Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Siku 14 zamuumiza kichwa Ancelotti


LONDON, England

KOCHA wa Chelsea, Carlo Ancelotti anaamini siku 14 zijazo ndiyo zitakuwa kipindi kigumu wakati mbio za kuwania ubingwa wa Ligi Kuu, zitakapokuwa zimeingia
katika mwezi wa mwisho.

Hivi sasa kikosi hicho cha Stamford Bridge, ambacho kilikuwa hakifanyi vizuri kwa sasa ndiyo kinaonekana kuwa mpinzani mkubwa wa Manchester United, baada ya kushuhudiwa Arsenal Jumapili ikifungwa na Bolton na kikosi hicho kitakutana na cha Sir Alex Ferguson Mei 8, mwaka huu kwenye Uwanja wa Old Trafford.

Mabingwa hao watetezi wanaamini kuwa wapinzani wao Arsenal, mwishoni mwa wiki hii wanaweza kuwapa hafueni wakati Manchester United itakapofunga safari hadi kwenye Uwanja wa Emirates ikisaka kuendelea kukaa kileleni kwa pointi nne.

Wakati Man United ikisaka pointi tatu kwa Arsenal, Chelsea wao watakuwa wakikabiliana na wapinzani wa Gunners katika ukanda wa Kaskazini mwa jiji la London, Tottenham siku moja kabla.

Akizungumzia kuhusu ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya West Ham, Ancelotti alisema: "Endapo tutaweza kuifunga Tottenham, tutaweza kuipa presha Manchester United wakati wa mechi dhidi ya Arsenal.

"Tuna mechi mbili muhimu. Ubingwa utaamuliwa ndani ya siku 14," aliongeza.

Mbali na kupigia mahesabu ubingwa huo ndani ya siku 14, Ancelotti pia alipuuza kuwepo kwa uwezekano wa ubingwa kuamuliwa kwa tofauti ya magoli, jambo ambalo halijawahi kutokea tangu Arsenal ilipoipiku Liverpool mwaka 1989.

Akizungumzia kuhusu kuwepo kwa uwezekano huo, kocha huyo alisema kuwa "Inaweza kutokea, hivyo jambo la muhimu tunahitaji kufunga mabao matatu na leo hatukustahili kufunga mabao matatu, lakini ni vizuri."

Kocha huyo wa zamani wa timu ya AC Milan, pia alisema kikosi chake hakiwezi kujizuia kupoteza pointi moja hadi mwishoni mwa msimu na akasema pia mechi dhidi ya Everton na Newcastle, ndizo zitakazotoa mwelekeo.

"Itakuwa vigumu kushinda mechi zote nne, tunakabiliwa na mechi ngumu," alisema. "Tunafahamu kwamba endapo tutapoteza mechi moja tutakuwa tumepoteza matumaini yetu na hapo ndipo itakapoanza presha," aliongeza.
 
Ferguson apiga mkwara wapinzani wake


BERLIN, Ujerumani

KOCHA Alex Ferguson, amewaambia wapinzani wake kuwa hakuna timu ambayo inaweza kuvunja ari ya vijana wake wa Manchester United.Manchester United jana
ilicheza mechi ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Schalke 04 nchini Ujerumani, Real Madrid au Barcelona mojawapo itacheza fainali katika Uwanja wa Wembley Mei 28, mwaka huu.

Fergie ametamba kuwa kati ya wapinzani wake, hakuna ambaye anaweza kuzuia hamu yake ya kutaka kupata mafanikio ya kutwaa ubingwa wa Ulaya kwa mara ya nne.

Alisema: "Kuhusu ubora wa timu, unachokiona kama ilivyokuwa dhidi ya Everton Jumamosi, timu hii haitasinzia.

"Hakuna nafasi kabisa kwa timu hii kukata tamaa. Hakuna nafasi. Ina ubora mkubwa."

Kocha huo alisema mshambuliaji wake, Wayne Rooney amerejesha kiwango chake.

Mchezaji huyo mwenye miaka 25, jana alitarajiwa kucheza katika Uwanja wa Gelsenkirchen, ambao alitolewa kwa kadi nyekundu wakati akiwa katika timu ya taifa ya England kwenye michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2006, kutokana na kumchezea faulo mlinzi wa Ureno, Ricardo Carvalho.

Lakini Fergie anaamini kuwa sasa mchezaji huyo, amejua umuhimu wake katika uchezaji.

"Ninafikiri kwamba Rooney, zaidi ya yeyote amejua kuwa uchezaji ni kitu ambacho kila wakati kitapimwa kwa sababu kuna matarajio kwake.
 
Elimu kikwazo kwa makocha Send to a friend Tuesday, 26 April 2011 20:46

Sweetbert Lukonge
NYOTA wa zamani Mwanamtwa Kihwelu na Sekilojo Chambua wamesema kiwango kidogo cha elimu kwa baadhi ya makocha nchini kinachangia kushusha viwango vya wachezaji pamoja na kuwafanya washindwe kufundisha soka nje ya nchi kama walivyo wenzao wa Kenya na Uganda.

Wakizungumza na Mwananchi kwa nyakati tofauti nyota hao waliowahi kuzichezea timu mbalimbali za Ligi Kuu pamoja na timu ya Taifa walisema kiwango kidogo cha elimu ndiyo kinachosababisha wachezaji kupotea mapema.

"Makocha wengi hapa nchini wanatakiwa kujiendeleza kielimu ili waweze kufikia viwango vya kimataifa katika fani ya ukocha kama walivyo wenzao wa Uganda na Kenya,"alisema Mwanamtwa.

"Bila ya elimu wasitegemee kabisa kuwa ipo siku watapata mafaniko katika maisha yao ya ukocha zaidi ya kuendelea kubanana na vitimu vya hapa nchini ambavyo huchangia kushusha viwango vya wachezaji badala ya kuviendeleza," alisema Chambua.

Walisema inasikitisha sana kwa sababu hata siku moja haijawahi kusikika kocha wa Tanzania kaiwezesha timu yoyote ya Afrika nje ya Tanzania kama walivyo wenzao wa Kenya na Uganda ambao wanafanya vizuri na kuongezea sifa nchi yao.
Walisema hata katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara makocha wa kigeni ndiyo wanafanya vizuri tofauti na wazawa jambo ambalo kwa namna moja ama nyingine linadhihilisha wazi kuwa makocha wetu hapa nchini wanapaswa kujiendeleza kielimu ili waweze kufikia mafaniko na kupata nafasi ya kufundisha soka nje ya nchi hali ambayo itasidia kwa kiwango kikubwa kuinua soka la Tanzania.
 
Iniesta aiota fainali ya Wembley Send to a friend Tuesday, 26 April 2011 20:44

MADRID, Hispania
Kiungo wa Barcelona, Andres Iniesta tayari ameashaanza kufikiria kucheza fainali ya Ligi ya Mabingwa kwenye Uwanja wa Wembley wakati timu yake ikijiandaa na mchezo wa nusu fainali dhidi ya Real Madrid.

"Nina ndoto ya kuelekea Wembley. Tunachotakiwa kufikiria kwa sasa ni kuifunga Madrid leo tukipata mabao mengi tutawaelekeza mashabiki wetu safari ya Wembley," Iniesta alisema kwenye mkutano wa habari.

"Itakuwa ni zawadi ya aina yake tukifanikiwa kutwaa taji la pili," alisema Iniesta, akimaanisha taji la ligi ni kama wamesharichukua na ubingwa wa ligi ya mabingwa utawakumbusha msimu wa 1992, 2006 na 2009 waliponyakuwa taji hilo.

"Tunatakiwa kupigana hadi dakika ya mwisho," alisisitiza, akijua kuwa Real wanahamu kubwa ya kutwaa taji la 10, na kumpa kocha Jose Mourinho taji la kwanza akiwa nchini Hispania kama walivyofanya kwenye Kombe la Mfamle waliposhinda dhidi ya vijana hao wa Catalan.

Barca wanajivunia mchezo wa kasi na pasi fupifupi, kitu ambacho kinawapa nafasi kubwa ya kumsambaratisha Mourinho anayejaribu kutegeza mafanikio yake ndani ya Real katika msimu huu wa kwanza.

Kama wakifanikiwa kupita hapo basi kuna uwezekano wa kurudia fainali ya 2009, kwa kucheza dhidi ya Manchester United au Schalke hapo Mei 28.

Lakini, Iniesta alikiri kuwa wanapaswa kusahau yaliyotokea kwenye Kombe la Mfamle walipofungwa kwa bao la kichwa la Cristiano Ronaldo na kuwafanya wapoteze ubingwa huo.

"Tunatakiwa kuendelea kucheza mchezo wetu wa kawaida, huku tukijaribu kulinda goli letu na kushambulia kwa malengo ya kupata bao la ugenini kitu ambaco kitakuwa kizuri kwetu," alisema Iniesta.

"Kila mechi ina mbinu zake tofauti na hii ni moja wapo kama itavyokuwa mechi ya marudiano," aliongeza Iniesta.
 
'Man Utd pazuri ila Inter ni zaidi' Send to a friend Tuesday, 26 April 2011 20:33

MILAN, Italia
KIUNGO wa Inter Milan, Wesley Sneijder ambaye hivi karibuni amehusishwa na kutaka kujiunga na Manchester United ameisifu klabu hiyo ya England kuwa ni zuri, lakini akisisitiza bado anafuraha kuendelea kubaki Milan.

Kiungo huyo wa kimataifa wa Uholanzi amekuwa akisakwa kwa muda mrefu kwa ajili ya kuziba nafasi ya mkongwe Paul Scholes, japokuwa amekuwa na mafanikio ndani ya Milan kwa sasa, lakini maneno ya ukarimu ya Sneijder yanaamisha milangi ipo wazi kwake kujiunga na United hapo baadaye.

Akizungumza na televisheni ya Studio Ajax, akijibu swali: "Unataka kwenda United? alisema Ni timu. Lakini bado nina furaha kuwa Milan na sasa si muda wa kuwaza hayo."

Hata rais wa Inter, Massimo Moratti hakuonyeasha kupinga chochote kuhusu uwezekana wa kiungo huyo kuondoka San Siro. Akizungumzia suala hilo, bosi huyo alionyesha kuwa ni kweli United wanana na kiungo huyo, lakini hawajasema lolote kuhusu uhamisho wake.

ìNi wazi kuwa Manchester United wanamtaka Sneijder,î alisema Moratti. ìLakini, kitu pekee ninachokipenda ni kuonaSneijder anabaki hapa na kucheza kwa miaka mingi zaidi.î
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom