Microfinance: Nahitaji lending policy

Old Member (Retired)

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2012
Posts
3,401
Reaction score
1,610
Wakuu baada ya kutafuta microfinance kwa muda mrefu na kushindwana na wale wanaouza kwakuwa wao wamekuwa wakitaka ninunue pamoja na madeni wanaowadai wateja wao kitu ambacho sikuwa tayari na hilo kwakuwa uendeshaji wetu wa microfinance ni tofauti sana na uendeshaji wa watu wengi hivyo kununua madeni hayo ningejiingiza kwenye kazi ambayo sipo kuifanya kwasasa.

Sasa nilienda wizarani kuwasilisha maombi yangu ya kufungua microfinance na walinitajia vitu vya kuambatanisha katika maombi hayo, ninavyo vitu vyote isipokuwa lending policy.

Hivyo wadau naombeni mnisaidie sample ya lending policy ili mapema wiki hii nikasubmit application yangu japo wamesimama kutoa leseni za microfinance kwa muda.

Asanteni.
 
Kama unahitaji lending policy ambayo ni professional. Tutafute Anjoa kwa namba hizo hapo chini. Ushauri utatolewa bila malipo. Karibu sana.
 
Sasa naanza kuelewa umasikini wa waafrika ni UBINFSI NA UJINGA kwanini msiweke hapa maelezo ya kina kuhusu lending policy mnabaki kutoa na kutangaza biashara tu watanzania achene ubinafsi kama wa bibi zetu kushindwa kutufundisha uchawi wa kupaa na ungo
 
Watu wakae wadraft watengeneze na wawe wanazifanyia updates, we upewe Bure!!!! Ndio maana microfinance watu wanachemka wanashindwa. Biashara ya kukopesha si kutoa tu pesa hata kama unazo, unatakiwa upate consultant akupe ushauri general, akutayarishie policy na miongozo utakayoisimamia, akudraftie forms zote, mikataba etc.. We unataka upewe Bure duuh.. Wabongo msirahisishe mambo kila jambo Lina utaalamu wake.
 
Sasa we unadhani hicho unachokizungumza kinaugumu kama unavyoeleza wanawakamata wajinga tu kwakua hata ukienda hapo Blela utaelekezwa njisi ya kuandika hicho kitu wenzetu wampiga hatua hwana uchoyo unaouzungumza hapa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…