Mie sikani, mauno ulinikatia na mchezo waujua!

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Joined
Sep 24, 2010
Posts
219,468
Reaction score
911,184
Msema ukweli kipenzi cha Muumba hivyo sikani!
Ya kuwa mie nawe tulikuwa beneti sana tena sana!
Nakumbuka tulivyokutanishwa na aliyetutambulisha!
Unyenyekevu wako ulinikoga na Kiswahili kuniyeyuka!
Mie sikani mauno ulinikatia na mchezo waujua!

Haba haba hujaza kibaba na penzi la kasi tulilifukizia
Hapa na pale tukajikuta tumo ndani ya lindi la mahaba
Bila ya kutarajia tukajikuta kitanda twalala sote bila mbinde
Huko tulinogewa na hata kusahau kuwekana sawa ya kesho
Mie sikani mauno ulinikatia na mchezo waujua!

Kesho na kesho kutwa tuliiweka kapuni bila kukusudia
Bila ya kuipangilia mie nilijionea sawa na hata wewe vivyo
Hapa na pale mjuaji akaja na kutumbukia mawazoni mwangu
Kauli yake ilinitikisa na kesho yetu tukaipangilia bila zengwe!
Mie sikani mauno ulinikatia na mchezo waujua!



Kosa langu nielimishe hadi sasa kuniita mdanganyifu.
Hakuna ahadi niliyokupa au hata wewe kunipatia pia
Yawaje sasa udai umetapeliwa khali hatuna makubaliano?
Manung'uniko yako yamenifikia lakini mwenzio kakuwahi!
Mie sikani mauno ulinikatia na mchezo waujua!


Mengi unazoza lakini yote ni tisa tu hakuna jawabu.
Kama ungelikuwa makini ungelinitonya juu ya kesho yetu.
Mie nilidhani tunapita tu na hivyo sikukutilia maanani
Mbona mwenzio aling'aka na kutaka ajue yatakayomsibu?
Mie sikani mauno ulinikatia na mchezo waujua!
 
Ulimuaminisha sana kiunon kanogewa,
Si lazima kwa maneno hata vitendo vya changia,
Na inavyoonekana si mara moja umemuingia,
Ungesema kama umewahiwa malalamiko hayo yasingetokea.
 
maneno yako yakuhadaa, yalimwacha kazuba, Asijue la kufanya, kesho yake ikifika,chonde chonde ruta, usimtupe mwana.
 
Last edited by a moderator:
sasa wewe ulidhani viuno vya bure bure?
halafu ulivyomfukuzia si ulimwambia unataka muwe wote maishani?
iweje umemtosa?
 
Rutashubanyuma, sasa kama alikukatia mauno kweli unakumbuka uliyo ahidi wakati upo kwenye kazi? anake nijuavyo mim yakikukolea utaahid wewe hata usiyokuwa nayo Asprin kwakuwa wewe ni babu hebu mwambie huyu manakae naskia bibi alikukoleza kweli na mauno yake.
 
Last edited by a moderator:
So wakati uko naye huyo mnyenyekevu (anayekuTII) mkata nauno, u started seing someone else? Duh!


Kaunga unafikiri leo nimekulegezea masharti lol.....................utii nao lazim auje na maelekezo ya kesho na kesho kutwa bila y ahayo ujue mambo yanaweza kwenda mrama..........................
 
Last edited by a moderator:
maneno yako yakuhadaa, yalimwacha kazuba, Asijue la kufanya, kesho yake ikifika,chonde chonde ruta, usimtupe mwana.

Mapi nani kwakwambia ana mtoto wangu?........................lol hii ni simulizi tofauti na ile ya wakati ule
 
Last edited by a moderator:

gfsonwin basi mweleze anikumbushe bila ya kukumbushia..................lol
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…