Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
-
- #1,581
Obotte; Wasanii ondoeni tofauti zenu
Saturday, 25 December 2010 11:28
Elizabeth Suleyman
MSANII nyota kutoka nchini Malawi Anna Obotte, amewaasa wasanii wa Tanzania kupendana na kuondoa tofauti zao, hususani katika kipindi hiki cha msimu wa kuelekea sikukuu ya Krismas na mwaka mpya, na badala yake wamgeukie Mungu zaidi.
Akizungumza na starehe katika mahojiano maalumu, msanii Anna ambaye anakubalika kupitia tasnia ya muziki ndani ya Malawi na nchi jirani, anasema wasanii wa hapa nchini wana mwamko wa uimbaji sana, ila tatizo ni kwamba hawapendani na sababu ni wivu uliokithiri miongoni mwao.
Obotte anasema, kwa upande wake anamshukuru Mungu mwaka huu unatofauti sana kwake na miaka mingine, kwani amepata mafanikio makubwa kupitia tasnia hiyo.
"Nina kila sababu ya kumshukuru Mungu, kwa uzima alionijalia hadi leo na mwaka huu nimemuona akinipigania na kunipa mafanikio, tofauti na miaka ya nyuma," anasema Obotte
Anasema sikukuu hizi, ziwe funzo kwa wasanii wa bongo kuhakikisha mwaka huu wanasherehekea kwa upendo na amani bila kubaguana wala kuendekeza chuki.
"Kwa jinsi ninavyoijua Tanzania kama nchi ya amani na upendo, nilijua pia wasanii wake nao wana upendo, lakini nimeshangaa kuona wasanii hususani wa Injili wamekuwa na wivu wa kukataa hata kuwainua wenzio kiushauri," anasema
Anna aliongeza, kwa kuwataka wasanii wa Tanzania hususani wa muziki wa Injili wajue kuwa wanamwimbia Mungu na sio fedha wala chuki, badala yake waimbe kwa kudhamiri ili jamii imgeukia Mungu kupitia uimbaji.
Hata hivyo msanii huyo kutoka Malawi, anasema amekuwa akiridhika na kile anachokipata na kwamba Albamu yake iliyobeba wimbo wa ‘Niseme nisiseme' yenye nyimbo nane, ambayo iko sokoni hivi sasa imekuwa ikifanya vema na kukubalika na mashabiki.
Na kwamba mwezi April mwakani anatarajia kutoa Video yake kali, nayo itakuwa na nyimbo nane kama kawaida.