Barcelona yatoa zawadi ya Krismasi
Sunday, 19 December 2010 20:00
BARCELONA, Hispania
MABINGWA watetezi wa ligi kuu ya Hispania Barcelona wameiachapa Espanyol bao 5-1 katika mechi ya ligi kuu na kupata ushindi wa 10 mfululizo hivyo kuiacha Real Madrid kwa pointi tano katika msimamo wa ligi.
Katika mechi hiyo Pedro Rodriguez alifunga mabao mawili na David Villa pia alifunga mabao mawili huku Xavi Hernandez akifunga bao moja, ambapo bao la Espanyol lilifungwa na Osvaldo.
Katika mechi nyingine ya ligi kuu ya Hispania, Villarreal iliichapa Mallorca bao 3-1. Mabao ya Villarreal yalifungwa na Santiago Cazorla na Giuseppe Rossi huku bao la Mallorca likifungwa na Jonathan de Guzman.
Pia timu ya Athletic Bilbao iliichapa Levante 2-1 na Deportivo La Coruna ilitoka sare ya bao 1-1 na Sporting Gijon.
Huko mjini ATHENS, Ugiriki, wachezaji wa Panathinaikos walijikuta wakikimbizwa uwanjani na mashabiki wao baada ya timu hiyo kufungwa bao 1-0 na timu ya Volos katika mechi ya ligi kuu ya nchi hiyo.
Baada ya mechi kumalizika mashabiki wengi wa Panathinaikos waliwatupia vitu mbalimbali wachezaji wao na kuharibu vibaya sehemu ya jukwaa wanalokaa watu muhimu na hivyo kusababisha hasara kubwa.
Mashabiki wa Panathinaikos walionyesha dalili za kutaka kuwafanyia vurugu wachezaji wao tokea wiki iliyopita, ambapo katika mechi dhidi ya Asteras ambayo walitoka sare ya 0-0 kabla ya mechi kuanza mashabiki hao walishika bango ambalo lilikuwa likisomeka,"sisi hatuna kazi nyinyi ni matajiri mnaoishi maisha ya anasa"...."Tunaishiwa uvumilivu". Katika mechi hiyo mashabiki wa Panathinaikos muda mwingi walikuwa wakiwazomea wachezaji wao.
Mjini Berlin, Timu ya Nuremberg iliichapa bao 3-1 Hannover katika mechi ya ligi kuu nchini Ujerumani.
Mabao ya Nuremberg yalifungwa na Andreas Wolf na lingine lililitokana na beki wa Hannover, Steven Cherundolo ambaye alijifunga katika mechi hiyo huku bao la Hannover likifungwa kwa mkwaju wa penati na Sergio Pinto.
Mechi nyingine nchini humo ilikuwa ni kati ya Mainz dhidi ya St.Pauli ambapo Mainz iliibuka na ushindi wa bao 4-2, pia Borussia Dortmund, ilijikuta ikichapwa bao 1-0 na Eintracht Frankfurt.
Huko mjini MILAN, Italia, timu ya Roma imeichapa AC Milan bao 1-0 ambapo bao la Roma lilifungwa na Marco Borriello katika mechi ya ligi kuu ya Italia.
Milan ambayo ina pointi 36 ndiyo inayoongoza ligi kuu ya italia, lakini ili kuendelea kuongoza ligi hiyo ilikuwa ikitegemea mechi za jana za timu za Juventus, Napoli na Lazio ambazo zipo nyuma yake.
Mjini LONDON, Uingereza timu ya West Ham ilitoka sare ya bao 1-1 na Blackburn hivyo kuendelea kushika mkia katika ligi kuu ya Uingereza.
Mjini PARIS, Ufaransa timu ya Rennes iliichapa Valenciennes bao 1-0