Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 524
- 829
Mwanzoni mwa Mwezi Machi, 2025 mdau aliripoti Meli ya New Mv Victoria Hapa Kazi Tu kutofanya kazi, na niliona mamlaka husika zilitolea ufafanuzi suala hilo kwamba meli ilikuwa imesitisha huduma kwa ajili ya matengenezo ya kawaida ambayo ufanyika mara moja kwa mwaka yakihusisha ukaguzi.
Meli hii imekuwa msaada mkubwa kwetu wafanyabiashara hasa katika kusafirisha mizigo, kwa sasa tunapata changamoto kubwa katika gharama za usafiri.
Wafanyakazi na vibarua waliokuwa wanafanya kazi kwenye meli hiyo nao wapo njiapanda, huku kukiwa hakuna taarifa za Wazi zinazoeleza meli hiyo itarejea lini kuanza safari kama kawaida.
Mamlaka ni vyema zikatueleza kwa kina nini kinaendelea maana tumekuwa na matarajio kwamba huduma zitarejea ndani ya muda mfupi lakini mpaka sasa ni Mwezi mzima umepita hakuna huduma na hazijatolewa taarifa zaidi.
Pia soma:
~ Nimekosa huduma ya Meli ya MV. Victoria, inadaiwa haifanyi kazi wiki ya pili sasa, Mamlaka mbona mpo kimya?
~ TASHICO: Ni kweli huduma za Meli ya MV Victoria zimesimama kwa ajili ya service ya kawaida
~ TASHICO: MV. Victoria itaendelea kusimamisha huduma kwa muda wa mwezi mmoja kwajili ya kufanya 'service'