Michezo magazetini leo...

Michezo magazetini leo...

Status
Not open for further replies.
Mtemvu bado 'pasua kichwa' Yanga


Na Elizabeth Mayemba

UTEUZI wa Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu kuwa mdhamini wa Yanga limeonekana kuendelea kuwaumiza vichwa wanachama wa klabu hiyo, ambao wanashinikiza ufanyike Mkutano Mkuu wa dharura ili wajue
mbivu na mbichi.

Wanachama hao wanapinga uteuzi wa Mbunge huyo kwa madai kwamba ana asili ya Simba na pia hajawahi kujitokeza hata siku moja kuisaidia timu kwa namna yoyote walau maji ya kunywa kwa wachezaji.

Pia wanachama hao wanautaka mkutano huo wa dharura kwa kuwa mambo ndani ya Yanga kwa sasa yanakwenda ndivyo sivyo, likiwemo suala la klabu hiyo kuwa kampuni huku viongozi wakiwa hawana umoja.

Hivi karibuni mmoja wa wadhamini wa klabu hiyo, Yusuf Manji alimpendekeza Mtemvu kuwa mmoja wa wajumbe wa bodi ya udhamini, hali ambayo imepingwa vikali na baadhi ya wanachama.

Wakizungumza Dar es Salaam jana kwa nyakati tofauti wanachama hao walidai kwamba wanaona mambo hayaendi sawa ndani ya klabu hiyo na kuna maamuzi yanayofanyika, lakini baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji hawafahamu lolote.

"Ukikaa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji ukiwauliza kuhusiana na suala zima la uteuzi wa Mtemvu au Yanga kuwa kampuni, hawafahamu lolote sasa tunataka kuelezwa haya maamuzi yamepitishwa na viongozi wangapi,? alihoji mmoja wa wanachama hao ambaye hakutaka kuandikwa jina lake gazetini.

Alisema inaonekana wazi kwamba kuna baadhi ya viongozi wa klabu hiyo, hawana msimamo katika maamuzi yao na inaonekana wamekuwa wakiamrishwa kila kitu na mtu mmoja, hali ambayo inazua hofu ndani ya Yanga.

Mwanachama mwingine ambaye hakutaka kuandikwa jina, alisema endapo viongozi hawatakuwa na msimamo wana hofu klabu yao itaelekea kubaya na kwamba wanasikia klabu hiyo inataka kuwa kampuni ili hali wanachama hawajajulishwa lolote.

"Sasa hivi klabu hii inaelekea kubaya sisi kama wanachama tumechoshwa na hali hii na sasa hivi hatutakubali kuendeshwa na mtu yeyote, maana tunaona kama ni utumwa," alisema mwanachama huyo.Hata hivyo kuna taarifa kwamba baadhi ya wazee wa klabu hiyo, jana na juzi walikuwa na kikao na Manji kujaribu kuweka mambo sawa.
 
Tamasha la Wanyambo laiva Dar


Na Nayla Abdulla

KAMATI ya Maandalizi ya Tamasha la Utamaduni la kabila la Wanyambo wanatarajia kukutana leo katika Kijiji cha Makumbusho, Dar es Salaam kwa ajili ya kupanga taratibu za maandalizi ya tamasha hilo.Tamasha hilo la
Wanyambo linatarajia kuanza Januari kuanzia kesho hadi Januari 23, mwaka huu.

Awali tamasha hilo lilipangwa kufanyika Novemba, mwaka jana lakini liliahirishwa kutokana na shughuli za Uchaguzi Mkuu wa nchi uliofanyika Oktoba 31.

Akizungumza Dar es Salaam jana Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Daniel Rutasyamka alisema tamasha hilo litakuwa ni la siku tatu na litahusisha wasanii mbalimbali kutoka Wilaya za Karagwe na Kyerwa pamoja na wadau wengine.

Alisema mambo yatakayofanywa katika tamasha hilo ni maonesho ya ngoma za Wanyambo, Vyakula vya asili, vinywaji vya asili, zana za asili, mila na desturi, nyumba za asili, kazi za mikono, maandishi ya methali, warsha na kongamano zinazozungumzia maendeleo ya Karangwe na Kyerwa pamoja na vivutio mbalimbali vinavyopatikana katika wilaya ya Karagwe na kyerwa.

"Ili tamasha hili liweze kufanikiwa, juhudi za Wanyambo wote waishio Dar es Salaam zinahitajika, hivyo ni muhimu wanyambo wote wa Dar es Salaam kuhudhuria kikao cha kesho (leo)cha maandalizi kitakachofanyika katika kijiji cha makumbusho,"alisema Rutasyamka.

Alisema tamasha hilo litafanyika jijini Dar esSalaam kwa mara ya kwanza na linategemewa kuwa kiungo muhimu kati ya Wanyambo waishi Dar es Salaam na Wilaya za Karagwe na Kyerwa.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom