Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
-
- #1,341
Kaburu ampeleka Uhuru India
na Mwandishi wetu
MAKAMU mwenyekiti wa mabingwa wa soka Tanzania Bara, Simba Wekundu wa Msimbazi Geofrey Nyange Kaburu, alitarajiwa kuondoka jana jioni sambamba na Uhuru Selemani kwenda India kwa ajili ya matibabu ya mchezaji huyo. Mshambuliaji huyo mwenye kasi na chenga, amekuwa akisumbuliwa na majeraha ya nyama za paja na kumfanya kuwa nje ya dimba kwa muda mrefu.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Kaburu alisema kwa mujibu wa daktari wa Uhuru hapa nchini, ametoa ruhusa ya kwenda kutibiwa zaidi nchini India na atakaa huko kwa siku saba.
Makamu huyo mwenyekiti aliongeza kuwa wakati Uhuru akikaa kwa siku saba yeye baada ya siku mbili atarejea nchini ili kuendelea na majukumu mbalimbali ya klabu yake.
Mchezaji huyo alikuwa mchango mkubwa kwa klabu yake na hata timu ya taifa, Taifa Stars, ambako mara amekuwa akiitwa, kabla ya kupatwa na majeraha hayo.