Michezo mikubwa inayotarajiwa kuchezwa leo, Oktoba 24, 2026

Michezo mikubwa inayotarajiwa kuchezwa leo, Oktoba 24, 2026

carbohydates

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2026
Posts
260
Reaction score
607
Michezo mbalimbali ya soka inatarajiwa kuchezwa leo katika ligi tofauti duniani, ikiwemo Ligi Kuu ya England, Hispania, Ufaransa na ligi ya Tanzania.

Tukianza na Ligi Kuu ya England, kuna michezo minne inayotarajiwa kuchezwa. Mchezo wa kwanza ni Aston Villa dhidi ya Manchester City, utakaopigwa saa 8:45 mchana. Mchezo wa pili ni Arsenal dhidi ya Everton, unaotarajiwa kuanza saa 11 jioni. Mchezo mwingine ni Coventry City dhidi ya Fulham, huku mchezo unaotarajiwa kuvuta hisia za mashabiki wengi ukiwa ni Chelsea dhidi ya Tottenham Hotspur.

Nchini Hispania, michezo kadhaa pia inatarajiwa kuchezwa, ikiwemo Rayo Vallecano dhidi ya Elche, Racing de Santander dhidi ya Espanyol, Valencia dhidi ya Villarreal, pamoja na Atlético Madrid dhidi ya Deportivo La Coruña.

Nchini Ujerumani, kuna michezo mbalimbali inayotarajiwa kuchezwa, ikiwemo Augsburg dhidi ya Union Berlin, Köln dhidi ya Schalke 04, pamoja na michezo mingine ya ligi hiyo.

Kwa upande wa Tanzania, ratiba inahusisha michezo mitatu. Pamba Jiji itakuwa na kibarua dhidi ya TRA United saa 10 jioni, huku JKT Tanzania ikitarajiwa kukutana na Kagera Sugar saa 12 jioni. Mchezo mwingine ni kati ya Namungo FC na Coastal Union.

Pia unaweza kutizama Ratiba ya leo kwa michezo mikubwa Duniani

Ligi Kuu ya England : Premier League


15:30 Aston Villa vs Manchester City

18:00 Arsenal vs Everton

18:00 Coventry City vs Fulham

20:30 Chelsea vs Tottenham Hotspur

Ligi Kuu ya Hispania :LaLiga

16:00 Rayo Vallecano vs Elche

18:15 Racing Santander vs Espanyol

20:30 Valencia vs Villarreal

23:00 Atlético Madrid vs Deportivo La Coruña

Ligi Kuu ya Ujerumani :Bundesliga

16:30 Augsburg vs Union Berlin

16:30 Köln vs Schalke 04

16:30 Mainz 05 vs Werder Bremen

16:30 Paderborn vs Hamburger SV

16:30 RB Leipzig vs Elversberg

19:30 Borussia Dortmund vs Eintracht Frankfurt

Ligi Kuu ya Italia :Serie A

16:00 Cagliari vs Bologna

16:00 Como vs Sassuolo

19:00 Napoli vs Roma

21:45 Lazio vs Parma

Ligi Kuu ya Ufaransa: Ligue 1

21:45 Lens vs Paris FC
 
Shukrani sana kwa hii taarifa rasmi, wale wa kubet waanze kuchanga kalata zao
 
Back
Top Bottom