Miezi 6 ya Mkataba wa Simba S.C na EAGGroup, Haya ndiyo yaliyofanyika

Miezi 6 ya Mkataba wa Simba S.C na EAGGroup, Haya ndiyo yaliyofanyika

sembo

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
4,350
Reaction score
3,451
Mnamo 01.04.2015 Klabu ya Simba S.C iliingia mkataba wa MIAKA MITANO na kampuni EAG Group Limited ambao utahusu kuitafutia na kusimamia biashara au biashara mbadala zinzoiingizia au zitakazoiingizia klabu hiyo Mapato.
Tukiwa tunaelekea kutimiza miezi 6 tangu tuingie mkataba na hii kampuni bora kabisa katika masuala ya kutangaza brand ya kampuni au taasisi, ushauri wa jinsi gani uwekeze.. n.k... EAGGroup imeifanyia yafuatayo Simba S.C mpaka sasa;

22.06.2015: Kuzindua Tovuti ya Klabu.
Lengo kuu la kuzindua tovuti hii [ http://simbasports.co.tz ] bora kabisa kuwahi kushuhudiwa ukanda wa CECAFA ni kukuza mawasiliano na wadau wake mbalimbali hususani; wanachama, wapenzi, vyombo vya habari na wadau wengine muhimu.
Tovuti hii sio tu itaiwezesha Simba kuwapa wadau wake taarifa mbalimbali bali pia itatumika kwa ajili ya uuzaji wa
vifaa na bidhaa mbalimbali za Simba S.C.
Baadhi ya mambo yaliyopo katika website hiyo, hapo 👇👇.
https://www.jamiiforums.com/sports/882018-hongera-uongozi-wa-simba-kwa-website-bora.html

02.07.2015: Kuzindua Kadi za Ki-Electronic.
Kuonesha ni kwa jinsi gani Simba S.C imejipanga, ilizindua kadi mpya, ambapo kila mwanachama atapata bima ya maisha inayojulikana kama "Simba Pamoja".
Bima hii itampatia mwanachama ambaye amelipa malipo yake ya mwaka ya uanachama fedha taslimu zisizopungua Sh. 250,000 ikiwa atapata msiba kwa kufiwa na mtoto, mke au kufariki dunia yeye mwenyewe.
Source: Simba yazindua kadi za ki-electronik

03.07.2015: Kuzindua huduma ya Simba News.
Lengo kuu la huduma hii ni ni kuwapatia wateja wanaotumia mitandao ya Tigo na Voda taarifa zinazoihusu klabu ya Simba popote walipo nchini.
Ili kujiunga na huduma hizi unatakiwa kutuma neno kuu SIMBA kwenda 15460. Utakapo jiunga tu mteja utapokea habari kila siku na utatozwa kiasi cha shilingi za kitanzania 150 kwa siku.
Na kwa siku utapokea kiwango cha chini cha habari nne (04) zina zohusu klabu ya Simba.
Source: MICHUZI BLOG: SIMBA SPORT CLUB YAZINDUA HUDUMA MPYA YA SIMBA NEWS

27.07.2015: Kuzindua uuzaji wa jezi katika Duka la Mtandao.
Mtandao wa Klabu ya Simba kwa kushirikiana na Jumia walizindua huduma ya kununua jezi za Simba kupitia duka la mtandao la Jumia [ www.jumia.co.tz ]. Dhumuni la huduma hii ni kuwapatia wapenzi wa klabu ya Simba njia bora ya kuweza kununua jezi popote walipo
Tanzania.
Jinsi ya kununua Uzi wa Mnyama mtandaoni.. Pita hapa 👇👇
https://www.jamiiforums.com/sports/897211-jinsi-ya-kununua-jezi-za-mpya-za-simba-mtandaoni.html

26.09.2015: Kuzindua Tuzo za mwezi kwa Wachezaji wake.
Katika Tuzo hizo, wanachama na wapenzi wa Simba na wapenda michezo ndio watakao chagua mchezaji bora wa mwezi kwa kutuma jina la mchezaji wanayempendekeza kwenda kwenye namba 15460.. na hii ni kwa wale tu ambao wamejiunga na Simba News kupitia mtandao wa Voda na Tigo wataweza kupiga kura kuchagua mchezaji bora wa mwezi wa Simba.
Source: SIMBA DAMU FANS: SIMBA YAANZISHA TUZO ZA MWEZI KWA WACHEZAJI WAKE

NB: Katika miezi sita tu ya mkataba wao wa miaka mitano.. EAGGroup imeonesha ni kwa jinsi gani imedhamiria kuifanya Simba S.C iwe klabu ya Kiulaya Ulaya [na si kimataifa].
Kama kwa mda mfupi tuu huu Simba S.C imekua mfano wa kuigwa katika ukanda huu wa CECAFA.. sipati picha baada ya miaka mitano, itakua imefika wapi?!

Mungu ibariki EAGGroup, Mungu ibariki Simba S.C.
 
Umesahau pia wamefanikisha kipigo kutoka kwa Yanga
 
Nilidhani utasema mpaka sasa mmeingiza klabuni shilingi ngapi, kuliko kuonyesha uzinduzi tu
 
Kuzindua bila kuonesha status ya mlichopanga ni kazi bure. Tulitegemea kuona taarifa ya utekelezaji ya mid year yenye akili.
 
Ndani ya miezi sita eag group imewaletea vifaa bora ImageUploadedByJamiiForums1443500928.643438.jpg
 
Kuzindua bila kuonesha status ya mlichopanga ni kazi bure. Tulitegemea kuona taarifa ya utekelezaji ya mid year yenye akili.

Mkuu.. kua na subira.. taarifa ya utekelezaji "yenye akili" hutolewa mbele ya wenye timu "wanachama" katika Mkutano Mkuu.. Pia kumbuka kuna baadhi ya Huduma zimeanzishwa hata miezi 2 hazijamaliza.. sasa unatoa vipi ripoti?
Nilichokifanya hapa.. nu kuonesha ni kwa jinsi gani EAGGroup wanakesha mchana na usiku ili kuitoa Simba ilipo na kuipeleka katika levo zingine.
cc Nyenyere
 
Last edited by a moderator:
Vipi uwanja umeishia wapi

Jukumu kuu la EAGGroup ni kuhakikisha Simba S.C inaingiza mapato kutokana na biashara inazofanya.. Baadhi ya mapato hayo, ndo yatatumika katika uendelezaji wa ujenzi wa Simba Complex iliyopo Bunju.. Kua na subira Mkuu, mambi mazuri yanakuja.
 
Ndani ya miezi sita eag group imewaletea vifaa boraView attachment 292451

Hilo ni Jukumu la wadhamini wakuu ambao ni Kilimanjaro lager.. Baadhi ya majukumu yao ni kutoa vifaa vya michezo [ jezi. viatu. mipira.. n.k] ambavyo vitatumiwa na timu katika msimu mzima.. na hivyo vifaa tulikabidhiwa kabla ya ligi kuanza.
Nadhani kuna tatizo katika mtunza vifaa wetu [kit manager] maana katika mechi ya ufunguzi Manyika Jr. alivaa jezi ya Angban.. Leo tena Papa N'Daw anakuja na hili.. Hii haikubaliki hata kidogo katika Simba S.C.. Hatua lazima zichukuliwe.
 
Mkuu.. kua na subira.. taarifa ya utekelezaji "yenye akili" hutolewa mbele ya wenye timu "wanachama" katika Mkutano Mkuu.. Pia kumbuka kuna baadhi ya Huduma zimeanzishwa hata miezi 2 hazijamaliza.. sasa unatoa vipi ripoti?
Nilichokifanya hapa.. nu kuonesha ni kwa jinsi gani EAGGroup wanakesha mchana na usiku ili kuitoa Simba ilipo na kuipeleka katika levo zingine.
cc Nyenyere

Mkuu Sembo kama uliyosema hapo juu n ya kweli then uko kwenye forum isiyosahihi
 
Mkuu Sembo kama uliyosema hapo juu n ya kweli then uko kwenye forum isiyosahihi

Mkuu huo ndo ukweli, mchanganuo wa kipi kimepatikana na kama kimetumika.. kimetumika vipi.. hutolewa mbele ya wanachama katika Mkutano Mkuu.
Unasema nipo kwenye forum isiyosahihi... ni forum gani iliyosahihi?
 
Mkuu huo ndo ukweli, mchanganuo wa kipi kimepatikana na kama kimetumika.. kimetumika vipi.. hutolewa mbele ya wanachama katika Mkutano Mkuu.
Unasema nipo kwenye forum isiyosahihi... ni forum gani iliyosahihi?

Haya masuala ilibidi uyapeleke kwenye mkutano wa wanachama kama ulivyosema, hiyo ndio forum sahihi
 
Back
Top Bottom