Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Wasanii Moro kuhamasisha Katiba mpya


na Joseph Malembeka, Morogoro


MJADALA wa haja ya kuandikwa Katiba mpya hapa nchini umeingia katika hatua nyingine baada ya taasisi isiyo ya kiserikali ya 'Tanzania Youth Culture Development Centre (TYCDC), ya mjini hapa kukusudia kuanzisha shindano la msanii bora wa maandalizi ya katiba mpya kupitia sanaa. Mwenyekiti Mtendaji wa TYCDC, Mwajabu Kibwana alisema hayo mjini hapa na kuongeza kuwa, lengo la kituo hicho kuanzisha mpango huo ni kuongeza msukumo kwa wananchi kuielewa, ili washiriki vema katika kutoa maoni sahihi jinsi wanavyotaka katiba hiyo iwe.
"Mbali na ufafanuazi wa Katiba katika mpango kazi huu tunaotaraji kuuanza mwezi ujao, tumekusudia pia kuibua nyimbo za mambo ya kitaifa yanayogusa maisha ya watu, kama kukomesha rushwa, ufisadi na masuala ya uchaguzi na zile za mapenzi ambazo zimezoeleka," alisema Mwajabu.
Mwajabu alisema, mbali na kufanya kazi ya kurekodi na kuzitangaza kazi za wasanii nchini, Taasisi hiyo ilitathimini na kubaini kuwa, ipo haja kwa wasanii hususan muziki na maigizo kushirikishwa katika mchakato huo wa mapambano.
Alisema, tayari wasanii mbalimbali maarufu nchini kutoka mkoani hapa na mikoani, wameonyesha ari ya kushirikisha vipaji vyao katika mchakato huo, akiwamo ‘Mchizi Koto'.
Hii ni taasisi ya pili kuanzisha mashindano mkoani hapa, ambako mbali na kuanzishwa kwa ajili ya kurekodi na kuzitangaza kazi za wasanii, pia inajihusisha na uboreshaji sanaa mkoani hapa.
 
Tamasha la Pasaka 2011 kushirikisha nchi sita


na Dennis Fussi


MSAMA Promotion kwa mara nyingine imeandaa tamasha kubwa la nyimbo za kumsifu Mungu litakalofanyika Sikukuu ya Pasaka Aprili 24 mwaka huu, maarufu zaidi kama ‘Tamasha la Pasaka' kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya ‘Tamasha la Pasaka', Alex Msama, alisema kwamba, tamasha hilo mwaka huu litakuwa na utofauti mkubwa ikilinganishwa na mengine yaliyopita, kwani limeboreshwa zaidi.
Msama alisema kwamba, tamasha la mwaka huu limekuwa na maboresha makubwa kwa ajili ya kukidhi matakwa ya wapendwa wengi.
"Kwanza kabisa, tofauti na matamasha yaliyopita, mwaka huu tutakuwa na waimbaji wengi zaidi wa muziki wa injili kutoka nchi za nje. Kutakuwa na waimbiaji kutoka nchini Kenya, Uganda, Zambia, Afrika Kusini, Rwanda na Jamhuri ya DR Congo, ambapo lengo kubwa ni kulifanya tamasha hili la Pasaka mwaka huu kuwa na utoauti," alisema Msama.
Aidha, Msama aliongeza kuwa, baada ya tamasha hilo jijini Dar es Salaam pia litafanyika katika mikoa ya Shinyanga Jumatatu ya Pasaka Aprili 25 na Mwanza Aprili 26, ambako itakuwa ni sikukuu ya Muungano.
Moja ya maboresho makubwa katika Tamasha la Pasaka mwaka huu, Msama alisema kwamba litakuwa na kiingilio rahisi zaidi, ili kila mmoja aweze kuhudhuria na kupata baraka kutoka kwa waimbaji hao wanaomsifu Mungu.
"Waimbaji wote maarufu wa muziki wa Injili watakuwepo, kwani tumejipanga vizuri mno kuhakiksha kwamba tamasha hili litakuwa gumzo kila mahali. Mwaka jana hatukuweza kuandaa Tamasha la Krismasi, hivyo nguvu zote tumezielekeza katika tamasha hili la Pasaka," alisema Msama.
Msama aliongeza kwamba, kutokana na ukubwa na maboresho mazuri zaidi ya tamasha hilo, kamati ya maandalizi imewashirikisha watu 50, wakiwa ni wachungaji na wainjilisti lengo likiwa ni kuwawezesha watu wengi waweze kubarikiwa kiroho kwa kuwa tamasha hili ni la kumsifu Mungu.
"Wapendwa wajiandae kushiriki kwa wingi, kwani watashiba kiroho kutokana na kuwa na waimbaji wengi wenye hamasa ya kiroho," alisema.
Hata hivyo, alifafanua kuwa mikoa mingine hawajaitupa, bali pia watafika katika mikoa mbalimbali kama vile Mbeya, Dodoma, Iringa, Arusha, Kilimanjaro na mingineyo.
Aidha, Msama alisema kwamba, kwa kuwa tamasha hili lipo kwa ajili ya watu anakaribisha maoni kutoka kila sehemu ya Tanzania na yataheshimiwa lengo likiwa kuliboresha zaidi.
 
Tamasha la Pasaka 2011 kushirikisha nchi sita


na Dennis Fussi


MSAMA Promotion kwa mara nyingine imeandaa tamasha kubwa la nyimbo za kumsifu Mungu litakalofanyika Sikukuu ya Pasaka Aprili 24 mwaka huu, maarufu zaidi kama ‘Tamasha la Pasaka’ kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya ‘Tamasha la Pasaka’, Alex Msama, alisema kwamba, tamasha hilo mwaka huu litakuwa na utofauti mkubwa ikilinganishwa na mengine yaliyopita, kwani limeboreshwa zaidi.
Msama alisema kwamba, tamasha la mwaka huu limekuwa na maboresha makubwa kwa ajili ya kukidhi matakwa ya wapendwa wengi.
“Kwanza kabisa, tofauti na matamasha yaliyopita, mwaka huu tutakuwa na waimbaji wengi zaidi wa muziki wa injili kutoka nchi za nje. Kutakuwa na waimbiaji kutoka nchini Kenya, Uganda, Zambia, Afrika Kusini, Rwanda na Jamhuri ya DR Congo, ambapo lengo kubwa ni kulifanya tamasha hili la Pasaka mwaka huu kuwa na utoauti,” alisema Msama.
Aidha, Msama aliongeza kuwa, baada ya tamasha hilo jijini Dar es Salaam pia litafanyika katika mikoa ya Shinyanga Jumatatu ya Pasaka Aprili 25 na Mwanza Aprili 26, ambako itakuwa ni sikukuu ya Muungano.
Moja ya maboresho makubwa katika Tamasha la Pasaka mwaka huu, Msama alisema kwamba litakuwa na kiingilio rahisi zaidi, ili kila mmoja aweze kuhudhuria na kupata baraka kutoka kwa waimbaji hao wanaomsifu Mungu.
“Waimbaji wote maarufu wa muziki wa Injili watakuwepo, kwani tumejipanga vizuri mno kuhakiksha kwamba tamasha hili litakuwa gumzo kila mahali. Mwaka jana hatukuweza kuandaa Tamasha la Krismasi, hivyo nguvu zote tumezielekeza katika tamasha hili la Pasaka,” alisema Msama.
Msama aliongeza kwamba, kutokana na ukubwa na maboresho mazuri zaidi ya tamasha hilo, kamati ya maandalizi imewashirikisha watu 50, wakiwa ni wachungaji na wainjilisti lengo likiwa ni kuwawezesha watu wengi waweze kubarikiwa kiroho kwa kuwa tamasha hili ni la kumsifu Mungu.
“Wapendwa wajiandae kushiriki kwa wingi, kwani watashiba kiroho kutokana na kuwa na waimbaji wengi wenye hamasa ya kiroho,” alisema.
Hata hivyo, alifafanua kuwa mikoa mingine hawajaitupa, bali pia watafika katika mikoa mbalimbali kama vile Mbeya, Dodoma, Iringa, Arusha, Kilimanjaro na mingineyo.
Aidha, Msama alisema kwamba, kwa kuwa tamasha hili lipo kwa ajili ya watu anakaribisha maoni kutoka kila sehemu ya Tanzania na yataheshimiwa lengo likiwa kuliboresha zaidi.
 
Miss Progress amwaga chozi Arusha


na Mwandishi wetu, Arusha


MISS Progress International, Julieth Lugembe, jana aliangua kilio wakati alipotembelea Shule ya Sekondari Mukidoma mkoani humo na kukutana na watoto wenye ulemavu wa ngozi ‘albino' wanaosoma katika shule hiyo.
Julieth ambaye yuko kwenye ziara ya kujua matatizo wanayokabiliana nayo albino, alishindwa kujizuia kulia baada ya mmoja wa wasichana wanaosoma shuleni hapo kueleza matatizo yake yanayomfanya ashindwe kusoma vizuri.
Msichana huyo, Dorcus Meela, ambaye yuko kidato cha tatu alisema, yeye alifiwa na wazazi wake wote wawili na hana msaada wowote, hali ambayo inafanya asipate mahitaji yake muhimu.
Alisema, ndugu wamemtenga kwa kuwa yeye ni mlemavu wa ngozi na kutokana na tatizo la ngozi yake, hawezi kufanya vibarua ambavyo vingeweza kumpa kipato ili apate fedha za matumizi.
Mwingine, Maria Charles, huku akieleza kuwa mama yake ni mchuuzi katika soko kuu la Moshi, mkoani Kilimanjaro alitanabaisha kuwa:
"Mi huwa nalazimika kuvuta kurudi shule, mama yangu anafanya kazi ambayo haiwezi kunipatia mahitaji muhimu, nakosa viatu, nakosa madaftari, baba yangu aliondoka tangu nilipozaliwa, naishi kwa kusaidiwa tu na watu, kama hapa sina viatu," alishindwa kuendelea kuzungumza na kuangua kilio kilichopokewa na mrembo huyo wa dunia na kufanya ofisi ya mkuu wa shule kupatwa na ukimya kwa muda.

Katika shule hiyo, pia wanafunzi wengine walisema, wazazi wao wengi waliwakimbia baada ya kuzaliwa na hata wale waliopo, hawana uwezo wa kuwasomesha ingawa walishukuru uongozi wa Makidoma kwa kugharamia masomo yao.
Ziara ya Julieth imeratibiwa na Kampuni ya One Touch Solutions inayoandaa shindano la Miss Progress Tanzania na kudhaminiwa na Shirika la Ndege la Precision Air, Kampuni ya simu ya Airtel na Hoteli ya Corridor Springs Arusha.
Matatizo yaliyoelezwa katika ziara hiyo ni pamoja na kukosekana kwa magodoro ya kulalia, vyandarua, madaftari, sabuni, ambako ilielezwa Empirial na Dettol zinawasaidia kwa ajili ya ngozi zao pamoja na lensi kwa ajili ya kusomea.
Akijibu changamoto hizo, Julieth aliahidi kusaidia upatikanaji wa mahitaji hayo na kurejea tena shuleni hapo ili kuona kitakachokuwa kimepatikana.
"Kwakweli inanisikitisha, lakini nawataka msikate tamaa, tutasaidia kuhakikisha tunapunguza haya matatizo hata kama si kumaliza kabisa, lakini naahidi kurudi tena hapa mwezi ujao kuona nini ambacho ninaweza kutatua," alisema.
Awali alionana na watoto wa shule ya msingi, ambao wengi wao walionekana kukosa sare za kanisani, vitabu, madaftari, magodoro na vyandarua.
Julieth yuko katika ziara ya kutambua matatizo yanayowakabili watu na wototo wenye ulemavu wa ngozi, kabla ya kuwapelekea msaada sahihi.
Alipokuwa Shinyanga katika kituo cha Buhangija, mrembo huyo alikuta watoto wanalala watatu watatu katika kitanda kimoja chenye ukubwa wa futi mbili na nusu, hali ambayo ni hatari kwa afya zao.
Watoto hao mbali ya kuomba magodoro na vitanda pia waliomba kupatiwa televisheni ili waweze kujua yanayoendelea duniani.
 
Ni sarakasi tupu Yanga SC


na Makuburi Ally


UNAWEZA kusema ni sarakasi tupu zinaendelea ndani ya klabu ya Yanga, huku hoja kubwa ikiwa utendaji wa mfadhili wa klabu hiyo Yusuf Manji.
Kwa takriban siku nne sasa tangu Januari 21, baada ya viongozi wa matawi ya Yanga chini ya Mwenyekiti wake, Mohammed Msumi, kukutana makao makuu ya klabu hiyo makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani na kutoa maazimio kadhaa ikiwamo kutaka Mwenyekiti, Llyod Nchunga, asimamishwe na Kamati ya Utendaji kwa kukiuka taratibu na utawala huku wakimtuhumu pia Manji kuwa fedha zake ndizo zinaiharibu klabu hiyo.
Baada ya mkutano juzi aliibuka Nchunga na kudai haukuwa halali huku akiapa kuwa hawezi kujiuzulu na kuwa waliohusika kuuandaa watachukuliwa hatua ikiwamo kusimamishwa uanachama.
Wakati hali ikiwa hivyo, jana kwa nyakati tofauti yameibuka makundi mengine mawili nayo yakiwa na hoja mbalimbali.
La kwanza ni wanachama 30 baadhi yao akiwa Shabani Omar, Kondo Kipwata, Thomas Mdeka na wengineo, ambao walidai kuwa Manji ana uwezo mkubwa na nia ya dhati ya kutunza mali za Yanga na kuwa walihudhuriwa mkutano wa Msumi kwa kudanganywa na mambo mengi.
Walisema, baada ya kufanya utafiti walibaini kuwa kikao hicho kilifadhiliwa na adui yao, ambaye anataka kuwavuruga Wanayanga kwa manufaa yake, ingawa hawakumtaja kwa jina.
Walisema shutuma anazotupiwa Manji hazina ukweli kwani Novemba aliuomba uongozi kufuata maagizo ya wanachama ya mwaka 2008 walioagiza kwamba wanataka kujua mahesabu ya fedha za klabu yao.
"Yusuf amekuwa akiwataka viongozi kutoa hesabu za mapato na matumizi katika siku 100 walizokaa ofisini ambayo yanafikia shilingi bilioni moja", walisema.
Waliongeza kuwa mkutano ulielezwa kuwa ilikuwa lengo la Manji kuanzisha kampuni, lakini ukweli ni kwamba suala la kampuni limo kwenye Katiba ya Yanga na hakuna kitu chochote kipya kinachoanzishwa.
Kwa upande wao, wazee wakiongozwa na Yusuf Mzimba nao katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), walitoa wito kwa wanaotaka mfadhili na mdhamini wao Manji aachie madaraka, watoe sababu za msingi zitakazosababisha aachie ngazi.
Mzimba alisema hatua ya wao kutoa kauli hiyo imetokana na mmoja wa wanachama wa Yanga, kutoa tamko kwamba anayevuruga Yanga ni Manji, hivyo hana budi kuachia madaraka hayo.
Mzimba alisema wanaomkataa Manji hawaitakii mema Yanga, kwa sababu wao wanaipenda na Manji ndiye anafanikisha maendeleo ya timu hiyo.
"Manji ndiye analipa makocha, viongozi na masuala mengine yanayoihusu Yanga, yeye anafanikisha, sasa wanachotaka ni kipi? Ama wanataka kuirudisha Yanga ilipotokea kwenye migogoro ambayo ilikuwa kila uchao!" alisema Mzimba.
Mzimba alitoa wito kwa wanachama wa Yanga walioko mikoani kuwaunga mkono kutokana na baadhi ya wenzao kutaka kuchafua hali ya hewa ndani ya klabu hiyo.
Alisema wakimpoteza mfadhili kama Manji, kumpata mwingine kama yeye ni kazi ngumu, kwa sababu walishawahi kumpata Abbas Gulamali ambaye walimpoteza, ndani ya muda wote huo, klabu iliendeshwa kama yatima.
Naye Hassan Hashim Mhika, alimtaja mmoja wa wanachama (jina linahifadhiwa), aliyedai kuwatukana kwa madai kwamba waliitwa na Manji na kuteta nao, hali ambayo iliwaudhi hadi kufikia uamuzi wa kutoa tamko.
Mhika alisema wao si wanachama bali wao ni wazee wa Yanga ambao wako katika timu hiyo tangu haina hata kiti cha kukalia, hivyo vijana wadogo waliokuta maghorofa wawaheshimu.
Mhika alisema wanayetaka achukue nafasi ya Manji ajitokeze wamfahamu na si kupigana vita ya chini chini, la sivyo wamtafutie kazi nyingine hata kama ni uvuvi.
Wazee wengine waliowasindikiza wenzao ni Mussa Mapande, Hashim Mohamed, Yusuf Kupela, Masoud Abdallah, Abdallah Juma, Said Bakari Mtopale, Bilal Chakupewa na Abdallah Rashid.
Katika hatua nyingine, uongozi wa Yanga umeingia mkataba wa mwaka mmoja na Kocha Msaidizi, Fred Felix Minziro kuwa kocha msaidizi akichukua nafasi ya Salvatory Edward.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga, alisema Minziro ni kocha mwenye mipangilio ambayo itaisaidia Yanga kufika mbali kimashindano.
Naye Minziro alisema kwa kuwa kazi yake anaifahamu, yuko tayari kutekeleza maendeleo ya Yanga kwa sababu ndiyo fani yake.
Minziro alisema atampa ushirikiano Kocha Mkuu, Kostadin Papic, kwa sababu ndiye mkuu wake wa kazi.
 
Ni kivumbi Simba vs Azam leo


na Dina Ismail


LIGI Kuu ya soka Tanzania Bara inaendelea tena leo, ambapo mabingwa watetezi Simba ya Dar es Salaam inashuka katika dimba la Uhuru kukwaana na ‘Wauza Koni' Azam FC katika mechi ya mzunguko wa pili wa ligi hiyo.
Simba inatarajiwa kushusha jeshi lake la maangamizi, likiongezewa nguvu na wachezaji wake waliokuwa katika timu ya taifa ‘Taifa Stars' iliyokuwa ikishiriki mashindano ya Nile Basin yaliyomalizika nchini Misri hivi karibuni na wenyeji kutwaa ubingwa.
Mchezo wa leo unatarajiwa kuwa mgumu kutokana na kila timu kuwa na malengo yake, lakini kubwa ni ubora ulizonazo timu hizo, ambazo zimesheheni wachezaji nyota na wenye uwezo wa hali ya juu katika kusakata kabumbu.
Pamoja ubora wa wachezaji wake, kila moja itataka kuibuka na ushindi ili kupata pointi tatu muhimu, huku Simba itaka kuendeleza ubabe kwa Azam na kurejea kileleni, kwani iliikandamiza mabao 2-1 katika mzunguko wa kwanza, wakati Azam itataka kushinda ili kulipa kisasi.
Azam inayonolewa na Mwingereza, Stewart John Hall, pamoja na kutaka kulipiza kisasi, lakini itataka kujipoza machungu ya kufungwa mabao 2-1 na Kagera Sugar katika mechi yao ya fungua dimba ya mzunguko wa pili iliyopigwa Januari 15 mwaka huu.
Hata hivyo Simba chini ya Kocha Patick Phiri wa Zambia, imetamba kuendeleza ubabe si kwa Azam tu, bali kwa timu zote itakazokutana nazo katika mzunguko huo wa lala salama ili kuhakikisha ubingwa unabaki Msimbazi mwaka huu.
Phiri alisema kuwa, mchezo wa leo pia utamsaidia kujua kiwango cha wachezaji wake katika kuelekea mechi ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Elan de Mitsoudje ya Comoro utakaopigwa ugenini Januari 30.
Wakati huo huo, Makuburi Ally anaripoti kuwa, maafande wa JKT Ruvu ya Pwani jana waliwapigisha kwata Toto African ya Mwanza na kuwalaza bao 1-0 kwenye Uwanja wa Uhuru.
Bao la ushindi la JKT lilifungwa na Hussein Bunu katika dakika ya 42.
Katika mechi hiyo, mwamuzi Hashim Abdallah wa Dar es Salaam alimtoa kwa kadi nyekundu Tete Kang'anga wa Toto African baada ya kumchezea vibaya Nashon Naftar wa JKT.



 
Ligi Wanawake Kinondoni sasa Feb. 2


na Makuburi Ally


LIGI ya Soka ya Wanawake Wilaya ya Kinondoni inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Februari 2 kwenye uwanja wa Shule ya Msingi Mwalimu Nyerere, Magomeni jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Chama cha Soka Wilaya ya Kinondoni (KIFA), Frank Mchaki, alisema awali ilikuwa ianze Desemba mwaka jana lakini wakaisogeza mbele kutokana na kutokamilika kwa taratibu za udhamini.
Mchaki alisema, taratibu za udhamini zilishaanza kufanyika, lakini baadaye mdhamini akapata dharura, hivyo wameona ni bora kuahirisha hadi atakaporejea, ambako ataendelea na udhamini wake.
Aidha, Mchaki alisema fomu kwa ajili ya ushiriki wa ligi hiyo zimeanza kutolewa tangu juzi katika uwanja wa Mwalimu Nyerere, itakapochezwa ligi hiyo.
Bingwa mtetezi wa Ligi ya Wanawake Kinondoni ni Mndela Queens huku nafasi ya pili inashikiliwa na Mburahati Queens.
Mchaki alitoa wito kwa wadau wa soka la wanawake, kuleta timu nyingi ili kuleta chachu kwa sababu ligi hiyo ndio kitovu cha ligi ya wanawake Tanzania.
 
Uongozi mpya MRFA wakabidhiwa madeni


na Joseph Malembeka, Morogoro


UONGOZI mpya wa Chama cha Soka Mkoa wa Morogoro (MRFA), umekabidhiwa rasmi ofisi huku ukirithi deni la shilingi 280,000 sambamba na ofisi hiyo kuwa na uhaba wa vitendea kazi.
Mbali na deni hilo lililotokana na mishara ya miezi mitatu kwa mhudumu wa ofisi hiyo na pango, ofisi hiyo ilikuwa na salio la shilingi 40,000 benki.
Katika makabidhiano hayo yaliyofanywa kwa uongozi mpya, mbele ya waandishi wa habari na Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Fikiri Juma katika ofisi za chama hicho zilizopo Uwanja wa Jamhuri mjini hapa juzi, hapakuwa na mpira wowote uliokabidhiwa kwa uongozi huo, mbali na takribani jozi 20 za jezi.
Baadhi ya vitu vingine vilivyokabidhiwa zikiwemo nyaraka za ofisi ni pamoja na kompyuta moja iliyokamilika aina ya Dell, typewriter mbili, printer moja, meza tatu, kombe moja kubwa, picha ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, Bendera ya Taifa na kitabu cha benki.
Akipokea vifaa hivyo, Mwenyekiti mpya wa MRFA, Pascal Kianga, mbali na kushukuru, aliahidi kuiendeleza ofisi hiyo na kuinua matumaini ya wapenzi wa soka mkoani hapa kwa kuinua kiwango cha mchezo huo.
 
10 wateuliwa baiskeli taifa


na Makuburi Ally


CHAMA cha Baiskeli Tanzania (CHABATA), na Chama cha Baiskeli Zanzibar (CHABAZA), vimechagua timu ya wachezaji 10 watakaounda timu ya taifa ya Tanzania.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa CHABATA, Lado Haule, alisema timu hiyo iliteuliwa Januari 9 baada ya mashindano ya kusherehekea Sikukuu ya Mapinduzi.
Haule alisema, iliundwa kamati ya watu sita watakaoiendeleza timu hiyo kabla ya kuikabidhi Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), kwa ajili ya mashindano ya kimataifa Julai.
Alisema kamati hiyo inaundwa na viongozi watatu kutoka Zanzibar na idadi kama hiyo ya Tanzania Bara, ambao watashughulikia masuala ya kambi, fedha, vifaa, michezo ya kimataifa, kuteua kocha, daktari na meneja wa timu.
Aidha, Haule alisema Februari na Machi mwaka huu, timu hiyo itakuwa katika maandalizi ya mashindano ya kimataifa, Aprili hadi Juni timu itakuwa kambini kabla ya kucheza michezo miwili, mmoja Tanzania Bara na wa pili Zanzibar ambao utateua timu ya wachezaji sita kutoka Zanzibar na Bara watakaounda timu ya Tanzania.
Haule aliwataja viongozi wa Zanzibar kuwa ni pamoja na Mwenyekiti wa CHABAZA, Silima Jafar Pande, Katibu Mkuu, Nassor Haji Nassor na Mweka Hazina, Saleh Kijiba Said, wakati wa CHABATA ni Mwenyekiti, Nazir Manji, Katibu Mkuu, Lado Haule na mweka hazina, Mgeni Bilal.
Wachezaji ni pamoja na Hamis Hussein, Richard Laizer, Mussa Milao, Kakaa Milio na Michael Simon wote wa Arusha, wengine ni Seni Konda, Miguru Mahona, Bingwa wa Vodacom Baiskeli Mwanza, Hamis Clement na Juma Pagala wote wa Shinyanga na Juma Lukondya wa Zanzibar.
 
Luvinga aibuka ‘Shujaa wa Safari Lager'


na Hellen Ngoromera


PAUL Luvinga, ametawazwa kuwa mshindi wa tuzo ya ‘Shujaa wa Safari Lager' hivyo kujitwalia kitita cha sh milioni 10 na kuwabwaga wenzake wawili.
Mshindi huyo, mkazi wa Sinza ‘E' jijini Dar es Salaam, aliibuka mshindi juzi usiku hivyo kujizolea kitita hicho sambamba na ngao, katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Kati ya fedha hizo alizopata, sh milioni tatu atatakiwa kuzitumia kwa ajili ya kuanzisha mradi wowote wa kusaidia jamii.
Luvinga alijizolea kura 1,055 kutoka kwa wananchi dhidi ya Messe Shayo wa Bomang'ombe Kilimanjaro aliyepata kura 665, na Leonard Mtepa wa Mwananyamala 138, ambao nao walipewa sh milioni moja kila mmoja.
Baada ya kutangazwa mshindi na Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Milton Mahanga, aliwapongeza washindi pamoja na waandaaji kwa juhudi zao za kusaidia jamii na kuomba kampuni mbalimbali kuiga mfano huo.
Alishinda kutokana na kuanzisha maktaba ya bure mtaani kwake, aliyoipa jina la Uldzungwa, hivyo kuweza kuwasaidia watu wa rika zote wakiwemo wanafunzi kujisomea.
Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya bia ya TBL ambao ndio waandaaji wa tuzo hiyo, David Minja, alisema walianza tuzo hiyo tangu Novemba 24 mwaka jana na waliiandaa ili kutambua juhudi za watu wanaoisaidia jamii.
 

Simba, Azam ni vita Taifa

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 22nd January 2011 @ 23:59

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara,Simba leo watakuwa na mtihani mgumu pale watakapoikabili Azam kwenye mechi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Tanzania Bara itakayochezwa kwenye uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Mechi hiyo ni ya kukata na shoka kutokana na timu hizo zote kupigania kurudi katika nafasi zake za awali kwenye msimamo wa Ligi hiyo.

Simba inaingia uwanjani ikiwa na lengo la kurudi kileleni baada ya kuenguliwa na mtani wake wa jadi Yanga iliyoifanyia mauaji AFC juzi baada ya kuifunga mabao 6-0.

Mabingwa hao watetezi kwa sasa wana pointi 27 wakiwa nafasi ya pili, wakiongozwa na Yanga kwa pointi moja, Yanga ina pointi 28.

Ushindi kwa Simba leo utaifanya kurudi kileleni, hata hivyo mechi hiyo si rahisi kwani Azam ni kati ya timu ambazo huwa zinakomaa zinapokutana na timu kubwa kama Simba na Yanga.

Hata hivyo, Azam ilianza vibaya mzunguko wa pili kwa kufungwa na Kagera Sugar nyumbani kwake Mkwakwani Tanga na kufanya iporomoke hadi nafasi ya tano kwenye msimamo kutoka nafasi ya tatu.

Katika mzunguko huu, Azam iko chini ya kocha Stewart Hall ambaye alipoanza kibarua chake aliahidi kumaliza utawala wa soka kwa timu za Simba na Yanga, na mechi ya leo ndio ya kwanza kwake kukutana na miamba hiyo.

Katika mechi ya mzunguko wa kwanza Azam ilifungwa ikiwa chini ya kocha wa Brazil Itamar Amorin.

Akizungumzia mechi hiyo, kocha wa Simba Patrick Phiri alisema amewaandaa wachezaji wake kwa ushindi kwani lengo lake ni kutetea ubingwa.

"Tunataka kutetea ubingwa, hivyo ni lazima tuanze ushindi kuanzia mechi yetu ya kwanza ya mzunguko wa pili wa ligi kuu,"alisema.

Simba ilicheza mechi yake ya kirafiki ya mwisho dhidi ya timu ya Atletico Paranaence kutoka Brazil Alhamisi iliyopita na kutoka sare ya bao 1-1.
 
Viongozi wa matawi Yanga walidanganywa

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 22nd January 2011 @ 23:57


VIONGOZI wa matawi ya klabu ya Yanga wamejutia kitendo chao ya kukutana Alhamisi iliyopita na kudai kuwa walifanywa hivyo kwa kudanganywa.

Viongozi hao wa matawi walikutana juzi na kutoa maelezo kwa Kamati ya Utendaji ikutane haraka ili imsimamishe Mwenyekiti wa klabu hiy Lloyd Nchunga mpaka hapo mkutano mkuu utakapoamua vinginevyo.

Aidha, viongozi hao walidai kutomtaka mfadhili wao Yusuf Manji kwa madai kuwa mfadhili huyo amekuwa akiwaendesha na kwamba anataka kuinunua Yanga.

Lakini badala yake viongozi hao jana walikutana na kutoa tamko la pamoja kwamba walifanya hivyo bila kufanya uchunguzi lakini baada ya kufanya utafiti wao waligundua kuwa walidanganywa.

Katika taarifa ya viongozi hao wapatao 30, ilisema: "Sisi wanachama tuliohudhuria kikao cha tarehe 21 mwezi wa Januari 2011, katika kikao hicho tulidanganywa mambo mengi, na baadae tulifanya utafiti wetu na kugundua kuwa kikao kile kilifadhiliwa na adui yetu mfanyabiashara mmoja ambaye tulimfukuza Yanga".

"Eti kikao gani cha ndani ya Yanga kinafanyika na waandishi wa habari wakiwa ndani? Tena mwandishi wa adui yetu anakuwa msemaji katika kikao hicho eti ofisa mmoja ambaye alifukuzwa na mfadhili wetu baada ya sisi kumshauri amfukuze tulipogundua anashiriki kuiba mali ya Yanga na ni msaliti wa klabu yetu, ndio anatumika kuwavuruga wanayanga," ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilisema, mkutano huo wa viongozi hao wa matawi ulielezwa kuwa lengo la Manji lilikuwa kuanzisha kampuni kitu ambacho waligundua si kweli kwani suala la kampuni lipo kwenye Katiba ya Yanga na hakuna kitu chochote kipya kilichokuwa kinaanzishwa.

"Barua ya Nchunga kwa Kifukwe (Francis mdhamini wa Yanga) ilikuwa ikitekeleza matakwa ya Katiba na pia ni jambo lililozungumzwa katika mkutano wa Kamati ya Utendaji iliyokutana Novemba 30 mwaka jana na wajumbe wakahudhuria na kupokea posho, wajumbe hao nao wanasema mkutano huo haukuwa halali tunawashangaa,"ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

Baadhi ya viongozi hao waliotoa tamko hilo ni Shaaban Uda Omar, Kondo Kipwata, Thomas Mdeka, Selemani Kato, Mikidadi Jagalaga, Masoud Saad na Ally Buto.

Naye Evance Ng'ingo anaripoti kuwa Wazee wa klabu ya Yanga wamewataka wanachama wa klabu hiyo wasiomtaka Manji kujiondoa uanachama.

Akizungumza kwa niaba ya wanachama 21 waliozungumza na waandishi wa habari jana katika ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo, Yusuph Mzimba alisema kuwa wanachama hao wanatumiwa.

 

Minziro atambulishwa rasmi Jangwani

Imeandikwa na Evance Ng'ingo; Tarehe: 22nd January 2011 @ 23:55

KOCHA msaidizi wa Yanga Freddy Minziro jana alitambulishwa rasmi katika klabu hiyo kazi iliyofanywa na Mwenyekiti Lyod Nchunga.

Minziro baada ya kutambulishwa alielezea mikakati yake ya kuinoa klabu hiyo na kusisitiza kuwa yupo tayari kufanya kazi na kocha mkuu Kostadin Papic ambaye mwanzo alikaririwa na vyombo vya habari akidai kuwa hakuwa tayari kufanya kazi na Minziro.

Alisema kuwa ataipeleka Yanga katika kiwango kikubwa zaidi ikiwa pamoja na kuimarisha kikosi hicho.

Minziro keshawahi kuichezea Yanga na kuifundisha mara kadhaa.

Kabla ya kujiunga na Yanga kwa mara nyingine, alikuwa akiifundisha timu ya vijana ya Ruvu Shooting ambayo iliibuka na ushindi wa Kombe la Uhai mwezi huu.

Nchunga alisema wameingia mkataba wa kocha huyo kwa mwaka mmoja na kwamba alishakutanishwa na Papic ambapo kila mmoja ameridhia kufanya kazi na mwenzake.
 
Mapunda, Mwaikimba bado waiota Stars

Imeandikwa na John Nditi, Morogoro; Tarehe: 22nd January 2011 @ 23:50

MLINDA mlango wa zamani wa timu ya Yanga na Taifa Stars, Ivo Mapunda pamoja na mshambuliaji wa zamani wa timu hizo Gaudence Mwaikimba wamejitokeza na kusema kuitwa kwao ama kutoitwa kwenye timu ya Taifa kupo mikononi mwa Kocha Mkuu Jan Poulsen.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti mjini hapa, mlinda mlango huyo aliyekuwa namba moja katika kikosi cha Yanga na timu ya Taifa chini ya Kocha Marcio Maximo ambaye hivi sasa anadakia African Lyon, alisema kuwa bado ndoto yake ya kurejea kuichezea timu ya Taifa haijafa.

"Kama mchezaji nitasema bado ndoto yangu kuwa siku moja nitaitwa na Mwalimu kuichezea timu ya Taifa, " alisema Mapunda.

Alisema, hata hivyo bila kuwepo kwa mabadiliko ya kuingizwa kwa damu changa ya wachezaji chipukizi na wenye vipaji timu ya Taifa itaendelea kufanya vibaya katika michuano yake kwa vile nchi nyingi za Kiafrika na Duniani zimewekeza katika soka la vijana.

"Hii kasumba ya kutafuta wachezaji wenye majina na timu kubwa haitusaidii kama taifa, wapo wachezaji wazuri vijana wadogo wenye kujituma ni vyema wakapewa nafasi ya kujaribu kuonesha uwezo wao kwenye kikosi cha timu ya Taifa" alisema Mapunda.

Alisema nchi kama Rwanda na Burundi na nyingine za Magharibi zimefanikiwa kuwa na vikosi imara kwa kuundwa na wachezaji vijana jambo ambalo Shirikisho la Soka Tanzania ( TFF) kutakiwa kulikazania hilo.

"Umri wangu ndiyo huo unakwenda ni wakati wa kuwapa vijana kuichezea timu ya Taifa wanaweza kufanya vizuri kutokana na maumbo yao," alisema Mapunda.

Naye Mshambuliaji wa zamani wa timu ya Yanga ambaye hivi sasa anaichezea Kagera Sugar, Mwaikimba, alisema bado anajiona ni mchezaji mwenye uwezo katika safu ya ushambuliaji na kutokuwemo kwenye kikosi cha timu ya Taifa hakumaanishi uwezo wake umeshuka.

" Wapo wanaonibeza kuwa uwezo wangu umeshuka katika safu ya ushambuliaji huo ni mtazamo wao wanaofikiria hivyo mimi bado uwezo wangu upo juu na kutochaguliwa kujiunga na timu ya Taifa hili ni jukumu la Kocha Mkuu na si mtu mwingine," alisema Mwaikimba.

Alisema sifa ya kuwa mshambuliaji ni kufunga mabao na kwamba katika Ligi Kuu ni kati ya wachezaji wanaoifungia mabao timu yake na kwamba ataendelea kufanya vizuri zaidi katika mzunguko wa pili wa ligi.

" Nafikiri watu wanapenda kumhukumu mtu bila kujali mchango wake katika timu iwe klabu ama kikosi cha Taifa nina imani ipo siku mwalimu wa timu ya Taifa ataniona na kuniita kwenye kikosi chake wapo wachezaji wanaojiona kuwa wao ndio wanaofaa kuichezea timu hii miaka nenda rudi na hawataki mwingine akiitwa,"alisema.

Hata hivyo Kocha Mkuu wa Stars Jan Poulsen alisema mwishoni mwa wiki kuwa ameshamwita mchezaji huyo mara mbili lakini ameshindwa kutumia nafasi.

 
Ligi ngumu- Kocha A. Lyon

Imeandikwa na John Nditi, Morogoro; Tarehe: 22nd January 2011 @ 23:45

KOCHA Mkuu wa timu ya African Lyon , Jumanne Charles, amesema bado mwelekeo wa Ligi Kuu katika mzunguko wa pili ni mgumu na kwamba hakuna timu yenye kujipa matumaini ya moja kwa moja ya kutwaa ubingwa wa Tanzania Bara pamoja na zenye hatari ya kushuka daraja msimu huu.

Charles alisema hayo juzi mjini hapa baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya timu ya Maji Maji ya mjini Songea uliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri wa mjini hapa na kutoka sare ya mabao 2-2.

Mchezo huo ulikuwa wa vuta ni kuvute na uliotawaliwa na kadi tatu nyekundu dhidi ya wachezaji wawili wa Maji Maji na mmoja wa African Lyon.

Hata hivyo timu ya Maji Maji ikiwachezesha baadhi ya wachezaji wake iliowasajili katika dirisha dogo, akiwemo Ulimboka Mwakingwe na Mohamed Kijuso wote kutoka Simba, ndiyo iliyoonesha kiwango kizuri cha mchezo huo lakini mapungufu ya wachezaji hao kulitoa mwanya kwa wapinzani wao kusawazisha bao hilo.

Kwa mujibu wa kocha Charles ligi bado ngumu kwa vile timu zote hazitaki kushuka daraja na zile zilizokuwa kileleni zinaongeza kasi ya kutaka kuendeleza wimbi la ushindi ili kujihakikishia zinatwaa ubingwa wa Tanzania Bara msimu huu.

Hata hivyo alisema kuwa matokeo hayo ya mchezo huo si mazuri kwake lakini moja ya mikakati aliyoiweka ni kuendelea kuzinoa idara zote ili kuwezesha kupata ushindi katika michezo mingine.

Pamoja na hayo alisema mkakati uliopo kwa hivi sasa ni kujinoa zaidi ili kuweza kuikabili Simba katika mchezo wao unaofuatia utakaofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

 
Wenye ulemavu wa ngozi wamliza Miss Progress

Imeandikwa na Mwandishi Wetu MISS; Tarehe: 22nd January 2011 @ 23:40 Imesomwa na watu: 17; Jumla ya maoni: 0



Mtoto Fatma akimbusu Miss Progress Julieth Lugembe (kulia) alipotembelea shuleni kwao Mukidoma, Arusha juzi.



Progress International, Julieth Lugembe, jana aliangua kilio wakati alipotembelea Shule ya Sekondari Mukidoma kukutana na watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaosoma katika shule hiyo.

Julieth ambaye yuko kwenye ziara ya kujua matatizo wanayokabiliana nayo wenye ulemavu huo, alishindwa kujizuia kulia baada ya mmoja wa wasichana wanaosoma sekondari kueleza matatizo yake yanayomfanya ashindwe kusoma vizuri.

Msichana huyo Dorcus Meela ambaye yuko kidato cha tatu katika shule hiyo alisema yeye alifiwa na wazazi wake wote wawili na hana msaada wowote hali ambayo inafanya asipate mahitaji yake muhimu.

Alisema ndugu wamemtenga kwa kuwa ni mlemavu wa ngozi na kutokana na tatizo la ngozi yake hawezi kufanya vibarua ambavyo vingeweza kumpatia kipato ili apate pesa ya kuondoa matatizo.

Mwingine Maria Charles huku akieleza kuwa mama yake ni mchuuzi katika soko kuu la Moshi, mkoani Kilimanjaro alisema:

"Mi huwa nalazimika kuvuta kurudi shule, mama yangu anafanya kazi ambayo haiwezi kunipatia mahitaji muhimu, nakosa viatu, nakosa madaftari, baba yangu aliondoka tangu nilipozaliwa naishi kwa kusaidiwa tu na watu, kama hapa sina viatu," alishindwa kuendelea kuongea na kuangua kilio kilichosababisha na Mrembo huyo wa Dunia kufanya ofisi ya mwalimu mkuu kupatwa na ukimya kwa muda.

Katika shule hiyo pia wanafunzi wengine walisema wazazi wao wengi waliwakimbia baada ya kuzaliwa na hata wale waliopo hawana uwezo wa kuwasomesha ingawa walishukuru uongozi wa Makidoma kwa kugharamia masomo yao.

Ziara ya Julieth imeratibiwa na Kampuni ya One Touch Solutions inayoandaa shindano la Miss Progress Tanzania, na kudhaminiwa na Shirika la Ndege la Precision Air pamoja na Kampuni ya simu ya Airtel na Hoteli ya Corridor Springs Arusha.

Matatizo yaliyoelezwa katika mazungumzo hayo ni pamoja na kukosekana kwa magodoro ya kulalia, vyandarua, madaftari, sabuni ambapo ilielezwa Emperial na Dettol zinawasaidia kwa ajili ya ngozi zao pamoja na lensi kwa ajili ya kusomea.

Akijibu kauli zao, Julieth aliahidi kusaidia upatikanaji wa mahitaji hayo na kuahidi kurejea tena shuleni hapo ili kuona nini kitakuwa kimepatikana.

"Kwakweli inanisikitisha lakini nawataka msikate tamaa tutasaidia kuhakikisha tunapunguza haya matatizo hata kama si kumaliza kabisa lakini naahidi kurudi tena hapa mwezi ujao kuona nini ambacho ninaweza kutatua," alisema.

Awali alionana na watoto wa shule ya msingi ambao wengi wao walionekana kukosa sare za kanisani, vitabu, madaftari pamoja na magodoro na vyandarua.

Julieth yuko katika ziara ya kutambua matatizo yanayowakabili watu na wototo wenye ulemavu wa ngozi kabla ya kuwapelekea msaada sahihi.

Alipokuwa Shinyanga katika kituo cha Buhangija, mrembo huyo alikutana na watoto wanaolala watatu watatu katika kitanda kimoja chenye ukubwa wa futi mbili na nusu hali ambayo ni hatari kwa afya zao.

Watoto hao mbali ya kuomba magodoro na vitanda pia waliomba kupatiwa televisheni ili waweze kujua yanayoendelea duniani.

Pia waliomba kupatiwa madaftari na vitabu vya shule ya msingi.
 
Maandalizi ya Ligi Taifa yaanza Mwanza

Imeandikwa na Grace Chilongola, Mwanza; Tarehe: 22nd January 2011 @ 23:30

KAMATI ya mashindano ya Ligi Kuu Taifa Mkoa wa Mwanza inatarajia kuanza ukaguzi wa viwanja vya michezo vinavyojitosheleza ambavyo vitakavyotumika katika ligi hiyo mkoani hapa.

Katibu wa Kamati hiyo, John Tegete aliliambia gazeti hili kuwa ukaguzi huo unatarajia kuanza mwisho wa mwezi huu kutokana na mashindano hayo kutarajiwa kuanza katikati ya Februari.

Alisema Kamati inataka kuvishirikisha viwanja vyote vya michezo vilivyopo mkoani hapa kutumika katika mashindano hayo hivyo kuziomba wilaya zenye viwanja visivyo na sifa kuanza kuvifanyia ukarabati mapema.

"Natambua Wilaya ya Misungwi hamna kiwanja chenye sifa hivyo tunawapa nafasi ya kurekebisha viwanja vyao vilivyopo kabla ukaguzi haujaanza iwapo wanataka mashindano hayo yafanyike pia katika wilaya yao," alisema Tegete.

Aliongeza kuwa nia ya Kamati ni kusambaza ligi katika viwanja vyote vya Mkoa wa Mwanza. Alisema timu 24 za mpira wa miguu zinatarajia kushiriki mashindano hayo ikiwa ni timu tatu kutoka kila wilaya.

Tegete alisema mwaka huu wanataka kuchezesha Ligi Kuu ya Taifa kisasa kwani hata waamuzi watafanyiwa majaribio ya vitendo na maandishi ili kupata waamuzi timamu.

Alisema anatarajia ligi hiyo itakuwa na ushindani mkubwa kutokana na timu nyingi kujiandaa vizuri hasa za wilaya za Ilemela na Nyamagana.

 
Nyota wa BSS ajivunia kukubalika

Imeandikwa na Joachim Nyambo, Mbeya; Tarehe: 22nd January 2011 @ 08:08
MSANII wa muziki bongoflava Beatrice William amesema mwaka 2010 ulikuwa wa mafanikio makubwa katika kazi yake kutokana na kuonekana kukubalika na mashabiki wa fani hiyo.

Akizungumza na HABARILEO mjini hapa jana, Beatrice aliyevuma mwaka jana na wimbo wa ‘Acha waone' alisema katika ziara alizofanya alibaini kazi zake kukubalika hali inayomfanya aone sasa anakaribia kutimiza ndoto yake kimuziki.

Msanii huyo ambaye ni zao la shindano la kuibua vipaji vya muziki nchini la Bongo Star Search (BSS) alisema tayari amekamilisha albamu yake aliyoipa jina la ‘Beatrice' iliyo na nyimbo 10.

Alisema albamu hiyo tayari ameiwasilisha kwa wakala wa usambazaji kazi za sanaa nchini GMC.

Beatrice alisema ameamua kuipa albamu hiyo jina lake kwa sababu nyimbo zote 10 zilizomo ni kali na ametumia muda mwingi kuitafutia jina, lakini akaona kuipa jina la wimbo mmoja kati ya zilizomo ni kutozitendea haki nyingine.

"Namshukuru Mungu mwaka jana nimekubalika na naamini huo ulikuwa mwanzo mzuri. Lakini nawataarifu mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwa sababu albamu yangu iko tayari na nimeipeleka kwa GMC hivyo, nasubiri kuitwa kwa ajili ya mikakati zaidi," Alisema Beatrice.

Alizitaja nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo ya kwanza katika maisha yake ya muziki kuwa ni pamoja na uliomtambulisha zaidi kwa wapenzi wa bongoflava ‘Acha waone', ‘Galuka', ‘Cheki sana', ‘Usikate tamaa' na ‘Acha hivyo'.

Nyimbo nyingine kwa mujibu wa Beatrice ni ‘Nakupenda sana', ‘Ndiyo sababu', ‘Mbele kwa mbele' na ‘Siri ya maisha na Dancefloor'.

Aliongeza kuwa albamu hiyo ilikamilika mwishoni mwa mwaka jana, lakini hakuona sababu ya kuingiza sokoni albamu hiyo Desemba na kuona ni vyema akafanya hivyo mwaka huu.

Alitoa mwito kwa wasanii nchini kujenga moyo wa kujituma na kujitolea hususan pale wanapopewa mialiko katika shughuli za kijamii akisema wasanii wengi wamekuwa wakizikimbia kwa sababu hazina maslahi.



 

Michuano ya gofu kufanyika viwanja vya JWTZ


Imeandikwa na Mbonile Burton; Tarehe: 22nd January 2011 @ 08:08

KLABU ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Lugalo imeandaa mashindano ya gofu ya aina yake yatakayofanyika Januari 29 kwenye viwanja vya klabu hiyo.

Akizungumza na HABARILEO Dar es Salaam jana, nahodha wa gofu klabuni hapo Sammuel Hagu alisema mashindano hayo yajulikanayo kama Bull of the Year 2010 (Fahali wa mwaka 2010) yatakuwa ya viwanja 54 na yatafanyika kwa siku moja.

Alisema kuwa mashindano hayo yamepangwa kufanyika kwa mtindo wa stable ford.

Kwa hali hiyo wachezaji watalazimika kucheza mizunguko mitatu ya viwanja 18 kwa siku, hali ambayo itakuwa ni mtihani mkubwa hasa kutokana na joto kali la Dar es Salaam.

"Yatakuwa mashindano magumu, lakini ndio nia yetu, ndio sababu tumeyaita bull, yeyote atakayefanikiwa kumaliza ndio atakuwa mshindi bila kujali pointi alizokusanya."

Hagu aliongeza kuwa hata kwenye marathon mpambano unakuwa mgumu na sio wote wanaoweza kumaliza hivyo, ndio sababu wameandaa mashindano hayo.

Alisema, mshindi wa kwanza hadi wa tatu wataondoka na zawadi nono. Hagu alisema pia kutakuwa na kundi la wasindikizaji ambalo wachezaji watapambana katika viwanja 36 na washindi wawili wataondoka na zawadi.

Pia alisema kutakuwa na zawadi ya mshindi kwa wanawake kwenye mashindano hayo ambayo kiingilio kitakuwa Sh 10,000.

Alisema, klabu mbalimbali zimealikwa kushiriki kwenye mashindano hayo ya aina yake.



 

Wadau kujadili soka Iringa leo


Imeandikwa na Frank Leonard, Iringa; Tarehe: 22nd January 2011 @ 08:08

CHAMA cha Soka Mkoa wa Iringa (IRFA) kwa kushirikiana na ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Iringa (RAS) imeitisha kongamano la kimkoa kujadili mustakabali wa maendeleo ya soka mkoani hapa.

Kongamano hilo litakaloshirikisha wadau mbalimbali wa soka mkoani hapa wakiwemo makatibu tawala wa wilaya zote saba za mkoa wa Iringa, litafanyika leo katika Ukumbi wa manispaa mjini hapa.

Kongamano hilo litakuwa la pili kufanywa na wadau wa soka mkoani hapa, baada ya la kwanza kufanyika mwaka 2004 kwa uratibu wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Iringa (IPC).

Akizungumza na HABARILEO mjini hapa jana, Katibu wa IRFA, Elliud Mvella alisema lengo la kongamano hilo ni kuangalia mkoa wa Iringa ulipotoka, ulipo na unapoelekea kisoka huku ikikumbukwa kwamba, kwa mara ya mwisho ilikuwa ni mwaka 1999 Iringa kuwa na timu ya Lipuli Ligi Kuu Tanzania Bara.

Alisema mambo mengine yatakayojadiliwa katika kongamano hilo ni pamoja na utawala wa soka mkoani hapa, muundo wa ligi wilaya na mkoa, masuala yanayohusu waamuzi na makocha, kukuza vipaji vya vijana, na ushiriki wa timu za mkoa wa Iringa katika mashindano ya kitaifa.

Wakati huohuo, Mvella ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) amewataka baadhi ya wanachama wa klabu ya Yanga kuacha chokochoko dhidi ya uongozi uliopo madarakani.

Mvella amesema chokochoko zinazoendelea kuripotiwa kwenye vyombo mbalimbali vya habari, hazina manufaa yoyote kwa maendeleo ya soka la Tanzania.

"Wanachama wanaodhani wanaweza kuwaondoa madarakani viongozi waliochaguliwa kihalali kabla ya kumaliza muda wao wanapoteza muda, kwa sababu viongozi hao hawataondoka hadi muda wao uishe kwa mujibu wa kanuni za sasa za TFF," alisema.


 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…