Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Dos Santos loaned to Racing Santander


storypage_APlogo_01.png







3 comments »

Updated Jan 31, 2011 8:17 PM ET
SANTANDER, Spain (AP)

Mexico forward Giovani Dos Santos has been loaned from Tottenham to Spain's Racing Santander until the end of the season.

TRANSFER SPECIAL

Keep up with all the biggest moves around the globe with our 2011 January transfer gallery.

The loan deal Monday includes an option for Racing to buy his rights.
The signing is the first for Racing's new owner Ahsan Ali Syed since the Indian businessman acquired the club on Friday.
The 21-year-old Dos Santos, who played for Mexico at last year's World Cup, came up through Barcelona's youth system before joining the English club in 2008.
This is Dos Santos third loan stint after moving to Tottenham. He appeared in five games for Spurs this season but none since Sept. 25.

 
Wolfsburg signs Koo, Tuncay, Orozco


storypage_APlogo_01.png







0 comments »

Updated Jan 31, 2011 1:54 PM ET
WOLFSBURG, Germany (AP)

Wolfsburg has signed South Korea international Koo Ja-choel from Jeju United, Tuncay Sanli from Stoke and teenager Yohandry Orozco of Venezuelan club FC Zulia.
Koo, 21, was top scorer at January's Asian Cup with five goals and has signed a 3 1/2-year contract, as has Tuncay, 29. While the 19-year-old Orozco signed a 4 1/2-year deal, the Bundesliga club said Monday.

TRANSFER SPECIAL

Keep up with all the biggest moves around the globe with our 2011 January transfer gallery.

"They are two versatile midfield players with very promising futures," Wolfsburg business manager Dieter Hoeness said.
Anderlecht said it has received "a nice transfer sum" from Wolfsburg for Jan Polak and that the Czech Republic midfielder is set to sign a deal to join the Bundesliga club through to the middle of 2013.
Polak scored nine goals in 109 matches for Anderlecht since joining in 2007 from German club Nuremberg. He has scored seven goals in 55 matches for the Czech Republic.
Kicker magazine said Wolfsburg was also seeking striker Patrick Helmes from Bundesliga rival Bayer Leverkusen and Czech Republic midfielder Jan Polak from Anderlecht before the transfer window shuts Monday. There was no confirmation from Wolfsburg.
Coach Steve McClaren is trying to invest the money earned from the transfer of striker Edin Dzeko to Manchester City, reported by the British media to be 27 million pounds ($42 million). Wolfsburg lost 3-0 at home to Borussia Dortmund on Saturday and is 12th in the Bundesliga.

The home of the best LIVE soccer and rugby awaits at FoxSoccer.tv -- don't miss a second of the action.

Last week, Wolfsburg signed striker Dieudonne Mbokani from Monaco.
Wolfsburg was trying to sign striker Jefferson Farfan from Schalke but the deal fell through Monday.
Schalke announced the transfer of Ghana midfielder Anthony Annan from Rosenborg. The deal will keep Annan with Felix Magath's team until the end of the 2013-2014 season.
Meanwhile, Stuttgart has confirmed the signing of another Asian Cup star, Shinji Okazaki of Japan, who scored three goals as he helped Japan win the title.
Also, Kaiserslautern said it had brought in midfielder Adam Hlousek from Slavia Prague on loan until the end of the season.

 
Yanga, Mtibwa jino kwa jino


Na Elizabeth Mayemba

VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga inashuka uwanjani leo kucheza na Mtibwa Sugar katika mwendelezo wa mechi zao za ligi hiyo
mzunguko wa pili.

Mechi hiyo itapigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaa ambapo Yanga inaongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 31 wakifuatiwa na Simba yenye pointi 27.

Yanga wanaingia uwanjani leo, huku wakiwa na kumbukumbu nzuri katika michezo iliyopita ya ligi hiyo baada ya kushinda mechi mbili mfululizo ambapo waliwasambaratisha vibonde AFC ya Arusha mabao 6-1 na baadaye wakaifunga Polisi Dodoma mabao 2-0.

Akizungumzia mchezo wa leo, Kaimu Kocha wa Yanga, Felix Minziro alisema mchezo huo utakuwa mgumu kwa sababu mzunguko huu ni wa lala salama hivyo kila timu inajidhatiti kwa ushindi.

Alisema siku hadi siku anapokaa na timu hiyo mpya kwake anazidi kupata nayo uzoefu na kugundua kasoro ndogo ndogo, ambazo ameanza kuzifanyia kazi.

Naye Kocha Msaidizi wa Mtibwa Sugar, Mecky Maxime alisema wamejiandaa vizuri kwa ajili ya kuondoka na pointi tatu.

"Safari hii Yanga wasitarajie mteremko kupitia kwetu na sisi pia tunatafuta pointi tatu, hivyo mchezo wa leo utajaa upinzani mkali sana," alisema Maxime.

Alisema timu yake ipo vizuri na wachezaji wake wana ari kubwa ya ushindi, kikubwa ni wao wenyewe kucheza kwa kujituma ili washinde.

 
TFF yapangua ratiba Ligi Kuu


Na Addolph Bruno

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limeifanyia marekebisho ratiba ya Ligi Kuu kwa kubadilisha michezo minne ya raundi ya pili
kwa sababu mbalimbali.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Ofisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema sababu za mabadiliko hayo ni kutokana na mwingiliano katika baadhi ya michezo ya ligi hiyo na Chama cha Mpira wa Miguu Ethiopia, kuchelewa kutaja tarehe ya mechi ya maruadiano ya Kombe la Shirikisho kati ya Yanga na Debebit FC.

Mchezo huo umepangwa kuchezwa Ethiopia kati ya Februari 11, 12 na 13 mwaka huu baada ya mchezo wa awali kuchezwa Jumamosi iliyopita katika Uwanja wa Uhuru, Dares Salaam ambapo timu hizo zilitoka sare ya mabao 4-4.

Wambura alisema kutokana na chama hicho kuchelewa kutaja tarehe ya mchezo wa marudiano, mchezo wa Ligi Kuu namba 96 wa Yanga dhidi ya Kagera Sugar uliopangwa kuchezwa Februari 16 katika Uwanja Kaitaba mjini Bukoba umesogezwa mbele kwa siku moja, ili kuwapa nafasi Yanga kucheza na Dedebit.

Alisema michezo mingine iliyofanyiwa marekebisho ni mechi namba 85 kati ya Azam FC dhidi na Toto African uliopangwa kuchezwa leo katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam utachezwa Februari 4 kwenye uwanja huo.

Wambura alisema mechi namba 89 kati ya Simba na Polisi Tanzania, ambao awali ulipangwa kuchezwa Februari 5 mwaka huu katika Uwanja wa Jamhuri Dodoma, sasa utafanyika Februari 6 katika uwanja huo.

"Mabadiliko ya mchezo huu yametokana na Chama Cha Mapinduzi (CCM), kuutumia uwanja wake huo kwa ajili ya sherehe za kuzaliwa kwa chama hicho ambapo kitaifa zinafanyika mkoani Dodoma," alisema Wambura.

Alisema michezo mingine iliyofanyiwa marekebisho ni kati ya JKT Ruvu dhidi ya African Lyon, uliopangwa kuchezwa Februari 5 kwenye Uwanja wa Uhuru sasa utachezwa Februari 7 katika uwanja huo.

Wakati huohuo, Wambura alisema kutakuwa na semina elekezi kuhusu mashindano ya Copa Coca-Cola mwaka huu ambayo itafanyika Februari 5 kwenye ukumbi wa Manispaa ya Temeke, Dar es Salaam ambayo itashirikisha makatibu wakuu wa vyama vya mpira wa miguu vya mikoa.

Alisema michuano hiyo mwaka huu itaanzia katika ngazi ya Wilaya ambapo imepangwa kuanza Machi Mosi hadi Aprili 10, mwaka huu na katika ngazi ya Mkoa itachezwa kati ya Aprili 23 hadi Mei 7.

Ofisa huyo alisema ngazi ya kanda ya michuano hiyo itachezwa katika mikoa ya Dares Salaam, Mwanza na Arusha kuanzia Juni 6 wakati katika ngazi ya Taifa hatua ya 16 bora itachezwa kwenye kitua kimoja cha Dar es Salaam kuanzia Juni 25 hadi Julai 2, mwaka huu.
 
BFT yaziangukia kampuni kudhamini ngumi


Na Mwali Ibrahim

SHIRIKISHO la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT), limetoa wito kwa kampuni mbalimbali kudhamini mashindano ya wazi ya ngumi hizo, yaliyopangwa kufanyika
Dar es Salaam Februari 26 hadi Machi 5, mwaka huu.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Msemaji wa BFT, Eckland Mwaffisi alisema mashindano hayo yanatarajia kushirikisha zaidi ya mikoa 20 ya Tanzania.

Alisema lengo la mashindano hayo ni kutafuta timu ya taifa, ambayo itaiwakilisha Tanzania katika mashindano mbalimbali ya kimataifa ikiwemo michezo ya Mataifa ya Afrika 'All African Game' iliyopangwa kufanyikia Maputo, Msumbiji Septemba 2011.

"Mbali ya mashindano hayo, timu hii ambayo itachaguliwa na Kocha Mkuu Hurtado Pimenter, itaiwakilisha Tanzania katika michezo ya Olympic, ambayo itafanyika London, Uingereza Julai 2012," alisema Mwaffisi.

Aliongeza kuwa, gharama za mashindano hayo ni zaidi ya sh. milioni 25 ambazo hadi sasa hakuna kampuni, taasisi au shirika ambalo limethibitisha kutoa udhamini wao.

Mwaffisi alisema, umefika wakati wa kampuni mbalimbali kutoa udhamini katika mchezo huo wenye historia ya kuitangaza Tanzania kimataifa, ili uweze kufika mbali zaidi.

"Leo hii mchezo wa soka ndiyo unaopewa kipaumbele zaidi kuliko michezo mingine, ambayo kama itapewa udhamini na wachezaji kuandaliwa vizuri, wataiwezesha Tanzania kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa na kuondoa dhana iliyojengeka kwa wachezaji wetu kuitwa watalii," alisema.
 
Tyson apata mtoto wa tisa


NEW YORK, Marekani

BINGWA wa zamani wa masumbwi katika uzani wa juu, Michael Tyson na mkewe Lakiha Spicer Tyson, wamepokea mtoto mwingine baada ya
mwanamke huyo kujifungua mtoto wa kiume.

Vyanzo vya habari vilivyopo karibu na wanandoa hao, vilieleza kwamba familia hiyo ilipokea mtoto huyo wiki iliyopita na kwa sasa, Tyson na Lakiha wana furaha kubwa na kila mmoja anajivuna.

Wanandoa hao ambao tayari wana mtoto mmoja, ambaye wamemzaa pamoja aitwaye Milan alikuwa bado hajapewa jina.

Taarifa hizo za furaha zilikuja ikiwa ni miezi 18, tangu afariki mtoto wa Tyson aliyekuwa na umri wa miaka minne Exodus, aliyefariki mwaka 2009.

Tyson tayari alishaoa mara mbili kabla, wakiwemo waigizaji Robin Givens na Monica Turner na amezaa watoto watano Rayna, Amir, Mikey, Miguel na D'Mato, kutoka katika ndoa zake na marafiki zake wa kike.

Bondia huyo mstaafu mwenye umri wa miaka 44, ambaye ndiye bondia wa kwanza kutwaa taji la uzani huo akiwa na umri mdogo, baada ya kushinda taji hilo mwaka 1986 anafikiriwa kuingiza dola milioni 300 katika kipindi cha kazi yake, lakini Mei mwaka jana akadaiwa kifilisika ila akasema kuwa anajisikia mwenye furaha katika nafasi aliyopo.

 
Yanga kumkosa Shungu, atakiwa Rayon Tuesday, 01 February 2011 21:28

kocha%20shungu.jpg
Raoul Shungu

Jackson Odoyo na Sosthenes Nyoni
WAKATI mwenyekiti wa Yanga Lloyd Nchunga akidhibitisha kuwa Kocha wa zamani wa timu hiyo, Raoul Shungu ni miongozi mwa makocha 20 kutoka nje ya nchi waliomba kumridhi Mserbia Kostadin Papic mmiliki mpya wa timu ya Rayon Sports ya Rwanda Albert Rudatsimburwa amemtaka kocha huyo kuinoa timu hiyo.

Yanga imepokea jina la kocha huyo siku chache baada ya Rudatsimburwa kutangaza mikakati ya kumnasa kocha huyo kuanzia Januari 13.

Mmiliki huyo aliyesaini mkataba wa miaka saba na timu hiyo alitangaza mikakati hiyo huku akidai kuwa kocha huyo ndiye kocha mwenye viwango vya ubora kwa hivi sasa atakayeweza kuipatia timu hiyo mafanikio.

ìHakuna shaka kwamba Rayon Sport ni timu kubwa lakini kitu cha msingi kinachotazamwa kwa sasa ni kuona timu inaongozwa na wataalam waliobobea katika michezo na ndiyo maana nimeahidi kumrudisha kocha Shungu kwa sababu ni kocha mwenye viwango vya uboraî alisema mmiliki huyo katika mahojiano maalum na redio ya Contact FM ya nchini Rwanda.

Hata hivyo taarifa zaidi zinaeleza kuwa kocha huyo alitarajiwa kukutana na mmiliki huyo Ijumaa iliyopita kwa ajili ya mazungumzo zaidi juu ya mkataba wake mpya ndani ya timu hiyo kongwe katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati.

Hatua ya kutangazwa kwa Shungu ni baada ya Kosta Papic kubwaga manyanga kwa sababu mbalimbali na sasa timu hiyo iko chani ya kocha mteule, Fred Felix Minziro.

Hata hivyo, ilielezwa kuwa kocha huyo ni kati ya makocha waliokuwa na mpango wa kuajiriwa Yanga, mwingine aliyekuwa katika mpango huo ni kocha wa zamani wa SC Villa, Sam Timbe.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Yanga, Lloyd Nchunga amemtaka Papic kuilipa klabu ya Yanga mshahara wa mwezi mmoja kwa vile alipotangaza kujiuzulu kwenye barua yake alitoa notisi ya siku 30.

Nchunga katika taarifa yake alisema, pamoja na kutoa notisi hiyo, alitakiwa kuendelea na kazi hadi hapo notisi hiyo itakapoisha na mechi ya Dedebit alitakiwa kukaa benchi lakini Papic hakufanya hivyo.

Wakati hayo yakiendela, Yanga leo itashuka dimbani kukabiliana na Mtibwa Sugar katika mpambano wa ligi kuu utakaofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo utakuwa ni jaribio la pili la kocha, Minziro 'Majeshi' baada ya kuachiwa mikoba na aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Mserbia Kostadin Papic ambaye hivi karibuni alitangaza kuachia ngazi kukinoa kikosi hicho.

Awali Minziro aliiongoza Yanga kupata sare ya mabao 4-4 dhidi ya Dedebit ya Ethiopia katika mpambano wa Kombe la Shirikisho uliofanyika wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mechi ya leo inazikutanisha timu hizi zikiwa zimetofautiana kwa pointi nane katika msimamo wa ligi ambazo ni 31 za Yanga zinazoifanya iongoze ligi hiyo na 23 za Mtibwa iliyoshikilia nafasi ya nne.

Pamoja na yote hayo historia inabashiri tutarajie mchuano mkali hasa kutokana na kufungana bao 1-1 katika mtanange wa mzunguko wa kwanza uliofanyika mjini Morogoro licha ya kuwa Mtibwa ilifungwa mabao 2-1 katika Kombe la Mapinduzi.

Akizungumzia mechi hiyo Minziro ambaye alijiunga na Yanga kama kocha msaidizi akitokea Ruvu Shooting alisema: "Angalau sasa ninaweza kusema nimewafahamu wachezaji wangu licha ya kukaa nao kwa kipindi kifupi.

"Nimejaribu kuangalia upungufu na mazuri ya wachezaji wangu kupitia mazoezi ya wiki mbili na katika mechi dhidi ya Dedebit, stamina ni kati ya huo upungufu tumefanya mazoezi sana hivyo sina shaka tutaipiga Mtibwa."

Naye kocha wa Mtibwa Mkenya Tom Olaba aliliambia Mwananchi jana kuwa haoni sababu ya timu yake kushindwa kuondoka na pointi tatu leo akisema ameifuatilia Yanga kugundua ina kasoro nyingi.

"Ninaifahamu Yanga sielewi ni kwanini tulishindwa kuwafunga wakati ule lakini hawatishi sana. katika sehemu ya ulinzi kinacho wasaidia ni kwamba wanakipa mzuri ingawa si sababu ya msingi ya kutunyima ushindi...nina uhakika safari hii tutawafunga," alisema Olaba.

Baadhi ya nyota wanaotarajia kuchungwa leo ni pamoja na washambuliaji Jerison Tegete, Davis Mwape na Iddi Mbaga kwa upande wa Yanga wakati Mtibwa ni Omari Matuta, Salum Machaku na Shaanan Nditi.

Add this page to your favorite Social Bookmarking websites

Last Updated on Tuesday, 01 February 2011 22:42 Comments




0 #1 Kasuku 2011-02-02 11:07 Yebo yebo mmejiloga wenyewe, mnaanza kutapa tapa sasa, mjiandae kwa vichapo mfululizo kwa kila mechi, mmesha kuwa gunia la mazoezi, hata [NENO BAYA] atajipigia.
Quote

 
Papic abanwa Yanga

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 2nd February 2011 @ 09:09

UONGOZI wa Yanga umempa masharti matatu aliyekuwa kocha wake mkuu Kostadin Papic ambayo anatakiwa kuyatimiza ndipo aondoke nchini.

Wiki iliyopita, Papic aliandika barua ya kujiuzulu nafasi yake akidai kuwa uongozi umekiuka makubaliano yao kwa kumletea kocha msaidizi ambaye hajampendekeza.

Yanga imemuajiri Freddy Minziro kama kocha msaidizi kitendo kilichomkera Papic ambaye alisema hawezi kuwa na kocha msaidizi aliyetoka kufundisha klabu ya ligi kuu ambayo Yanga inashiriki.

Katika vyombo mbalimbali vya habari jana, Papic alikaririwa akisema kwamba anadai fedha zake Yanga ndipo aondoke.

Lakini habari za uhakika kutoka kwa uongozi wa juu wa Yanga zilizopatikana Dar es Salaam jana, zilisema Papic hana anachodai Yanga na amepewa masharti matatu ambayo anatakiwa amjibu mfadhili Yusuf Manji ndipo aondoke.

"Wala hadai, alishalipwa mshahara wake Sh milioni 12.8 mpaka mwezi wa pili, na kwanza yeye ndio anatakiwa ailipe Yanga kwa sababu hakufuata masharti ya kuvunja mkataba… "Sisi kama uongozi tuliipata barua ya kujiuzulu kwa Papic na tukamwambia hawezi kuondoka nchini bila kumjibu mfadhili wetu maswali mengi tuliyo nayo," alisema kiongozi mmoja mwenye nafasi kubwa Yanga.

"Kwanza tulimwambia aeleze kwanini ameitia hasara klabu katika usajili wa Keneth Asamoah, mchezaji ambaye klabu imepoteza fedha nyingi halafu mwisho wa siku akashindwa kucheza.

"Cha pili tulichomwambia ni kwamba atueleze utata wa usajili wa kipa Ivan Knezevic ‘Mzungu' na deni lake la Sh milioni 3.7," alisema kiongozi huyo.

Akitoa ufanunuzi wa suala hilo la kipa Mzungu, kiongozi huyo alidai, Papic alikopa Sh milioni 4 kwa uongozi na alipopewa hakurudisha badala yake akasema atamlipa Knezevic deni lake la usajili, lakini alipoulizwa kipa huyo alisema kwamba bado anadai.

"Na kingine tunataka atoe mchanganuo wa fedha za usajili kwa kila mchezaji, maana hawajamaliziwa fedha zao kwani katika mikataba waliambiwa wakicheza nusu ya mechi za msimu watamaliziwa, lakini wapo waliofikisha masharti hayo na fedha zao hawajapewa, yote hayo tunataka ayatolee ufafanuzi ndio aondoke, vinginevyo haondoki, hata akipanda ndege tutamshusha," alisema.




 
TFF yapangua tena ratiba ya ligi
Tuesday, 01 February 2011 20:55

Clara Alphonce
SHIRIKISHO la Soka Tanzania, TFF, limepangua tena ratiba ya Ligi Kuu ya Vodacom kwa michezo mitatu kwa sababu mbalimbal.

Hii ni mara ya pili tangu kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi TFF, kubadilisha ratiba, awali walibadilisha ratiba hiyo baada ya timu za Dar es Saalam zilizokuwa zimeamia viwanja vya mikoani baada ya Uhuru kufungwa kuruhusiwa kutumia uwanja huo wa Uhuru katika mzunguko huu.

Afisa Habari wa TFF, Boniface Wambura alisema kuwa wameamua kusogeza mbele michezo nitatu ambayo ni Simba na Polisi Dodoma uliokuwa uchezwe Februali 5 sasa utasogezwa mbele kwa siku moja na utacheza Februari 6 katika Uwanja wa Jamuhuri Dodoma.

Alisema kuwa sababu zilizowafanya wasongeze mchezo huo ni kutokana na CCM kuutumia uwanja huo kwa kufanyia sherehe za kuadhimisha miaka 34 ya Chama hicho.

Mchezo mwingine ambao umepelekwa mbele ni mchezo wa Yanga na Kagera Sugar ambao ulitakiwa kuchezwa Februari 16, sasa utachezwa Februari 17 katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Alisema sababu za kupeleka mbele mchezo huo ni kutokana na timu ya Dedebit ya Ethiopia mpaka sasa kutosema mchezo wa marudiano utakuwa lini kwa hiyo wamesogeza mbele kwa tahadhali kama mchezo huo utachezwa Februari 13 Yanga watashindwa kuwahi tarehe 16 kuwa Bukoba.

Pia alisema marekebisho mengine ni ya mechi ya Azam na Toto African ambayo ilipangwa kufanyika leo lakini haiwezekani siku moja kukawa na michezo miwili ya ligi katika uwanja mmoja hivyo umesogezwa mbele mpaka Februari 4 utachezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Jijini Dar es Salaam.

 

Temeke United, Prisons zabanwa

Imeandikwa na Anna Makange, Tanga; Tarehe: 2nd February 2011 @ 08:55
TIMU ya Temeke United jana ilitoka sare ya pili ya bila kufungana dhidi ya Polisi Morogoro katika mechi ya fainali za Ligi Daraja la Kwanza iliyofanyika kwenye Uwanja wa Mkwakwani mjini hapa.

Hiyo ni sare ya pili kwa Temeke United baada ya kutoka sare kama hiyo dhidi ya Rhino juzi. Kwa upande wa Polisi Morogoro, ilipoteza mechi ya kwanza kwa kufungwa mabao 2-0 na Moro United.

Mechi hiyo ya jana ilionekana kuwa ngumu kwa timu zote kwani zilioneshana upinzani mkubwa.

Akizungumzia mechi hiyo, kocha wa Temeke United William John alisema timu yake inahitaji kujiamini zaidi na kuonesha umakini katika mechi zake ili ishinde.

Kocha wa Polisi Moro, John Tamba alisema timu yake ilionesha udhaifu kwenye umaliziaji kwani ilipata nafasi nyingi za kufunga lakini ikashindwa kuzitumia.

Katika mechi nyingine iliyochezwa mapema jana, timu ya Prisons ilitoka sare ya bila kufungana na Rhino.

Mchezo huo ulikuwa wa vuta nikuvute kwani kila upande ulionekana kusaka ushindi kwa udi na uvumba lakini hadi inamalizika hakuna aliyeliona lango la mwenzake.

Ligi hiyo inaendelea tena leo kwenye uwanja huo ambapo Moro United itacheza na Coastal Union na Villa Squard itamenyana na Morani FC.

 
Mfalme Yusuf kurejea jukwaani Valentine Day


na Abdallah Menssah


amka2.gif
MKURUGENZI Mkuu wa mabingwa wa mipasho, Jahazi Modern Taarab, Mzee Yussuf ‘Mfalme' amebainisha kuwa hivi sasa yuko fiti na kwamba hivi karibuni ataanza kuonekana kwenye maonyesho mbalimbali ya kundi lake hilo.
Akizungumza kisiwani Unguja juzi, Yussuf alisema, onyesho lake la kwanza kupanda jukwaani litakuwa ni lile litakalofanyika siku ya mkesha wa Siku ya Wapendanao ‘Valentine Day', Februari 13, kwenye ukumbi wa Travertine Hotel, Magomeni jijini Dar es Salaam.
Alisema, katika onyesho hilo, pamoja na burudani nyingine zote, atawafariji mashabiki waliomkosa kwa kipindi kirefu, kwa kuimba vibao vyake vyote alivyovifyatua tangu alipoanzisha kundi la Jahazi Modern.
"Hivi sasa ninaendelea vema na wiki ijayo nitarudi hospitali kufungua hii ‘POP' ambapo baada ya hapo nitakuwa huru kuanza kazi jukwaani," alisema Yussuf ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Klabu ya Yanga.
Akizungumzia zaidi onyesho lake hilo la kwanza kupanda jukwaani, Yussuf alisema kuwa, ana hakika litajaa msisimko wa aina yake, kwani atashiriki pamoja na wanenguaji wa kundi lake kumwaga shoo kabambe.
Aidha, Yussuf alivitaja baadhi ya vibao anavyotarajia kuviimba katika onyesho hilo kuwa ni ‘VIP Nafasi Yangu', ‘Nakula kwa Nakshi Nakshi', ‘Tupendane Wabaya Waulizane', ‘Daktari wa Mapenzi' pamoja na ‘My Valentine'.
Alisema kuwa, kibao ‘My Valentine' kitakuwa maalum siku hiyo, ambako atakiimba akiwa amekaa chini mbele ya jukwaa kuonyesha kuwa hata yeye pia alikuwa akiwakumbuka mno mashabiki pamoja na wapenzi wake.
"Nawaomba mashabiki pamoja na wapenzi wangu wote wafike kwa wingi katika onyesho hilo nililoliandaa kwa ajili yao," alisema Yussuf, mahiri kwa uimbaji, utunzi na upapasaji kinanda.
Kadhalika, Yussuf alieleza kuwa, Valentine Day yaani Februari 14, burudani hiyo itahamia Temeke jijini Dar es Salaam, kwenye ukumbi wa Buliyaga Bar.
 
Waimbaji nyimbo za Injili watakiwa kujiheshimu kimavazi


na Danson Kaijage, Dodoma


amka2.gif
WAIMBAJI wa nyimbo za Injili nchini wametakiwa kutovaa mavazi yasio ya heshima kwa sababu hayamtukuzi Mungu wanayemwimbia.
Wito huo ulitolewa jana mjini hapa na Mchungaji msaidizi wa Kanisa la Free Pentecostal Church of Tanzania (FPCT), Joab Ngambiye, wakati wa uzinduzi wa albamu ya ‘Mwisho wa Mambo Yote'.
Albamu hiyo iliandaliwa na Kwaya ya Beroya Christian ya kanisa la Pentecostal la Nkhungu mkoani Dodoma.
"Siku hizi baadhi ya waimbaji wa nyimbo za injili, wanavaa mavazi yanayovaliwa na makahaba badala ya yale yanayomtukuza Mungu," alisema.
Aliongeza kuwa, mavazi ndiyo yanayomtambulisha mtu, cheo chake na thamani ya mtu aliyevaa.
Kwa upande wake, kiongozi wa kwaya hiyo, Ezekiel Mwadomba, alisema mauzo ya albamu hiyo yatatumika katika kuhakikisha jamii inayowazunguka inapata elimu, afya na malezi bora.
"Jamii lengwa ni watoto wanaoishi katika mazingira magumu, yatima, wajane na wale wasioweza kujimudu," alisema.
Zaidi ya shilingi milioni 1.1 zilipatatikana katika tamasha hilo ambalo limezijumuisha kwaya mbalimbali za Mkoa wa Dodoma.
 
Papic azuiwa Dar


na Dina Ismail


amka2.gif
LICHA ya Kocha wa Yanga, Mserbia Kostadin Papic, kutoa masharti magumu ya kuendelea kuinoa timu hiyo ili apate mwanya wa kutimka, mambo yamemgeukia na kutakiwa kubaki hadi atakapotoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo.
Hiyo inatokana na Papic aliyekatisha mkataba wa kuinoa timu hiyo akipinga kuchomekewa Msaidizi, Fred Felix Minziro, kutakiwa kutoa kwanza ufafanuzi wa mambo hayo ikiwamo masuala ya fedha za usajili.
Habari zilizopatikana jijini Dar es Salaam kutoka ndani ya Yanga zinasema, uongozi umemtaka Papic atoe maelezo na uthibitisho wa nyaraka za usajili wa wachezaji, akiwemo Mghana Kenneth Asamoah aliyeishia benchi kwa kukosa kibali cha uhamisho wa kimataifa (ITC).
Mbali ya kutaka kumbana kuhusu hilo, pia Yanga inataka Papic aendelee na kazi yake, kwani alitoa notisi ya siku 30 ya kuacha kazi wakati tayari akiwa amelipwa mshahara wake hadi Februari 15.
Chanzo hicho cha uhakika kinasema kuwa hadi muda huo Papic ameshalipwa sh 12,835,000.
"Kwa maana hiyo, Papic hawezi kuondoka kwa sasa kwani yeye bado ni mwajiriwa wa Yanga na ameshachukua mshahara hadi wa Februari 15," kilisema chanzo hicho.
Chanzo hicho kilionyesha kushangazwa na kocha Papic kushindwa kukaa katika benchi la Yanga siku ilipokwaana na Dedebit ya Ethiopia, kwa sababu mkataba bado unamtambua.
"Tunasikia anataka kuondoka, lakini kwa mazingira yaliyopo Papic hawezi kuondoka kwa sababu kama amevunja mkataba na Yanga, alipaswa kurejesha fedha ya hadi Februari 15 aliyochukua," kilisisitiza chanzo hicho na kuongeza:
"Kuna mambo kama matatu hivi ambayo Papic anapaswa kutupatia maelezo ya kuridhisha, vinginevyo hawezi kuondoka nchini labda ‘apae kwa ungo,' wengi hawajui kinachoendelea, kuna mambo anatakiwa kuyajibu kwanza," kilisema chanzo hicho.

Kati ya mambo hayo ni Papic kueleza vipi Yanga ilisajili kwa gharama kubwa wachezaji wa kimataifa kama Kenneth Assamoh na wengineo, lakini wakiishia benchi.
Aidha, Papic ametakiwa kabla hajaondoka nchini aeleze utata wa usajili wa kipa Mserbia, Ivan Knezevic na deni lake la sh milioni 3.7 sambamba na sh milioni 4 ambazo alizikopa tangu Agosti 2010.
"Kwa mfano kipa Mserbia, ameshindwa kuonyesha kiwango kama Papic alivyokuwa anadai...usajili wa huyu ulifanya kutemwa kwa Marashi (Steven) ambaye kiuchezaji, ni mzuri kulikoa huyo Mserbia," kiliongeza chanzo hicho.
Aidha, kocha huyo ametakiwa atoe ufafanuzi wa fedha za usajili wa kila mchezaji na uthibitisho wake kuwa alichukua kiasi gani na nini kimebaki kwa sababu suala hilo lilikuwa chini ya kocha huyo kwa asilimia 100.
Tangu Kamati ya Utendaji ya Yanga imwidhinishe Minziro kuwa Kocha Msaidizi, Papic amesusa kuifundisha timu hiyo akisema si chaguo lake, hivyo amekuwa akitaka kulipwa stahili zake.
 
Simba kuifadhili Toto Africa


na Mwandishi wetu, Mwanza


amka2.gif
MWANACHAMA wa Wekundu wa Msimbazi, Simba ya jijini Dar es Salaam anayeishi Mwanza, Idrissa Hassan, amejitolea kuifadhili Toto Africa katika mechi zake za Ligi Kuu Bara zilizobaki ili isishuke daraja.
Hassan ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba tawi la Mkoa wa Mwanza, alisema jijini hapa jana kuwa, yeye ni mpenzi wa Wekundu wa Msimbazi ila anawaomba Wanamsimbazi wenzake wasimuelewe vibaya kwa msaada anaotaka kuutoa kwa Toto Africa.
Alisema, bila ya kuwepo kwa Toto Africa Mwanza asingeweza kuiona Simba na kwamba, hata wale wapenzi wa timu nyingine wanaziona timu zao zikija kucheza mjini hapa kutokana na kuwepo kwa Toto Ligi Kuu.
"Najulikana kabisa kwamba mimi ni Simba damu, sasa leo Toto ikishuka daraja sitaweza kuiona Simba Mwanza, labda niende Dar au mikoa mingine yenye timu zilizo Ligi Kuu, hata na hilo si kwangu tu halikadhalika hata kwa wapenzi wa Yanga, Mtibwa hapa Mwanza, hawataziona hizo timu hapa bila ya kuwepo Toto," alisema.
Alisema, atakuwa bega kwa bega na Toto ambayo Wana Simba wengi wanaamini ni tawi la mahasimu wao Yanga, katika mechi zote zilizobaki, ili kuhakikisha timu hiyo haishuki daraja na kusisitiza kuwaomba Wana Msimbazi wenzake wasimuone amewasaliti.
"Nasisitiza kuwaomba Wana Simba wenzangu wasifikiri ninawasaliti, nia yangu ni kutaka Toto ibaki ligi kuu ili niendelee kuiona Simba hapa Mwanza na hata hivyo nitakuwa nao (Simba), bega kwa bega kwenye mechi yao na Toto, mimi ni mwenzao kabisa," alisema.
Pia aliwataka wapenzi wa michezo katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na wadau wengine, kujitokeza kuisaida klabu hiyo pekee iliyobaki Ligi Kuu katika mikoa ya ukanda huu ili Leo ligi hiyo inaendelea tena ambako wenyeji Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya' wataikaribisha Moro United huku Villa Squad ikivaana na Morani FC.


h.sep3.gif


juu
 
TFF yachakachua ratiba Ligi Kuu


na Mwandishi wetu


amka2.gif
MWANACHAMA wa Wekundu wa Msimbazi, Simba ya jijini Dar es Salaam anayeishi Mwanza, Idrissa Hassan, amejitolea kuifadhili Toto Africa katika mechi zake za Ligi Kuu Bara zilizobaki ili isishuke daraja.
Hassan ambaye pia ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Simba tawi la Mkoa wa Mwanza, alisema jijini hapa jana kuwa, yeye ni mpenzi wa Wekundu wa Msimbazi ila anawaomba Wanamsimbazi wenzake wasimuelewe vibaya kwa msaada anaotaka kuutoa kwa Toto Africa.
Alisema, bila ya kuwepo kwa Toto Africa Mwanza asingeweza kuiona Simba na kwamba, hata wale wapenzi wa timu nyingine wanaziona timu zao zikija kucheza mjini hapa kutokana na kuwepo kwa Toto Ligi Kuu.
"Najulikana kabisa kwamba mimi ni Simba damu, sasa leo Toto ikishuka daraja sitaweza kuiona Simba Mwanza, labda niende Dar au mikoa mingine yenye timu zilizo Ligi Kuu, hata na hilo si kwangu tu halikadhalika hata kwa wapenzi wa Yanga, Mtibwa hapa Mwanza, hawataziona hizo timu hapa bila ya kuwepo Toto," alisema.
Alisema, atakuwa bega kwa bega na Toto ambayo Wana Simba wengi wanaamini ni tawi la mahasimu wao Yanga, katika mechi zote zilizobaki, ili kuhakikisha timu hiyo haishuki daraja na kusisitiza kuwaomba Wana Msimbazi wenzake wasimuone amewasaliti.
"Nasisitiza kuwaomba Wana Simba wenzangu wasifikiri ninawasaliti, nia yangu ni kutaka Toto ibaki ligi kuu ili niendelee kuiona Simba hapa Mwanza na hata hivyo nitakuwa nao (Simba), bega kwa bega kwenye mechi yao na Toto, mimi ni mwenzao kabisa," alisema.
Pia aliwataka wapenzi wa michezo katika mikoa ya Kanda ya Ziwa na wadau wengine, kujitokeza kuisaida klabu hiyo pekee iliyobaki Ligi Kuu katika mikoa ya ukanda huu ili Leo ligi hiyo inaendelea tena ambako wenyeji Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya' wataikaribisha Moro United huku Villa Squad ikivaana na Morani FC.
 
Copa Coca-Cola 2011 yaiva


na Makuburi Ally


amka2.gif
MAKATIBU wakuu wa vyama vya soka vya mikoa hapa nchini, wanatarajiwa kushiriki semina elekezi kwa ajili ya mashindano ya vijana chini ya miaka 17 ‘Copa Coca-Cola' keshokutwa kwenye ukumbi wa Manispaa ya Temeke, jijini Dar es Salaam.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, alisema jijini nDar es Salaam jana kuwa semina hiyo ni kuelekea kuanza michuano hiyo ambayo kwa ngazi ya wilaya imepangwa kuanza Machi Mosi hadi Aprili 10 kabla ya kufuatiwa na mikoa Aprili 23 hadi Mei 7.
Wambura alisema, ngazi ya kanda michuano hiyo itachezwa katika vituo vya Dar es Salaam, Mwanza na Arusha kuanzia Juni 6 wakati ngazi ya taifa itakayoanza hatua ya 16 bora hadi fainali itachezwa Dar es Salaam Juni 25 hadi Julai 2.
 
Ngumi Mwanza wawaangukia wadau


na Sitta Tumma, Mwanza


amka2.gif
CHAMA cha Ngumi za Ridhaa Mkoa wa Mwanza (MBA), kimeiomba serikali kupitia kwa waziri wake wa Habari, Michezo na Utamaduni, Dk. Emmanuel Nchimbi, kukisaidia vifaa zikiwemo fedha kwa ajili ya kuandaa timu bora ya ngumi ya mkoa huo itakayokwenda kushiriki mchezo huo ngazi ya taifa jijini Dar es Salaam.
Chama hicho kinahitaji msaada mkubwa kutoka serikalini na kwa wadau mbalimbali wa michezo, ili kuwawezesha vijana waliopo kambini kufanya mazoezi kwa kutumia vifaa, na kwamba msaada huo wa fedha utasaidia kuwahudumia mabondua hao ili waweze kufanya vizuri katika michuano hiyo itakayofanyika Februari 26 mwaka huu.
Katibu Mkuu wa MBA, Michael Changarawe alitoa wito huo jana jijini hapa, wakati alipozungumza na Tanzania Daima juu ya maandalizi ya kambi ya timu hiyo mkoani hapa.
Alisema, tatizo kubwa linalokikabili chama hicho ni ukosefu wa vifaa na fedha, hali ambayo inawapa wakati mgumu vijana kushiriki kambi hiyo kwa ajili ya kujifua na mashindano hayo.
"MBA Mwanza hatuna fedha wala vifaa vya mazoezi, vijana wanafanya mazoezi kwa sababu tu wanapenda ngumi, lakini tunahitaji msaada ili tuweze kuwaandaa vijana wazuri. Vijana wengine wametoka wilayani lakini hawana fedha na imenilazimu kukaa nao nyumbani kwangu wakati huu tunaandaa timu kwenda Dar es Salaam... tunaiomba Serikali na wadau mbalimbali watusaidie kwa mchango wowote ule ili tufanikishe," alisema Changarawe ambaye pia ni Makamu wa Rais wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa Tanzania (BFT).
Alisema, siku zote Mkoa wa Mwanza umekuwa ukitoa wachezaji wazuri wa ngumi kisha kuliletea heshima kubwa taifa katika medani ya mchezo huo kimataifa, hivyo unahitajika msaada wa kuuwezesha mkoa kupeleka wachezaji wazuri watakaokwenda kuunda timu nzuri na imara ya taifa.
 

Yanga, Mtibwa jino kwa jino leo


Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 2nd February 2011 @ 08:42



BAADA ya kutoka kubanwa mbavu kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho kwa kulazimishwa sare ya mabao 4-4 dhidi ya Dedebit ya Ethiopia mwishoni mwa wiki iliyopita, Yanga leo inarudi kwenye ligi ya nyumbani ambapo itamenyana na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Sare ya Yanga kwenye michuano ya kimataifa imeiweka kwenye wakati mgumu katika mechi ya marudiano itakayochezwa Ethiopia wiki mbili zijazo kwani itatakiwa kushinda ili isonge mbele.

Mechi ya leo ni muhimu kwa Yanga kushinda ili kurudisha imani kwa mashabiki wake, baada ya kuwapigia ‘kelele' kwa kuonesha kiwango kibovu katika mechi dhidi ya Dedebit.

Licha ya hilo, lakini ushindi kwa Yanga leo utaifanya izidi kujikita kileleni.

Kwani kabla ya mechi ya leo inaongoza msimamo kwa tofauti ya pointi nne ikifuatiwa na Simba yenye pointi 27 na Mtibwa ni ya nne ikiwa na pointi 23, nafasi ya tatu inashikiliwa na Azam yenye pointi 26.

Katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa kwenye uwanja wa Jamhuri Morogoro mwishoni mwa mwaka jana, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1, Yanga ikisawazisha dakika za mwisho baada ya kuchez muda mrefu ikiwa nyuma kwa bao 1-0.

Mechi ya leo kila timu inaingia ikiwa na kumbukumbu yake katika mechi za mwisho ambapo Yanga iliifunga Polisi Dodoma mabao 2-0 huku Mtibwa ikitoka sare ya mabao 2-2 dhidi ya Majimaji.

Kocha wa Mtibwa Sugar, Tom Olaba aliliambia gazeti hili jana kuwa anafahamu ugumu na umuhimu wa mechi ya leo.

"Hizi timu kubwa zina mambo yake kwa maana hiyo najua ugumu wa mechi ya kesho (leo), na pia umuhimu wake, kwani tukishinda tutakuwa tumejisogeza kwenye msimamo," alisema Olaba.

Kocha wa Yanga Fredy Minziro alisema anataka kushinda mechi ya leo ili ajikite kileleni mwa msimamo na kwamba wachezaji wake wako kwenye ari ya ushindi.

"Mashabiki wetu wasiwe na hofu kwa sare ya Dedebit, timu yangu iko vizuri na wachezaji wanaendelea na mazoezi kama kawaida, Mtibwa naijua ni timu nzuri, lakini nataka kushinda," alisema.



 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom