Smt016
JF-Expert Member
- Jan 11, 2016
- 3,012
- 4,300
Leo droo imetoka kwa upande wa michuano ya klabu bingwa Africa na Kombe la shirikisho CAF. Binafsi naona uwezekano wa timu za Tanzania kufika mbali zaidi kwa kuweza kutinga hatua za makundi.
Upande wa Yanga, naweza sema wana mechi mbili ngumu na ugumu unakuja kwavile timu inayocheza nayo ni moja ya taifa lenye mafanikio kisoka tofauti na Tanzania. Inabidi wajipange sana ili kuweza kuwatoa ukizingatia wanaanzia nyumbani. Naona kabisa wakiwa serious mapema kwa maandalizi ya kimfumo (chemistry), kimbinu na kiutimamu wa mwili (match fitness) wanaweza kabisa kuwatoa hawa wanaijeria.
Mechi inayofuata wakiwatoa wanaijeria watakutana na timu kutoka Ethiopia ama Sudan ni mechi ambayo inaweza kuwa nafuu kwa Yanga hivyo kama watachanga vizuri karata zao watafuzu makundi bila shida.
Upande wa Simba
Pia naiona ikiingia makundi kwa mara nyingine tena
Mechi yao kati ya timu kutoka Botswana ama timu kutoka Africa ya kati ni mechi nyepesi sana kwa Simba kufuzu kwenda makundi.
Azam nao wana nafasi ya kufika mbali, wana mechi ngumu moja tu dhidi ya pyramid ila mechi yao ya kwanza dhidi ya Wasomali naona akifuzu.
Kwa Biashara pia nawaona wakivuka hatua ya awali na huenda ikawa ni timu ambayo inaweza ikafanya vyema zaidi ya Namungo walichokifanya msimu uliopita, kama tu watakuwa na morali nzuri.
Yote kwa yote tuziombee timu zetu zifanye vifuri na mwisho wa siku Tanzania tutawale soka la Africa kwa ngazi ya vilabu.
Viongozi na benchi la ufundi ni wakati wenu kutengeneza majingira mazuri na pia kutengeneza timu nzuri za kuweza kufanya Timu zetu ziingie makundi.
Kila la kheri