mdhalendo
Mimi natumia hii huduma na so far naona ipo vizuri. Ninakaribia miezi miwili na mtandao ulisumbua kama mara mbili, ila badda ya mda mfupi tatizo liliisha.
Kuna vitu inabidi ufanye, kwenye hiyo Fast Mile router kuna taa pale juu zipo tatu, kama haziwaki nenda kwenye settings na uziwashe, halafu jaribu kuiweka hiyo router sehemu iliyo wazi, wanashauri sana kuiweka karibu na dirisha ili upate signals vizuri.
Pia unaweza ukawa unaizungusha hiyo router, na kucheki taa zinavyowaka, taa ikiwa moja signal ni hafifu, taa mbili signal ni ya wastani, na taa tatu signal zipo vizuri. Mda huo pia angalia nembo ya 5G iwe imewaka. Isipowaka 5G jua unapata 4G.
KIngine nilichogundua kwenye hii router ni kuwa unaweza ukarusha wireless ya 5G na 4G, so devices kadhaa zikaunga 5G nyingine 4G. Jaribu kuhakikisha hiyo pia, unaweza kuta una connect kwenye 4G tu.
Kupata speed nzuri inategemea na package uliyochukua, package ya 30Mbps, ambayo itakupa hadi 4
MBps / sec kwenye kudownload, ambayo kwa famiilia ya watu wachache (chini ya watu 5) ni nzuri.
Mimi natuma na familia, na nilijaribu kustream 1444p kwa devices 4 bila shida yeyote.
4K ilikuwa inasumbua kidogo, ila nilipopunguza devices pia ikawa vizuri.
So, cha msingi ni angalia 5G signals za sehemu yako, jitahidi router uiweke sehemu nzuri.