
Halafu wakongwe wengine wakiwamo wale wa miondoko ya taarabu, watakuwa wakialikwa kwa wiki hii huyu na wiki nyingine yule, kulingana na matakwa na maombi ya mashabiki.
Binafsi, kama mdau nambari moja wa sanaa na burudani, nachukua fursa hii kusema kuwa; ‘karibu sana ‘Usiku wa Kale', lakini... tunaomba onyesho hilo libebe maana iliyokusudiwa.
Kwanza kabisa, naupongeza uongozi wa ukumbi huo, hususan Mkurugenzi, Hamis Slim na Meneja wake, Richard Yalomba ‘Bob Rich' kwa kuweza kutubunia kitu ambacho kitatufariji sisi wakongwe.
Hii ni kwasababu, wakongwe tumetokea kusahaulika, ama kwa lugha nyepesi tumebwagwa. Nasema hata mkituambia sisi wazee hatukawii kupandisha ‘tempo' kwa vitu vidogo.
Mara nyingi tumeongopewa tu, mimi naita hivyo kwasababu ni uzushi mtupu. Matamasha uchwara yamekuwa yakiandaliwa eti kutuenzi na hatimaye kuwa kama nguvu za soda.
Wakati mwingine tumefanyiwa danganya toto hata vyama tunavyovitegemea kutokana na kubeba dhamana husika kama vile kile cha muziki wa dansi (CHAMUDATA).
Eti kulishaanzishwa timu ya taifa ya kurindimisha muziki, wakaiita ‘Tanzania All Stars', tukaambiwa itakuwa ikikusanya wakongwe mahiri na kuivisha vibao motomoto mara kwa mara, waapi!
Mbali ya kudanganywa na baba yetu huyo mzazi (CHAMUDATA), hujitokeza pia wazushi wengine na kujifanya wanaanzisha maonyesho maalumu ya kutumbuiza muziki wa kale bila mafanikio.
Ndiyo maana nikasema, karibu sana ‘Usiku wa Kale', lakini... tunaomba onyesho hilo libebe maana inayokusudiwa.
Isije ikatokea badala ya kuita bendi kongwe kuturindimishia vibao vya zamani, mkawa mnazialika bendi za dansi za kizazi kipya. Chonde chonde, hatutaki ndombolo siye.
Tena hapa naomba nisisitize zaidi kuwa, tunataka muziki wa kale haswa, yaani hata kama mtakuwa mnazialika bendi kama Sikinde, Vijana jazz na Msondo Ngoma, muwape masharti.
Kwasababu ingawa nao hao ni wakongwe lakini wapo hadi leo kwenye gemu na ili kwenda na wakati nao wameamua kuanza kutunga vibao vilivyokaa ki ndombolo ya solo.
Mkiwaleta Sikinde, sawa lakini muwaambie bayana kuwa tunataka ‘Kasimu', ‘Selina', ‘Barua Toka kwa Mama', ‘Dar es Salaam Air Port', ‘Uhuru wa Zimbwabwe' na ‘Nawashukuru Wazazi'.
Kadhalika, mkiwaalika Msondo nao wapeni laivu kuwa, tunahitaji watupigie ‘Mama Nipeleke kwa Baba', ‘Nisingekukimbia', ‘Uzuri Si Shani', ‘Zarina' na angalau ‘Namsaka Mbaya Wangu' na ‘Faulata'.
Ama kama mtatuletea Vijana Jazz, basi nyimbo zao ziwe ni ‘Maisha ya Ambha', ‘Kuruka Ukuta', ‘Gubu la Mume', ‘Hekaheka' au kama mkija mbele sana basi labda ‘Sifa za Stella' na ‘Mondinde'.
Hata hivyo, hii isiwavunje moyo Mkurugenzi Slim na Meneja wako, Bob Rich, nimejaribu kuyasema haya mapema ili kuwatahadharisha tu katika mchakato wa moja na mbili ya kuwekana sawa.
Yote kwa yote, tunausubiri kwa hamu huo ‘Usiku wa Kale' na mimi ni mmoja wa wale wanaoandaa mashati ya kubana, mabuga na raizon kwa ajili ya kuvivaa kila Jumatano.
Leo napenda niishie hapa, nikiwaaga kwa kaulimbiu inayosema; ‘Koroboi ni koroboi na umeme ni umeme daima!'.
Wadau wangu leo hii ni Dogo Baraka ‘Jembe', Mohammed Mtwale, Yahya Rajab ‘West', Bilsan Hemed, Asha Salum, Wastara Said Makumbato na Ikota Mhamila.
Wengine ni Said Makorokoto, Rehema idd, Hassan na Hussein, Aziza Issa, bila kumsahau Rajab Mhamila ‘Super D Mnyamwezi' anayetuuzia Enzoy watoto wa kiume.
 
Waliowapoteza warembo wajitokeza


na Ruhazi Ruhazi


BAADA ya washiriki wa Miss Tanzania ngazi ya vitongoji mwaka juzi, kutoa malalamiko kwenye baadhi ya vyombo vya habari kuhusu uongozi wa Chuo cha Tanzania Education College cha jijini Dar es Salaam kutokomea kusikojulikana, uongozi umejitokeza.
Akizungumza waandishi wa habari juzi jioni jijini Dar es Salaam, mmoja wa viongozi hao, Elias Mbeki, alisema kuwa hawakukimbia kama ilivyodaiwa bali kilichojitokeza ni chuo hicho kuhamishwa.
Alisema kuwa, wamesikitishwa sana na taarifa hizo kwa kuwa wanafunzi hao wangeweza kuwasiliana nao hata kwa njia ya simu na kufahamishwa kilichojitokeza, kuliko kukimbilia kwenye vyombo vya habari.
Akifafanua alisema kuwa, chuo hicho kilichokuwa Kariakoo, kilipata jengo maeneo ya Ubungo karibu na Kanisa la Mchungaji Gwajima, hivyo wakalazimika kuhama na walitoa taarifa kwa asilimia kubwa ya wanafunzi.
"Kwa kweli tumesikitika kusikia kuwa tumefunga chuo na kukimbilia kusikojulikana, hawa waliosema hivi walikuwa likizo na hawakuwa na mawasiliano na sisi wala wanafunzi wenzao, sasa wamerudi na kukuta tumehama nadhani hawakuwa hata na namba zetu za simu hili ni kosa lao," alisema Mbeki.
Alisema kuwa chuo hicho kinachotoa mafunzo mbalimbali ikiwamo ualimu, kompyuta, utalii, uandishi wa habari na utangazaji, mawasiliano na mengineyo, kimesajiliwa kihalali hivyo haiwezekani kikafungwa bila wanafunzi kushirikishwa.
Aliwataka wazazi wenye wanafunzi wanaosoma chuoni hapo na wale wanaotaka kuwapeleka watoto wao, kutokatishwa tamaa na kilichojitokeza, kwa vile ilikuwa ni kukosekana kwa mawasiliano baina yao na wanafunzi wachache kutoka mikoani.
 
Hassan: Siwazi kurejea Extra Bongo


na Abdallah Menssah


KIONGOZI wa bendi ya Manchester Musica, Adam Hassan, ameweka wazi kuwa hana mpango wa kurejea katika bendi yake ya zamani ya Extra Bongo hata baada ya kumaliza mkataba wake ndani ya bendi hiyo inayotumia mtindo wa ‘Wana Kamtekenya'.
Hassan, mahiri wa ucharazaji wa gitaa la solo katika bendi hiyo, aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam katika mazungumzo maalum na mwandishi wa habari hizi, juu ya mustakabali wa bendi yake ya Manchester Musica, yaliyofanyika nyumbani kwake, Kiwalani.
"Unajua, nishakutana mno na maswali ya mashabiki mbalimbali, wakihoji kama nitarejea tena Extra Bongo nitakapomaliza mkataba wangu wa miaka miwili hapa Manchester Musica, sasa naweka bayana kuwa, sifikirii kitu kama hicho," alisema Hassan.
Aidha, Hassan alieleza kuwa, hatarejea Extra Bongo kwasababu, ameridhika na kipato anachopata hivi sasa katika bendi ya Manchester
Musica pamoja na ushirikiano wa kweli na dhati kutoka kwa wasanii wenzake na viongozi wa ngazi za juu chini ya Jerome Mponda.

Alisema kuwa, anachofikiria sasa ni kuongeza mkataba katika bendi hiyo mara utakapomalizika huku akieleza kuwa, iwapo kutakuwa na lolote la
ziada katika mkataba mpya anaotaka kuingia tena, atafanya mazungumzo na viongozi wa juu wa Manchester Musica ili waendelee kuwa pamoja.
 
Simba yashindwa kwenda Brazil
• Atletico ya kweli yaichapa Corinthias Brazil

na Waandishi wetu


MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Simba ya jijini Dar es Salaam, jana walishindwa kukata tiketi ya kwenda Brazil kurudiana na Atletico Paranaense baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na timu hiyo, katika mchezo wa kirafiki ulipigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Simba ambao jana walionyesha kandanda safi na kukitawala kipindi cha kwanza, walifanya shambulizi lingine dakika ya 15 kupitia kwa Rashid Gumbo na Mussa Hassan Mgosi na kupata kona doto mbili, ambazo ziliokolewa na mabeki wa Atletico.
Timu hizo ziliendelea kushambuliana kwa zamu ambapo Simba ilifanikiwa kujipatia bao la kuongoza dakika ya 44 baada ya Mgosi kuunganisha krosi safi ya Gumbo ambaye jana alionyesha kiwango kizuri; bao ambalo lilidumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo Simba waliendelea kucheza kwa kuonana na kulisakama lango la Atletico, lakini washambuliaji wake walishindwa kutumia nafasi nyingi walizozipata.
Wabrazil hao walipata pigo dakika ya 66 baada ya beki wao Bruno Costa kupewa kadi nyekundu baada ya kumkwatua Ochieng, lakini waliendelea kucheza kwa ‘jihadi' na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 81 kupitia Ramon Machada ambaye alifanikiwa kuwatoka mabeki wa Simba na kuachia shuti lililomuacha kipa Juma Kaseja akiwa ameduwaa.
Simba: Juma Kaseja, Juma Jabu, Haruna Shamte, Juma Nyoso, Meshack Abel, Jerry Santo, Rashid Gumbo Patrick Ochieng, Mohammed Banka, Mgosi na Mbwana Samatta.
Katika hatua nyingine, wakati ikidaiwa kuwa hapa nchini kuwa mechi mbili za kimataifa za kirafiki dhidi ya klabu za Yanga na Simba za jijini Dar es Salaam, Atletico Paranaense ya Brazil, imeendelea na mechi zake za Ligi Kuu ya Brazil ‘Serie A' ambapo usiku wa kuamkia jana Alhamisi, ilikuwa ikichuana na Corinthians PR na kushinda ugenini.
Kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo, inayonolewa na kocha Mbrazil, Sergio Soares, mechi hiyo ilichezwa kwenye dimba la Estádio Janguito Malucelli, mjini Curitiba, katika Jimbo la Paraná nchini humo na Atletico kuwaduwaza wenyeji wao kwa mabao 2-1 na kujisogeza juu katika msimamo wa ligi hiyo.
Adriano Gabiru wa Corinthians, alitangulia kuwapatia bao wenyeji bao kunako dakika ya 35 ya mchezo huo na hadi filimbi ya mapumziko inapulizwa, wenyeji walikuwa mbele kwa bao hilo, huku Atletico wakiwa hawajapata kitu.
Kipindi cha pili, mshambuliaji, Henan Faria Silveira, aliisawazishia Atletico dakika ya 78 ya mchezo huo, kabla ya kiungo mshambuliaji, Madson Formagini Caridade, kuifungia bao la ushindi dakika ya 80 na kuibua shangwe za mashabiki wachache waliosafiri na timu hiyo.
Katika muendelezo wa mechi za klabu hiyo, Jumamosi Januari 22, Atletico Paranaense inatarajia kurudi kwenye dimba la nyumbani la Arena da Baixada, (zamani Estádio Joaquim Américo Guimarães), linalobeba watazamaji 37,490, kuwakaribisha Iraty katika michuano ya Kombe la Copa do Brasil, kabla ya Jumatatu Januari 30 kuwakaribisha Roma Esporte de Apucarana katika mechi ya ligi.
 
Simba yashindwa kwenda Brazil
• Atletico ya kweli yaichapa Corinthias Brazil

na Waandishi wetu


MABINGWA wa soka Tanzania Bara, Simba ya jijini Dar es Salaam, jana walishindwa kukata tiketi ya kwenda Brazil kurudiana na Atletico Paranaense baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 na timu hiyo, katika mchezo wa kirafiki ulipigwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Simba ambao jana walionyesha kandanda safi na kukitawala kipindi cha kwanza, walifanya shambulizi lingine dakika ya 15 kupitia kwa Rashid Gumbo na Mussa Hassan Mgosi na kupata kona doto mbili, ambazo ziliokolewa na mabeki wa Atletico.
Timu hizo ziliendelea kushambuliana kwa zamu ambapo Simba ilifanikiwa kujipatia bao la kuongoza dakika ya 44 baada ya Mgosi kuunganisha krosi safi ya Gumbo ambaye jana alionyesha kiwango kizuri; bao ambalo lilidumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi ambapo Simba waliendelea kucheza kwa kuonana na kulisakama lango la Atletico, lakini washambuliaji wake walishindwa kutumia nafasi nyingi walizozipata.
Wabrazil hao walipata pigo dakika ya 66 baada ya beki wao Bruno Costa kupewa kadi nyekundu baada ya kumkwatua Ochieng, lakini waliendelea kucheza kwa ‘jihadi’ na kufanikiwa kupata bao la kusawazisha dakika ya 81 kupitia Ramon Machada ambaye alifanikiwa kuwatoka mabeki wa Simba na kuachia shuti lililomuacha kipa Juma Kaseja akiwa ameduwaa.
Simba: Juma Kaseja, Juma Jabu, Haruna Shamte, Juma Nyoso, Meshack Abel, Jerry Santo, Rashid Gumbo Patrick Ochieng, Mohammed Banka, Mgosi na Mbwana Samatta.
Katika hatua nyingine, wakati ikidaiwa kuwa hapa nchini kuwa mechi mbili za kimataifa za kirafiki dhidi ya klabu za Yanga na Simba za jijini Dar es Salaam, Atletico Paranaense ya Brazil, imeendelea na mechi zake za Ligi Kuu ya Brazil ‘Serie A’ ambapo usiku wa kuamkia jana Alhamisi, ilikuwa ikichuana na Corinthians PR na kushinda ugenini.
Kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo, inayonolewa na kocha Mbrazil, Sergio Soares, mechi hiyo ilichezwa kwenye dimba la Estádio Janguito Malucelli, mjini Curitiba, katika Jimbo la Paraná nchini humo na Atletico kuwaduwaza wenyeji wao kwa mabao 2-1 na kujisogeza juu katika msimamo wa ligi hiyo.
Adriano Gabiru wa Corinthians, alitangulia kuwapatia bao wenyeji bao kunako dakika ya 35 ya mchezo huo na hadi filimbi ya mapumziko inapulizwa, wenyeji walikuwa mbele kwa bao hilo, huku Atletico wakiwa hawajapata kitu.
Kipindi cha pili, mshambuliaji, Henan Faria Silveira, aliisawazishia Atletico dakika ya 78 ya mchezo huo, kabla ya kiungo mshambuliaji, Madson Formagini Caridade, kuifungia bao la ushindi dakika ya 80 na kuibua shangwe za mashabiki wachache waliosafiri na timu hiyo.
Katika muendelezo wa mechi za klabu hiyo, Jumamosi Januari 22, Atletico Paranaense inatarajia kurudi kwenye dimba la nyumbani la Arena da Baixada, (zamani Estádio Joaquim Américo Guimarães), linalobeba watazamaji 37,490, kuwakaribisha Iraty katika michuano ya Kombe la Copa do Brasil, kabla ya Jumatatu Januari 30 kuwakaribisha Roma Esporte de Apucarana katika mechi ya ligi.
 
TFF yakiri udhaifu wa utendaji


na Ruhazi Ruhazi


KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Angetile Osiah ‘Ngeta', jana alikiri udhaifu kwa watendaji wa shirikisho hilo ambao wamesababisha kutotolewa kwa leseni ya mshambuliaji mpya wa Majimaji ya Songea, Ulimboka Mwakingwe ‘Uli'.
Osiah aliwaambia waandishi wa habari jijini Dar es Salaam kuwa watendaji walishindwa kuwasiliana, hivyo kusababisha leseni ya mchezaji huyo kutopatikana mapema kama wenzake.
Alisema, hata hivyo baada ya klabu yake kulalamika, wamebaini kuwa ni makosa ya watendaji ndio yaliyosababisha mchezaji huyo asipatiwe leseni yake, hivyo kushindwa kuitumikia klabu yake hadi sasa.
"Suala la Mwakingwe lilitokana na mawasiliano mabovu kati ya watendaji wa TFF, lakini tumeshalimaliza tatizo hili na kiongozi wao alikuja kuichukua leo ‘jana;' hivyo kama itawahi ataruhusiwa kucheza mechi yao ya leo ‘jana'," alisema Osiah.
Aidha Osiah alisema kuwa TFF imewapa mwongozo wale wote wanaozialika timu kutoka nje ya nchi kwa nia ya kuja kucheza nchini, kwamba kuanzia sasa watalazimika kuacha kiasi cha fedha ya utangulizi kama dhamana ili kuepuka suala la waratibu kuingia mitini na kuziacha timu zikitaabika.
"Hatutaki tukumbwe na aibu ya timu kutelekezwa, hivyo tumetoa mwongozo kwa wote watakaotaka kuzileta timu kutoka nje na pia tumewaambia kuwa watalazimika kuweka kwanza Deposit," alisema Osiah.
 
Poulsen visingizio kibao

Imeandikwa na Evance Ng'ingo; Tarehe: 21st January 2011 @ 08:36

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars Jan Poulsen amesema safu yake ya ulinzi haikuwa ya kuridhisha ndiyo maana walifungwa mabao mengi katika michuano ya Bonde la Mto Nile iliyomalizika Jumatatu wiki hii mjini Cairo, Misri.

Poulsen aliyasema hayo alipozungumza na waandishi wa habari jana juu ya safari ya Misri, ambapo Stars ilifungwa mabao 5-1 na Misri, ikatoka sare ya bao 1-1 na Burundi na Uganda kabla ya kufungwa mabao 2-1 na Sudan.

"Nashangazwa na magoli mengi tuliyofungwa yalikuwa ni ya kichwa hali inayoonesha kuwa beki haikuwa ya kuridhisha," alisema.

Alisema kuwa tofauti na mwaka jana ambapo walishinda mechi sita, kutoka sare mechi mbili na kupoteza mechi mbili pia, lakini mwaka huu wamefungwa michezo miwili, sare mbili na hawakushinda katika michezo minne waliyocheza.

Poulsen alisema, kingine kilichowafanya waboronge kwenye michuano hiyo ni maandalizi madogo waliyoyafanya.

Alisema kuwa tofauti na michuano mingine kama vile Chalenji iliyofanyika mwishoni mwa mwaka jana timu yake hiyo iliandaliwa vyema na iliweza kushinda lakini michuano ya Mto Nile maandalizi yalikuwa ni ya kushtukiza.

Alisema kuwa ili timu hiyo kuweza kujiandaa vyema na michuano mingine mikubwa inatakiwa kupata michezo mingi hasa kutoka timu za bara la Ulaya na America ili kujifunza aina nyingine ya mchezo.

Alisema, kwa muda mrefu maandalizi yao yamekuwa ni kujipima na nchi za Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi lakini ni vyema wakajipima zaidi kwa Brazil na nchi nyingine kubwa.

Alifafanua kuwa kwa sasa anajiandaa kuifundisha timu namna ya kuikabili Jamhuri ya Kati katika mechi itakayofanyika Machi mwaka huu ambapo anatafuta video za michezo ya timu hiyo.

Akizungumzia suala la mabadiliko ya wachezaji ayafanyayo kama yana athari kwa timu, alisema kuwa wachezaji wanafundishwa fomula ya mchezo hivyo haoni kama kuna tatizo katika kuwabadilishabadilisha.

Kuhusu mchezaji Gaudensi Mwaikimba, Poulsen alisema kuwa mchezaji huyo amepewa nafasi mara mbili na kushindwa kuonesha uwezo hivyo sio busara kuendelea kumuita.

Pia alifafanua kuwa kwa sasa inatakiwa nguvu zaidi kuwekezwa kwa wachezaji wa timu ya vijana kwa kuwa ndio watakaoweza kuibeba timu ya Taifa.

" Mfano ni kama kwa timu ya Rwanda ambao inafanya vyema sana nchini kwao ikilinganishwa na timu ya vijana ya nchi nyingi kwa sasa, tuwekeze huko zaidi ili tufanikiwe," alisema.

 
Nyota wa BSS ajivunia kukubalika

Imeandikwa na Joachim Nyambo, Mbeya; Tarehe: 22nd January 2011 @ 08:08

MSANII wa muziki bongoflava Beatrice William amesema mwaka 2010 ulikuwa wa mafanikio makubwa katika kazi yake kutokana na kuonekana kukubalika na mashabiki wa fani hiyo.

Akizungumza na HABARILEO mjini hapa jana, Beatrice aliyevuma mwaka jana na wimbo wa ‘Acha waone' alisema katika ziara alizofanya alibaini kazi zake kukubalika hali inayomfanya aone sasa anakaribia kutimiza ndoto yake kimuziki.

Msanii huyo ambaye ni zao la shindano la kuibua vipaji vya muziki nchini la Bongo Star Search (BSS) alisema tayari amekamilisha albamu yake aliyoipa jina la ‘Beatrice' iliyo na nyimbo 10.

Alisema albamu hiyo tayari ameiwasilisha kwa wakala wa usambazaji kazi za sanaa nchini GMC.

Beatrice alisema ameamua kuipa albamu hiyo jina lake kwa sababu nyimbo zote 10 zilizomo ni kali na ametumia muda mwingi kuitafutia jina, lakini akaona kuipa jina la wimbo mmoja kati ya zilizomo ni kutozitendea haki nyingine.

"Namshukuru Mungu mwaka jana nimekubalika na naamini huo ulikuwa mwanzo mzuri. Lakini nawataarifu mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwa sababu albamu yangu iko tayari na nimeipeleka kwa GMC hivyo, nasubiri kuitwa kwa ajili ya mikakati zaidi," Alisema Beatrice.

Alizitaja nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo ya kwanza katika maisha yake ya muziki kuwa ni pamoja na uliomtambulisha zaidi kwa wapenzi wa bongoflava ‘Acha waone', ‘Galuka', ‘Cheki sana', ‘Usikate tamaa' na ‘Acha hivyo'.

Nyimbo nyingine kwa mujibu wa Beatrice ni ‘Nakupenda sana', ‘Ndiyo sababu', ‘Mbele kwa mbele' na ‘Siri ya maisha na Dancefloor'.

Aliongeza kuwa albamu hiyo ilikamilika mwishoni mwa mwaka jana, lakini hakuona sababu ya kuingiza sokoni albamu hiyo Desemba na kuona ni vyema akafanya hivyo mwaka huu.

Alitoa mwito kwa wasanii nchini kujenga moyo wa kujituma na kujitolea hususan pale wanapopewa mialiko katika shughuli za kijamii akisema wasanii wengi wamekuwa wakizikimbia kwa sababu hazina maslahi.

 
Michuano ya gofu kufanyika viwanja vya JWTZ

Imeandikwa na Mbonile Burton; Tarehe: 22nd January 2011 @ 08:08

KLABU ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo imeandaa mashindano ya gofu ya aina yake yatakayofanyika Januari 29 kwenye viwanja vya klabu hiyo.

Akizungumza na HABARILEO Dar es Salaam jana, nahodha wa gofu klabuni hapo Sammuel Hagu alisema mashindano hayo yajulikanayo kama Bull of the Year 2010 (Fahali wa mwaka 2010) yatakuwa ya viwanja 54 na yatafanyika kwa siku moja.

Alisema kuwa mashindano hayo yamepangwa kufanyika kwa mtindo wa stable ford.

Kwa hali hiyo wachezaji watalazimika kucheza mizunguko mitatu ya viwanja 18 kwa siku, hali ambayo itakuwa ni mtihani mkubwa hasa kutokana na joto kali la Dar es Salaam.

"Yatakuwa mashindano magumu, lakini ndio nia yetu, ndio sababu tumeyaita bull, yeyote atakayefanikiwa kumaliza ndio atakuwa mshindi bila kujali pointi alizokusanya."

Hagu aliongeza kuwa hata kwenye marathon mpambano unakuwa mgumu na sio wote wanaoweza kumaliza hivyo, ndio sababu wameandaa mashindano hayo.

Alisema, mshindi wa kwanza hadi wa tatu wataondoka na zawadi nono. Hagu alisema pia kutakuwa na kundi la wasindikizaji ambalo wachezaji watapambana katika viwanja 36 na washindi wawili wataondoka na zawadi.

Pia alisema kutakuwa na zawadi ya mshindi kwa wanawake kwenye mashindano hayo ambayo kiingilio kitakuwa Sh 10,000.

Alisema, klabu mbalimbali zimealikwa kushiriki kwenye mashindano hayo ya aina yake.

 
Michuano ya gofu kufanyika viwanja vya JWTZ

Imeandikwa na Mbonile Burton; Tarehe: 22nd January 2011 @ 08:08

KLABU ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo imeandaa mashindano ya gofu ya aina yake yatakayofanyika Januari 29 kwenye viwanja vya klabu hiyo.

Akizungumza na HABARILEO Dar es Salaam jana, nahodha wa gofu klabuni hapo Sammuel Hagu alisema mashindano hayo yajulikanayo kama Bull of the Year 2010 (Fahali wa mwaka 2010) yatakuwa ya viwanja 54 na yatafanyika kwa siku moja.

Alisema kuwa mashindano hayo yamepangwa kufanyika kwa mtindo wa stable ford.

Kwa hali hiyo wachezaji watalazimika kucheza mizunguko mitatu ya viwanja 18 kwa siku, hali ambayo itakuwa ni mtihani mkubwa hasa kutokana na joto kali la Dar es Salaam.

“Yatakuwa mashindano magumu, lakini ndio nia yetu, ndio sababu tumeyaita bull, yeyote atakayefanikiwa kumaliza ndio atakuwa mshindi bila kujali pointi alizokusanya.”

Hagu aliongeza kuwa hata kwenye marathon mpambano unakuwa mgumu na sio wote wanaoweza kumaliza hivyo, ndio sababu wameandaa mashindano hayo.

Alisema, mshindi wa kwanza hadi wa tatu wataondoka na zawadi nono. Hagu alisema pia kutakuwa na kundi la wasindikizaji ambalo wachezaji watapambana katika viwanja 36 na washindi wawili wataondoka na zawadi.

Pia alisema kutakuwa na zawadi ya mshindi kwa wanawake kwenye mashindano hayo ambayo kiingilio kitakuwa Sh 10,000.

Alisema, klabu mbalimbali zimealikwa kushiriki kwenye mashindano hayo ya aina yake.

 
Atletico yaongoza kwa kucheza rafu, kutoa mpira nje Friday, 21 January 2011 20:23

Beki wa timu ya Atletico, Fransegio Barbosa akijiandaa kumkabili mshambuliaji wa Simba, Mussa Hassan Mgosi wakati wa mechi ya kirafiki ya kimataifa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Picha na Jackson Odoyo

Calvin Kiwia
PAMOJA na mabingwa wa ligi ya Vodacom Tanzania bara,Simba kutoka sare ya 1-1 na Atletico Paraniense ya Brazili mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam Wabrazili hao waliongoza kutoa mpira nje na kucheza rafu.

Atletico Paraniense ilitoa mpira nje mara 23, wakati Simba ikitoa 19, ilicheza rafu 12 ambazo zilipelekea wachezaji wake wawili kupewa kadi za njano na nyekundu kwa Bruno Batista aliyetolewa kwa kuchezea vibaya Patrick Ochan na Leonardo da Silva aliyezawadiwa kadi ya njano.

Simba liweza kufika langoni kwa Atletico mara 11 wakati wapinzani wao walifika mara 9 na kupata kona mbili kwenye mchezo huku Simba ikipata tatu.

Mshambuliaji wa Simba, Musa Mgosi aliongoza kwa kuoteamara zote tatu wakati Wabrazili waliotea mara mbili.

Kwa upande wa Simba, Meshack Abel aliongoza kutoa mpira nje akiwa ametoa mara tisa dhidi ya 19, walizotoa timu hiyo huku beki wa kushoto wa Atletico Bruno Costa akiongoza kwa upande wa timu yake akiwa ametoa mara 14 dhidi ya 23 ilizotoa timu yake.

Mohamed Banka na Jerry Santo ndio waliongoza kwa kutoa pasi mbovu kwenye mchezo huo, Banka alitoa pasi tano kwa Atletico wakati Santo akitoa pasi nne ambazo zilishindwa kuwafikia walengwa.

 
Kiwango champa marafiki Ochan
Friday, 21 January 2011 20:18

Sweetbert Lukonge
UWEZO mkubwa wa kusakata soka ulionyeshwa na kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Simba, Patrick Ochan katika mchezo wa fainali ya Mapinduzi na ule wa kirafiki dhidi ya Atletico ya Brazil umemuongezea marafiki ndani ya klabu hiyo.

Akizungumza na Mwananchi juzi mara baada ya kumalizika kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Atletico, Ochan alisema mapokezi mazuri aliyopata kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo yameonyesha marafiki ndani ya klabu hiyo.

Alisema baada ya mechi ya Fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Yanga alipofanikiwa kutoa pasi za mwisho za mabao yote mawili yaliyofungwa na Musa Mgosi pamoja na Shija Mkina kwa hakika mashabiki wengi walibadili mtazamo wao na kumwona kuwa anahitajika katika kikosi hicho.

"Ninafurahi kupata marafiki wengi kwa sasa katika timu yangu kwani hapo mwanzoni baada ya kujiunga na Simba kwa hakika sikuwa na marafiki wengi kama iilivyo sasa baada ya mechi ya dhidi yaYanga na mchezo wa leo (juzi) dhidi ya Atletico.

"Mapokezi makubwa niliyoyapata kutoka kwa mashabiki wengi walikuwa wamefurika uwanjani hapa huku wengine wakionekana kupinga maamuzi ya kocha kunitoa uwanjani na nafasi yangu ikachukuliwa na Ally Shibori kusema kweli yamenifariji na kujiona kuwa sasa nihatajika kuitumikia Simba kwa mafanikio zaidi," alisema Ochan.

Katika hatua nyingine mchezaji huyo wa kimataifa kutoka nchini Uganda amewataka wapenzi na mashabiki wa timu hiyo kuendelea kuwaunga mkono wachezaji wote wa timu hiyo katika harakati zao za kuwania ubingwa Ligi Kuu ikiwa ni pamoja na kufanya vizuri katika mashindano ya kuwania ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…