JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Michuano ya Mchezo wa Gofu ya Kilimanjaro Golf Tourney ‘Mount Kilimanjaro Klassic’ ambayo imepangwa kufanyika Arusha, wiki ijayo, imefutwa na wachezaji husika ambao walikuwa katika maandalizi ya mwisho kwa ajili ya kushiriki wamejulishwa.
Michuano hiyo ilikuwa itumike kama sehemu ya kutangaza utalii wa Tanzania kama ilivyofanyika mwaka jana na kuhudhuliwa na aliyekuwa Waziri wa Utalii, Damas Ndumbaro.
Waandaaji wa michuano hiyo ni International Sports Management (ISM) wakishirikiana na Tanzania Golf Union, sababu za kutofanyika kwa michuano hiyo haijawekwa wazi.
Barua ya kusitishwa kwa michuano hiyo imeeleza kuwa washiriki wote kila mmoja atapatiwa Dollar 1,000 ili kupunguza gharama ambazo watakuwa wameshatumia katika maandalizi yao kuelekea michuano hiyo ikiwemo gharama za hoteli, ndege n.k
Michezo hiyo ilikuwa imepangwa kuanza Aprili 7 na kumalizika Aprili 10, 2022
Source: TanzaniaTimes.net