Michuano ya CHAN yasogezwa mbele hadi mwezi August, 2025

Michuano ya CHAN yasogezwa mbele hadi mwezi August, 2025

Michuano ya CHAN ambayo ilipangwa kuanza kututuma vumbi kuanzia mwezi ujao Sasa imepigwa Danadana Mpaka mwezi August mwaka huu.

Miongoni mwa sababu za Ratiba hiyo ni kutokukamilika kwa baadhi ya miundombinu kwa nchi ya Kenya, Tanzania na Uganda.

Pia, CAF wametafuta Muda ambao mashindano yote yamemalizika katika Bara la Afrika.

Hii itapelekea wachezaji wengi kutokuwa na Muda wa kupumzika na hata Ligi kuu Tanzania Bara inaweza kurejea hivi karibuni.

Umepokeaje taarifa hii??View attachment 3201887
Waafrica tabu sana. Kweli sie bado wakutawaliwa tuu
 
Ngoja tusubiri press release ya bodi ya ligi kesho, najua ligi kuu inaendelea kuanzia J3
 
Sikuelewa hapo. Najua Tanzania+Kenya+Uganda wanaandaa CHAN 2027, imekuwaje ihairishwe kutoka 2024 ilhali ilikuwa imepangwa kufanyika 2027? Au wanazungumzia prelimineries ambazo zinafanyika nchi mbalilmbali za Afrika, siyo Tanzania+Kenya+Uganda tu.
 
AFCON ndio 2027
Chan ndio 2024/5

Moja ya vigezo ili tufanye afcon ilikuwa lazima tuandae chan
 
Back
Top Bottom