Michezo michafu ya CCM yaanza kuwarudia na kuliangamiza Taifa. Tumeshakuwa kuwa Lawless Country

Michezo michafu ya CCM yaanza kuwarudia na kuliangamiza Taifa. Tumeshakuwa kuwa Lawless Country

Lord Denning

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2015
Posts
23,491
Reaction score
57,973
Kwa sababu iliwapendeza wao waliona sawa pale Mwambe alipojiondoa Chadema alafu akaendelea kuwa mbunge wa CCM kipindi cha awamu ya 5 kinume kabisa cha Katiba na Sheria za Nchi.

Kwa sababu iliwapendeza wao, wakaona sawa kabisa wabunge 19 wa Chadema walipoendelea kuwa wabunge baada ya kufukuzwa uanachama wa Chadema kinyume kabisa na Katiba na Sheria za Nchi.

Kwa sababu iliwapendeza wao waliona sawa Ester Matiko kuendelea kuwa mbunge kwa ticketi ya Chadema huku akiwa amefukuzwa Chadema alafu wakamlipa kiinua mgongo cha Ubunge kisha akaenda kuchukua fomu ya Kugombea Ubunge wa CCM kwa kudai alishajiunga na CCM tangu mwaka 2022.

Wakaona sawa kina Jesca Kishoa, Nusrat Hanje na Salome Makamba kuhudhuria vikao vya CCM wakiwa wanatambulika kama wabunge wa Chadema wakati walishafukuzwa uanachama wa Chadema kinyume kabisa na Katiba na Sheria za Nchi.

Leo uzandiki walioufanya umeanza kuwarudia na Nchi yetu imegeuka rasmi kuwa nchi isiyozingatia utawala wa Sheria. ACT Wazalendo wametembelea kwenye uzandiki uleule wa CCM kwa kudai Luhaga Mpina alijiunga nao siku nyingi wakati kwenye Bunge lililovinjwa mwezi huu Agosti amemaliza kama Mbunge wa CCM na kulipwa kiinua Mgongo kama Mbunge wa CCM aliyemaliza muda wake.


Tumekuwa rasmi a Lawless Country.

Polee kwetu.
Screenshot_20250820-172548_X.jpg


No Reforms No Election ✊️✌️
 
Back
Top Bottom