Michezo ya Olympic Tanzania inatia aibu

Ma bounser wote wanalinda kwenye club za usiku,hatuna hata mrusha mkuki kweli!
Wizara ya michezo ijiongeze kwa kweli.Hatujawa wachovu kiasi hicho,kuna viongozi hawatekelezi majukumu yao ipasavyo
 
Hii ndio olimipiki tanzania itakwenda kushiriki!!! So usijali mtoa mada!!!! Na washiriki watakua wengi sana

 
Asa kama hata TV zimeshindwa kuonesha ufunguzi tu hiyo hamasa itoke wapi yani kila station imeng'ang'ania tamthiliya,music,na mavipindi ya kina lady haha na sijui nani ,na hili li Startimes linangoja makombe ya saa kumi usiku ndio waoneshe pumbavu sana TV station zote hasa TBBsi.
 
Sisi wataalam wakukimbizana na michepuko bahati mbaya haijachaguliwa kuwa mojawapo ya michuzo ya Olympic [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Serikali mchezo pekee ambayo ndio imejitahidi kuwekeza japo na penyewe ni kwa kujivuta vuta ni mpira wa miguu, ama hakika kwa uwekezaji uliyofanywa kwenye football kipindi cha JK kama isingekuwa magumashi,kujuana juana kwingi, siasa michezoni pamoja na upuuzi mwingine mwingi basi leo hii tungekuwa level moja na taifa kama la Ethiopia na hata hii michuano ya olympic mwaka huu bila shaka tungekuwa na timu ikituwakilisha.

Kwa bahati mbaya sana kwenye soka tumeshindwa na hatuoneshi kuwa na interest na michezo mingine kama ilivyo kwenye mpira na ndio maana hakuna uwekezaji wowote wa maana unaolenga kuibua na kuendeleza vipaji kwenye michezo kma kikapu,ndondi,mbio ndefu,karate,mieleka,kuogelea,tenesi n.k.
 
Tanzania haitii aibu bali inavuna ilichopanda, jiulize kama mtanzania umeshiriki vipi kwenye maandalizi yaliyotuletea mavuno haya?
 
Kila kitu mnailaumu serikali huku wazazi wenyewe hamziheshimu ndoto za watoto wenu katika michezo.....

Kila mzazi anataka mtoto wake awe daktari, mhandisi , karani n.k
..
Hao wanamichezo tutawapata wapi
Sasa mzazi kama una akili timamu unaweza kumshaur mwanao awe mwana michezo kwenye nchi ambayo simba leo inaadhimisha miaka 80 bado haina hata swimming pool ya mazoezi.
Yanga nayo inakodiwa kama ukumbi wa sherehe, mpitlra unaishia kigamboni.

ukimshauri mwanao akazane atimize ndoto zake ktk michezo ktk nchi hii mzazi unapaswa upimwe akili kama iko sawa sawa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…