Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
- #1,821
TP Mazembe yaiwinda Simba
Imeandikwa na Mwandishi Wetu; Tarehe: 28th December 2010 @ 09:36 Imesomwa na watu: 315; Jumla ya maoni: 0
Kikosi cha timu ya TP Mazembe Englebert ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambayo bingwa mtetezi wa ligi ya mabingwa barani Afrika.
KATIKA kile kinachoonekana kutaka kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa kwa mara ya tatu mfululizo, wapinzani wanaotarajiwa kukutana na Simba kwenye michuano hiyo, TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeimarisha kikosi chake kwa kusajili wachezaji wa kimataifa wa Zambia wa wawili.
Simba ina nafasi kubwa ya kukutana na mabingwa hao watetezi wa Ligi ya Mabingwa endapo itaitoa Elan de Mitsoudje ya Comoro katika raundi ya awali.
Mkurugenzi wa habari wa Mazembe, Eddy Kabelu alithibitisha hayo mjini Lubumbashi juzi kwamba timu hiyo imekamilisha mkataba wa mwaka mmoja na kipa wa Zambia, Kalilou Kakonje ambaye amemaliza mkataba wake na klabu ya Ligi Kuu ya Afrika Kusini, AmaZulu Agosti.
Klabu hiyo pia imemsajili kiungo aliyekuwa akiwaniwa na Mamelodi Sundowns, Rainford Kalaba na kufanya kikosi hicho kuwa na wachezaji sita kutoka Zambia akiwepo Given Singuluma, Hichani Himonde, Sunzu Stopila na beki Emmanuel Mbola.
Mazembe walipoteza mechi ya fainali ya Kombe la Dunia, Abu Dhabi kwa mabao 3-0 dhidi ya Inter Milan, lakini sasa mmiliki wa klabu hiyo na gavana wa jimbo la Katanga, Moise Katumbi anasema anataka kushinda michuano ijayo inayoandaliwa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).
"Tulifanya Afrika nzima kujisikia fahari," alisema Katumbi. "Hatukucheza kwa sababu ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, bali Afrika kwa ujumla.
Na napenda kupeperusha bendera ya Afrika juu, sitaki kuzungumzia kuhusu mwamuzi wa fainali lakini kila mmoja aliona alivyosimamia mchezo.
"Natamani ningewahamasisha Fifa kuangalia baadhi ya waamuzi wao, inakatisha mno tamaa kwa namna mwamuzi alivyochezesha, lakini hiyo ni historia.
"Tutajifunza kutokana na uzoefu huo na tunatumaini tutakuwa jasiri zaidi ya mwaka huu.Dunia haiwezi tena kudharau soka ya Afrika.
"Ukiangalia soka kimataifa hasa Ulaya ambako ipo juu, utagundua kila timu kubwa Hispania, England, Italia, Ujerumani na Ufaransa inaongozwa na mchezaji wa Afrika.
Nafikiri kama wakichagua kikosi cha kucheza na kila bara, Afrika inaweza kushinda michuano.
"Muangalie Didier Drogba, Samuel Eto'o, Michael Essien, Asamoah Gyan, Kevin Prince-Boateng, Stephen Pienaar, Yaya Toure, kwa uchache ningependa kuona michuano kama hiyo ikitokea kwa kuandaliwa na Fifa ili tuone nani ataibuka shujaa.
Lakini TP Mazembe tutaendelea kupeperusha bendera ya Afrika. Ujio wa Kakonje kutoka Lusaka na kutua Lubumbashi kunaonekana kama njia ya kumtaka kipa Robert Kidiaba kuimarika zaidi.
Kipa huyo mfupi alikuwa tegemeo timu ilipofika fainali ya Klabu Bingwa ya Dunia. Kakonje anaelewa ujio wake kwenye nafasi hiyo utamtaka kuongeza jitihada zaidi ingawa tayari amefanya mazoezi na miamba hao kwa miezi mitano kabla ya kusaini mkataba rasmi.
Kipa huyo namba mbili wa Chipolopolo atajiunga na TP Mazembe Januari 4 kuanza maandalizi ya msimu.
Mazembe wataanza kutetea taji lao dhidi ya mshindi kati ya mabingwa wa Comoro, Mitsoudje au miamba wa Tanzania, Simba.