Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,184
- Thread starter
- #4,621
Taifa U-20 kujipima kwa Azam U-20 Wednesday, 02 February 2011 21:34
Kalunde Jamal
TIMU ya soka ya taifa ya vijana ya U-20 ambayo ipo kambini kujiandaa na Michezo ya Olimpiki, Jumapili inatarajia kushuka dimbani kucheza mechi ya kirafiki na timu ya soka ya Azam ya U-20 katika mchezo w akujipima nguvu.
Kocha wa timu hiyo, Jamhuri 'Julio' Kihwelo aliiambia Mwananchi kuwa vijana wake wanaendelea vizuri na mazoezi na mpaka sasa hakuna majeruhi.
"Tutacheza na Azam ili kuendelea kuwanoa vijana na kuwaimarisha ili wasiogope kucheza na timu yoyote watakayokutana nayo hasa katika michuano hii mikubwa watakayoshiriki hivi karibuni," alisema kocha huyo.
Alisema kuwa mchujo wa kuwapata wachezaji 25 wa U-20 ambao watajiunga na kambi ya U-23 ili kuanza maandalizi ya Olimpiki, utafanyika kesho asubuhi.
"Wachezaji wote wana uwezo na wapo vizuri kiasi kwamba inakuwa ngumu kuteuwa hao wachezaji 25 na kujua nani aende nani abaki," alisema Kiwhelo.