Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
- #1,681
FRAT bado yaikomalia TFF
Monday, 27 December 2010 09:23
Sweetbert Lukonge
BAADHI ya viongozi wa Chama cha Waamuzi wa Soka nchini (FRAT) wamelitaka Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kutoa ufafanuzi wa kina juu tuhuma za madai ya kukatwa baadhi ya majina ya waamuzi kwenye orodha ya FIFA.
Wakizungumza na Mwananchi jana kwa sharti la kutotajwa majina yao viongozi hao walisema kuwa TFF inatakiwa kutoa ufafanuzi wa kina juu ya tuhuma hizo ili kujua ni sehemu gani yenye makosa katika suala hilo.
ìLicha TFF hivi karibuni kutoa ufafanuzi juu ya tuhuma za kuyaondoa baadhi ya majina katika orodha iliyotumwa FIFA kwa lengo la kupitishwa katika orodha ya waamuzi wa kimataifa bado shirikisho hilo linatakiwa kutoa ufafanuzi wa kina juu ya jambo hilo.
ìKutokana na taarifa mbalimbali ambazo tumekuwa tukipata kutoka kwa baadhi ya viongozi wa shirikisho hilo, inasemakana TFF iliyaondoa majina ya waamuzi hao na kupitisha ya wale ambao ilikuwa ikiwahitaji.
ìHaingii akilini kuwa FIFA itoe agizo la mdomo juu ya kuwasimamisha waamuzi kwa ajili ya uchunguzi bila ya barua na baadaye FIFA iwatumie katika mashindano ya kimataifa lakini waamuzi hao wakosekane katika orodha ya wale walioteuliwa katika orodha ya waamuzi wa kimataifa, hivyo tunaomba ufafanuzi zaidi,î walisema viongozi hao.
Kwa upande wake Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limesema kuwa halihusiki na tuhuma hizo isipokuwa liliwasilisha majina yote FIFA ya waamuzi wote waliofikia vigezo vinavyotambuliwa kimataifa na endapo kama jina la mwamuzi yeyote halipo katika orodha iliyorudi basi hajakidhi vigezo.
Kaimu katibu mkuu wa TFF, Sunday Kayuni alisema kuwa miongoni mwa vigezo hivyo ni pamoja na Waamuzi waliopendekezwa kuwa waamuzi wa kimataifa ni lazima wawe wamefaulu jaribio la utimamu wa mwili katika eneo husika miezi minne kabla ya tarehe ya mwisho ya kuchaguliwa kwa waamuzi.
Mbali na hilo pia wawe wamefaulu vipimo vya afya zao ili kuthibitisha wanaweza kutimiza majukumu ya uamuzi katika kipindi cha miezi minne kabla ya kuchaguliwa kwa orodha ya waamuzi wa kimataifa.
Hata hivyo Chama wanachama ni lazima kipeleke FIFA matokeo yenye mpangilio wa ubora wa waamuzi wanaopendekezwa yanayotokana na alama walizopata kutokana na michezo waliochezesha katika Ligi Kuu miezi 12 kabla ya kuchaguliwa.
ìKuna vigezo vingine vingi, lakini hivi ni baadhi tu, hivyo kutokana na vigezo hivyo kama mwamuzi hana ni lazima jina lake halitopitishwa katika orodha ya waamuzi wa kimataifa kwa sabubu hajakidhi viwango na sifa zinazotakiwa.
ìKutokana na hali hiyo wale ambao majina yao hayakupitishwa inawezekana kabisa hawakukidhi viwango hivyo, hivyo TFF hatupaswi kulaumiwa kwa hilo, sisi tupo kuhakikisha kila mdau anapata haki kwa mujibu wa kanuni na sheria na zile za FIFA," alisema Kayuni.