Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
-
- #4,581
Panga pangua Ligi Kuu kama kawa
Imeandikwa na Evance Ng'ingo; Tarehe: 2nd February 2011 @ 08:26
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limefanya marekebisho ya ratiba ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo mechi kati ya Azam FC na Toto African ya Mwanza iliyokuwa ichezwe leo itachezwa keshokutwa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana Ofisa habari wa TFF Boniface Wambura alisema kuwa mechi hiyo ya 85 imesogezwa mbele kutokana na mabadiliko ya kawaida ya ratiba hiyo na kwamba itachezwa Uwanja wa Uhuru.
Mechi nyingine iliyobadilishwa ni kati ya Polisi Dodoma na Simba ambayo ilipangwa kuchezwa Februari 5 mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma ambayo kwa sasa imepangwa kufanyika Februari 6 katika uwanja huohuo.
Wambura alisema, mabadiliko ya mechi hiyo ya Polisi Dodoma ni kutokana na taarifa waliyopata kuwa Chama Cha Mapinduzi kitautumia uwanja huo kwa ajili ya sherehe za kuzaliwa kwa chama hicho.
Wambura alisema kuwa katika mchezo wa 90 ambao ni kati ya JKT Ruvu na African Lyon uliokuwa ufanyike Februari 5 Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam sasa utafanyika Februari 7 kwenye uwanja huohuo.
Pia alisema, mabadiliko mengine ni katika mechi kati ya Kagera Sugar na Yanga iliyokuwa ichezwe Februari 16 mwaka huu katika Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba imesogezwa mbele kwa siku moja na sasa itachezwa Februari 17 katika uwanja huohuo.
Aidha Wambura alisema marekebisho zaidi huenda yakafanyika baada ya Chama cha Soka cha Ethiopia kutaja terehe ya marudiano ya mechi ya Kombe la Shirikisho kati ya Dedebit na Yanga itakayofanyika kati ya Februari 11, 12 au 13.