Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
-
- #1,481
Machuppa, SMG waitwa Stars
Imeandikwa na Grace Chilongola, Mwanza; Tarehe: 24th December 2010 @ 23:59
WASHAMBULIAJI Athumani Machuppa anayecheza soka ya kulipwa Sweden na Saidi Maulidi ‘SMG anayecheza Angola wameitwa kwenye kikosi cha timu ya soka ya taifa, Taifa Stars kitakachokwenda Cairo, Misri kwa ajili ya michuano maalumu ya mto Nile.
Mbali na wachezaji hao ambao hawajaitwa Stars kwa takriban miaka mitatu, mshambuliaji wa Yanga Jerryson Tegete, mchezaji mpya wa Simba Ally Ahmed ‘Shiboli' na mchezaji wa Kagera Sugar Godfrey Taita nao wameitwa kwenye kikosi cha timu hiyo.
Tegete aliachwa takribani mara mbili na Kocha Mkuu wa Stars Jan Poulsen.
Katika kikosi cha jana kilichotangazwa kwenye Uwanja wa Nyamagana mjini hapa na Kocha Msaidizi wa Stars Silvestre Marsh, mshambuliaji Gaudence Mwaikimba ameachwa pamoja na kiungo wa Simba Mohamed Banka ambao walikuwapo kwenye kikosi cha Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars' kilichotwaa ubingwa wa Kombe la Chalenji katikati ya mwezi huu.
Michuano ya mto Nile inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Cairo, Misri Januari 5 na Stars itaingia kambini keshokutwa kabla ya kuondoka Januari 2.
Timu hiyo itakuwa kambini chini ya Marsh na kocha wa makipa Juma Pondamali na Kocha Mkuu Poulsen ambaye yuko nyumbani kwao Denmark kwa mapumziko ya sikukuu za mwisho wa mwaka ataungana nayo Cairo, Januari 3.
Mbali na Tanzania, nchi nyingine zinazoshiriki katika michuano hiyo inayoshirikisha nchi zilizo ukanda wa ziwa Victoria na mto Nile ni Kenya, Rwanda, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Eritrea, Ethiopia, Sudan na wenyeji Misri.
Lengo la michuano hiyo ni kuhamasisha kutunza vyanzo vya maji kwa ajili ya vizazi vijavyo.
Kwa mujibu wa ratiba, Stars itaanza kufungua dimba la michuano hiyo dhidi ya wenyeji Misri Januari 5 saa moja jioni, kabla ya mechi hiyo Kenya itacheza na Sudan saa kumi jioni.
Stars itacheza mechi nyingine dhidi ya Sudan Januari 11 kabla ya kumenyana na Kenya Januari 14 na kisha itamaliza na Uganda Januari 17.
Kikosi kamili: Makipa ni Juma Kaseja (Simba), Shaaban Kado (Mtibwa) na Said Mohamed (Majimaji). Walinzi ni Shadrack Nsajigwa, Stephano Mwasika , Nadur Haroub ‘Canavaro'(Yanga), Aggrey Morris, (Azam), Kelvin Yondani, Jumma Nyosso, (Simba).
Viungo ni Idrissa Rajabu (Sofapaka, Kenya), Nurdin Bakari, Abdi Kassim ‘Babi', (Yanga), Shaaban Nditti (Mtibwa) Henry Joseph, (Norway), Jabir Aziz.
Washambuliaji ni Salum Machaku (Mtibwa), Mrisho Ngassa (Azam), Nizar Khalfan, (Canada), Godfrey Taita (Kagera Sugar), Athuman Machuppa, (Sweden), Jerry Tegete, (Yanga) Said Maulid(Angola) na Ali Ahmed Shiboli (Simba)