Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Yanga bado ugonjwa wa moyo
• Refa Kidiwa alizua Songea

na Makuburi Ally


amka2.gif
TIMU ya Yanga ya jijini Dar es Salaam jana ilishindwa kupoza hasira za mashabiki wake ambao waliishuhudia ikikutana na kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Mtibwa Sugar baada ya kushuhudiwa ikikabwa koo na Majimaji ya Songea na kulazimishwa sare ya bila kufungana.
Katika mchezo huo uliopigwa Uwanja wa Majimaji mjini Songea, ulikuwa wa vuta ni kuvute ingawaje uliathiriwa na mvua kubwa iliyonyesha mjini humo hiyo jana.
Timu zote zilishambuliana kwa zamu, ingawa wenyeji walishindwa kucheza kwa kujituma hasa ukizingatia walikuwa uwanja wa nyumbani.
Katika dakika ya 88, beki wa Yanga, Nadir Haroub ‘Canavaro’, alifanya kazi ya ziada kuokoa mpira uliokuwa unaelekea wavuni.
Kwa sare hiyo Yanga bado iko kileleni ikiwa na pointi 32 ikifuatiwa kwa karibu na watani wao Simba yenye pointi 30 ingawa zimepishana kwa michezo miwili.
Mara baada ya mechi hiyo, mwamuzi Ibrahim Kidiwa Mdudu wa Tanga pamoja na wasaidizi wake walikumbana na kashikashi ya mashabiki na wachezaji wa Yanga kwa madai ya kutoa maamuzi ya utata na kuwafanya polisi kuingilia kati na kuwatoa chini ya ulinzi.
Baada ya mechi ya jana, Yanga itashuka dimbani katika mchezo wa marudiano wa Kombe la Shirikisho (CAF), dhidi ya Dedebit unaotarajia kuchezwa kati ya Februari 11 na 13, jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Katika mchezo wa awali uliopigwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga ililazimisha sare ya mabao 4-4.
Katika mechi nyingine za Ligi Kuu Bara, Kagera Sugar iliwaliza ndugu zao Mtibwa Sugar kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Kaitaba Bukoba, huku AFC ikizinduka na kuwatoa nishai maafande wa Ruvu Shooting Stars kwa bao 1-0 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.
 
Wagosi wapunguzwa kasi, sare zaiandama TMK


na Safari Chuwa, Tanga


amka2.gif
WENYEJI wa Fainali ya Tisa Bora Ligi Daraja la Kwanza, Coastal Union ‘Wagosi wa Kaya' jana walipunguzwa kasi na timu inayoburuza mkia, Morani FC ya Manyara, baada ya kulazimishwa sare ya 1-1 kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini hapa.
Coastal ambayo ilikuwa imeanza kwa kishindo kwa kushinda mechi mbili mfululizo, jana ilijikuta katika wakati mgumu baada ya vijana hao kutoka Manyara ambao hawajashinda mchezo hata mmoja, kuanza kujipatia bao katika dakika ya 44, mfungaji akiwa Babu Ally, baada ya kupiga shuti kali lililomshinda kipa wa Wagosi, Godson Mmasa na kujaa wavuni, bao lililodumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili kulianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu, lakini walikuwa ni Coastal Union waliofanikiwa kupata penalti dakika ya 66 baada ya mshambuliaji wake Unio Dau kuangushwa eneo la hatari. Tuta hilo lilitiwa kimiani na Mohammed Issa.
Hata hivyo Coastal walipata pigo dakika ya 80 baada ya mwamuzi Simon Mbelwa wa Pwani kumzawadia Kibabu Chandinga kadi nyekundu baada ya kumchezea vibaya Babu Ally wa Morani. Hadi filimbi ya mwisho inapulizwa timu hizo zilitoka nguvu sawa ya bao 1-1.
Katika mechi ya kwanza kwenye uwanja huo, Moro United na Temeke United nazo ziliendeleza wimbi la sare baada ya kufungana bao 1-1.
Walikuwa ni Moro United walioanza kucheka na nyavu dakika ya 17 mfungaji akiwa Henry Ngoye baada ya kupokea pande safi kutoka kwa Bakari Mpakala ambalo lilidumu hadi mapumziko.
Kipindi cha pili, Temeke walibadilika na kulisakama lango la wapinzani wao na kufanikiwa kuchomoa katika dakika ya 76 kupitia kwa Paul Malipesa baada ya kupiga mpira wa adhabu ndogo uliokwenda moja kwa moja wavuni.
Ligi hiyo leo ni mapumziko ambako itaendelea tena kesho kwa maafande wa JKT Oljoro ya Arusha kuvaana na Villa Squad ya Dar es Salaam huku Tanzania Prisons ya Mbeya ikipepetana na Temeke United ya Dar es Salaam.


h.sep3.gif

 

Yanga yabanwa


Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 5th February 2011 @ 23:59
YANGA imeendelea kutia doa rekodi yake kwenye Ligi Kuu Tanzania Bara baada ya kung'ang'aniwa kwenye Uwanja wa Majimaji na kutoka sare ya bila kufungana dhidi ya Majimaji ya Songea.

Matokeo hayo yamekuja siku chache baada ya Yanga kutoka kupata kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mechi nyingine ya ligi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa Dar es Salaam Jumatano iliyopita.

Kabla ya mechi ya Mtibwa Sugar, Yanga ilikuwa haijafungwa mchezo wowote tangu ianze Ligi Kuu.

Katika mechi ya jana iliyokuwa ikichezwa huku mvua nyingi ikinyesha, Yanga haikuonesha ufundi wowote na Majimaji ilifanya mashambulizi ya mara kwa mara langoni kwa wapinzani wao na kukosa mabao kadhaa ya wazi.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga iendelee kuongoza kileleni kwa pointi 32 na ikiwa imecheza mechi nyingi zaidi ya mtani wake wa jadi Simba.

Yanga imecheza mechi 15 wakati Simba leo itacheza mechi yake ya 14 dhidi ya Polisi Dodoma.

Katika mechi nyingine ya ligi iliyochezwa jana, AFC iliona mwezi baada ya kuifunga Ruvu Shooting bao 1-0 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha.

Hata hivyo, pamoja na ushindi huo AFC bado iko mkiani mwa Ligi hiyo ikiwa na pointi nane.

Bao la AFC lilifungwa na Abdallah Juma katika dakika ya 30 ya mchezo huo uliokuwa wa vuta nikuvute.

Aidha kwenye Uwanja wa Kaitaba, Kagera Sugar iliichapa Mtibwa Sugar bao 1-0. Ligi hiyo inaendelea tena leo kwenye Uwanja wa Jamhuri Dodoma pale bingwa mtetezi Simba itakapomenyana na Polisi ya huko.

Simba leo ina nafasi nzuri ya kurejea kileleni baada ya Yanga jana kutoka sare. Simba ina pointi 30 na Yanga 32, ikishinda leo itakuwa na pointi 33 na hivyo kurejea tena kileleni ilikoenguliwa tangu kuanza kwa mzunguko wa pili wa ligi hiyo.

Hata hivyo mechi ya leo haitarajiwi kuwa rahisi kwa Simba, kwani katika mechi ya mzunguko wa kwanza iliyochezwa, mabingwa hao walifungwa na Polisi.



 
Wapalestina kutua Dar leo


na Makuburi Ally


amka2.gif
TIMU ya Taifa ya Palestina inatarajiwa kuwasili nchini leo mchana kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Taifa Stars utakaopigwa Jumatano kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura, msafara wa timu hiyo utakuwa na wachezaji 22 na viongozi sita.
Wambura alisema baadhi ya viongozi wa Palestina wamewasili jana kwa ajili ya maandalizi ya timu yao, ambayo itafikia Hoteli ya Tansoma, Mnazi Mmoja jijini, ambako Rais wa TFF, Leodegar Tenga atakuwa na mkutano na waandishi wa habari baada ya timu hiyo kuwasili.
Mechi hiyo kwa Stars ni sehemu ya maandalizi ya mechi zake za kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika (CAN), mwaka 2012, Guinea ya Ikweta na Gabon.
 
Waandaaji Tamasha la Pasaka wapewa 5

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 5th February 2011 @ 23:55
NAIBU Waziri wa Uchukuzi, Dk. Athuman Mfutakamba amelisifia tamasha la Pasaka kwa kusema ni jambo jema zaidi kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji ya biashara wanawake wajane.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari juzi na Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ni kuwa Naibu Waziri ameguswa na shughuli ambazo waandaaji wa tamasha hilo Kampuni ya Msama Promotions inafanya.

"Tunashukuru kwamba Naibu Waziri ameguswa na namna tamasha letu linavyoshughulika na kuwasaidia watoto yatima na wajane.

"Alisema amefarijika mno na muamko huu na kuwa huu ni mfano wa kuigwa kwani ni watu wachache mno wanaoweza kuandaa matamasha kama haya na fedha zinazopatikana kuwasaidia yatima na wajane," alisema Msama akimkariri Mfutakamba.

Msama alieleza kuwa Mtufakamba amesema kwa kiasi kikubwa tamasha hilo pia litasaidia kupunguza tatizo la ajira kwa vijana, kwani wengi hivi sasa wameamua kujikita katika muziki wa Injili kwa ajili ya kumuimbia Mungu na kujipatia kipato.

Tamasha la Pasaka linatarajiwa kufanyika Aprili 24 mwaka huu siku ya sikukuu ya Pasaka katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam na baadaye kufanyika mjini Shinyanga Jumatatu ya Pasaka Aprili 25 na jijini Mwanza Aprili 26, lengo lake kubwa mwaka huu ni kwa ajili ya kuwasomesha yatima na kuwasaidia mtaji wa biashara wanawake wajane.


 

ZIFF, Bongo Movies ndani ya Iran

Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 5th February 2011 @ 23:50
ZANZIBAR International Film Festival (ZIFF) bado imedhamiria katika kukuza soko la filamu za hapa nyumbani na katika kufanya hivyo iko mjini Tehran, Iran katika tamasha kubwa la Fajr International Film Festival linaloambatana na Iran Film Market.

ZIFF inajaribu kupata wasambazaji, wazalishaji ama wawekezaji wa filamu duniani ambao wangependa kununua, kusambaza, kutengeneza ama kufanya kazi ya pamoja na kiwanda cha filamu hapa Bongo.

"Kwa wakati huu ilikuwa rahisi kupata filamu toka Steps na Pilipili kwa ajili ya kuja kuangalia soko huku Mashariki ya Kati na Asia, natumai mambo yataenda vizuri, napenda kusisitiza umuhimu wa kufanya kazi nzuri ili zipate kuuzika," alisema Meneja wa ZIFF, Daniel Nyalusi aliyeko Iran.

Pia ZIFF imeenda kuangalia namna ya kupata wawekezaji wa tasnia hii ili kuleta uchangamfu kwa watengenezaji wa ndani na pia kupata filamu toka nchi mbali mbali zitakazooneshwa katika tamasha la mwaka huu Juni 18 - 26, 2011.


 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom