Michuano hii kinachotakiwa ni point 3 muhimu lakini kocha wa Simba ajiangalie kwa mbinu zake nilishasema kuna kilio kinakuja asipobadilika!

Makavuli

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2024
Posts
1,425
Reaction score
1,829
Mbinu za uyu kocha ni zile zile abadiliki nilikwishasema kwenye bandiko langu lililopita nilipomfatilia kwenye mechi 5 zilizopita za ligi,,anapokutana na kocha anayecheza kimbinu anapata tabu sana!

Dk zote 90 ukiondoa goli la penalty ambalo na lenyewe lilisababishwa na makosa binafsi ya beki wa Bravos akuna cha maana walichofanya Simba kimbinu!

Kocha wa Bravos na timu yake wajilaumu wao wenyewe kutoondoka na alama Leo hii nafikiri kukosa uzoefu kumechangia kukosa matokeo wametengeneza nafasi ikiwemo mkwaju wa penalty wameshindwa kutumia!

Lakini pia kwa anayeangalia Mpira kiufundi na sio matokeo nafikiri atakuwa ameona mipira inayopigwa katikati ya mabeki wa Simba imekuwa inawapa shida kubwa sana na sio kwenye mechi hii tu bali kwenye mechi zote walizocheza karibu 5 tatizo Limekuwa ni hilo!

Angalia upangaji wa kikosi wa Simba na sub zake utapata majibu!

Soma Pia: Full time: Simba SC 1 - 0 Bravos do Maquis FC | CAF CC | Benjamin Mkapa Stadium | 27-11-2024


Uwezi kuwa unategemea magoli ya penalty tu ndio yakuokoe Kuna siku utopata iyo penalty utafanyaje!

Second half Simba inakata upepo zile beki za kulia na kushoto kapombe na Tshabalala ni majanga inawezekana ni Umri umewatupa mkono lakini wanakata moto sana!

Tunaendelea kuwakumbusha kocha wenu asipobadilika kimbinu Kuna jambo litawakuta muda sio mrefu!
 
Kama yanayowakuta wenzetu midomo fc
 
Kocha wa simba mpumbavu sana, anamuacha Mavambo na Ateba nje wakati hii mechi alitakiwa atoke na matokeo makubwa. Shenzi sana
Huo ni Mpira uwezi kuingia na matokeo utaumbuka afu mbona kwenye Mpira tupo wengi sana kila mtu anataka kuongelea ? ivi hamna burudani zingine wengine mkaongelee zungumzieni hata vigodoro na Ngoma za asili huku kwny football waacheni wanaojua
 
Mkuu simba bado inatengeneza kikosi, hayo yote unayosema upo sahihi kabisa. Usajili wa simba msimu huu ni takataka kabisa yani Hao kina Fernandez, Ahoua, mutale ni wachezaji wa kawaida sana makosa mengi sana sidhani kama wanaweza kuifikosha simba inapotaka pia kapombe na zimbwe washachoka kabisa.
 
Kocha wa simba mpumbavu sana, anamuacha Mavambo na Ateba nje wakati hii mechi alitakiwa atoke na matokeo makubwa. Shenzi sana
Unajua kwa mashabiki wasiojua Mpira ndio watashupaza shingo lakini uyu kocha wenu kimbinu ni mweupe sana mtakuja kuukubali huu ukweli uko mbeleni,,aiwezekani kocha unaenda mechi ya 8 na mbinu zile zile,,alikuwa anasema muunganiko bado lakini keshacheza mechi kibao na mbinu zake zile zile kauka nikuvae!
 
Tulia timu ya Taifa imeshinda na Tanzania yote ina furaha baada ya ubaya ubwela kufedhehesha wananchi
Imeshinda kwa pira makande pira la kuomba mechi iishe na upo nyumbani kwako🤣🤣
 
Wewe ni mtaalam ambaye inabidi jf sport tukuheshimu kwa simba hii isipobadilisha kocha Robo hatuchezi yaani inaonekana anakariri alichojifunza kwenye kozi ya ukocha hana Akili ya kujiongeza kama kocha nilikuwa sielewi kwa nini kwenye kazi waajiri wanataka uzoefu huyu kocha hastahiri kuendelea na kibarua chake pale Simba hamuwezi kumsifia golikipa kwenye mechi ya nyumbani tena dhidi ya timu kaliba ya Bravo.
 
Kila timu ilipata penati nakubaliana na wewe kitu kimoja huyu kocha akipata goli moja anaridhika mapema .
 
Mkuu shida sio kutengeneza kikosi kwani kocha kacheza mechi ngapi mpaka sasa na anao muda Gani kwenye timu? Lakini pia tungeona basi mbinu zake zinabadilikabadilika kulingana na timu wanayocheza nayo lakini mkuu hilo alipo kwa kocha uyu kama utakuwa na jicho la kuwafatilia Simba kimbinu na kiufundi utakubaliana na Mimi!
 
Huu ushauri ungeutoa kwa kocha wa utopolo ambaye hana point wala goli la penati
 
"Kocha wa Bravos na timu yake wajilaumu wao wenyewe kutoondoka na alama Leo hii nafikiri kukosa uzoefu kumechangia kukosa matokeo wametengeneza nafasi ikiwemo mkwaju wa penalty wameshindwa kutumia!"

Hii paragraph imeshiba.
 
Kila timu ilipata penati nakubaliana na wewe kitu kimoja huyu kocha akipata goli moja anaridhika mapema .
Lakini mkuu ebu ifatilie Simba kwenye mechi 6 zilizopita aina yao ya uchezaji kimbinu utakuja kuikubali hoja yangu,,
Nadhani ni mbinu za kocha ndio zinawaangusha pakubwa,,uliona yanga walianza hivi hivi kigoli kimoja kimoja lakini walikuwa wanakipata kwa shida kumbe ndio walikuwa wanaelekea shimoni hivyo hivyo kilichofata unaona wanakipata stahili yao!
 
Imeshinda kwa pira makande pira la kuomba mechi iishe na upo nyumbani kwako🤣🤣
We utopolo mbona unahangaika na timu yetu lakini? Jana tuu umetoka kulitia aibu taifa🤣🤣 huo ushauri wapelekee kina Aziz k na pacome waache kucheza kama walevi shisha zitawaua na huyo dube k vant zitamuua mechi nzima ni kuanguka tuu, SIMBA NGUVU MOJA.
 
Nyumba yako imeungua unajifanya unajari kwa jirani,haya mliocheza vizuri jana mna point ngapi?
 
Huu ushauri ungeutoa kwa kocha wa utopolo ambaye hana point wala goli la penati
Sawa Haina shida mashabiki aina yenu wapo wengi na Wala uwezi kunizuia kusema nilichokiona
 
Endeleeni kutuita 'tusiojuampira', sisi Kikubwa tumeshinda
 
Sawa Haina shida mashabiki aina yenu wapo wengi na Wala uwezi kunizuia kusema nilichokiona
Hauna nguvu za kushauri walioshinda, wakati jana tu ulikuwa miongoni mwa mashabiki walioangua kilio mbele ya camera za youtube TVs
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…