Michuano ya CECAFA Kagame cup ibadilishwe jina

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Wakati dunia ya leo inapinga udikteta bado nchi za Africa Mashariki na ya kati zinaukumbatia kufa na kupona !

Ni nani hapa jf na kwingineko asiyeufahamu udikteta wa Kagame , kwanini mmenyamazia michuano ya vilabu vya nchi hizi kutukuza jina lake ?

Natoa wito kwa Musonye na viongozi wengine wa cecafa kuondoa jina la Dikteta Kagame haraka sana na kurejesha jina halisi la michuano hii , njaa isiwe kisingizio .

Naomba kuwasilisha
 
Unafikiri jina limekaa bure mkuu? Jamaa ndio mdhamini mkuu wa hayo mashindano. Ilichukua muda mrefu kumpata mdhamini,ndo PK akajitokeza kuokoa jahazi.
Mitizamo yetu ya kisiasa isitufanye tuwe vipofu wa baadhi ya mazuri ya PK.
 
Mzee muda wote unawaza siasa wengine haturi hizo siasa zinazowalisha nyinyi.
 
Unafikiri jina limekaa bure mkuu? Jamaa ndio mdhamini mkuu wa hayo mashindano. Ilichukua muda mrefu kumpata mdhamini,ndo PK akajitokeza kuokoa jahazi.
Mitizamo yetu ya kisiasa isitufanye tuwe vipofu wa baadhi ya mazuri ya PK.
Ugaidi wa dunia unafadhiliwa kwa fedha nyingi mno lakini unapigwa vita kila kukicha , njaa isituvue nguo
 
Aidha jina lilitoka kwa mkataba ama cecafa wametoa kwa heshima na shukrani kwa mh PK
Kagame ndio mdhamini unategemea nini..
"Baniani mbaya kiatu chake dawa"

Ligi kuu tanzania ilikuwa inaitwa vodacom premier league kipindi voda mdhamini
Uingereza huko carling cup aimekuwa carabao cup
Ligi yao ilikuwa inadhaminiwa na Barclays nadhani jina la ligi ulikuwa unalijua sasa haina mdhamini inaitwa EPL
Nadhani kule COSAFA
Wana michuano inaitwa CASTLE
S.A kuna michuano inaitwa nedbank
Etc

Hakuna jinsi labda aje mdhamini mwingine au kagame mwenyewe achague jina jingine, maana CECAFA hawawezi kubadili jina kienyeji tu.
 
Cecafa ni yetu , tuiokoe dhidi ya madikteta
 
Haya masiasa mimi siyapendi!! Yaani tusione mazuri sababu ya ulaji wa mtu khaaa! Hapana bana sisi tunajua umuhimu wa michuano hii so hatutoingiza siasa, kwa mfano tukimtoa kagame utadhamini wewe haya mashindano? Yaani upo radhi kitu kizuri kiharibike afu huna ushauri wowote wa nini kifanyike kama akiondoka mdhamini!! Nenda cecafa ukiwa na dau au mtafute mwenye sau zito akadhamini na sio kupandikiza watu chuki ili wewe ushibe
 
Mkuu PK hana dogo atatuma majasusi wake wakudedishee!
 
Kagame anatakatisha pesa kupitia michezo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…