Kumbuka kwenye dirisha la Januari, Klopp alitumia Pauni 75 milioni kupata huduma ya beki wa kati, Virgil van Dijk, kuja kucheza na Joel Matip, aliyembeba bure kabisa, Joe Gomez aliyenaswa kwa Pauni 3.5 milioni kutoka Charlton Athletic na Andrew Robertson aliyenaswa kwa Pauni 10 milioni kutoka Hull City.
Kisha Klopp akawanunua viungo wa kuwalinda mabeki wake hao, Naby Keita kwa Pauni 52.75 milioni kutoka RB Leipzig na Fabinho kutoka AS Monaco. Lakini, Mbrazili Fabinho bado hajaanza kutumika.
Klopp ameona pesa inalipa na mkwanja mrefu aliotumia kwenda kutengeneza safu yake ya ulinzi, umelipa pia. Kwenye Ligi Kuu England, kikosi hicho cha Anfield kimecheza mechi tatu, ugenini na nyumbani, lakini kwa mabeki waliotumika hadi sasa, hawajaruhusu bao lolote kwa dakika 270 walizocheza.