Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Mabondia kumi kuunda timu ya taifa


Na Amina Athumani

KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya ngumi za riadha, Hurtado Primentel anatarajia kuchagua mabondia 10 wa taifa kwa ajili ya mashindano ya
Mataifa ya Afrika 'All Afrika Game' yatakayofanyika Oktoba mwaka huu Maputo, Msumbiji.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), Makore Mashaga alisema kocha huyo atachagua kikosi hicho katika michuano ya taifa itakayofanyika Februari 26, mwaka huu.

Alisema mbali na kuchagua kikosi hicho ambacho kitaanza mazoezi chini ya kocha huyo pia atachagua wachezaji wengine 10 wa akiba na mabondia vijana 20 wataunda timu ya B ya taifa itakayokuwa chini ya makocha wazawa.

Mashaga alisema tayari BFT, imeshaanza mchakato wa kusaka wafadhili kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo makubwa ya Afrika.

 
Adebayor kukipiga kwa mkopo Real Madrid


MADRID, Hispania

MSHAMBULIAJI wa Manchester City, Emmanuel Adebayor anajiandaa kujiunga Real Madrid kwa mkopo, baada ya klabu hiyo ya Hispania kutangaza
makubaliano yamefikiwa wakati ukitafutwa uwezekano wa kusajiliwa kwa mkataba wa kudumu katika ya majira ya joto.

Suala ya la vipimo kuhusu mchezaji huyo, lilitarajiwa kufanyika jana mjini Madrid kabla ya mkataba huo kusainiwa na endapo vinara hao wa ligi ya Primera Liga, wataamua kumnunua mwishoni mwa msimu huu ada yake itakuwa ni pauni milioni 18.

Ripoti zinaeleza kwamba kocha wa Real Madrid, Jose Mourinho anajivunia kumsainisha mshambuliaji huyo kutokana na mshambuliaji wake, Gonzalo Higuain kuwa majeruhi huku Karim Benzema akiwa ameshindwa kuonesha kiwango chake.

Taarifa iliyotumwa katika tovuti ya klabu hiyo ilisomeka kwamba: "Real Madrid na Manchester City wamefikia makubaliano ambayo itashuhudiwa Emmanuel Adebayor, akicheza kwa mkopo kwenye klabu yake ya zamani.

"Mchezaji atabaki Real Madrid hadi mwishoni mwa msimu huu, wakati klabu ikiangalia uwezekano wa kumnunua," iliongeza taarifa hiyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya timu ya Hamburg, kuiwekea ngumu klabu hiyo ya Bernabeu kumrejesha mchezaji wake wa zamani. Ruud van Nistelrooy mapema mwezi huu na Real ndipo ikaamua kuelekeza nguvu zake kwa mchezaji asiyefanya vizuri Manchester City, Adebayor ambaye anatimiza miaka 27 mwishoni mwa mwezi ujao.
 
Arsenal yapenya fainali Kombe la Ligi


LONDON, Uingereza

ARSENAL imefuzu fainali ya Kombe la Ligi, baada ya kuichapa Ipswich mabao 3-0 katika mechi ya nusu fainali iliyochezwa Uwanja wa Emirates usiku wa
kumkia jana.

Kocha wa timu hiyo, Arsene Wenger amefurahi na kusema kama watatwaa ubingwa huo itawaongezea ari wachezaji wake na kuwafurahisha mashabiki.

Miamba hiyo ya Emirates, ililazimika kusubiri hadi dakika 30 za mwisho kuweza kupata magoli ambayo yataifanya kucheza fainali kwenye Uwanja wa Wembley na kufufua matumaini ya kuanza kupata kombe msimu huu.

Arsenal ilipata mabao mawili ya haraka kupitia kwa Nicklas Bendtner na Laurent Koscielny na kisha kupata bao jingine lililowekwa kimiani na Cesc Fabregas, ikiwa zimesalia dakika 13 na kufanya Gunners kusonga mbele kwa uwiano wa mabao 3-1.

Katika fainali itakayochezwa Uwanja wa Wembley Februari 27, mwaka huu Arsenal watakutana na Birmingham City au West Ham United.

Arsenal ililazimika kujituma ili kuibuka na ushindi, baada ya kufungwa bao 1-0 katika mechi ya kwanza iliyochezwa katika Uwanja wa Portman Road, hadi zilipobaki dakika 15 kipindi cha pili walikuwa bado wako nyuma.

Ipswich ambayo inacheza Ligi Daraja la Kwanza ilicheza kwa kujituma, lakini mshambuliaji wa Denmark, Bendtner ambaye amekuwa akihusishwa na habari za kuondoka katika klabu hiyo katika kipindi cha usajili mdogo mwezi huu, alifunga bao dakika 61, baada ya kupasiwa mpira mrefu na akamfunga kipa, Marton Fulop.

Mlinzi wa Kifaransa, Laurent Koscielny alifunga bao jingine dakika tatu baadaye na kuifanya Arsenal kuwa mbele kwa mabao 2-0 na uwiano kuwa mabao 2-1 .

Mchezaji Jason Scotland alipata nafasi nzuri kuisawazishia Ipswich, lakini shuti lake liliokolewa na Wojciech Szczesny, kabla ya nahodha wa Arsenal, Cesc Fabregas kufunga bao jingine dakika ya 77 akitumia vyema pasi kutoka kwa Andrei Arshavin.

Akizungumzia ushindi huo kocha wa Arsenal, Arsene Wenger alisema hii inaweza kutufanya kupata kombe la kwanza kati ya mengi msimu huu.

"Tunajaribu kushinda kila kitu tunachoweza. Kama tunaweza kushinda hili itakuwa ni presha ya kushinda katika mashindano mengine," alisema.

Alisema msimu huu malengo yao ni kutwaa makombe na kama watafanikiwa hilo wanaweza kufikia malengo mengine.Arsenal haijatwaa kombe katika misimu mitano mfululizo. Katika msimu huu iko katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu England, hivyo kuwa miongoni mwa timu zinazopewa nafasi kutwaa ubingwa pia imo kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Wachezaji wa timu hiyo, pamoja na mashabiki wamekuwa na hamu kubwa ya kuona timu yao ikitwaa kombe la ubingwa wa Ligi Kuu England pamoja na Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambalo hawajawahi kulitwaa pamoja na kufika fainali.

Timu hiyo imekuwa ikitumia wachezaji vijana.
 
Tamasha la Pasaka lawaendea wakali ‘bondeni'


na Mwandishi wetu


amka2.gif
WAJUMBE wa Kamati ya maandalizi ya tamasha la Pasaka ya Msama Promotions wanatarajiwa kwenda nchini Afrika Kusini kukutana na wasanii wa Injili maalumu kuja kupamba tamasha hilo.
Waimbaji hao wa muziki wa Injili watakaoteuliwa, watapata nafasi ya kuja nchini kwa ajili ya kutumbuiza kwenye tamasha kubwa la nyimbo za kumsifu Mungu litakalofanyika sikukuu ya Pasaka Aprili 24 mwaka huu katika ukumbi wa Dimond Jubilee jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati ya Msama Promotions, waandaaji wa tamasha hilo, Alex Msama, lengo la kamati hiyo kwenda nchini humo ni kuangalia waimbaji wa muziki wa Injili wenye majina makubwa, ambao watakuwa na sifa ya kuja kutumbuiza katika tamasha hilo kubwa hapa nchini.
Aidha, Msama alisema, waimbaji wanane wa muziki wa Injili kutoka Kenya na saba wa Rwanda wamethibitisha kushiriki.
"Tumewapata waimbaji nane wa injili kutoka Kenya ambao wamethibitisha kuja nchini kutumbuiza siku ya tamasha la Pasaka na wengine saba kutoka nchini Rwanda," amesema Msama.
Msama aliongeza, kutafanyika mchujo mkubwa kati ya waimbaji hao 15 kutoka Rwanda na Kenya ili kuwapata wawili watakaotumbuiza katika tamasha la Pasaka.
"Ingawa wamethibitisha waimbaji 15 mpaka sasa kutoka nchi mbili za Kenya na Rwanda, lakini tutafanya mchujo kwa ajili ya kuwapata waimbaji wawili kwa ajili ya tamasha hilo," alisema Msama.
Msama alisisitiza kuwa, tamasha la mwaka huu litakuwa na utofauti mkubwa ikilinganishwa na matamasha mengine yaliyopita, kwani limeboreshwa zaidi.
Msama alisema baada ya tamasha hilo la Diamond Jubilee Aprili 25, siku itakayofuata, mashambulizi yatahamia Shinyanga kabla ya kuelekea CCM Kirumba, jijini Mwanza Aprili 26, siku ya Muungano.
 
Filamu ya Shoga hadharani mwezi ujao


na Nasra Abdallah


amka2.gif
FILAMU ya aina yake inayokwenda kwa jina la ‘Shoga' inatarajiwa kuzinduliwa rasmi Februari 4 mwaka huu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, mtunzi wa filamu hiyo, Hissani Muya maarufu kwa jina la ‘Tino', alisema mashabiki watarajie kupata mafunzo ya kutosha kutoka kwenye filamu hiyo, hasa wale wenye tabia hizo za kishoga ambazo sio nzuri na hazipendezi machoni mwa jamii.
Akielezea sababu ya kuigiza filamu yenye maudhui hayo, Muya alisema, ni kipindi kirefu sasa tangu Tanzania izinduke katika uigizaji wa filamu, ambazo nyingi kati ya hizo zikiwa zinaongelea mapenzi kati ya mwanamke na mwanaume, huku ikisahaulika kuwa kuna mahusiano ya namna hiyo kwa jinsia ya wanaume kwa wanaume.
"Mie nimeona nitoke kivingine, kwani ukweli ni kwamba suala hili lipo na kama waigizaji, hatuna budi kutoa elimu ili kuweza kukomesha watu wenye tabia za namna hiyo," alisema Muya.
Aliwataja baadhi ya wasanii ambao amewashirikisha katika filamu hiyo iliyotengenezwa na Sofia Records, kuwa ni pamoja na Chemundu Gwao, Jacqueline Walper, Dude, Aunt Ezekiel, Magali na Miamba, maarufu kwa jina la Pasta pamoja na Tino ambaye ndiye mhusika mkuu.
 
Tamasha la Busara lang'ara Afrika


na Andrew Chale


amka2.gif
TAMASHA la muziki la Sauti za Busara 2011, ambalo hufanyika Februari kila mwaka visiwani Zanzibar, ndilo tamasha pekee kubwa kwa Afrika Mashariki na la tatu barani Afrika katika kuinua sanaa ya muziki na wasanii, imefahamika.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa tamasha hilo, Yusuph Mahmoud ‘DJ Yusuph' wakati wa utambulisho rasmi kwa waandishi wa habari na wadau mbalimbali.
DJ Yusuph alisema kuwa tamasha hilo la Sauti za Busara ambalo mwaka huu litafanyika Februari 9 hadi 13 Ngome Kongwe, ni moja ya matamasha yenye mvuto wa kipekee barani Afrika na ubora wake huo unajidhihirisha kila mwaka, ambapo msimu huu ni wa nane tokea kuanzishwa mwaka 2004.
"Tunajivunia kwa Tamasha la Busara kufanyika Tanzania, hivyo kazi zake zimeonekana sehemu mbalimbali na kwa sasa ndilo pekee Afrika Mashariki kwa upande wa muziki na la tatu kwa Afrika, hivyo ni nafasi ya pekee kujivunia tamasha hili ambalo kila mwaka huileta dunia visiwani Zanzibar," alisema DJ Yusuph.
Aidha, katika utambulisho huo, msanii Juma Nature, ambaye atashiriki kwa mara ya pili kwenye tamasha hilo, alisema kuwa, amejiandaa kuonyesha uwezo wake wa sanaa kwa kuimba ‘live' bila kutumia ‘CD'.
"Mwaka huu nimejiandaa kuonyesha uwezo wangu katika kuimba bila kutumia CD, mimi kama Nature tutafanya kweli pamoja na bendi ya Jagwa," alisema Nature.
Mbali na msanii huyo, kwa upande wake kiongozi wa bendi ya Twanga Pepeta, Luiza Mbutu, alisema kuwa watafanya mambo mapya visiwani humo ili kuonyesha umwamba wao.
Baadhi ya makundi na wasanii watakaoshiriki mwaka huu ni pamoja na Jahazi Modern Taarab, Twanga Pepeta na Mlimani Park Orchestra, Wanyambukwa Artist, Jagwa Music na Nyota Kali Band (Tanzania).
Mengine ni Kwani Experience (Afrika Kusini), Culture Musical Club, Bi. Kidude, Maulidi ya Homu ya Mtendeni, Mohamed Ilyas & Nyota Zameremeta (Zanzibar), Bismillah Gargar (Kenya), Djeli Moussa Diawara (Guinea), Yaaba Funk (Uingereza) na mengineyo.



h.sep3.gif

 
Bonanza la waandishi Februari 12


na Khadija Kalili


amka2.gif
KWA mara nyingine Kampuni ya simu ya Airtel imeandaa bonanza kwa waandishi wa habari litakalofanyika Februari 12 kwenye viwanja vya Posta, Kijitonyama jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Mkuu wa Habari na Mahusiano wa Airtel, Mutta Muganyizi alisema tamasha hilo linatarajiwa kuwakutanisha wanahabari kutoka vyombo mbalimbali vya habari.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha kampuni hiyo, Beatrice Singano, alisema hatua hiyo ina lengo la kuimarisha ushirikiano baina ya Airtel na vyombo vya habari nchini na kwamba, bonanza hilo litaziwezesha pande hizo mbili kufahamiana na kuendeleza mahusiano zaidi.
Alisema wanahabari wamekuwa na mchango mkubwa katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii hivyo wameona moja ya njia ya kuonyesha thamani waliyonayo ni kukutana na kuburudika kwa pamoja kupitia michezo.
Aliongeza kuwa wameandaa burudani na michezo mbalimbali ya kubahatisha, ambako wanahabari wataweza kujishindia zawadi tofauti kutoka Airtel.
Michezo itakayokuwepo ni pamoja na soka, netiboli, kuvuta kamba, mbio za magunia, kuimba na kucheza muziki wa dansi.
Aliongeza kuwa taratibu nyingine kuelekea tamasha hilo zitaendelea kutolewa kadiri siku zitakavyosonga mbele.
Hii ni mara ya pili kwa Airtel kuandaa bonanza kwa wanahabari nchini, ambapo mwaka jana iliandaa wakati huo ikijulikana kama Zain.


h.sep3.gif


juu
 
Azam FC moto uleule


na Makuburi Ally


amka2.gif
TIMU ya AFC ya Arusha jana iliendelea kuwa ‘nyanya' katika Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kukubali kipigo cha mabao 5-1 kutoka kwa Azam FC kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
AFC katika mchezo wake wa kwanza wa raundi ya pili ya ligi hiyo waliocheza na Yanga walikubali kipigo cha mabao 6-1, katika dimba hilo, hivyo kuwa na rekodi ya kukubali mabao 11 katika mechi mbili.
AFC ilianza kupokea kipigo cha mabao hayo katika dakika ya pili ya mchezo kwa bao la John Bocco baada ya kazi nzuri na Ramadhani Chombo ‘Redondo' kabla ya yeye mwenyewe kuongeza la pili dakika ya 26 akiunganisha krosi safi ya Jabir Aziz.
Azam ambao mchezo uliopita iliitoa nishai Simba kwa kuichapa mabao 3-2, waliendelea kulisakama lango la AFC na kufanikiwa kuongeza la tatu dakika ya 41 lililowekwa wavuni na Bocco aliyefanikisha kazi nzuri ya Mrisho Ngassa, mabao yaliyodumu hadi mwamuzi Peter Mujaya anapuliza filimbi ya mapumziko.
Kipindi cha pili Azam walirejea kwa nguvu mpya na kufanikiwa kufunga bao la nne dakika ya 47 mfungaji akiwa Ngassa kabla ya kukandamiza la tano dakika ya 76 kwa kichwa akiunganisha krosi ya Peter Ssenyonjo, kabla ya AFC kujipatia bao la kufutia machozi dakika za lalasalama kupitia kwa Jimmy Mwaisondola kwa kichwa.
Matokeo mengine katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro, Toto Africans ilikubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa Ruvu Shooting.
Mabao ya washindi yalifungwa na Charles Michael na Hassan Dilunga huku la Toto likifungwa na Hussein Swedi.
Huko Manungu Turiani, Mtibwa iliponea chuchupu kulala kwa Majimaji baada ya kulazimisha sare ya 2-2. Mabao ya Wanalizombe yalifungwa na Kassim Kilungo na Mohammed Kijuso huku ya Mtibwa yakifungwa na Omar Matuta na Ally Mohamed ‘Gaucho'.
 
Yanga: Papic alikuwa msumbufu
• Watamba kuiangamiza Dedebit, kambi yahama Jangwani

na Dina Ismail


amka2.gif
UONGOZI wa klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam umesema hauwezi kupoteza muda kila kukicha kwa ajili ya kujadili matatizo ya Kocha wake Mkuu Mserbia Kostadin Papic, ambaye juzi alitangaza kubwaga manyanga.
Kocha huyo alifikia hatua ya kuachana na Yanga kwa kile kinachodaiwa kupinga kuongezwa kwa Fred Felix Minziro kama kocha msaidizi wa timu hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga alisema, uongozi kamwe hauwezi kupangiwa masharti na mtu ambaye wamemuajiri.
Alisema kwa muda mrefu kocha huyo amekuwa akileta mizengwe ya hapa na pale sambamba na kutishia kuondoka, lakini uongozi hauwezi kufuatilia mambo yake kila siku kwani kuna mengi ya kufanya.
"Sisi tumemuajiri hivyo anawajibika kufuata kilichomleta si kutupangia viongozi cha kufanya, tuna mambo mengi ya kujadili si masuala yake kila kukicha, mwache aende Yanga itabaki pale pale," alisema.
Nchunga aliongeza kuwa hata kama wangesikiliza matakwa yake ya kumuondoa Minziro ni wazi kuwa, angetoa jambo jingine ili mradi tu kutaka kuusumbua uongozi.
Kwa mantiki hiyo, Nchunga amewataka Wanayanga kutulia, kwani pamoja na kuondoka kwa kocha huyo, timu ipo katika hali nzuri chini ya Minziro tayari kwa mechi yao ya Kombe la Shirikisho (CAF), dhidi ya Dedebit ya Ethiopia Jumamosi.
Waethiopia hao wanatarajiwa kuwasili alfajiri ya leo tayari kwa mechi hiyo ya kwanza, ambapo Yanga imejinasibu kuibuka na ushindi mnono.
Katika hatua nyingine, kambi ya wachezaji wa Yanga jana ilihamishwa kutoka katika makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Jangwani na Twiga na kwenda katika Hoteli ya High Level.
Habari zilizopatikana jana zinadai kwamba, lengo la kuhamisha kambi hiyo ni katika kuwapa utulivu wachezaji pamoja na usalama wao kuelekea katika mechi hiyo muhimu.
 
Simba matumaini makubwa Comoro


na Dina Ismail


amka2.gif
MABINGWA watetezi wa Ligi ya Soka Tanzania Bara, Simba wameondoka jana asubuhi na msafara wa watu 24 kwenda visiwani Comoro wakiwa na matumaini makubwa ya kushinda mechi yao ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Elan de Mitsoudje ya huko Jumapili.
Wakizungumza kabla ya kukwea pipa, wachezaji hao walijinasibu kuwatoa nishai wapinzani wao hao ugenini kabla ya kuja kuwasukumizia mbali katika mechi ya marudiano itakayopigwa nchini.
Nahodha wa Simba, Nico Nyagawa alisema wanakwenda kwa lengo la kushinda mchezo huo ili kujiwekea mazingira mazuri katika mechi ya marudiano.
Alisema, morali huo unatokana na maandalizi mazuri waliyoyapata kwa zaidi ya wiki tano, ambapo umahiri wao umedhihirika katika mechi za kujipima nguvu.
"Tunakwenda tukiwa na nguvu na mkakati wa kuhakikisha tunaibuka na ushindi, tunaomba dua za Watanzania na Wanasimba kwa ujumla ili zitusaidie," alisema Nyagawa.
Msafara huo ambao uko chini ya Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba, Maestro Ibrahim Masoud pia yumo Kocha Mkuu, Mzambia Patrick Phiri akisaidiwa na Amri Saidi.
Wachezaji walioondoka ni pamoja na Juma Kaseja, Ali Mustafa ‘Barthez', Salum Kanoni, Ramadhan Haruna, Juma Jabu, Juma Nyosso, Kelvin Yondan, Jerry Santo, Meshack Abel, Abdulhalim Homoud, Mohammed Banka na Nico Nyagawa.
Wengine ni Hillary Echessa, Amri Kiemba, Rashid Gumbo, Patrick Ochan, Emmanuel Okwi, Musa Mgosi, Shija Mkina, Ali Ahmed Shiboli na Mbwana Samatha.


h.sep3.gif


juu
 
Waamuzi waonywa rushwa, pombe


na Victor Masangu


amka2.gif
WAAMUZI wa soka wametakiwa kuachana na tabia ya kupokea rushwa wakati wanapopangwa kuchezesha mechi mbalimbali na badala yake waikwepe na kuhakikisha wanazingatia sheria zote 17 za mchezo huo kwa lengo la kuepukana na migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara inayosababishwa na vitendo vya rushwa. Agizo hilo lilitolewa na Diwani wa Kata ya Mailimoja iliyopo wilayani Kibaha, Andrew Lugano, wakati wa sherehe za kufunga kozi ya waamuzi wa soka iliyofanyika kwenye ofisi za Chama cha Soka Mkoa wa Pwani (COREFA).
Lugano alisema anachukizwa na vitendo vya kutoa na kupokea rushwa vinavyosababisha kwa kiasi kikubwa kudidimiza maendeleo ya mchezo huo kutokana na kufanya maamuzi ambayo ni kinyume na taratibu zilizowekwa.
Diwani Lugano alisema kwamba, endapo mwamuzi anapoamua kuchukua rushwa kwa lengo la kupindisha sheria 17 za mchezo huo na kuipendelea timu ya upande fulani ili iweze kushinda na ikabainika amefanya hivyo, inaweza kujikuta yupo katika utata mkubwa.
"Kwani anaweza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kusimamishwa kuchezesha kwa kipindi cha muda fulani, ama kufungiwa kabisa kuchezesha mechi yoyote kulingana na kosa alilolifanya.
"Jamani hii kazi ya uamuzi wa mchezo wa soka inahitaji uvumilivu wa hali ya juu, kwani pindi unapokuwa uwanjani halafu ukakiuka sheria 17 za mchezo wa soka, utakuwa katika wakati mgumu wakati wote na kwa upande wangu niwapeni siri, mimi mwenyewe nilikuwa mwamuzi katika miaka ya nyuma na nilishachezesha mechi mbalimbali kubwa lakini wkati mwingine niliweza kumaliza mpira lakini nikisindikizwa na farasi na wakati mwingine ninapiga kipenga huku nikiwa mbali kwa kuhofia kipigo," alisema Lugano.
Kadhalika, katika hatua nyingine, Lugano alisema kwamba ili waamuzi waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi na bila ya kuwa na matatizo, wanapaswa pia kuachana na kunywa pombe kupita kiasi, kwani kufanya hivyo kunaweza kumsababishia kufanya maamuzi ambayo si sahihi pindi anapokuwa uwanjani akichezesha mechi.
Pia aliwataka wadau wa soka wa Wilaya ya Kibaha na Mkoa wa Pwani kwa ujumla, hasa kwa upande wa kina mama kujitokeza kwa wingi katika kusomea fani hiyo ya uamuzi wa mchezo wa soka ili kuwa na waamuzi wengi wenye taaluma katika sekta ya mchezo huo ambao pia wataweza kusaidia katika kuchezesha michezo mbali mbali.
Naye mkufunzi wa mafunzo hayo, Charles Ndagala, alisema kwamba washiriki hao ambao wamepata mafunzo hayo kwa siku 10 ana imani wataweza kufanya kazi ya uamuzi wa mchezo wa soka na kwamba wataweza kuleta chachu zaidi ya kuleta maendeleo kutokana na mchango wao.
Kozi hiyo ambayo imeandaliwa na Chama cha Soka Wilaya ya Kibaha (KIBAFA), imefadhiliwa na Chama cha Soka Mkoa wa Pwani (COREFA), imejumuisha washiriki mbalimbali kutoka Mkoa wa Pwani wapatao 16 ambapo kati yao wawili ni wanawake.
Washiriki waliohudhuria kozi hiyo ni, James Ngombo, Jeremia Komba, Ally Salehe, Saijaona Liswele, Athuman Gila, Kimweli Hamisi, Shaban Langweni, Germanus Mtolela, Ester Kalale, Hambali Mshana, Hemed Kupaza, Abeid Yasini, Hassan Kanji, Edwin Bageka, Lonjin Mnzavas pamoja na Zaina Mkindi.



h.sep3.gif

 
...Wapinzani wao watua usiku wa manane
Wednesday, 26 January 2011 20:42

Mwandishi Wetu
WAPINZANI wa Yanga katika michuano ya Kombe la Shirikisho, Dedebit Sports ya Ethiopia walitarajiwa kuwasili usiku wa manane wa kuamkia leo, tayari kwa mchezo wa kwanza wa kombe hilo utakaopigwa kesho kwenye Uwanja wa Taifa.

Kundi la watu 24 linaloundwa na wachezaji 18 na viongozi sita ndiyo wanaounda msafara wa timu hiyo kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo yenye maskani yake kwenye mji wa Addis Ababa.

Dedebit ambayo haina jina kubwa katika mashindano ya klabu Afrika, zitapambana kesho kabla ya kurudiana kati ya Februari 11 na 13.

Mbali na Yanga, timu nyingine ya Tanzania inayowania kombe hilo linaloshikiliwa na FUS Rabat ya Morocco walilolitwaa mwaka jana ni KMKM ya Zanzibar itakayokuwa ikimenyana na DCMP kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Kikosi kamili cha Dedebit kinaundwa na:- Beniam Habtamu Mekonnen, Micheal Sisay Asegedom, Mengestu Asefa Sendeku, Girmu Seyoum Welde, Adamu Mohamude, Berhanu Bogale Bogale na Wendosen Mikias Mashedo.

Wachezaji wengine ni Semere Yemane Haile Silase, Mesfin Wendemu Endalayu, Mulugeta Miheret Akele, Ephrem Zeru Negasi, Shehabe Gebrial Ahmed, Tadele Mengesha Mergiya,Behailu Assefa Gobeze,Danial Derbe G/micheal,Getaneh Kebede Gibto,Dawit Fekadu Demise na Temesgen Tekle Ageze.

Msafara huo unaongozwa na Rai wa klabu hiyo, Kanali Awel Abdurahim na kiongozi wa timu, Aleka Gebre Egizabihere Abreha na mchuaji misuli Tibebe Aleme. Kocha mkuu ni Gebre Medhin Haile na kocha msaidizi, Zelalem Shiferawu wakati kocha wa makipa ni TsegaZeabe Asegedom.

Hata hivyo, Yanga inaweza kutumia nafasi ya kutokuwepo kipa namba moja wa timu hiyo na timu ya taifa ya Ethiopia, Jemal Tassew kuumia mguu wa kulia wakati wa mazoezi na kukimbizwa hospitali ya Yordanos na kuwekewa plasta ngumu, POP.

Kipa huyo atakuwa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja pamoja na kiungo mahiri wa timu hiyo, Fitsum Teferi ambaye haijulikani atapona lini baada ya kuumia bega.
 
Azam yapaa Ligi Kuu
Wednesday, 26 January 2011 20:41

Jessca Nangawe
AZAM FC imeendeleza wimbi la ushindi baada ya jana kuibanjua AFC Arusha mabao 5-1 katika mechi ya Ligi Kuu iliyopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Hicho ni kipigo kingine kwa AFC inayoelekea kurudi Daraja la Kwanza, baada ya kuzabuliwa mabao 6-1 na Yanga katika mechi nyingine ya ligi hiyo wiki iliyopita.

Azam yenye pointi 26, ilipata bao la kwanza katika dakika ya pili lililofungwa na John Bocco baada ya kupata pasi Mrisho Ngassa aliyewatoka mabeki wa AFC wakati bao la pili liliwekwa kimiani na Ramadhani Chombo katika dakika ya 26 kwa kumalizia mkwaju uliogonga mwamba na kurudi uwanjani.

Wanalambalamba hao walioifunga Simba mabao 3-2, walipata bao la tatu katika dakika ya 42, safari hii Boko akifunga bao lake la sita katika msimamo. Ngassa aliongeza la nne kwa shuti la mbali dakika ya 63 kabla ya kufunga lingine dakika ya 76.

Bao la kufutia macho kwa AFC, lilipatikana dakika ya 90 kupitia kwa Jimmy shoji kwa kichwa baada ya kupata pasi ya Emmanuel Panju.

Naye Juma Mtanda anaripoti kutoka Morogoro, kuwa Ruvu Shooting imeichapa Toto African ya Mwanza mabao 2-1 katika mchezo mwingine wa ligi hiyo kwenye Uwanja wa Jamhuri.

Toto ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 34 kupitia kwa Hussein Sued kabla ya Charles Michael kuisawazishia Ruvu katika dakika ya 46. Hassan Dilunga aliizamisha toto dakika ya 72 kwa bao murua baada ya kumlamba chenga kipa wa Toto, Wilbert Mwita.

Kwenye Uwanja wa Manungu, Turiani, Mtibwa Sugar na majimaji ya songea zimetoka sare ya kufungana mabao 2-2 katika mchezo mkali wa ligi hiyo.

Ligi hiyo inaendelea tena leo kwa mchezo kati ya JKT Ruvu dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.


 
Dalglish wants greater progress






Updated Jan 26, 2011 7:51 PM ET
Liverpool manager Kenny Dalglish has no intention of settling for seventh place after a 1-0 victory over Fulham lifted his side to their highest position in the Barclays Premier League this season.
John Pantsil's 52nd-minute own goal turned out to be the decisive moment in the game, although up to that point the major talking point revolved around assistant referee Mick McDonough.


McDonough incorrectly flagged Fernando Torres offside as he raced on to Raul Meireles' sixth-minute through-ball to slot past goalkeeper David Stockdale.
Fortunately for Liverpool it did not matter and the Reds secured back-to-back wins for the first time since early November.
But although seventh represents a considerable improvement in a season when, under predecessor Roy Hodgson, they dropped into the relegation zone, Dalglish cannot be satisfied.
"I think we are better than that," he said.
"It is getting a bit more realistic but we are not getting carried away with being seventh - that is not where this football club wants to be.
"We want to be further up than that but to do that we have to win more games and that is what we will try to do, starting against Stoke next Wednesday."
Asked what his long-term objective was he replied: "To beat Stoke next Wednesday, the same we have done here since I can remember.

Sat., Jan. 22
Wolves 0-3 Liverpool |Recap
Arsenal 3-0 Wigan | Recap
Everton 2-2 West Ham | Recap
Man Utd 5-0 Birmingham | Recap
Newcastle 1-1 Tottenham | Recap
Fulham 2-0 Stoke City | Recap
Blackpool 1-2 Sunderland | Recap
Aston Villa 1-0 Man City | Recap
Sun., Jan. 23
Blackburn 2-0 West Brom | Recap
Mon., Jan. 24
Bolton 0-4 Chelsea | Recap
Tue., Jan. 25
Blackpool 2-3 Man Utd | Recap
Wigan 1-2 Aston Villa | Recap
Wed., Jan. 26
Liverpool 1-0 Fulham | Recap BPL Scores | Table | Fixtures

"We have never come in at the start of the season and said 'we're going to do this or that', we just went out to do the best we could.
"At the end of the season we added up the points to see where we were and I don't any reason to change that.
"It never did us any harm. It is the only way I know, that is the way I was brought up."
On the game he felt his side did well to keep the determined Cottagers at bay.
"I think Fulham will be feeling a little hard-done by because they will think they deserved something from the game," he added.
"But there have been many games when we thought we deserved more from it than we got.
"Tonight the boys showed a great deal of determination and effort and it is great credit to them after a hard run of games.
"I think that type of victory tonight has been a long time coming because we worked hard we got a little bit of good fortune.
"We had some bad luck because Fernando's goal was onside but we never got it so kept going.
"Referees make bad decisions, we make bad decisions and players make bad decisions.
"It is just the way of life."
Fulham boss Mark Hughes also felt his side deserved more from the game.
"We are shaking our heads in there," he said.
"I've been involved in many teams as a player and a manager coming here where we've been totally dominated and been lucky to get anything.
"Tonight was the complete opposite. To take the game to Liverpool and not get anything was disappointing."
 
Giggs tips Fergie to stay for years






Updated Jan 26, 2011 7:21 PM ET
Ryan Giggs believes Sir Alex Ferguson could carry on for another five years at least as Manchester United manager and remain at the helm well into his seventies.

Sat., Jan. 22
Wolves 0-3 Liverpool |Recap
Arsenal 3-0 Wigan | Recap
Everton 2-2 West Ham | Recap
Man Utd 5-0 Birmingham | Recap
Newcastle 1-1 Tottenham | Recap
Fulham 2-0 Stoke City | Recap
Blackpool 1-2 Sunderland | Recap
Aston Villa 1-0 Man City | Recap
Sun., Jan. 23
Blackburn 2-0 West Brom | Recap
Mon., Jan. 24
Bolton 0-4 Chelsea | Recap
Tue., Jan. 25
Blackpool 2-3 Man Utd | Recap
Wigan 1-2 Aston Villa | Recap
Wed., Jan. 26
Liverpool 1-0 Fulham | Recap BPL Scores | Table | Fixtures

The club's record appearance holder says his veteran boss, who turned 69 last month, has an enduring passion for the game.
In an interview with Sky TV magazine, Giggs said: "I really do not see him (Ferguson) finishing any time soon, he will go on, at least another five years.
"His desire gets stronger. After a Champions League game we can get back at 3.30am and then a few hours later he will be the first in at the training ground.
"Earlier in the season we had a virus at the club. He got it himself and was dying during the week, really sick, but come the day of the game, he was there in the dug-out. He just loves the challenge."
Giggs intends to follow Ferguson and become a manager somewhere. He is currently taking his A coaching badge.
He added: "I want to remain in football so I can continue to do something I have done since school. If I have a day off I am bored.
"I hope I can be a good manager, I like helping players and improving them. But the life expectancy of a manager is just 18 months, so you do not get long."
 
Baridi yaitesa Simba Comoro

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 27th January 2011 @ 07:24
TIMU ya Simba iliwasili salama jana Visiwa vya Comoro huku kukiwa na hali ya hewa ya baridi, ambayo imeanza kuwasumbua baadhi ya wachezaji.

Akizungumza kutoka Comoro jana, Kocha Mkuu wa timu hiyo Patrick Phiri alisema licha ya kuwepo baridi, lakini ana matumaini makubwa ya vijana wake kufanya vizuri.

"Dar es Salaam hali ya hewa ni joto kali, lakini huku sasa ni baridi kiasi kwamba inatubidi tuizoee, lakini kwa vile tumewahi kufika tuna matumaini makubwa mambo yatakuwa mazuri.

"Si baridi kali sana, lakini inatutesa, huwezi ukalinganisha na hali ya Dar es Salaam, " alisema Phiri na kuongeza kuwa kikosi chake kipo imara kwa mchezo dhidi ya Elan Club de Mitsoudje Jumapili katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Nahodha wa timu hiyo, Nico Nyagawa alisema, licha ya kuwepo baridi, lakini pia jana mvua kubwa ilinyesha na kuwa leo wataanza rasmi mazoezi kujiandaa na mchezo huo.

Jana Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu' alikaririwa na gazeti hili akisema wanaelekeza nguvu zao kwenye mechi hiyo na kuwa wamesahau masuala yanayohusiana na mchezo wao na Azam Jumapili, ambapo Simba ilifungwa mabao 3-2.

Kabla ya kufungwa na Azam, pia Simba ilifungwa na mabingwa wa Zambia, Zesco katika mchezo wa kirafiki na kufungana bao 1-1 na Clube Atletico Paranaense ya Brazil katika mchezo mwingine wa kirafiki.

Wachezaji waliopo Comoro ni Juma Kaseja na Ali Mustapha, wakati mabeki ni Haruna Shamte, Juma Jabu, Juma Nyoso, Kelvin Yondan na Meshack Abel.

Viungo ni, Abdulhalim Humuod, Rashid Gumbo, Nico Nyagawa, Mohamed Banka, Jerry Santo, Hilary Echesa, Amri Kiemba, Patrick Ochan. Washambuliaji ni: Mbwana Samatta, Emmanuel Okwi, Ali Ahmed Shiboli, Shija Mkina na Mussa Hassan.

Kama Simba ikifanikiwa kuwatoa Wacomoro itakumbana na timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ‘DRC', ambayo ni bingwa mtetezi wa michuano hiyo.

Wakati huohuo, Kocha Mkuu wa Yanga, Kostadin Papic aliyetangaza kujiuzulu kuinoa timu hiyo juzi, jana asubuhi aliwaaga wachezaji wa timu hiyo.

Habari zilizopatikana kutoka kwa wachezaji wa Yanga na kuthibitishwa na Ofisa Habari wa klabu hiyo, Luios Sendeu ni kuwa Papic alifika kambini na kuwatakia kila la heri wachezaji hao katika mechi yao ya Kombe la Shirikisho Jumamosi.

"Ni kweli Papic amefika kambini na kuwaaga wachezaji, lakini mpaka sasa sijapata taarifa kama ameshawasilisha barua yake ya kuachia ngazi kwa Mwenyekiti au la.

"Kama itakuwa hivyo, sisi tutaendelea na mambo yetu na timu itakuwa chini ya Fred Minziro kwa mechi ya Jumamosi," alisema Sendeu.


 
Ngasa aipaisha Azam

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 27th January 2011 @ 07:24
WASHAMBULIAJI wa Azam, Mrisho Ngasa na John Bocco jana walizidi kuonesha makali yao baada ya kuiongoza timu hiyo kupata ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya AFC Arusha kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Ushindi huo wa Azam umekuja siku chache baada ya Jumapili kuifunga Simba mabao 3-2 katika mchezo mwingine wa Ligi Kuu Tanzania Bara, lakini pia kipigo hicho cha AFC ni cha pili mfululizo baada ya Ijumaa iliyopita kufungwa mabao 6-1 na Yanga katika ligi hiyo.

Azam sasa imefikisha pointi 26 ikishika nafasi ya tatu nyuma ya Simba yenye pointi 27 na Yanga inayoongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 31.

Katika mchezo wa jana Ngasa na Bocco kila mmoja alifunga mabao mawili, wakati bao lingine likifungwa na Ramadhan Chombo ‘Redondo', huku lile la AFC likifungwa na Jimmy Mwaisondola dakika za majeruhi.

Licha ya kuiwezesha Azam kupaa kileleni, lakini pia Ngasa na Bocco wameongeza idadi ya mabao ya kufunga katika kuwania ufungaji bora wa ligi hiyo.

Ngasa sasa anaongoza katika ufungaji akiwa amefunga mabao tisa akifuatiwa na Gaudence Mwaikimba aliyefunga nane na Jerry Tegete na Bocco wenye mabao sita kila mmoja.


 

Ligi Arusha kuanza Feb.6


Imeandikwa na John Mhala, Arusha; Tarehe: 26th January 2011 @ 23:59

LIGI ya Taifa ngazi ya Mkoa wa Arusha inatarajia kuanza Februari 6 mwaka huu kwa kushirikisha timu 13.

Kaimu Katibu wa Chama Cha Soka Mkoa wa Arusha (ARFA), Gerad Munis alisema kwa mujibu wa kanuni kila wilaya inatakiwa kutoa timu tatu kushiriki ligi ya mkoa.

Munis alisema ligi hiyo itakuwa ya kituo kimoja tu na kuwa michezo yote itachezwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid mjini Arusha.

Munis alisema ni wilaya tatu tu kati ya sita za mkoa wa Arusha zenye ligi ya kueleweka na zina uwezo wa kutoa timu hizo kwa mujibu wa kanuni.

Alitaja wilaya hizo ni Arusha, Arumeru na Monduli, lakini Longido, Karatu zinashindwa kuleta idadi hiyo na mbali ya hilo wilaya ya Ngorongoro haijawahi kuleta timu hata moja katika miaka mingi ya soka mkoani Arusha.

Alisema mwaka huu Longido imeleta timu moja ya Namanga Star, badala ya timu tatu na imeshalipa ada ya ushiriki ya Sh 120,000 na Karatu mpaka sasa haijaleta majina ya timu shiriki na haijathibitisha kushiriki ligi hiyo.

Munis alisema kutokana na hali hiyo Kamati ya Utendaji ya ARFA, imeamua kuongeza timu kutoka wilaya za Arusha na Arumeru ili ligi hiyo iweze kuwa na msisimko mkubwa na ushindani wa kutosha na kupata bingwa wa uhakika.

 
Ngumi Tanga wajipanga mashindano ya Taifa

Imeandikwa na Anna Makange, Tanga; Tarehe: 26th January 2011 @ 23:55

CHAMA cha Ngumi Mkoa wa Tanga(TABA) kiko kwenye maandalizi ya mashindano ya klabu bingwa ya mkoa ili kupata wawakilishi katika mashindano ya Taifa.

Akizungumza na HabariLeo jijini hapa, Katibu wa TABA, Hassan Hashim alisema mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika mapema mwezi ujao na yatashirikisha klabu mbalimbali kutoka maeneo tofauti ya mkoani hapa.

Alisema lengo la mashindano hayo yatakayofanyika katika Uwanja wa Mkwakwani ni kutafuta
mabondia wa uzito mbalimbali watakaouwakilisha mkoa kwenye mashindano ya klabu bingwa ya taifa.

"Tunatarajia kuandaa timu nzuri kwa ajili ya kushiriki kwenye Mashindano hayo ya taifa yatakayoanza kutimua vumbi Dar es Salaam kati ya Februari 25 hadi Machi 6 mwaka huu," alisema.

Katibu huyo alisema mpaka sasa tayari klabu zaidi ya tano kutoka mjini Tanga, Handeni na Muheza zimejitokeza kushiriki michuano hiyo.

Hasim alizitaka klabu nyingine zaidi kujitokeza kushiriki michuano hiyo ili kuibua na

kukuza vipaji vipya pamoja na kuimarisha timu ya mkoa wa tanga itakayoshiriki michuano ya taifa mwaka huu.

 
Mashindano ya skwashi Bell Jan.30

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 26th January 2011 @ 23:50

MICHUANO ya skwashi ya Bell mwezi huu yamepangwa kufanyika Januari 30 kwenye viwanja vya Klabu ya Gymkhana Dar es Salaam.

Nahodha wa Skwashi klabuni hapo Marwa Busigara alisema mashindano hayo ya kila mwezi
yanayoshirikisha wanaume na wanawake yanafanyika kwa siku moja.

"Tumeandaa mashindano ya Bell Januari 30, yatakuwa ya kwanza kwa mwaka 2011," alisema. Busigara alisema mashindano hayo yamekuwa na mafanikio makubwa tangu kuanzishwa mwaka jana.

Alisema wanatarajia wachezaji kutoka Zanzibar, Arusha na Tanga watakuja kushiriki ili kufanikisha mashindano hayo ambayo yamepata umaarufu mkubwa mwaka jana.

Nahodha huyo ambaye ana maliza muda wake alisema kiingilio katika mashindano hayo kimepangwa kuwa Sh 10,000.

"Nawaomba wachezaji wengi wajitokeze kushiriki na kujenga urafiki kupitia michezo," alisema.

Michuano hiyo inaweza kuwa ya mwisho kwa uongozi wake kabla ya uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika mwezi ujao.

 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom