Michezo(Tetesi & Usajili).

Michezo(Tetesi & Usajili).

niyo%2Bpic.jpg

Dar es Salaam. Haruna Niyonzima anakiri kwa sasa hana furaha ndani ya Simba kwa vile hachezi, ila anafichua pia hakuondoka Jangwani kwa ugomvi hivyo kama klabu yake hiyo ya zamani itamtaka hana noma kurejea tena kikosini kupiga mzigo.
Kiungo huyo fundi alisema kilichomuondoa Yanga ni kushindwana masilahi, lakini hata leo wakitaka kumrejesha kwa kile alichokuwa akikitaka hana kinyongo kutua Jangwani kwani ni klabu anayoiheshimu na aliyoitumikia kwa mafanikio.
 
Niyonzima alijiunga Simba msimu uliopita akitokea Yanga mara baada ya kushindwa kufikia makubaliano ya kuongeza mkataba mpya na klabu yake ya zamani na kufanya maamuzi ya kujiunga na timu hiyo.
Akizungumza na Mwanaspoti, Haruna alisema Yanga amecheza kwa mafanikio makubwa na ndio timu aliyocheza misimu mingi zaidi anaiheshimu na anaamini sikuikitokea nafasi ya kucheza tena anaweza kufanya ivyo kwasababu hakuondoka kwa ugomvi.
"Kwasasa ni mchezaji wa Simba kwasababu nina mkataba nao lakini pia naiheshimu Yanga kwasababu imenipa mafanikio makubwa siwezi nikasema Simba nimefika na ndio nitakapomalizia maisha yangu ya soka lakini kwa upande wa Tanzania kama ntashindwa maisha ya Simba na nikapata nafasi timu nyingiune basi iwe ni Yanga,"alisema.
 
Niyonzima alisema mpira ndio maisha yake hivyo hawezi kuchagua timu ya kucheza kambi ni popote kikubwa anachokiangalia ni pesa na aliweka wazi kuwa alikuwa anatamani sana kubaki Jangwali lakini kutokana na kushindwa kufikia makubaliano ndio sababu iliyomuondoa kikosini hapo.
"Yanga wangenipa pesa niliyokuwa nahitaji sizani kama ningekuwa Simba nipo hapa kwasababu tulifikia makubaliano japo kuna baadhi ya matatizo yaliyopo baina yangu na uongozi yanayonifanya nisicheze ila mimi ni mchezaji wa Simba," alisema.
MAISHA YAKE SIMBA
"Sina maisha ya furaha katika timu yangu kwasababu sipati nafasi ya kucheza tofauti na maisha niliyokuwa nayo Yanga, nilikuwa na furaha kwasababu nilikuwa muhimu katika kikosi cha kwanza nilikuwa nacheza dakika zote ninazotakiwa kucheza siwezi nikasema ninamaisha mazuri Simba wakati sipati nafasi ya kucheza," alisema.
 
Niyonzima aliweka wazi kuwa yeye ni mchezaji wa Simba lakini hayupo katika kikosi cha wachezaji wa timu hiyo kutokana na matatizo yaliyopo baina yake yeye na uongozi ambayo hakutaka kuyaweka wazi.
Alisema hawezi kuweka wazi tatizo hilo litabaki kuwa siri yake yeye na uongozi huku akiongeza kuwa ndio sababu iliyomfanya aweze kuchelewa kujiunga na timu na kuongeza kuwa hatua ya mazungumzo kuhusiana na tatizo hilo limefika sehemu nzuri muda wowote watakapolikamilisha atajiunga na timu.
"Najua kuna mashabiki wamenimisi na wanatamani kuniona nikicheza napenda kuwaambia kuwa wataniona saizi wasubili nimalizane na uongozi mambo yakiwasawa nitacheza," alisema Niyonzima.
 
jicho%2Bpic.jpg


Dar es Salaam. Mtindo wa ushangiliaji wa kuziba jicho mmoja wa mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere umeanza kuteka hisia za mashabiki wake.
Kagere alianza kufanya hivyo katika mashindano ya Kombe la Kagame ambapo Simba ilimaliza mshindi wa pili, huku Azam FC ikitetea ubingwa wa taji hilo, alikuwa akifunga bao anajiziba jicho moja, wakati mwingine anatembea kama ameshika mkongojo.
 
Baada ya juzi Jumatatu Kagere kuifungia timu yake mabao 2-0 dhidi ya Mbeya City, mashabiki Simba walianza kuigiza mtindo wake ya kuziba jicho moja, huku wakiungana naye katika furaha yake.
Katika pita pita mtaani Mwanaspoti limebaini namna mtindo huo ilivyopata umarufu kwani katika vijiwe utawasikia ukimuona Kagere kaziba jicho moja ujue Simba imeralua mtu.
Mwanaspoti imewahi kumuuliza Kagere kuhusiana na aina hiyo ya ushangiliaji, aliifafanua kuwa akiwa na furaha na hasa akatimiza malengo yake uwanjani basi furaha yake anaiwasilisha kwa staili hiyo.
"Napenda kufanya kazi nzuri na zenye viwango vya juu, mtindo zangu zote ninazoshangilia ndani yake zinakuwa zimebeba furaha, sipendi kufanya kazi kwa ulegevu," alisema Kagere.
 
nevilee%2Bpic.jpg

London, England. Siku za Jose Mourinho kubaki Manchester United zinahesabika na huenda akatupiwa virago kabla ya Sikukuu ya Krismasi.
Nahodha wa zamani wa Man United, Gary Neville amesema Mourinho anapitia kipindi kigumu katika maisha yake ya soka.
“Angalia sidhani kama ana kikosi cha kwanza cha wachezaji 11 bora. Amekuwa na mfumo wa kubadili kikosi kila mchezo,” alisema mchambuzi huyo wa soka.
Neville alisema Man United imeyumba muda mrefu na haina uwezo wa kutosha kushindana na timu zenye kikosi imara kama Tottenham Hotspurs.
 
Kipigo cha mabao 3-0 ilichopata Man United katika mchezo wa juzi usiku dhidi ya Tottenham Hotspurs kimemuweka kwenye mazingira magumu.
Mourinho anapewa asilimia 10/11 kubaki Old Trafford baada ya kupoteza mechi mbili za Ligi Kuu England msimu huu.
Kipigo cha nyumbani Old Trafford kitamuweka matatani kocha huyo wa zamani wa timu za FC Porto, Inter Milan, Real Madrid na Chelsea.
Kocha wa zamani wa Real Madrid, Zinedine Zidane anapewa nafasi ya kuchukua mikoba ya Mourinho akifuatiwa na Mauricio Pochettino anayeinoa Spurs.
Mourinho ameibua mzozo na vigogo wa Man United baada ya kunyimwa fedha za kufanya usajili wa nyota wapya majira ya kiangazi.
Hiki ni kipigo cha pili kwa Man United baada ya mchezo uliopita kulala mabao 3-2 dhidi ya Brighton na kuweka rekodi ya kupoteza mechi mbili za mwanzoni mwa msimu tangu mwaka 1992.
Man United inatarajiwa kumenyana na Burnley Jumapili wiki hii.
 
maisha%2Bpc.jpg

MAISHA ndivyo yalivyo. Unahitaji kuwa na pesa kufanya unachotaka kukifanya. Kawaulize Liverpool watakuthibitishia hilo.
Mwaka jana walitumia Pauni 34.3 milioni kunasa huduma ya Mohamed Salah kutoka AS Roma, akawafungia mabao 36 kwenye mechi 40 tu. Yalikuwa matumizi mazuri ya pesa, ambayo kimsingi ndiyo yaliyokuwa makubwa zaidi kutumika kwa mchezaji mmoja katika kikosi hicho chini ya Kocha Jurgen Klopp.
 
Mo Salah ameleta mambo matamu, Liverpool imefika hatua ya fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya na kama si makosa ya kipa wake, basi mambo yangekuwa mengine kabisa katika fainali hiyo iliyocheza dhidi ya Real Madrid.
Kuona hivyo, kwenye dirisha la uhamisho wa majira ya kiangazi ya mwaka huu, Klopp ameamua kuingia zake sokoni na kutumia pesa nyingi tena kutafuta kile anachokitafuta. Akamnasa kipa Alisson Becker kutoka AS Roma kwa ada ya Pauni 67 milioni, kulifanya goli la timu hiyo kuwa salama tofauti na ilivyokuwa wakati wa Loris Karius.
 
Kumbuka kwenye dirisha la Januari, Klopp alitumia Pauni 75 milioni kupata huduma ya beki wa kati, Virgil van Dijk, kuja kucheza na Joel Matip, aliyembeba bure kabisa, Joe Gomez aliyenaswa kwa Pauni 3.5 milioni kutoka Charlton Athletic na Andrew Robertson aliyenaswa kwa Pauni 10 milioni kutoka Hull City.
Kisha Klopp akawanunua viungo wa kuwalinda mabeki wake hao, Naby Keita kwa Pauni 52.75 milioni kutoka RB Leipzig na Fabinho kutoka AS Monaco. Lakini, Mbrazili Fabinho bado hajaanza kutumika.
Klopp ameona pesa inalipa na mkwanja mrefu aliotumia kwenda kutengeneza safu yake ya ulinzi, umelipa pia. Kwenye Ligi Kuu England, kikosi hicho cha Anfield kimecheza mechi tatu, ugenini na nyumbani, lakini kwa mabeki waliotumika hadi sasa, hawajaruhusu bao lolote kwa dakika 270 walizocheza.
 
Klopp amewatumia mabeki wake wote na hakika wameonyesha mpira upo kwenye pesa kutokana na kikosi hicho cha Anfield kutoruhusu mpira wowote kwenye wavu wake huku washambuliaji wake kina Mo Salah na Sadio Mane wakitupia kwenye nyavu za wapinzani mara saba hadi sasa. Wakaki unasoma hapa, Liverpool ndio inayoongoza msimamo wa Ligi Kuu England kwa kukusanya pointi tisa kwenye mechi tatu, mabao saba ya kufunga na haijafungwa bao lolote.
Hii imeonyesha mpira wa sasa upo kwenye pesa, uwekezaji wa kutumia pesa nyingi kwenye beki wa kati na kipa umeleta matunda huko Anfield baada ya kucheza kwa dakika 270 kwenye Ligi Kuu England hadi sasa na haijafungwa bao lolote.
 
jeventus%2Bpic.jpg


Rome, Italia. Cristiano Ronaldo amefanya mazoezi ya aina yake akiwa na matumaini ya kufunga bao lake la kwanza kwa ‘Kibibi Kizee’ cha Turin Juventus, Jumamosi wiki hii.
Ronaldo ameonekana akifanya mazoezi magumu ya kupiga mashuti na kuruka kupiga mipira ya kichwa ikiwa ni maandalizi ya kuikabili timu iliyorejea Ligi Kuu Italia Parma.
Mshambuliaji huyo hajafunga bao katika mechi mbili za Ligi Kuu Italia msimu huu tangu alipojiunga na Juventus akitokea Real Madrid majira ya kiangazi.
 
Mshambuliaji huyo hajafunga bao katika mechi mbili za Ligi Kuu Italia msimu huu tangu alipojiunga na Juventus akitokea Real Madrid majira ya kiangazi.
Baadhi ya wachezaji wa Juventus walioshindwa kufunga bao katika mechi mbili za awali, walionekana kuiga mbinu za nguli huyo wa zamani wa Manchester United.
Licha ya Juventus kushinda mechi hizo, Ronaldo aliyenunuliwa kwa Pauni88 milioni, hakufunga bao katika mashindano hayo.
Ronaldo alikosa bao katika mchezo ambao Juventus ilishinda mabao 2-0 dhidi ya Lazio wiki iliyopita na baadhi ya wadau wa soka wamedokeza nyota huyo hana furaha.
Awali, katika mchezo wa ufunguzi wa ligi hiyo Juventus ilishinda mabao 3-2 ilipovaana na Chievo.
Juventus ilianza kujinoa Jumatatu kujiandaa na mchezo dhidi ya Parma na baadhi ya nyota wake akina Douglas Costa, Daniele Rugani na Leonardo Bonucci walionyesha viwango bora.
 
Karius: Klopp wanted me to stay

Loris Karius says Jurgen Klopp was keen to keep him at Liverpool this season before sanctioning his loan move to Besiktas.
 
Back
Top Bottom