aleesha
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 798
- 1,178
Wakati mmoja kulikuwa na mazungumzo mengi juu ya Stars na uwakilishi hafifu wa Zanzibar. Zikaja kelele kuwa wanaojadili hili ni kuchanganya mchezo na siasa. Wazanzibari hawa utashangaa kama kweli walifurahia gani kukubaliwa kwefu CAF wakati ule au walifurahishwa zaidi CAF ilipoondosha uanachama wetu.
DAB
Lakini Mungu ni mkubwa zaidi, siku niliposikia anapelekwa DAB kuwa ndie mjumbe mkuu mhamasishaji wa serikali kwa Stars, nikajuwa mara hii watanzania kwa makusudi watagawiwa kirahisi kabisa kwa sababu ya udhaifu wa fikra wa huyu aliepelekwa. Haiyumkini kummurika DAB pekee bila kujiuliza zaidi uelewa na ufaham wa aliempeleka.
Uwaze
Yapaswa pia ufikiri zaidi kuwa kwa muda mchache wa majivuno ya Bashite hadharani huku akiwabughudhi wengine, Stars ikawa na wapenzi wachache waliotamani wasonge mbele. Na mara hii haikuwa wale wakawaida wazenj wanaolalamika uwakilishi mdogo katika suala ambalo si sehemu ya Muungano, bali watanganyika waliofikwa shingoni na uwepo wa huyu kijana na mdomo wake ulioshiba kero, dharau, ubabe na unafik usio mithilika.
Somo
1. Mungu kawaumbua wanafik wanaopiga kelele kubwa za siasa na michezo kuchanganywa wakati Zanzibar inapojadili uwakilishi wake mdogo kwenye michezo nje na ndani. Maana kwa mara ya kwanza Bashite kafungua hasa maana halisi ya siasa na michezo kwa kuiwekea Stars mzigo wa ilani ya chama, kuwa ni milki ya CCM na hasa kuwa ushindi wake ni ushindi wa CCM.
2. Hio ndio siasa na michezo na sio wanaojadili haki ya uwakilishi dhaifu wa mmoja hasa katika jambo ambalo si sehemu ya yaliomo kwenye kapu la Muungano. Michezo huwa sehemu ya utambulisho wa nchi, ustaarabu wake, historia yake. Halkadhalika mafanikio yake ni lazima michezo ibebe umoja, haki na ishara ya matarajio mema. Bashite kaudhihirisha ulimwengu namna ya nchi ilivyogawanyika sababu ya kufikiri nguvu, kibri, majivuno na mdomo ni fanaka.
3. Vile vile kwa Zanzibar, uwepo wa nchi unaendeana moja kwa moja na uwakilishi wa nchi husika katika mashindano nje. Hapa ndipo ile “Symbol” ya jamii, ustaarabu wake, mafanikio na historia yake yanapowekwa bayana na uwepo wa nchi kubainika. Na hivyo kelele za Zanzibar kujiwakilisha yenyewe haziwezi kuisha hasa pale inapoamini kuwa ni nchi inayobaki kuwa nchi ikiwa na mipaka ya yepi ya Muungano na yepi ya kwake mwenyewe. Hio si michezo na siasa bali mjadala kuhusu haki ya kushiriki au kujumuishwa kushiriki na kwa formula gani.