SoC04 Michezo ni chanzo cha ajira Tanzania ikiwekezwa vizuri

SoC04 Michezo ni chanzo cha ajira Tanzania ikiwekezwa vizuri

Tanzania Tuitakayo competition threads

hauleibrahim

Senior Member
Joined
May 17, 2024
Posts
183
Reaction score
125
Tz yetu hii imejikita kwenye michezo michache sana na hiyo michezo serikali ndio hitoa sapoti Kwa kiasi chake ila mm Kwa miaka kumi ijayo ni wkati wa serikali pamoja na wadau wote nchini kuunga mkono michezo yote halali inayoweza kuongeza Pato la taifa na kuongeza ajira Kwa vijana.

Michezo yote huleta ajira tuangalie michezo ambayo tukiwekeza vizuri itapunguza ukosefu wa ajira Kwa vijana wengi tz.

Mpira wa miguu. huu ni mchezo pendwa duniani na kimekuwa ni chanzo Cha ajira iwe Kwa wasomi mpaka wasio wasomi mpira wa miguu unachukua watu wote bila ubaguzi wa wew wa chuo mm Wala saba. hpa serikali iongese nguvu kuisapoti tff ili hata walau ligi yetu iweze kuwa na vilabu 20 na visiwe 16 kama sasa. kama vilabu vitakuwa vingi timu nyingi za mkoa vijana wake watapata ajira humo kwenye timu na kujipatia ujira na kupunguza wimbi la vijana kukaa vijiweni hasa wale wenye vipaji vya mpira.

Mchezo wa ngumi: ni mchezo pendwa duniani ila pia ni mchezo unao toa mabilionea kama ilivyo katika soka ni vizuri seriKali ishirikiane na wadau kuboresha miundombinu na kuitangaza ngumi ili vijana wenye vipaji na mwamko wa kujiunga na michezo ya ngumi wajiunge hii itapunguza kama sio kumaliza wimbi la vijana kukosa ajira hasa Kwa wasomi na wasio wasomi mitaaani.

Tennes: huu ni mchezo unao chezwa tz pia na huko duniani n vizuri seriKali ikaupa kipaombele kikubwa pia ili wapenda tenes wapate kujiajiri humu pia ni mchezo unao weza kuchukua Rika zote za wasomi na wasio wasomi Kwa hiyo serikali inatakiwa kuipa nguvu michezo ili kuongeza upana wa ajira Kwa vijana wenye kupenda mchezo kama tenesi

Basketball: ni mchezo unao chezwa ulimwenguni kote unatoa mabilionea pia unachezwa na vijana Rika lote wasomi na wasio wasomi serikali ikiboresha huu mchezo ukawa kila mikoa Ina timu au Kuna ligi ya timu nyingi za mpira wa kikapu vijana wengi watajiajiri humo Kwa wapenda mpira wa kikapu na kupunguza wimbi la vijana kukimbilia soka na huko kukosa nafasi.mpira wa kikapu utaaajiri wasomi na wasio wasomi mtaani.

Gofu: gofu inaonekana ni mchezo wa matajiri ila sio kweli ni mchezo unao chezwa na kila mtu hapa ni wajibu wa serikali kuipronote gofu na kuipa nguvu wale vijana wanao penda gofu waingie kwenye gofu kucheza na kujipata kiajira humo gofu ni mwokozi pia ni mchezo unao chezwa duniani kote na pia nichanzo Cha ajira Kwa waliomo.

Mziki: huu ni chezo mwingine unao ajiri vijana wengi wasomi na wasio wasomi na unatoa matajiri wakubwa duniani. kwa wale vijana wasio penda michezo mingine mingi huenda wakapenda mziki nao wkajikitw hapa na kupata ajira zao za kujiajiri au kuajiliwa chini ya kampuni kubwa za miziki kama wasafi n.k ni vizuri seriKali ikawekeza nguvu kwenye miziki aina yote ili iweze kuwa na nguvu vijana wnao penda miziki waingie humo. uzuri wa miziki inaachukua wachezaji mpka waombaji wenyewe Kwa hiyo itaongeza nafasi za vijana kujiajiri Sasa n wajibu wa serikali kusapoti huo mziki na mipango iliyomo ya watu waliopo kwenye tasnia ya miziki.

Hiyo ni michezo michache yenye maarufu na inayoweza ajili vijana wengi walio soma na wasio soma japo IPO michezo mingine mingi mikubwa ila mm hiyo niliyo itaja nikwa sababu haichagui elimu ila ni kipaji chako na juhudi japo IPO mingine pia ila Kwa wenzetu walisha piga hatua kuifanya ni michezo Bora kwetu ni ngumu kuwekeza humo.

Michezo kama ikizingatiwa na serikali kama chanzo Cha ajira na kuwekeza nguvu zao vijana wengi watajipata haraka kimaisha na utajiri maana michezo niliyotaja n michezo inayochukua timu ama kuanzisha timu toka ngazi za chini huko ambako ndiko kuliko chimbuko la vijana wetu walio wasomi na wasio wasomi.

Michezo ni chanzo Cha ajira isiyo na masharti Kwa wachezaji ni jukumu Sasa la serikali kuunga mkono juhudi za wadau ili kama sisi tumeshindwa kupata ajira michezo itusaidie hata Kwa wasio na elimu ituokoe.

Wenzetu michezo walisha iweka kwenye mfumo wa ajira ndo mana wenzetu vijana wadogo wna utajiri mkubwa mifumo Bora iliyowekwa na serikali zao kuithamini michezo yoyote halali ndani ya nchi zao.

Tuisapoti michezo michezo ni mwokozi mkubwa Kwa maisha ya vijana kimaisha bora

Michezo ni chanzo kikubwa Cha ajira ikiwekwa vizuri miaka ijayo kumi mpka mitano serikali itapunguza kama sio kumaliza kabisa tatizo la ajira Kwa vijana wasomi na wasio wasomi.
 
Upvote 2
Basketball: ni mchezo unao chezwa ulimwenguni kote unatoa mabilionea pia unachezwa na vijana Rika lote wasomi na wasio wasomi serikali ikiboresha huu mchezo ukawa kila mikoa Ina timu au Kuna ligi ya timu nyingi za mpira wa kikapu vijana wengi watajiajiri humo
Mchezo wangu pendwa.

Tuisapoti michezo michezo ni mwokozi mkubwa Kwa maisha ya vijana kimaisha bora

Michezo ni chanzo kikubwa Cha ajira ikiwekwa vizuri miaka ijayo kumi mpka mitano serikali itapunguza kama sio kumaliza kabisa tatizo la ajira Kwa vijana wasomi na wasio wasomi.
Na bila kusahau kuwa, kwa kuwa michezo ni sehemu ya starehe, kumbe basi kuinua uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla kutawezesha michezo kiotomati. Hiyo ni kwa sababu watu wengi watakuwa na pesa za kuspend kwenye michezo na burudani mahitaji ya msingi yakishakamilika.
 
Back
Top Bottom