Michuano ya CHAN yasogezwa mbele hadi mwezi August, 2025

Michuano ya CHAN yasogezwa mbele hadi mwezi August, 2025

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
Michuano ya CHAN ambayo ilipangwa kuanza kututuma vumbi kuanzia mwezi ujao Sasa imepigwa Danadana Mpaka mwezi August mwaka huu.

Miongoni mwa sababu za Ratiba hiyo ni kutokukamilika kwa baadhi ya miundombinu kwa nchi ya Kenya, Tanzania na Uganda.

Pia, CAF wametafuta Muda ambao mashindano yote yamemalizika katika Bara la Afrika.

Hii itapelekea wachezaji wengi kutokuwa na Muda wa kupumzika na hata Ligi kuu Tanzania Bara inaweza kurejea hivi karibuni.

Umepokeaje taarifa hii??
1736873995167.jpg
 
RAISI WA caf amehairisha michuano ya caf mpaka Aug na sio Feb kama iliivyokuwa mwanzon

Habari ZAIDI zinasema MH RAISI amesema ANAHITAJI michuano yenye utayari furaha na amani na sio SEHEMU Moja iwe tayari nyingine bado

HATA hivyoo amesema mpaka sasa Kenya wako asilimia 30 tuya maandalizi

Droo iliyopangwa kesho Iko palepale na MH RAISI amejipanga na changamoto za maswali
 
Mm mwenyewe nilikuwa najiuliza mbona sioni viwanja na miundombinu ya ko host hayo mashindano hapa Tanzania?
 
Kenya wametuponza....wako slow sana....; mwezi august alhaly wako clabu bingwa Dunia..na misri wapo chan .wataathirika sana
 
Mama katuponza .ameshindwa kukamilisha ujenzi wa viwanja badala yake amekazana kununua magoli Kwa milioni tano
 
Kiwanja cha Amani Zanzibar hakijamaliza hata mwaka Toka kitengenezwe, Motsepe na kamati zake walivyokuja kukikagua wakasema hakifai, sasa hivi wametoa makapeti Yao ya nyasi bandia kiwanja Kiko wazi unabaki unaniuliza Kwan mkandarasi aliyejenga Ina maana alitumia vigezo vya ZFF ama FIFA?
 
Wamekikataa kwakuwa kina nyasi bandia
 
Hizo timu za North Africa walishajitoa, ila Morocco walisema kama watashiriki wataleta timu ya under15
 
Kiwanja cha Amani Zanzibar hakijamaliza hata mwaka Toka kitengenezwe, Motsepe na kamati zake walivyokuja kukikagua wakasema hakifai, sasa hivi wametoa makapeti Yao ya nyasi bandia kiwanja Kiko wazi unabaki unaniuliza Kwan mkandarasi aliyejenga Ina maana alitumia vigezo vya ZFF ama FIFA?
Nashangaa watu wanalaumu Kenya walati hata Tanzania hatukuwa tayari. Uwanja wa Amani niliukataa ulivyofunguliwa tu kwenye ile Mapinduzi Cup ya kwanza nikasema lile kapeti ni low quality.

Uwanja wa Mkapa nao ni hivyo hivyo tu, maboresho ya kikanjanja ya watu ambao hawako serious.
 
Back
Top Bottom