Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Stars bado sio riziki


na Mwandishi Maalum, Cairo


amka2.gif
TIMU ya soka ya Tanzania ‘Taifa Stars' jana ilizikosa sh milioni 40 baada ya kushindwa angalau kutwaa nafasi ya tano ya mashindano yanayoshirikisha nchi za ukanda wa Bonde la Mto Nile baada ya kukubali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Sudan, mchezo uliochezwa mjini hapa.
Taifa Stars na Harambee Stars zilipoteza nafasi ya kunyakua ubingha wa mashindano hayo baada ya kufungwa katika hatua ya nusu fainali ambako fainali za mashindano hayo zimewakutanisha Misri na Uganda katika fainali.
Matokeo ya mchezo wa juzi ya nusu fainali ya michuano hiyo kati ya timu ya Taifa ya Kenya 'Harambee Stars' na Misri 'Farao' uliomalizika kwa Misri kuibuka na ushindi wa mabao 5-1.
Ushindi kama huo iliupata Misri katika mchezo wake wa ufunguzi dhidi ya Tanzania 'Taifa Stars', ambayo yenyewe jana iliadhibiwa kwa mabao 2-0 katika mchezo wa kusaka mshindi wa tano.
Stars iliyokuwa kundi A ikiwa na timu za Uganda, Burundi na wenyeji Misri.
 
CHANETA kuwapiga msasa makocha


na Samia Mussa


amka2.gif
CHAMA cha Netiboli Tanzania (CHANETA), kinatarajiwa kuwa na semina ya kuwapiga msasa makocha wote wa daraja la pili, inayotarajia kuanza Februari 3-13 mkoani Morogoro.
Kwa mujibu wa Kaimu Katibu Mkuu wa CHANETA, Rose Mkisi, semina hiyo itahusisha makocha waliopitia mafunzo ya daraja la kwanza kwa lengo la kuwanoa ili kuleta mapinduzi kwa mchezo wa netiboli.
"Tumeamua kuandaa semina ili kuwanoa makocha ambao ndio chachu ya kusaka vipaji vya wachezaji wa netiboli ili tulete mapinduzi ya mchezo huo," alisema Mkisi.
Alisema semina hiyo itakuwa na ada ya ushiriki ambapo kila mshiriki atatakiwa kutoa sh 40,000 atakayolipia kwenye akaunti ya NMB 01J 20005551500.
Mkisi alisisitiza kuwa kocha anayetaka kushiriki mafunzo hayo ahakikishe anathibitisha mapema ushiriki wake ili chama kiweze kujiandaa kwa mambo mbalimbali ya kuhakikisha semina hiyo inafanyika.
Aidha alitoa wito kwa makocha kujitokeza kwa wingi kupata mafunzo hayo ili kuhakikisha wanapata mafunzo yatakayosaidia kuibua vipaji vya mchezo huo sehemu mbalimbali hapa nchini.



h.sep3.gif
 
Kagera Sugar yaiwahi Ruvu Shooting


na Ruhazi Ruhazi


amka2.gif
TIMU ya soka ya Kagera Sugar ya Bukoba, mkoani Kagera, iliondoka Tanga jana na kutua mjini Morogoro, kupiga kambi ikisubiri pambano lao na Ruvu Shooting Jumatano ijayo katika Uwanja wa Jamhuri Morogoro.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu jana akiwa mjini Morogoro, kocha msaidizi wa timu hiyo Mrage Kabange alisema wachezaji wote wako katika hali nzuri.
Alisema wanatarajia kuendeleza wimbi la ushindi waliloanza nalo katika mechi ya kwanza ya mzunguko wa pili walipoizabua Azam FC kwa mabao 2-0 wakiwa ugenini jijini Tanga.
Kocha huyo alisema wanafahamu kuwa mchezo huo utakuwa mgumu, lakini vijana wameapa kufanya jihadi uwanjani ili kuondoka na pointi zote tatu.
"Ndugu yangu tunashukuru kwamba hivi ninavyoongea na wewe tumeshafika Morogoro tunasubiri mechi yetu na Ruvu Shooting hapo Jumatato tukiwa na matumaini makubwa ya ushindi," alisema.
Aliwataka wakazi na wenyeji wa Kagera kwa ujumla wao kuiombea dua timu yao iweze kuendeleza furaha ya ushindi ili mwisho mwa msimu timu iweze kupata moja ya nafasi mbili za uwakilishi wa nchi kimataifa.
 
Pascal Ndomba kuzipiga Jumamosi


na Ruhazi Ruhazi


amka2.gif
BINGWA wa masumbwi wa Afrika Mashariki, uzani wa Super Middle, Pascal Ndomba ‘Kimondo' wa Kyela, anatarajiwa kupanda ulingoni Januari 22 kuzipiga na Mbwana Ally wa Dar es Salaam.
Akizungumza na mwandishi wa habari hizi jijini Dar es Salaam jana, mratibu wa pambano hilo Omari Yazidu alisema pambano litafanyika kwenye ukumbi wa Chuga, ulioko Kasumulu mpakani mwa Tanzania na Zambia.
Alisema pambano hilo lisilo la ubingwa la raundi nane na litatanguliwa na mapambano kadhaa yakiwahusisha mabondia kutoka hapo mpakani, Mbeya na Dar es Salaam.
Yazidu alisema katika kuhamasisha ngumi kwa wanawake nchini, wamepanga moja ya mapambano ya utangulizi liwakutanishe Fatuma Yazidu na Hamisa Willy ambalo litakuwa la raundi nne uzani wa Fly.
Mratibu huyo aliwashukuru Kampuni ya usafirishaji ya SABCO kwa kukubali kudhamini usafiri wa kutoka Dar es Salaam kwenda Kyela na akawataka wadau wengine kufuata nyayo zake.
 
Viongozi Yanga aibu hii ya nini?

ban_tahariri.jpg

amka2.gif
TIMU ya soka ya Yanga, jana ilikuwa icheze mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya mabingwa watetezi wa Zambia, ZESCO United katika Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.
Kwa upande wa Yanga, ni mechi muhimu kwake kutokana na kukabiliwa na raundi ya pili ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara iliyoanza mwishoni mwa wiki na mtihani wa michuano ya kimataifa.
Kama ilivyo kwa mtani wake Simba itakayoshiriki ligi ya Mabingwa Afrika, Yanga inakabiliwa na michuano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (Caf), kampeni za michuano yote ikianza kati ya Januari 28 na 30.
Yanga itaanzia kampeni hiyo kwa kuikaribisha Dedebit ya Ethiopia kabla ya kuifuata mjini Addis Ababa, wiki mbili baadaye ambapo mshindi wa jumla, atakutana na Haras El Hadoud ya Misri.
Kwa upande wa Simba, wao wataanzia kampeni nchini Comoro dhidi ya Elan Club ya mjini Mitsoudje kabla ya kuwakaribisha Wacomoro hao nchini wiki mbili baadaye.
Kama Simba watawang'oa Wacomoro hao, watakutana na timu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo ambao ni mabingwa mara mbili mfululizo wa michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kwa mantiki hiyo, mechi za kirafiki za kimataifa kwa timu za Simba na Yanga, ni zenye umuhimu mkubwa kwa maana ya kuwajengea wachezaji uwezo na uzoefu zaidi katika mechi za kimataifa.
Kwa kulitambua hilo, ndiyo maana awali ilipiga marufuku mechi za kirafiki kutokana na kuanza kwa raundi ya pili ya Ligi Kuu, lakini kwa umuhimu wa mechi za kirafiki hasa kwa Simba na Yanga kwa kipindi hiki, wakatoa baraka timu hizo kucheza na ZESCO United.
Kwa manufaa ya wawakilishi wetu katika michuano ya kimataifa na soka ya Tanzania kwa ujumla wake, TFF ikaridhia kuahirisha mechi za kwanza za raundi ya pili ya Ligi Kuu kwa Simba na Yanga.
Juzi, Simba ilicheza na Wazambia hao na kufungwa mabao 2-1, hivyo jana ilikuwa zamu ya Yanga kucheza na ZESCO United kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam.
Kwetu Tanzania Daima, tunaandika maoni haya kuonyesha kusikitishwa kwetu na hatua ya Yanga kukacha mechi hiyo ya kirafiki kwa madai ya kikosi chake kutokamilika.
Tunasikitishwa na hilo kwa sababu, sio kitendo hicho kimeutia aibu uongozi wa klabu hiyo tu, pia kinaashiria kuwepo kwa matatizo mengi katika klabu hiyo kuanzia benchi la ufundi hadi uongozi kwa ujumla.
Katika hali ya kawaida, haingii akilini kuelezwa Yanga imeshindwa kucheza na Zesco jana kwa sababu ya kukabiliwa na majeruhi na pengo la wachezaji watano waliopo kwenye kikosi cha timu ya taifa nchini Misri.
Hoja hii inakosa nguvu kwa sababu, kama si kucheza na Wazambia, Yanga jana ilikuwa icheze mechi ya Ligi Kuu dhidi ya Mtibwa Sugar.
Katika hali ya kawaida, kama kweli hoja ya Yanga ni majeruhi, tusema wasingecheza na Mtibwa Sugar hiyo jana hivyo pointi kwenda kwa wapinzani wao kwa kisingizio cha majeruhi.
Tanzania Daima tunakwenda mbali zaidi na kujiuliza, kweli wachezaji wa Yanga ukiondoa walipo Stars, hawana uwezo hata wa cheza mechi ya kirafiki dhidi ya ZESCO United?
Tunapotafakari aibu hii kwa Yanga, moja ya klabu kongwe nchini, tunafika mahali tunahoji umakini wa viongozi wa benchi la ufundi na viongozi wa Yanga kwa ujumla kwani kulikuwa hakuna sababu ya kuhofia mechi hiyo ya kirafiki.
Yawezekana kweli kikosi kina majeruhi kadhaa, lakini pia tujiulize hivi Yanga imesajili wachezaji wangapi?
Ni kweli Yanga imekosa wachezaji wa kucheza mechi ya kirafiki au kuna tatizo kubwa zaidi limejificha nyuma ya mpango huu?
Tunamaliza maoni haya huku tukisisitiza kuwa, tumesikitishwa na hatua ya Yanga kutocheza mechi ya kirafiki dhidi ya ZESCO Utd kwa sababu ilikuwa na umuhimu mkubwa na ndiyo maana hata mechi za Ligi Kuu ziliahirishwa.
Viongozi wa Yanga kwa ujumla wake, wafike mahala wabadilike, woga wa mechi hauwezi kuisadia timu hiyo kwani mechi za kirafiki ni kipimo tu, pia kufungwa ni sehemu yamchezo na kujifunza.
 
Serikali isaidie Kickboxing
ban.mtazamo.jpg

Andrew Chale

amka2.gif
MCHEZO wa Kickboxing ni moja ya michezo yenye changamoto nyingi ambazo zikifikiwa malengo yaliyokusudiwa yataleta maendeleo kwa wapambanaji na wawakilishi wetu hapa nchini.
Bila shaka wengi mtakubaliana na mimi juu ya hili kwa serikali kujitokeza sasa na kuweka changamoto kwa kuinua mchezo huu ambao tayari unazidi kukua kwa kasi hasa baada ya wadau kujitahidi kuuendeleza kwa kutumia vyanzo vyao ikiwemo vya mapato na utaalam.
Mara zote wadau wamekuwa wakijitokeza kuchangia michezo mingine huku wakisahau kuchangia mchezo huu wa Kickboxing ambao utaliingizia heshima taifa iwapo utaendelezwa zaidi.
Sote tunafahamu wapo wataalam wa mchezo huu mmojawapo ni bingwa wa mabara Japhet Kaseba kwa kuwa mstari wa mbele kwa kufanikisha maendeleo yake hapa nchini.
Tanzaniaina vijana wengi ambao wana vipaji vya michezo mbalimbali ikiwemo Kickboxing lakini wameshindwa kujitokeza kuvionyesha na vikajulikana zaidi lakini vinaishia ukingoni, hivyo ni jukumu la idara husika za serikali kuchukua hatua za haraka kunusuru hilo.
Hivi karibuni mmoja wa wadau wa michezo hapa nchini alisema kuwa kiwango cha ukuaji wa michezo hapa nchini ni cha mashaka kwani licha ya wanamichezo kutumia akili na maarifa yao bado wanakosa msaada wa kuendelezwa.
Kwa mtazamo wangu nadhani muda sasa umefika kwa serikali kuonyesha nia ya dhati ili kukuza vipaji vya Watanzania katika mchezo wa kickboxing, ikiwa ni pamoja na kuwa na timu maalum ya taifa kwa upande wa Kickboxing sambamba na kupatiwa mkufunzi wa kigeni kama ilivyo michezo mingine.
Hadi sasa Tanzania bado tunasuasua hasa katika michezo tunayoiwakilisha nchi ikiwemo Olimpiki na Jumuiya ya Madola, ambapo serikali kupitia idara zake mara zote imekuwa ikijitambua kuwa inaenda kushiriki kwa nguvu moja na kurudi na ushindi, lakini kinyume chake inarudi mikono mitupu.
Kwa mtazamo wangu wadau mbalimbali akiwemo mbunge wa jimbo la Kinondoni, Idd Azzan, kwa kutambua umuhimu wa michezo amejitokeza kuuinua kwa nguvu zote ili kuleta changamoto kama ilivyo kwa michezo mingine.
Bila shaka serikali ina changamoto kubwa kufanikisha hilo hasa kwa kupanga mikakati endelevu ambayo itainua michezo yote ukiwemo huu.
Mikakati hiyo ni pamoja na kuandaa taratibu za kufundisha makocha wa hapa Tanzania na kuwaandaa wataalam ili kuleta changamoto ili kuwa na wapiganaji wa kutumainiwa wa kickboxing hapa nchini.
Hivyo basi, kwa mtazamo huu msisitizo na mikakati zaidi kwa kuhakikisha tunaona mchezo huu ukikua kupitia wadau ambao ndio tegemeo la maendeleo ya michezo.
Ni hakika kama Tanzania tutaendeleza mchezo huu tutaongeza heshima kubwa sambamba na kuongeza ubora ambao utafanya nchi itambulike zaidi kama ilivyo kwa mataifa mengine duniani kote.
Bila shaka serikali huu ndio wakati wake kushirikiana na wadau wa mchezo huu sambamba na Japhet Kaseba ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kuinua mchezo huu hapa nchini; ni dhahiri kama itaungana naye basi mchezo huu utafika mbali na kujiongezea viwango vya kimataifa.
 
Kumbe wanaoongoza soka ndio wanaoua soka
ban.blank.jpg

Mwandishi wetu

amka2.gif
MAKALA yangu ya wiki iliyopita nilizungumzia kuhusu wadau wa soka la Tanzania kuwa sasa wamewachoka makocha wazawa na makala ile baada ya kushuhudia mpambano mkali katika kipindi cha ITV kiitwacho Spoti Kizaazaa, kipindi ambacho kiliwashirikisha wadau mbali mbali na asilimia zaidi ya 80 waliokuwepo ukumbini hapo walionekana kuwaponda makocha wazawa; waliwashambulia kuwa hawana elimu ya kutosha, wanawagawa wachezaji, wanapangiwa listi ya kucheza na viongozi wao, hawajiamini, hawajui kuongea Kiingereza ingawa wanaowafundisha ni Waswahili na mambo mengi tu kwa wataalam hao.
Baada ya makala ile kutoka nilipata simu nyingi na sms nyingi kutoka kwa watu mbalimbali na karibu zote zilionyesha kutupa lawama kwa viongozi wa soka letu na kamwe si kwa makocha, wadau ambao wengi wao waliomba nisiwataje kwa majina yao kwa sababu zao binafsi. Mmoja alinieleza, "Mzazi inasikitisha mno tena sana pale viongozi na hasa wa hizi klabu zetu kubwa ambazo ni kioo chetu, wanatumia fedha nyingi kusajili kwa maana ya kununua wachezaji toka nje ya nchi, kuajiri makocha toka nje ya nchi na wanawalipa fedha nyingi mara 10 zaidi ya msaidizi wake ambaye ni mzawa, wanatumia fedha nyingi kwa kuiandaa timu ikiwa ni pamoja na kuiweka timu katika kambi nzuri na kula vizuri, lakini ajabu mwisho wa siku wanahakikisha wanatafuta ushindi kwa njia za haramu na kutumia mapesa mengi kuwashinda Mtibwa, JKT, Kagera hata na Toto nje ya uwanja; ni kichekesho kweli kweli!!!!!"
Hapo mdau huyo anajiuliza kuna sababu gani ya kuajiri kocha kutoka nje ya nchi na kumtengenezea CV nzuri na kumfanya aonekane bonge la kocha kumbe wapi na kumfanya mzawa aonekane hana thamani.
Mdau mwingine alisema kama kweli hawa makocha wageni wana uwezo wa kutisha mbona wanapocheza mechi za kirafiki na timu hizi wenyewe wanaziita ndogo ndogo kama JKT wanafungwa, mechi ambazo viongozi hao wanaoongoza soka hawatumii nguvu za ziada za nje ya uwanja, mbona mashindano ya kimataifa hatufiki mbali ukiondoa ile ya kocha James Siang'a ambaye ni jirani yetu, Kenya wametufikisha wapi?!!!!
Naye mzee Komanya wa Musoma akiongea kwa uchungu zaidi iliniambia: "Hivi kweli pale TFF kuna takwimu za kuonyesha tumetoka wapi, tuko wapi na tunakwenda wapi?
Hivi ni lini TFF na CECAFA watakaa chini na kuamua kuanzisha ligi ya klabu ili kuifanya ligi yetu isiwe na ‘big 2' iwe na ‘big 4' kama Ligi ya England ambapo timu nne za juu zote zinapigana kuwakilisha nchi na zingine za katikati nazo zinashiriki katika UEFA ndogo."
Anashangaa mzee yule wa Musoma hivi kweli inaingia akilini mchezaji wa Simba analipwa sh mil. moja, anakabana na mchezaji wa Toto wote wako ligi moja mshahara wake sh 40,000 halafu wadau tunapiga kelele makocha wazawa ndio wanaua soka, hivi kweli tuko duniani kweli au tunadanganyana.
Mdau mwingine aliyenitumia ujumbe wa sms ni Phillbert Rwezaula anasema, "Bwana Kenny mi' ni mmoja wa waliokuwa wanatazama kile kipindi cha Spoti Kizaazaa lakini baadaye nilizima nilipoona watu mpaka mate yanawatoka walipokuwa wanatoa hoja zisizo na mashiko kuhusu makocha wazawa, Watanzania wengi wanajua kutuhumu, hivi hao kina Kaburu wameshatoa sh ngapi kwenda kumsomesha kocha, kila siku tunasikia kaenda kuchukua mchezaji mara Uganda mara Kenya mara Burundi kwa gharama kubwa wakati wangewekeza hizo pesa kwa makocha wazawa kama Amri Saidi tungepata wachezaji wazuri hapa hapa nyumbani.
"Sekilojo Chambua aliahidiwa na Yanga wangemsomesha je wamemsomesha? Kiko wapi?
Tatizo si makocha wazawa tatizo ni viongozi wa mpira hawajasomea soka labda nao sasa tupate wa kigeni.
"Hakuna viongozi wanaoweza kusimamia soka Tanzania ikakua hata wakitokea hawawezi kukubalika, unajua kaka watu wanachanganya mambo kuwa soka linaweza kuongozwa kama ukijua sana kuongea mambo ya soka basi unafaa kuongoza, hii ni field inahitaji uelewa zaidi kuliko kuongea sana au kucheza mpira kwa upeo mkubwa, ili kujua kinachohitajika!
"Makocha wa kigeni wangapi wameleta kombe zaidi ya huyu wa sasa tena baada ya kuwekeza nguvu nyingi, kaka Mwaisabula usikate tamaa mabadiliko yatakuja tutaachana na watu wanaojiita wa mpira tutapata viongozi wenye uelewa."
Tatizo la soka la nchi yetu si makocha wazawa au wa kigeni ni viongozi wa soka ambao wenyewe muda wote wanafikiria ushindi wao utapatikana nje ya uwanja yaani wenyewe wanasema "Football Fitna" hawana mipango endelevu ambayo itamsaidia kocha kuweka utaratibu wake mzuri, viongozi wa leo hawafikirii kuwa na eneo lao zuri na kubwa kwa ajili ya mazoezi na mechi, ili kumfanya kocha awe ana "program" ya kuwa na timu zaidi ya tatu katika eneo lake kama zilivyotimu za wenzetu, sisi tunasubiri mizengwe ya nje ya uwanja na ikishindikana basi jumba bovu linamwangukia kocha tena akiwa mzawa ndio balaa zaidi.
Matatizo ya viongozi wa soka na hasa klabu hawaangalii mbali; wanaangalia kushindana sisi kwa sisi tu ndio maana tukitoka nje hatufiki robo fainali shukuru Mungu, wadau sasa tunafika mahali angalau sasa tunaanza kuwakumbuka kina Tabu Mangara, Kondo Kipwata na David Jimmy Ngonya.
Wadau wengi walikiri kuwa soka letu linaporomoshwa na walioomba dhamana ya kuongoza soka, kama hivyo ndivyo imefika wakati kama kweli tunataka kuendeleza soka ndani ya ardhi yetu ni kutoyafumbia macho maovu ya viongozi hao na kuwasema hadharani kuwa sasa kununua mechi basi, na sisi tunaosimamia sheria kama kweli tunanunuliwa ili kupindisha sheria tuseme basi, tuliache soka lenyewe liamue mshindi ndani ya dakika 90 kama ilivyo kwa wenzetu walioendelea, zaidi ya hapo tutaendelea kuwaona kina TP mazembe wakitawala soka la Afrika na sisi tukibaki kupigania majungu kila kukicha.
Binafsi sina matatizo na ujio wa makocha wa kigeni ndani ya nchi yetu kwangu mimi ni moja ya changamoto sana na yapo mambo ambayo nadhani tunajifunza kwao na hata umma kwa ujumla, mfano ni hili sakata la Fred Minziro na Papic hapo ndipo utakapoona upeo wa viongozi wetu wa soka ulivyo; mimi sitaki niingie ndani zaidi lakini ni kichekesho!!!! Akili yangu inakataa kukubali!!!!! Nabaki nimeduwaa kesho utasikia wazawa hawafai, tatizo langu ni makocha wazawa kutothaminiwa kabisa na kuendelea kuwa Deiwaka hata katika timu za taifa.
Makala yangu ijayo nitamtafuta mmoja wa viongozi waliopita katika klabu hizi kongwe aliyekuwa na msimamo wa kutisha ambaye alikuwa hakubali suala lolote linalohusiana na kushinda nje ya uwanja na ambaye mara zote alichaguliwa bila kufanya kampeni alifuatwa tu na wanachama na kuambiwa njoo mzee uchukue nafasi yako. Baba wa Taifa anasema kuongoza watu ni mzigo mtu safi hakimbilii Ikulu kwa kuwa anajua ni mzigo lakini ukimwona anakimbilia tena kwa kuhonga huyo ni wa kuogopwa kama……..viongozi wa leo wanataka uongozi ndio wametufikisha hapa.



h.sep3.gif

Mwandishi wa makala hii ni mfanyakazi wa mamlaka ya usimamizi bandari kitengo cha uhandisi DSM pia ni kocha anapatikana 0713243711 au Email kennymwaisabula@yahoo.com
 
TFF ijifunze kwa Kaseja
ban.blank.jpg

Haji Kalili

amka2.gif
Hivi karibuni Kamati ya Rufaa ya Shirikisho la Soka Tanzania Bara (TFF) inayoongozwa na aliyekuwa Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana ilimuachia huru golikipa wa mabingwa watetezi nchini, klabu ya Simba ya jijini kutokana na utata uliokuwa umegubika adhabu iliyotokana na sababu kwamba, Juma Kaseja hakupeana mikono na mahasimu wao, Yanga katika mchezo wao uliochezwa katika uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Baada ya adhabu ile Simba iliwasilisha rufaa TFF kupinga adhabu aliyopewa kipa huyo tegemeo wa timu hiyo.
Kaseja alifungiwa na Kamati ya Mashindano kutocheza michezo mitatu na kulipa faini ya sh 500,000 kwa kosa la kugoma kupeana mikono na wachezaji wa Yanga katika mechi ya Ligi Kuu iliyopigwa Oktoba 16 mwaka huu katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo Simba ilitandikwa bao 1-0.
Awali TFF kupitia Kaimu Katibu Mkuu wake, Sunday Kayuni ilitangaza kumfungia Kaseja kwa kosa la kugoma kumpa mkono aliyekuwa mgeni rasmi katika mechi hiyo Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro, lakini katika barua ya kufungiwa kwa kipa huyo kwenda kwa Simba wakalichakachua kosa hilo.
Hali hiyo ilizua malalamiko kutoka kwa wadau mbalimbali na kuona TFF inafanya shughuli zake kwa ubabaishaji kutokana na kujikanganya katika sakata hilo kutokana na ushahidi wa picha mbalimbali zilizoonyeshwa na vyombo vya habari vikimuonyesha Kaseja akipeana mkono na Kandoro huku baadhi ya viongozi wa TFF wakimtetea kipa huyo aliyeibuka mchezaji bora katika michuano ya Chalenji iliyomalizika mwishoni mwa mwaka jana kwa kikosi chake kutwaa ubingwa.
Ipo haja na kila sababu kwa TFF kujifunza kutoka Mashirikisho mengine ya Soka ya Kimataifa kama Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Shirikisho la Soka la Afrika (CAF) na Shirikisho la Soka la Uingereza.
Hakuna ulazima wa kila tukio linalotokea uwanjani litatuliwe kwa adhabu na kujenga mazingira yanayoonyesha kuna uonevu wa dhahiri kwa wachezaji fulani.
Yapo matukio ambayo ni mifano hai ya kuonyesha hakukuwa na ulazima wa kutoa adhabu kama ilivyotokea hivi karibuni na kuzua tafrani kubwa na kuonyesha ubabaishaji ndani ya TFF.
Katika mechi ya marudiano ya hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya waliokuwa mabingwa watetezi, TP Mazembe ya Jamhuri ya Demokrasi ya Congo na Esperance ya Tunisia ambapo Mazembe walifanikiwa kutetea taji lao kama walivyofanya miaka 42 iliyopita walipoutwaa ubingwa mara mbili mfululizo,1967 na 1968.
Fainali hiyo iliyopigwa kwenye uwanja wenye uwezo wa kubeba zaidi ya watu 65,000, mjini Rades, nje kidogo ya jiji la Tunis, wachezaji wa Esperance wakati wakikabidhiwa zawadi zao ikiwa ni pamoja na beji na kushikana mikono na wageni waalikwa walionyesha vitendo ambavyo kama TFF ingekuwepo kule basi adhabu kali ingewaangukia.
Mgeni rasmi alikuwa rais wa CAF, Issa Hayatou, baadhi ya wachezaji wa Esperance baada ya kuvalishwa beji walizivua, wengine walipokea mikononi badala ya kuvalishwa na wengine pamoja na viongozi wao waliamua kushikana mikono ili kukwepa kupeana mikono na wageni waalikwa kabisa tukio ambalo lilionekana kumkera dhahiri Hayatou.
Katika mashindano ya Kombe la Dunia yaliyomalizika hivi karibuni kwa mara ya kwanza barani Afrika, nchini Afrika Kusini, aliyekuwa kocha wa Brazil Carlos Dunga alitoka kwa hasira bila kupeana mkono na mwenzake wa timu ya taifa ya Uholanzi Bert Van Marwijk baada ya kufungwa.
FIFA kwa kitendo kile hawakuchukua hatua yoyote, walikaa kimya.
John Terry wa Chelsea na Wayne Bridge wa Manchester City waliingia katika mgogoro mkubwa wa kuchukuliana mpenzi na katika mechi baina ya timu zao wakati wakipeana mikono Wayne Bridge kwa makusudi kabisa aliukwepa mkono wa Terry kwa sababu ya tofauti zao, je, FA ya England iliwachukulia hatua gani?
Naye Kaseja akumbuke kuwa nidhamu ndiyo kitu cha kwanza katika maendeleo ya soka, kupitia adhabu ambayo iilitupiliwa mbali na kamati ya rufaa aendelee kuwa na nidhamu ingawa aliyekuwa Kocha wa Taifa Stars, Mbrazil Marcio Maximo aliwahi kumuondoa katika kikosi cha timu hiyo kwa tuhuma za utovu wa nidhamu.
Hili lilimpunguzia Maximo uungwaji mkono kutoka kwa baadhi ya wadau wa soka nchini kwani uthibitisho wake ulikuwa mgumu na kwa bahati mbaya hakuwa tayari kuweka bayana madudu ya Kaseja.
Kusafishwa kwa Kaseja na Kamati ya Rufaa ya TFF hakumaanishi kwamba ni msafi, ana matatizo yake na anapaswa kujirudi na kujirekebisha pale penye makosa. Ni wakati wake wa kuuthibitishia umma kuwa adhabu ile haikuwa sahihi.
Hivi lipi ni kosa kubwa kati ya kumsimamisha rais na viongozi wengine wa soka wakisubiri wimbo wa Taifa upigwe na usipigwe au kutopeana mikono baina ya wachezaji? Hivi madudu haya TFF yataisha lini?
Kwanini TFF isijifunze kutoka mashirikisho mengine ya soka?
 
Ngeta mbona unaanza kutuangusha TFF?
ban.nachonga.jpg

Tullo Chambo

amka2.gif
ASALAAM Aleykhum wapenzi na wadau wa Uwanja wa Kuchonga, amani ya bwana iwe nanyi. Bila shaka mu wazima wa afya na mnaendelea na majukumu ya ujenzi wa Taifa, kwa wale ambao hali zao si shwari tunawaombea nafuu.
Ni Jumatatu nyingine tunakutana Uwanjani, lengo likiwa kujadili na kupeana changamoto za kispoti, dhima kuu ikiwa kuleta ufanisi katika sekta hii nyeti katika jamii, michezo.
Kama ni mdau na shabiki, utakumbuka mada iliyowekwa uwanjani takribani wiki tatu zilizopita, ambayo ilikuwa na changamoto ya kuwakaribisha watendaji wapya ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).
Watendaji hao ni wanahabari, Katibu Mkuu Angetile Osiah ‘Ngeta', Ofisa Habari, Boniface Wambura na Ofisa Masoko na Mipango, Jimmy Kabwe. Wadau wa Uwanja tulinena hivi: "TFF Kweli mchawi mpe mwana akulelee."
Katika hilo tulijadili jinsi shirikisho hilo lilivyowapata watendaji hao wapya na hasa kulipongeza kuwa, pengine labda liliangalia jinsi ya kutatua baadhi ya matatizo yaliyoko, ambako kimsingi kutokana na fani ya wahusika tulijawa na imani ya kuwa, kweli upele umepata mkunaji.
Nikiwa bado na imani na watendaji hao, nilibaki nikisubiri kuona mwanzo wa watendaji hawa waliopewa dhima muhimu katika kuhakikisha soka la Tanzania linatoka hapa lilipo na kufika kule mamilioni ya Watanzania wanakoota.
Labda baadhi ya watu wanaweza kusema ni mapema mno, lakini hali halisi ndivyo ilivyo, mwanzo wa watendaji hawa unaanza kutia mashaka.
Ilikuwa imani yetu kuwa maneno ni kidogo ingawa wahusika wenyewe fani yao inahusu ‘kuchonga sana', lakini vitendo vingekuwa zaidi.
Lakini wadau wa Uwanja wa Kuchonga, walipatwa na butwaa hivi karibuni ambapo nadhani ulikuwa ni uamuzi wa jopo la wahusika wa hapo TFF makao makuu chini ya mtendaji mkuu, Katibu Mkuu, kuanza na maamuzi ya kinyonga.
Hivi karibuni, wadau wa soka katika kuhakikisha timu zetu zinatuwakilisha vema katika mashindano ya kimataifa yanazozikabili, waliamua kubuni ‘biashara' ya kuzisaidia katika maandalizi yao kwa kuzileta timu kutoka nchi mbalimbali.
Kwanza ililetwa AFC Leopards ya Kenya ambayo ilicheza na Simba na Yanga, kisha ikaletwa taarifa ya kuja kwa Sofapaka na Zesco ya Zambia.
Lakini katika hali ya kushangaza na kushtua, wakati ikiwa dakika za mwisho timu hizo kuwasili hapa nchini, TFF ilitoa taarifa rasmi kwa umma wa Watanzania kuwa kuanzia sasa mechi hizo hazitakiwi na kuwa wadau wanaozileta timu hizo lazima wapate baraka za shirikisho hilo.
TFF ikafika mbali zaidi, ikadai kuwa mechi hizo hazitakiwi hivi sasa kwa kuwa kuanzia Januari 15 ligi kuu mzunguko wa pili itakuwa inaanza mechi hizo haziwezi kuchezwa kwani kalenda yao hairuhusu.
Sijui kama uamuzi huo ulikuwa makini, lakini kwa upande wa pili ulikuwa na athari kubwa kwa pande zote, wadau waliozileta timu hizo na wawakilishi yaani klabu za Simba na Yanga.
Wakati wadau wakiamini mechi hizo hazipo, dakika za majeruhi TFF ikaibuka na kusahau ile kauli yake ya kusisitiza maamuzi yake kuwa kuanzia Januari 15 hakuna mechi za kirafiki hasa timu kutoka nje ya nchi, ikageuka na kudai sasa imebariki zichezwe eti kwa madai Chama cha Soka Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA), kimekamilisha mawasiliano nao.
Hakika kwa watu makini, kauli hizo za TFF na kilichokuja kujitokeza ni mwanzo wa udhaifu katika utendaji na maamuzi.
Hiyo inaonyesha wazi kabisa TFF ilikurupuka katika kutoa tamko lake na wala haikufikiria faida na hasara zake.
Kitendo kilichofanywa na wadau kuzileta timu hizo kimsingi si kibaya kabisa, kwani Simba na Yanga haziwezi kuiacha Ligi ya TFF na zikakimbilia mechi hizo za kirafiki, lakini cha kushangaza wahusika hao wa TFF wakakurupuka na kuzipiga stop, inasikitisha na inavunja moyo wadau.
TFF katika hilo mlivuka mipaka, maamuzi ya kucheza au kutocheza mechi hizo kimsingi yako chini ya klabu husika, ambazo zinatambua ratiba zao ikiwamo hiyo Ligi Kuu ya bara, sasa kujengea hoja kalenda ya TFF, hapo mlistaajabisha wadau wa soka.
Hoja ingekuwa wahusika lazima wapate baraka za TFF tu, mngeeleweka na wala miguno wala kelele zisingekuwepo.
Katika hili nakumbuka wosia wa Rais wa TFF, Leodegar Tenga, wakati akiwatambulisha wateule hao kwa waandishi wa habari, aliwasihi wachunge kauli zao ambazo zinaweza kuzua utata miongoni mwa wadau wa soka. Lakini hata maji hayakauka, wahusika hao wameanza kuibua sintafahamu. Leo hatutaki, kesho kama kinyonga tunakubali. Inaonyesha hakuna msimamo katika kile kinachoamuliwa TFF.
Hili ni moja tu, je masuala nyeti na yenye utata ambayo yamekuwa yakilikabili shirikisho hilo itakuwaje, si itakuwa migongano na mvurugano katika medani ya soka hapa nchini?
Ni hivi karibuni tu, TFF ilijivua nguo kwa kuibuka na madai ikimtuhumu Kipa wa Simba Juma Kaseja kuwa alimkimbia mgeni rasmi kumpa mkono katika mechi dhidi ya Yanga, kesho yake zikaonyeshwa picha Kaseja akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Abbas Kandoro, keshokutwa yake ikabadili eti hakuwapa mkono wachezaji wa Yanga. Inasikitisha.
Ngeta, Wambura tunawaamini sana katika dhamana mliyopewa hapo TFF, tena hasa katika masuala ya kutoa kauli, lakini katika hili mnaanza kutia wasiwasi au kutuangusha.
Utata huo wa kauli ni atatizo katika umma, hivyo kama alivyowaasa Tenga, zingatieni sana kauli mnazozitoa kwa wadau ili kuepusha msigano au madhara yanayoweza kuibuka kutoka na kauli hizo.
Bila shaka wahusika watalifanyia kazi kwa manufaa ya soka letu. Kila la heri tukutane wiki ijayo.
 
Under 20 kukusanywa wakati wa ligi
ban.blank.jpg

Mwandishi wetu

amka2.gif
NIANZE kwa kulipongeza Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwa kuamua kuzilazimisha timu zote za Ligi kuu ya soka Tanzania Bara kuanzisha timu za vijana chini ya miaka 20.
Baada ya kuona timu zinasuasua kuanzisha timu hizo, TFF ikaamua kuanzisha michuano maalumu kwa vikosi hivyo vya vijana vya timu zote za Ligi Kuu.
Aidha, TFF haikuishia kuanzisha mashindano pekee lakini ikaweza pia kusaka wadhamini ili kuhakikisha michuano hiyo haiwi mzigo na pia kuwahamasisha vijana kucheza kwa kujituma.
Kampuni ya Azam imekuwa ya kwanza kuitikia wito wa TFF wa kudhamini michuano hiyo kupitia maji ya kunywa ya Uhai, hivyo kuyafanya mashindano hayo kuitwa Uhai Cup.
Kwa hili ninawapongeza TFF kwa dhati, kwa sababu moja suala la kuanzisha timu za vijana lilipaswa kuwa sera ya msingi kwa kila klabu sio tu za Ligi Kuu lakini hata zile za mchangani.
Kuwa na timu ya vijana ni kujihakikishia kuendelea kuibua vipaji vya soka au mchezo mwingine wowote ingawa viongozi wengi wa klabu zetu wanaonekana ama hawajui umuhimu wake ama hawana nia ya dhati ya kuziendeleza klabu zao na soka kwa ujumla.
Kabla ya kulazimishwa na TFF kuanzisha timu za vijana karibu klabu zote zimekuwa zikitoa visingizio lukuki kuhalalisha kutoanzisha timu za vijana, kubwa zikilia ukosefu wa fedha.
Kilicho wazi ni kuwa klabu hizi zina fedha za kutosha kuendesha timu za vijana tena sio za chini ya miaka 20 pekee bali hata umri wa chini ya miaka 17 na 14, lakini tatizo ni mipango mibovu.
Viongozi wetu hawataki kujifunza kupitia kwa wenzetu, viongozi wanapowania uongozi wanakuwa na porojo nyingi lakini naona zote zinakuwa za kuombea kura.
Gharama za kuendesha timu za vijana sio kubwa za kupigia kelele kama wao wanavyojaribu kuiaminisha jamii siku zote.
Pia ni ukweli usiopingika kwamba gharama ambazo klabu inaweza kuingia kuwaandaa wachezaji kwa miaka mitatu, zinaweza kurudi iwapo watafanikiwa kumuuza mchezaji mmoja tu kwenye klabu kubwa za barani Ulaya.
Sasa swali tuendelee kulia kutokuwa na fedha huku wenzetu wa Afrika Maghraibi wakiuza wachezaji Ulaya au tukubali gharama ya muda lakini baadaye tunufaishwe na matunda ya kukuza vipaji?
Ni jambo baya kuona au kusikia kwamba eti hadi leo bado baadhi ya timu zinaendelea na mtindo wa kuwakusanya vijana kutoka mitaani kwa nia tu ya kushiriki michuano hiyo ya vijana ya Uhai Cup.
Huu ni upuuzi ambao nadhani TFF inapaswa kuufanyia uchunguzi wa kina na timu zitakazobainika zifutiliwe mbali, kwa sababu inaonekana haziko kwa ajili ya kuendeleza soka letu.
Wadau wa soka kwa ujumla wetu tunapaswa kuwa na sauti moja tunapoamua jambo, wanapojitokeza baadhi yetu wakazungumza na kunena kwa lugha nyingine isiyo ya soka hao sio wenzetu na hatupaswi kuwakumbatia.
Hawa viongozi wa klabu wanaotaka kuendelea kutoa mamilioni ya shilingi kuwanunua wachezaji kutoka nje wanapaswa kutupisha, wawaache wale watakaowaibua na kuwaendeleza vijana wetu kisha kuwaajiri baadhi yao kuzichezea timu zetu na wengine kuwauza nje.
Hatukatai kununua wachezaji kutoka nje lakini wawe wachache na ambao kweli wanastahili kuitwa wachezaji wa kulipwa lakini sio kumsajili mchezaji kwa mamilioni ya shilingi kwa sababu ya kupata asilimia kumi.
Kuna matatizo ya ajira kwa sasa hivi hatujui kuwa tukiwaandaa vijana wetu baadaye tutawaajiri kupitia soka.
Umefika muda wadau wote wa soka tuiunge mkono TFF, kwa hili la kuzilazimisha timu zote za soka nchini kuwa na timu za vijana ambazo zipo kiutendaji na sio kinadharia.
Huu mpango unaoendelea sasa wa viongozi wa Simba, Yanga na klabu nyingine za Ligi Kuu kukimbilia kumwaga mamilioni ya shilingi kila mwaka kwenda kusajili nje, unapaswa kukomeshwa.
Timu zisajili mchezaji kutoka nje pale ambapo zimelazimika kufanya hivyo; kwamba katika kikosi chao cha vijana hakuna mchezaji mwenye uwezo wa kumudu nafasi fulani, vinginevyo kwa staili hii hatufiki.
Nimalizie kwa kuwaomba watu binafsi, taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi, kujitokeza zaidi kudhamini michuano hiyo ya vijana, pamoja na timu zenyewe za vijana.
Naamini tukijitokeza kwa wingi na kuzidhamini, timu hizo na viongozi wa klabu wakaweka mkazo kwenye timu hizo, kwa miaka sita ijayo Tanzania itakuwa nchi ya kupigiwa mfano katika medani soka kote Afrika.
 
Mapinduzi Cup na utetezi dhaifu Yanga
ban.blank.jpg

Mwandishi wetu

amka2.gif
NILIKUWA mbele ya televisheni, usiku ule wa Januari 12, 2011 wakati wa mechi ya fainali ya Kombe la Mapinduzi, kati ya mahasimu wawili, Simba na Yanga, zote za jijini Dar es Salaam, zilipokutana uwanjani, Amaan, Zanzibar.
Kwa kutambua ukubwa wa majina ya timu hizo na wasifu wa makocha wake wa kigeni, nilitaraji kuona moja ya mechi bora kabisa ya msimu, hasa kutokana na ukweli kwamba mechi ile haikuwa na presha kubwa kwa yeyote kati yao, zaidi ya kile kinachosemwa, kulinda heshima.
Haikuwa na presha kwa sababu haikuwa ya Ligi Kuu Tanzania Bara, ambayo mshindi hupata pointi tatu zinazomfanya kupanda juu ya msimamo ili mwisho apate kuwa bingwa.
Simba ikiwa na kocha wake mwenye heshima kubwa pale Msimbazi, Patrick Phiri raia wa Zambia, huku Yanga nayo katika benchi lake la ufundi, likiongozwa na Mserbia, Kostadin Papic.
Kwa shabiki wa soka wa Tanzania, hasa anayefuatilia habari za timu hizo kwenye vyombo vya habari, jinsi wachezaji wake wanavyonadiwa, alitegemea kuona mechi nzuri, kwa maana ya utandazaji wa soka uliotulia, wenye hadhi sawa na timu hizo.
Lakini maskini ya Mungu, kama mtu alikuwa na akili na matarajio hayo, alichokiona siku hiyo ni tofauti kabisa.
Nimeshawahi kushuhudia mechi kadhaa baina ya timu hizi katika miaka ya karibuni na naweza kusema kwa dhati kabisa, mechi ya juzi ilikuwa ni mbovu zaidi kati ya zote nilizoziona.
Mbovu si kwa sababu mwamuzi wa mchezo aliharibu mpira kwa upendeleo, hapana, bado mbovu kwa sababu sikuona soka.
Baadhi ya mashabiki wanasema eti Simba walicheza vizuri, walimiliki mpira na kila aina ya sifa kwa kikosi cha Msimbazi. Sijui labda kwa vile kila mtu anakiamini anachokiona, lakini kwangu, sikuona soka lolote ambalo Simba inaweza kujivunia.
Labda kwa kuwa kati ya timu mbili uwanjani, moja inaweza kuwa afadhali, lakini kuuzungumzia mchezo wenyewe, kwa kweli ulijaa butua butua za kukera.
Kuna mchezaji kwa mfano, Abdulhalim Humud: nimesikia watu wakimsifu kwa kuonyesha kiwango kikubwa siku hiyo, sifa ambayo imetoka kwa kocha wake, Patrick Phiri.
Phiri anaweza kumsifu kwa kuwa alifanya vizuri katika majukumu aliyompatia uwanjani, lakini kwa mimi shabiki wa kawaida, nilichokuwa nikikiona kwake ni matumizi makubwa ya nguvu katika kuucheza mpira na pasi nyingi kutofika zilikokusudiwa.
Haikuwa mechi iliyokutanisha timu kubwa na zinazoiwakilisha nchi kwenye mashindano ya kimataifa. Nadhani mtu angefurahi zaidi kutazama mechi kati ya Mtibwa Sugar na Ruvu Shooting kuliko ile ya majuzi.
Baadhi ya watu, wakiwemo wachezaji wenyewe wanalaumu eti sehemu ya kuchezea.
Unafiki mtupu. Hivi kuna uwanja gani huku bara, ukiondoa viwanja viwili ambavyo ubora wake ni wa hivi karibuni wa Uhuru na Taifa, una sehemu nzuri ya kuchezea kuliko ule wa Amaan?
Sehemu ya kuchezea haiwezi kuwa sababu kubwa ya butua butua ile. Wachezaji wa timu zote mbili walikuwa na hofu ya mchezo. Na moja ya sababu ya hofu iliyowakumba na kuwafanya wasicheze vizuri, bila shaka ilitoka kwa viongozi wao, waliowaahidi fedha nyingi kama wataibuka na ushindi.
Matokeo ya mawazo ya kupata fedha nyingi baada ya mchezo, yaliwafanya ‘kupaniki'. Ushindi wa mabao 2-0 waliopata Simba, unaweza kuwafanya mashabiki wao kujisifu kwa kuwa umeingia katika rekodi, lakini kwa kiwango cha soka, timu zote zilistahili kutoka na sifuri.
Lakini kuna jambo lingine la kushangaza kwa matokeo ya mchezo huo. Kuna mashabiki, bila shaka wa Yanga, wanadai eti kufungwa kwao kulitokana na kukosekana kwa wachezaji wao walio na timu ya taifa, Taifa Stars, iliyo ‘matembezini' Misri.
Kwamba kama angekuwepo Nadir Haroub ‘Cannavaro', Shadrack Nsajigwa, Stephano Mwasika, Jerry Tegete, Nurdin Bakari, Abdi Kassim na Athuman Idd, basi mnyama asingetoka.
Inaweza kuwa na chembe za ukweli kutokana na kuwa hao ndiyo wachezaji wa kikosi cha kwanza Yanga, lakini unajiuliza, kwani na Simba nayo haikuwa na wachezaji katika timu ya taifa?
Simba pia iliwakosa Juma Kaseja, Juma Nyoso, Kelvin Yondani, Ali Ahmed ‘Shiboli'
na Rashid Gumbo. Licha ya hao, pia Waganda wake wawili, mshambuliaji Emanuel Okwi na beki Joseph Owino nao hawakucheza mechi hiyo.
Utetezi wa mashabiki wa Yanga juu ya wachezaji wao waliopo Stars unakosa nguvu na kwa kiasi kikubwa, unawavunja nguvu sana wachezaji waliobaki nyumbani.
Suala la kutokuwepo kwa wachezaji hao haliwezi kuwa tatizo la Yanga kucheza soka bovu na mbaya zaidi, kufungwa na Simba. Wachezaji wale wangeweza kuwemo kikosini na bado Simba wangeweza kushinda.
Somo moja ambalo uongozi wa Yanga unapaswa kujifunza kutokana na matokeo ya mchezo huo, ni kutulia katika usajili. Iache pupa. Yanga ambayo leo inajivunia ufadhili mkubwa wa fedha zinazotolewa bila ‘kuhoji' eti leo inalia si Yanga iliyocheza na Simba, eti ilikuwa timu B, inasikitisha kwa tathimini za kiufundi kocha kulilia wachezaji watao kutokuwepo huku pia ukiwa na nyota zaidi ya hao ‘Professionals' lakini bado kocha analia kupoteza mechi kisa baadhi ya wachezaji wako timu ya Taifa.
Inapaswa kufanya usajili ambao kila mchezaji anakuwa na sifa za kuchezea kikosi cha kwanza na anakuwa tayari kufanya hivyo wakati wowote.
Hoja za baadhi ya wachezaji kutokuwepo kikosini hasina mshiko, kwani ndio maana Papic aliwasajili akina Mwape, Boakye na hata Kipa Mzungu Ivan Knetevic na Mghana, kwani hao ni bora kuliko vipaji vilivyoko hapa nchini, ingekuwa tofauti hakuna haja ya kupoteza fedha kwenda kugharimia mchezaji Bara la Ulaya wakati ukijua anakuja kuwa mchezaji wa akiba.
 
Wakongo wametuona, sisi bado hatujioni
ban.blank.jpg

Ojuku Abraham

amka2.gif
JUZI wakati wa mechi ya mahasimu wa jadi kule Zanzibar, nilikuwa namsikiliza mchezaji wa zamani wa Simba na Yanga, Mwanamtwa Kihwelu ‘Diblo', akifanya tathmini yake kupitia kituo cha televisheni cha taifa wakati wa mapumziko.
Niliwahi kumuona akicheza enzi zake, kwa hiyo kile alichokuwa akikizungumza kuhusu mchezo ule, nilijua kinatoka kwa mtu anayezifahamu vema timu zote mbili, kwani aliwahi kuzichezea.
Nakumbuka pia aina yake ya uchezaji. Si tu alikuwa mmoja kati ya wachezaji wenye kipaji na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, bali pia aliweza kucheza kwa nguvu, kujituma na ‘hasira' ya ushindi.
Ungefurahi kuona kazi yake akicheza kama beki wa kulia, ungesuuzika kumuona akiwajibika katikati ya dimba akiwa kama kiungo mkabaji au mshambuliaji na usingesita kufurahishwa na jinsi alivyotekeleza majukumu yake akiwa mshambuliaji.
Mtwa alicheza namba nyingi kwa ufasaha, isipokuwa mlinda mlango. Unaweza kumfananisha na marehemu Said Mwamba ‘Kizota' linapokuja suala la kumudu kucheza namba nyingi uwanjani kwa ufasaha!
Uchezaji wake wa kujituma uwanjani ulimfanya kuwa lulu kwa kila timu aliyoichezea kiasi kwamba hadi wakati anaacha mpira, bado alikuwa katika kiwango bora.
Lakini pengine kwa sababu nilimuona Mtwa akizungumza katika runinga, lakini walikuwepo wachezaji wengine enzi zao, waliocheza soka kwa kujituma uwanjani.
Uliona wazi jinsi gani walivyokuwa na kiu ya ushindi na kwa kiasi kipi walichukia kufungwa. ‘Jihad' yao uwanjani ilitoa mchango mkubwa wa timu walizochezea. Chukulia kwa mfano uchezaji wa kujituma wa washambuliaji wa zamani wa Majimaji ya Songea na Simba, Bakari Idd na Madaraka Selemani.
Muda wote wa mchezo wanahaha uwanja mzima kuhakikisha wanapata nafasi ya kufunga na hata kama sio wao ndiyo wanaotumbukiza mpira wavuni, basi watakuwa na mchango kwa wenzao watakaofunga.
Walikuwepo pia wachezaji wengine wengi, kwa nyakati tofauti, ambao mchezo wao ulionekana wazi ni wa kujituma uwanjani.
Ni kutokana na kujituma kwao, ndiyo maana hata timu za wakati ule, zilikuwa na ushindani wa kweli kweli. Ili kupata namba katika timu, ilihitaji kujituma kweli kweli mazoezini.
Hali ni tofauti siku hizi. Wachezaji wetu wamekuwa legelege mno kiasi kwamba wengine hata kusukumwa hawapendi. Unamuona dhahiri kwamba amechukia baada ya kusukumwa.
Kauli ya hivi majuzi kutoka kwa wachezaji wa timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC), waliyoitoa huko Misri katika michuano inayoendelea ya Kombe la Mto Nile imenikuna mno.
Wakongo hao wanasema wachezaji wa Tanzania wana utoto mwingi, wanacheza bila malengo, hawana uchungu na hawajitumi. Wanashangaa unaweza kufungwa bao tano halafu mchezaji wenu hata mmoja hajapewa kadi ya njano.
Kwa tafsiri nyepesi, kauli ya Wakongo inamaanisha kwamba baada ya kufungwa bao zile nyingi, angalau wachezaji wa Tanzania wangeonyesha uchungu na hasira za kufungwa. Kwa maana hiyo, angalau wangepaniki kwa hamaki, kiasi kwamba angalau basi wangejibishana na mwamuzi au hata kumkwatua adui.
Lakini wachezaji wetu walionekana kufurahia tu na kuona jambo la kawaida kufungwa idadi ile kubwa ya mabao. Hawakuonyesha kuchukizwa na kipigo kile.
Wanasoka wetu hawana muda wa kujituma uwanjani kwa sababu tayari ni mastaa.
Kwao, kuchezea Simba, Yanga na sasa Azam, ndiyo mwisho. Wanaojituma ni wale ambao bado hawajafika katika timu hizi, siku wakifika, na kujituma kwao kunafikia mwisho.
Ukimuondoa nahodha Shadrack Nsajigwa na kidogo Mrisho Ngassa, ni vigumu kumpata mchezaji wa Taifa Stars anayecheza hasa kwa kujituma na uchungu kwa nchi yake.
Ni kipindi hiki ndicho tunachoshuhudia wachezaji wetu wanashindana kusuka nywele, kuvaa nguo zao milegezo ‘Kata K', kuvaa hereni na ubitozi mwingine mwingi.
Wanasema wanakwenda na wakati, kwa sababu akina Malouda kule England wanasuka nywele na kuvaa heleni. Lakini tofauti yao tunaiona uwanjani. Akina Malouda wanacheza kwa nguvu kweli kweli, wanashindana msuli hadi unapenda.
Huwezi kujua, kwa staili hizi za kusuka nywele, kuvaa heleni, kuvaa nguo zao Kata K na tabia zingine ambazo mazingira ya jamii ya kwetu yanaonyesha ni mambo ya kike, huenda muda siyo mrefu tutawashuhudia wachezaji wetu wakishindana kuongea kwa kubana pua!
Ni vizuri kama kauli ile ya wachezaji wa Kongo ikawa kama changamoto kwa wachezaji wetu, si wale walioko timu ya taifa tu, bali hata katiika ngazi ya klabu, kwa sababu soka ni mchezo wa ushindani.
Itazame ligi tunayoishabikia sana ya England inavyochezwa. Wachezaji wanacheza kwa nguvu muda wote wa mchezo na hakuna legelege, licha ya ukweli kwamba kutokana na fedha wanazopata, wangeweza kuwa na maringo hata uwanjani.
Wenzetu wanashindana ubishoo nje ya uwanja kwa sababu kila mtu ana fedha. Sisi tunaleta ubishoo ndani ya uwanja, matokeo yake ladha ya mchezo inapotea taratibu.
Kadiri miaka inavyozidi kusogea, wachezaji wa mfano wanazidi kupungua! Hili ni jambo la kulitafakari na kufanyiwa kazi ya ziada na wadau wa soka.



 
Yaliyotokea Misri kwa Taifa Stars ni funzo kwa viongozi wapya
ban.blank.jpg

Ramadhani Siwayombe

amka2.gif
WAKATI Kocha Mbrazil Marcio Maximo alipoanza kukinoa kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars' mwaka 2006 alianza na kikosi ambacho alikuta tayari kimechaguliwa ambacho alifunga nacho safari hadi Brazil kuweka kambi ya mwezi mmoja.
Kikosi hicho kiliporejea timu ilikuwa tayari inaanza kushiriki mashindano ya kusaka nafasi ya kucheza fainali za Afrika na kuanzia Senegal; Watanzania wakiwa na shauku ya kuona matunda ya Mbrazil huyo.
Kilichotokea katika mchezo huo ni kipigo cha mabao 4-0 na kuzuka mtafaruku katika timu hiyo uliopelekea baadhi ya wachezaji kuenguliwa katika kikosi hicho akiwemo golikipa Juma Kaseja.
Kama ilivyo kawaida Watanzania kila mmoja alieleza lake kuhusiana na kipigo hicho na wengine walitoa ushauri kusaidia marekebisho ya kikosi hicho ambacho mwisho wa safari ya kuwania tiketi ya kucheza fainali za Afrika ikashindikana.
Maximo wakati akijipanga upya kuanza ngwe nyingine ya kusaka mafanikio ya kikosi hicho alizunguka baadhi ya mikoa kuangalia vijana na hatimae aliibuka na akina Kigi Makasi, Jerry Tegete na wengineo.
Vijana hao ambao walikuwa bado hawajawa na majina aliweza kuwaunganisha katika kikosi chake kilichosafiri na kuweka kambi ya mazoezi nchini Denmark licha ya kuwa katika ziara hiyo vijana hao katika michezo ya kirafiki hawakupata nafasi kubwa lakini ilikuwa ni ya maana kwao safari hiyo.
Waliporejea kutoka Denmark kikosi kilianza kubadilika taratibu kwa kuongezeka kwa damu changa ambazo zililazimisha baadhi ya wachezaji wengi wakongwe walioenda Brazil kuenguliwa katika timu hiyo na vijana kuchukua nafasi.
Mtiririko huo ulipelekea angalau timu ya taifa kuanza kuonyesha mwanga wa safari tuliyokusudia kwenda baada ya kuamua kuwekeza katika soka la nchi hii na wadhamini wengi kujitokeza kuunga mkono jitihada hizo.
Hali kama ya miaka iliyopita inaanza kujirudia na kuleta mashaka kutokana na ujio wa kocha mpya wa timu hiyo, Mdenish, Jan Poulsen, badala ya kusonga mbele tunaanza kurejea tulikoaanzia.
Nalazimika kueleza hayo kwa kuwa viongozi waliokuwepo katika Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kipindi cha Maximo kwa kiasi kikubwa ni walewale ambao wapo hivi sasa ukiachilia kina Angetile Osiah (Katibu Mkuu), Boniface Wambura (Ofisa Habari) na Jimmy Kabwe (Ofisa Masoko na Mipango) ambao waliajiriwa mwishoni mwa mwaka jana.
Naeleza hivyo kutokana na TFF kuziba masikio na kulewa sifa za kunyakua kombe la mashindano ya Chalenji na kuamua kwa makusudi kukataa ushauri mbalimbali uliotolewa baada ya kupata mwaliko wa kuhudhuria mashindano yanayoshirikisha nchi wanachama zinazopitiwa na Mto Nile, yanayofanyika Misri ambayo ilitakiwa kupeleka timu ya vijana ili ipate uzoefu.
Sababu za mashabiki kutaka ipelekwe timu ya vijana ni kuanza kusaka timu ambayo baadaye itakuwa timu ya Taifa ya Tanzania baada ya akina Nsajigwa kuchoka zaidi, kwani wamebakiza miaka michache kuitumikia timu hiyo, hivyo hakuna mbadala wao ambao wameshaanza kuandaliwa ili kushika nafasi hiyo.
Mifano ni mingi duniani ambayo imetokea katika kipindi hiki kifupi tukianzia na Ghana baada ya kufanikiwa kuunda kikosi kizuri cha timu ya vijana kilichotwaa ubingwa wa dunia wa vijana waliamua sehemu kubwa ya vijana hao kuwakilisha nchi yao katika kombe la dunia.
Mfano mwingine ni katika mashindano ya kuwania kombe la Chalenji, yaliyofanyika hapa Tanzania mojawapo ya nchi mwalikwa, Ivory Coast licha ya kuwa na wachezaji wengi wa kulipwa waliamua kuleta kikosi cha vijana ambao wanawaandaa kwa ajili ya kuwakilisha nchi yao katika kikosi cha timu yao ya taifa.
Kwa mifano hiyo na mingine iliyopo mwaliko iliyoupata TFF kwa timu ya taifa kutakiwa kushiriki mashindano nchini Misri wangetumia kwa ajili ya kikosi cha vijana wakiwepo wazoefu wachache zaidi katika kikosi hicho.
Badala ya mfumo huo tumeshuhudia kuitwa kwa wachezaji kama Saidi Maulid, Athumani Machupa na wengineo na kuacha kutumia nafasi hiyo kwa vijana ambao ndio wanaanza kuchipuka kama kina John Boko, Himid Mao, Moshi Kazimoto na wengine.
Mbali na hao ilitakiwa TFF kuwaangalia wachezaji wa timu ya vijana waliotokana na mashindano ya Copa Coca Cola ambao walikwenda Brazil na baadae wa mwaka juzi walikwenda Afrika Kusini ambao walionekana kupata uzoefu lakini TFF vijana wale hawawataki kabisa.
Licha ya wadau wa soka, klabu na makocha wa soka kujitahidi kuelezea hilo lakini ilionyesha viongozi kuweka pamba masikioni wakitarajia timu hiyo inaenda Misri kuendeleza ushindi na kulinda heshima.
Nadhani ifike wakati tusiishi na kuendesha soka kwa kutegemea akili za ‘mitulinga' na kuacha mfumo rasmi wa kitaalam ili kufikia mafanikio tunayoyatarajia bila kutafuta njia za mkato.
Kamaakili ya kutegemea mafanikio itapatikana kwa njia za mkato, mkataba wa kocha huyu mpya utamalizika na hakutakuwa na jipya ambalo tutaona amelifanya kutokana na kila mara licha ya kujua bado tupo chini kwa kiwango cha soka letu lakini tunataka tuonekane tuko juu.
Njia sahihi kwa muda huu nguvu kubwa kuielekeza kwa kuandaa vijana wapya watakaotuletea mafanikio ya muda mrefu katika soka na kama inavyotokea kwa wenzetu duniani kote.
Zamaza akina Said Maulid, Athumani Machupa zimekwisha kabisa na si kwamba hawajui kucheza bali hawawezi tena kutusaidia katika mafanikio tunayoyakusudia ni lazima tukubali ukweli huu.
Hadi sasa tatizo kubwa la soka la nchi yetu hatuna wafungaji makini ama vijana wenye uwezo wa kufunga mabao, Poulsen anatakiwa awekeze nguvu kubwa katika hilo tuache ubabaishaji.
Ni wajibu wa Mkurugenzi wa Ufundi TFF, Sunday Kayuni, Mkurugenzi wa Utawala na wanachama, Mtemi Ramadhani, Rais Leodegar Tenga ambao watanzania wanaamini ni watu mliodumu katika soka kwa muda mrefu ambao wanaweza kubadili mfumo tunaoenda nao ambao hata nyie mnatambua hautaleta mabadiliko katika soka letu.
Nawakumbusha wakati Shirikisho la soka la Kimataifa (FIFA) miaka ya 1990 ilianzisha mradi wa kuzisaidia nchi changa katika soka ambazo ni wanachama wa FIFA kwa kuwapelekea makocha wa kunyanyua soka katika nchi hizo, Tanzania tulipata bahati ya kuletewa kocha Victor Stanslescu.
Sasa tujiulize toka wakati huo tumefanya nini kuhusu tatizo hilo je kuna wachezaji wapya wa nafasi hiyo walioandaliwa na hata kuwafikiria kupata nafasi ya kucheza nje ya nchi na kama hakuna tutawategemea kina Machupa hadi lini?
 
Uchaguzi Mkuu ZFA waota mbawa


Na Mussa Soraga, Zanzibar

UCHAGUZI Mkuu wa Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA), ambao ulikuwa ufanyike keshokutwa Nungwi mjini hapa umefutwa, baada ya Ofisi ya Mrajisi wa Vyama vya Michezo kutaka usitishwe.Agizo hilo limetolewa na
Mrajisi wa vyama hivyo, Mustafa Omari Abdallah ambaye alimwandika barua jana Katibu Mkuu wa ZFA, Mzee Zam Ali na nakala kutumwa kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na michezo, Abdillahi Jihad.

Barua hiyo ilieleza kuwa kwa mujibu wa mamlaka iliyonayo kisheria, ofisi yake imeitaka ZFA kusitisha uchaguzi huo wa marudi uliopangwa kufanyika Jumatano hadi hapo Mrajisi huyo atakapokaa meza moja na uongozi wa ZFA Taifa.

Mkutano wa pamoja kati ya Mrajisi huyo na uongozi wa ZFA utafanyika leo katika Ofisi za Baraza la Michezo la Zanzibar (BMZ).

"Ofisi ya Mrajisi wa Vyama vya Michezo kwa mamlaka iliyopewa kisheria, chini ya kifungu cha 19 (b) cha sheria namba 5 ya mwaka 2010 ya Baraza la Michezo la Zanzibar, inatoa agizo kuwa uchaguzi wa ZFA usimamishwe mara moja," ilisomeka sehemu moja ya barua hiyo.

Hata hivyo wakati barua hiyo inawasilishwa katika ofisi za ZFA, chama hicho kilikwishafanya maamuzi ya kutofanyika kwa uchaguzi huo kutokana na ombi la Mwenyekiti wa Kamati mpya ya Uchaguzi, Abdulghan Msoma.

Msoma, ambaye kamati yake imechukua nafasi ya kamati iliyovunjwa ya Ali Suleimnai Shihata, aliiomba ZFA kuuaghirisha uchaguzi huo hadi baadaye ili yeye na wajumbe wake wapate muda mzuri wa kujipanga.Alisema kazi ya kusimamia uchaguzi si nyepesi kwa sababu inahusisha masuala ya kisheria, hivyo aliomba muda zaidi kwa nia ya kuipitia katiba pamoja na kujiweka sawa kabla ya uchaguzi huo mpya haujafanyika.

Licha ya Msoma kutaka uchaguzi huo usogezwe mbele, alishauri uchaguzi mpya uwahusishe na wagombea wengine kwa vile ule awali uliofutwa na kamati ya Shihata ulikuwa batili.

 
Phiri: Wabrazil watatuonesha njia


Na Zahoro Mlanzi

KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Phiri amesema mchezo wao wa kimataifa dhidi ya Atletico Paranaence, kutoka Brazil ndiyo utakaompa hali halisi kuhusu kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara.Kauli hiyo imekuja, baada ya timu
yake juzi kupokea kipigo cha mabao 2-1 kutoka kwa Zesco ya Zambia katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa uliopigwa Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Phiri alisema kufungwa huko kumemfanya agundue kitu miongoni mwa wachezaji wake, kitu ambacho atakifanyia kazi kabla hajakutana na Wabrazili Januari 20, mwaka huu.

"Nimekubali matokeo kwani timu ilicheza chini ya kiwango, lakini nashukuru nimegundua matatizo kadhaa (bila kuyataja) ambayo katika mchezo unaofuata ndiyo utakaotoa picha kamili katika michezo ya Ligi Kuu," alisema Phiri.

Alikiri kuzidiwa katika kipindi cha kwanza kwani wapinzani wao, waliwakamata kila idara lakini anashukuru mabadiliko aliyoyafanya yalileta mabadiliko na hatimaye matokeo kuwa hayo.

Naye Kocha Mkuu wa Zesco FC, Fighton Simukonda akizungumzia mchezo huo ambapo alisema wamekuja nchini kufanya maandalizi kwa ajili ya Klabu Bingwa Afrika, hivyo hawatafanya masihara.

Alisema ndiyo maana wanacheza kwa nguvu na kasi, ili wachezaji wake wajiandae vizuri na watafanya hivyo kwa timu yoyote watakayokutana nayo.
 
Savio yaendeleza wimbi la ushindi


Na Amina Athumani

MABINGWA watetezi wa Ligi ya Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (RBA), Savio imeendeleza wimbi la ushindi katika mashindano ya ligi hiyo yaliyofanyika jana Uwanja wa ndani Taifa, Dar es Salaam ambapo timu hiyo
iliibuka na ushindi wa pointi 77-41 dhidi ya TP Stars.

Mabingwa hao ndiyo wanaoongoza katika msimamo wa ligi hiyo kwa kushinda michezo yote mitatu, iliyocheza tangu kuanza kwa ligi hiyo ambapo katika mchezo wa jana hadi kufikia mapunziko Savio ilikuwa ikiongoza kwa pointi 30-18.

UDSM ambayo ilizuiwa kuingia uwanjani wiki iliyopita kutokana na kutokamilisha taratibu za usajili wa wachezaji wake, jana ilifungwa na Tanzania Prisons kwa pointi 78-60. Timu hiyo iliruhusiwa baada ya kukamilisha usajiliwa wake.

Katika mchezo mwingine Vijana, iliibuka na ushindi wa pointi 60-55 dhidi ya Oilars huku, Chang'ombe United ikiilaza Airwing kwa pointi 82-55.

Akizungumzia michuano hiyo, Mkurugenzi wa Mashindano Chama cha Mpira wa Kikapu Mkoa wa Dar es Salaam (BD), Zabron Manase alisema ligi hiyo inaendelea vizuri ingawa bado mdhamini wa mashindano hayo hajapatikana.

"Tangu ligi hii ilipoanza wiki mbili zilizopita, tunaiendesha kama BD na hatujapata mdhamini yeyote hadi sasa hivyo tunaomba wadau wa mpira wa kikapu kujitokeza, ili kuidhamini ligi hii kwani timu zote zimeonesha ari ya kwa kushiriki kwa moyo mmoja bila ya kinyongo cha kukosa mdhamini," alisema Manase.

 
Villa kucheza mechi kibao za kirafiki


Na Shaban Mbegu

TIMU ya Villa Squad, imepanga kucheza mechi nyingi za kirafiki ili kujiandaa vyema Ligi Daraja la Kwanza hatua ya Tisa Bora iliyoapangwa kuanza Januari 30 mwaka huu.Akizungumza na mwandishi wa habari hizi Ofisa habari wa
Villa, Idd Godigodi alisema kwa sasa timu yake inaendelea na mazoezi ya kila siku ambayo yanafanyika kwenye Uwanja wake uliopo Jangwani.

"Katika kuhakikisha tunarudi Ligi Kuu msimu ujao, tumejipanga kuhakimisha tunacheza michezo mingi ya kujipima nguvu ambayo tuna imani itatusaidia katika hatua ya Tisa Bora," alisema Godigodi.

Godigodi alisema hadi sasa tayari wamecheza mechi 10 za kirafiki lakini wanatarajia kucheza mechi nyingine nyingi zaidi kwa ajili ya kujiimarisha kabla ya kuanza kwa Ligi hiyo.Alisema wameamua kuiandaa vyema timu hiyo kutokana na katika hatua hiyo ya Tisa Bora, timu nyingi zimejiandaa vizuri na kila moja inataka kucheza Ligi Kuu.

Timu zinazotarajiwa kucheza ligi hiyo ni TMK United, Villa, Moro United za Dar es Salaam, Polisi Morogoro, Moran ya Manyara, Coastal Union ya Tanga, Oljoro JKT ya Arusha, Rhino ya Morogoro na Prisons ya Mbeya zinatarajiwa kutoa nne zitakazocheza Ligi Kuu msimu ujao.

 
Ivory Coast, Congo kucheza fainali za Dunia Mexico


KIGALI, Rwanda

MABAO mawili yaliyofungwa kipindi cha kwanza na Diarrasouba Drissa na Kouassi Evrard, yaliiwezesha Ivory Coast kukata tiketi ya fainali za Kombe la Dunia la vijana wenye miaka chini ya 17.Katika mechi nyingine ya
Kundi B iliyopigwa kwenye Uwanja wa Umuganda mjini Gisenyi, timu ya Congo nayo iliungana na Ivory Coast baada ya kuichapa Mali mabao 2-1 na kukamilisha timu zitakazocheza nusu fainali ya vijana wenye miaka chini ya 17 ya Afrika na kukata tiketi ya fainali za Kombe la Dunia za vijana wenye miaka hiyo.

Mexico itakuwa mwenye wa fainali za U-17, zitakazofanyika Juni 2011.Tembo hao wadogo 'Elephants na Nge watoto' waliokuwa wakicheza kwenye Uwanja wa Kigali, hawakufanya makosa katika mchezo huo.

Lakini ilikuwa Tembo wadogo waliopata bao la kwanza, lililofungwa na Drissa dakika ya 12 na kuifanya timu yao iongoze. Ivory Coast walipata bao la pili kupitia kwa Kouassi, dakika moja kabla ya mapumziko katika mechi iliyochezeshwa na mwamuzi kutoka Angola, Martins Helder.

Bao la tatu la Ivory Coast lilifungwa na Lago Lionel na kuiweka timu yake katika hali nzuri ya kwenda nchini Mexico. Beki Sabally Adama, aliifungia Gambia bao, lakini beki wa timu hiyo Adama, aliunawa mpira ndani ya eneo la penalti na mwamuzi alimtoa nje kwa kadi nyekundu.

Bedi Guy Stephane aliifungia timu yake kwa mkwaju wa penalti na bao la nne liliwekwa kimiani na Guy Stephane.

Kwa ushindi huo, Ivory Coast itacheza na wenyeji Rwanda katika mechi ya nusu fainali ya michuano vijana ya Afrika wenye miaka chini ya 17.

Katika Uwanja wa Umuganda, Congo iliifunga Mali mabao 2-1 na kushika nafasi ta pili katika kundi lao.Congo walipata bao la kwanza dakika ya 50, lililofungwa na Christ Nkoukou na bao la pili liliwekwa kimiana dakika ya 55, kupitia kwa Stevy Epaku. Mali ilipata bao lake kupitia kwa Malick Berthe dakika ya 85.

Nusu fainali ya kwanza itachezwa kesho kwenye Uwanja wa Amahoro, kati ya mshindi wa Kundi A, Burkina Faso na Congo. Jumatano wenyeji Rwanda waliomaliza wakiwa wa pili katika Kundi A, wataumana na Ivory Coast waliokuwa wa kwanza katika Kundi B kwenye Uwanja wa Amahoro.
 
Toffees accept Blues' Pienaar bid




18 comments »

Updated Jan 16, 2011 2:05 PM ET
Everton manager David Moyes has confirmed the Toffees have accepted a bid from Chelsea for winger Steven Pienaar.

Wed., Jan. 12
Blackpool 2-1 Liverpool | Recap
Sat., Jan. 15
Chelsea 2-0 Blackburn | Recap
Man City 4-3 Wolves | Recap
Stoke City 2-0 Bolton | Recap
West Brom 3-2 Blackpool | Recap
Wigan 1-1 Fulham | Recap
West Ham 0-3 Arsenal | Recap
Sun., Jan. 16
Birmingham 1-1 Aston Villa | Recap
Sunderland 1-1 Newcastle | Recap
Liverpool 2-2 Everton | Recap
Tottenham 0-0 Man Utd | Recap
BPL Scores | Table | Fixtures

The Merseyside club have, though, turned down Tottenham's offer for the midfielder.
Moyes revealed on Friday the Toffees had accepted an offer for the South Africa international, who is out of contract at the end of the season, but did not name the club.
The Scot said after today's 2-2 draw with Liverpool at Anfield: "We have accepted an offer from Chelsea. Steven has not agreed terms with Chelsea.
"We've given his representatives a chance to talk to Chelsea but they've not got permission to talk to Tottenham because they've not offered the same money."
Chelsea are believed to have offered £3million for the South Africa midfielder, who was left out of the squad for Anfield after telling Moyes he did not want to be involved.
"Steven came to see me yesterday (Saturday) and said he didn't feel he was in the right place to play," added Moyes.
"I had a decision to make and I felt it would be better not to use him if that was the case.
"He will be in training tomorrow because at the moment we don't have a deal.
"If Tottenham offer the same money that may change or maybe he will agree terms with Chelsea."
 
Tottenham 0-0 Manchester United


RivalsDM



PRINT RSS

8 comments »

Updated Jan 16, 2011 1:37 PM ET
Ten-man Manchester United regained top spot in the Premier League and remain unbeaten after a 0-0 draw with Tottenham at White Hart Lane.
United right-back Rafael saw red after collecting his second caution with 16 minutes remaining, but the Red Devils repelled everything Spurs threw at them late on to earn a point.

Wed., Jan. 12
Blackpool 2-1 Liverpool | Recap
Sat., Jan. 15
Chelsea 2-0 Blackburn | Recap
Man City 4-3 Wolves | Recap
Stoke City 2-0 Bolton | Recap
West Brom 3-2 Blackpool | Recap
Wigan 1-1 Fulham | Recap
West Ham 0-3 Arsenal | Recap
Sun., Jan. 16
Birmingham 1-1 Aston Villa | Recap
Sunderland 1-1 Newcastle | Recap
Liverpool 2-2 Everton | Recap
Tottenham 0-0 Man Utd | Recap
BPL Scores | Table | Fixtures

Wayne Rooney brought a couple of smart saves from Tottenham goalkeeper Heurelho Gomes in the first half and Rafael van der Vaart also went close on two occasions for Tottenham.
But in the end the two sides cancelled each other out in a game which proved the title race is going to be tight right until the end.
The draw sees Tottenham, who have not beaten United since May 2001 in a run which now stretches 24 matches, stay fifth a point behind Chelsea and outside the Champions League places after a game which was long on effort and passion but short on quality.
The most explosive incident was the once concerning Rafael who was shown a yellow card for a foul on full-back Benoit Assou-Ekotto after having earlier been booked for a challenge on Wilson Palacios.
The young Brazilian raged at referee Mike Dean and kicked over a television sound boom as he left the pitch and the FA are likely to want to review the video. Rooney was also booked for his protests.
Yet while Tottenham showed how far they have come under Harry Redknapp it was United who also proved their resilience.
Ryan Giggs was named in the starting line-up for his 600th league appearance for United, just six behind the record of Sir Bobby Charlton.
Sir Alex Ferguson was also boosted by the fact that Rooney returned from an ankle injury after missing two games while Nemanja Vidic and goalkeeper Edwin van der Sar were also fit after recent absences.
Vidic's presence was crucial and he was instrumental in halting the forays of the pacy Aaron Lennon down Tottenham's right.
Due to injuries, Vidic and Rio Ferdinand have been in harness too infrequently in recent seasons. There is no doubt United look more solid when they are together.
It meant Peter Crouch, who had been preferred to Jermain Defoe, for the most part was contained and that has a knock-on consequence for Tottenham in that Van der Vaart is starved on the knockdowns which he has been so quick to exploit this season.
As it was United might have taken the lead in the first two minutes, Rooney being neatly played in by Dimitar Berbatov but skewing his right-foot shot across the face of the goal.

TRANSFER SPECIAL

Keep up with all the biggest moves around the globe with our 2011 January transfer gallery.

A flake of rust in that effort, although there was no sign of it after 22 minutes when Rooney, once again smartly served by Berbatov, brought a stumbling save from Tottenham goalkeeper Gomes.
United had their moments but in that first half the attacking impetus came from Tottenham and especially Gareth Bale who was beginning to give Rafael a torrid time down the left.
One of his trademark whipped-in crosses was inches away from being dispatched into the net by Crouch.
Van der Vaart looked to have cashed in on another raking Bale cross but could only manage to send his downward header into the side-netting.
It was all fast and frantic, strewn with errors and with no time for midfield players to settle on the ball.
Not surprisingly, it was a 45 minutes in which referee Dean was busy, booking Rafael, Wilson Palacios, Darren Fletcher and Van der Vaart, the latter for kicking the ball away.
It needed someone like David Beckham, up in the stands and who has been training with Tottenham this past week, to put his foot on the ball and bring a measure of control.
United began the second half with more composure. They might have taken the lead after 50 minutes when a Giggs corner was flicked goalwards by Michael Carrick but sailed just wide of the post.
A minute later Rooney burst through the middle to unleash a right-foot shot from the edge of the penalty area, only to be denied by a full-length diving save from Gomes.
The Tottenham goalkeeper was certainly the busier.
It was a match with lots of attacking endeavour from both sides but no-one seemed capable of creating the breakthrough.
There were claims for a penalty when Vidic blocked Van der Vaart's effort after clearly holding his shirt in the penalty area but the referee waved them away.
Then came Rafael's moment of madness, at which point United were happy with their point
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom