Michuano ya AFCON ya 2025 imesogezwa mbele mpaka Januari 2026

Michuano ya AFCON ya 2025 imesogezwa mbele mpaka Januari 2026

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) limeahirisha rasmi michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 na badala yake itafanyika Januari 2026.

Uamuzi huu umefanywa ili kuepusha mgongano wa ratiba na Kombe la Dunia la Vilabu la FIFA, linalotarajiwa kuanza Juni 15 hadi Julai 13, 2025, nchini Marekani.

Tarehe za awali za AFCON zilikuwa Juni 2025, hivyo Kupangwa upya huku kunamaanisha kuwa AFCON na Kombe la Dunia la FIFA 2026 zitafanyika mwaka huo huo, tofauti ikiwa ni miezi sita pekee.
 
Hakuna shida ila naona litakaribiana sana na lile la hapa kwetu 2027 au huenda wakasogeza mbele hadi 2028 ila ukweli Afcon ratiba zake zinageuka geuka sana ni kama hakuna watu makini kwenye kitengo Cha mipango
 
Kumbe ubabaishaji ni jambo la kawaida sana kwenye mashirikisho ya mpira wa miguu. Mwanzoni nilifikiri ni TFF yetu pekee ndiyo imejaa huo ubabaishaji.
 
Back
Top Bottom