Michezo ya Olympic Tanzania inatia aibu

Michezo ya Olympic Tanzania inatia aibu

gimanini

JF-Expert Member
Joined
Jun 20, 2015
Posts
1,798
Reaction score
1,857
Juzi michezo ya Olympic imeanza rasmi, tumeshuhuhudia nchi nyingi zikiwatuma wanamichezo wengi, lakini sisi Tanzania tumewakilishwa wachezaji wachache, kuna michezo mingi ambayo tunatakiwa kujiandaa na kushinda, mfano kulenga shaba, kurusha mikuki, kisahani, hata mieleka, ni aibu kama watanzania kushindwa kuwakilishwa katika michezo na wanamichezo mbalimbali huko RIO.
 
Michezo si kipaumbele kwetu...kipaumbele ni viwanda...acha kulalamika....fanya kazi kijana
 
Kila kitu mnailaumu serikali huku wazazi wenyewe hamziheshimu ndoto za watoto wenu katika michezo.....

Kila mzazi anataka mtoto wake awe daktari, mhandisi , karani n.k
..
Hao wanamichezo tutawapata wapi
 
Mchezo wetu sisi ni mmoja tu!!! Na hakuna duniani anaetushida!!!! Waweke uwanja wa vitanda uone!!!! Hata washirik watakua wengi na watajilipia mpaka nauli!!! Na medali haazita tosha!!!!
Hahahahahaha
 
Kila kitu mnailaumu serikali huku wazazi wenyewe hamziheshimu ndoto za watoto wenu katika michezo.....

Kila mzazi anataka mtoto wake awe daktari, mhandisi , karani n.k
..
Hao wanamichezo tutawapata wapi
Sasa mzazi anamuhamasishaje mtoto wakati viwanja vya michezo hamna open space zimeuzwa na kujengwa maghorofa na nyumba za starehe
 
Mchezo wetu sisi ni mmoja tu!!! Na hakuna duniani anaetushida!!!! Waweke uwanja wa vitanda uone!!!! Hata washirik watakua wengi na watajilipia mpaka nauli!!! Na medali haazita tosha!!!!
Huyo mchezo wa vitanda ukoje? Naomba ufafanuzi tafadhari
 
Sasa mzazi anamuhamasishaje mtoto wakati viwanja vya michezo hamna open space zimeuzwa na kujengwa maghorofa na nyumba za starehe
Penye nia pana njia lakini ukweli utabakia palepale....

Wazazi wa kitanzania hawaheshimu vipaji vya watoto wao...
 
Juzi michezo ya olimpiki imeanza rasmi,tumeshuhuhudia nchi nyingi zikiwatuma wanamichezo wengi,lakin sisi Tanzania tumewakilishwa wachezaji wachache,kuna michezo mingi ambayo tunatakiwa kujiandaa na kushinda,mfano kulenga shaba,kurusha mikuki,kisahani,hata mieleka,ni aibu km watanzania kushindwa kuwakilishwa ktk michezo na wanamichezo mbalimbali huko RIO.

Wewe umejiandaa kwa mchezo gani kati ya hiyo uliyotaja au umekazana kugonga keyboard?
 
Hata siasa ingewepo kwenye Olimpic tusingeweza ku-qualify kushiriki, angalia siasa zetu zilivyo ni za majungu, kulindana, uadui baina ya vyama na mtu mmoja mmoja, kutishana kwa nguvu ya dola, teuzi zenyewe ni za utata, kauli za mtu 1 ndio zinaongoza Taifa badala ya Katiba.
Kweli kabisa mkuu,hata sijui Tanzania tunaweza nini sasa.
 
Michezo si kipaumbele kwetu...kipaumbele ni viwanda...acha kulalamika....fanya kazi kijana
Viwanda tulishachemka tokea enzi!
Hebu taja viwanda vitatu ambavyo ndio kipaumbele chetu na ni kwa jinsi gani vimewanufaisha wananchi walalahoi!
Acha kuendeshwa na mihemko ya kisiasa!
 
Yetu ngono bwana ,kuogelea,sijui mikuki na visahani havituhusu
 
Nchi ya ajabu Sana, riadha haitakaa iendelee kamwe kabisa, kuna tatizo kwa Viongozi wa huu mchezo kubebana na kuweka watu wasio na sifa badala ya kutafuta vipaji vizuri. Ukiangalia walioenda huko Brazil ni wale wale failure wa miaka yote. Najiuliza hivi hakuna vipaji vipya? Tumeshindwa kabisa kutafuta vipaji vipya? Hao wameenda kutalii tu.
 
Mchezo wetu sisi ni mmoja tu!!! Na hakuna duniani anaetushida!!!! Waweke uwanja wa vitanda uone!!!! Hata washirik watakua wengi na watajilipia mpaka nauli!!! Na medali haazita tosha!!!!
Duh, unawajua mandingo tribe?,
 
Yetu ngono bwana ,kuogelea,sijui mikuki na visahani havituhusu
Mchezo wetu sisi ni mmoja tu!!! Na hakuna duniani anaetushida!!!! Waweke uwanja wa vitanda uone!!!! Hata washirik watakua wengi na watajilipia mpaka nauli!!! Na medali haazita tosha!!!!

ila sio kwa wanaume wa dar nao watatuaibisha
 
Ndiyo wakati Mwafaka wa kuanzisha Michezo mbali mbali hapa nchini
 
Back
Top Bottom