Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
-
- #4,821
Uchunguzi kuhusu nyimbo ya taifa kugoma unaendelea Friday, 04 February 2011 20:50
Sweetbert Lukonge
KAMATI ya kuchunguza tukio la kugoma kupigwa kwa nyimbo za taifa lilijitokeza katika mechi ya kimataifa kati ya Taifa Stars na timu ya taifa ya Morrocco imesema ipo katika hatua za mwisho kukamilisha uchunguzi wake juu ya suala hilo.
Tukio hilo la kugoma kupigwa kwa nyimbo hizo za taifa lilijitokeza katika mchezo huo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete ambaye alisimama kwa muda akisubiria kupigwa kwa nyimbo hizo bila ya mafanikio na baadaye akalazimika kurudi jukwaani mpaka kipindi cha pili cha mechi hiyo.
Akizungumza na Mwananchi jana Mwenyekiti wa kamati hiyo Hamidu Mbwezeleni alisema bado hajamaliza uchunguzi juu ya suala hilo na watakapokuwa tayari wataweka wazi kile walichobaini katika uchunguzi wao.
"Mpaka sasa katika uchunguzi wetu ambao tunaendelea nao tumeweza kubaini mambo mbalimbali ambayo kwa hakika yanazidi kutuongezea kazi ili kuhakikisha tunakamilisha uchunguzi kwa uhakika zaidi.
"Tumegundua kuwa kabla ya mechi hiyo kulikuwa na vikao mbalimbali vilivyoshirikisha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF),Wizara pamoja na wadau mbalimbali wa soka wakiwemo Polisi.
"Pomja na hilo kwa hakika mpaka sasa tumejikuta tunawahoji mpaka Wachina zaidi ni kuhakikisha tunajua nini chanzo cha tatizo hilo hivyo tunawaomba wananchi waendelee kuwa na subira na tutakapo kuwa tayari tutaweka wazi kazi yetu tuliyotumwa tuifanye," alisema Mbwezeleni.