Miezi ya wengine kuvuna na wengine kupoteza

Miezi ya wengine kuvuna na wengine kupoteza

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Mwezi wa kumi na mbili (December) na mwezi wa kwanza (January), ni miezi inayofanya jamii kutumia pesa sana na upande wa pili kunufaika sana.

Kwenye nyumba za ibada huwa ni msimu wa mavuno, huku upande wa pili ukiwa ni kugharamia (kutoa/kupoteza).

Kwenye majengo ya starehe, mapato yanaongezeka huku mwingine akiwa anapoteza.

Kwenye vyombo vya usafiri, abiria wanaongezeka na mapato kuongezeka pia.

Wamiliki wa mashule, hawa wanatamani mwezi wa kwanza ufike kwa haraka zaidi ili waweze kukusanya mamilioni. Huku wazazi na walezi wakitamani mwezi wa kwanza usifike kwa haraka ili waweze kujichanga upya katika ulipaji wa ada.

Kwa ujumla, wengi huwa wanasema mwezi wa kwanza ni mgumu, ila ni mwezi mzuri kwa wanaomiliki mashule, na wanatamani ufike haraka sana.​
 
Team Argentina odds zilikuwa 2.70...weka million 5 upate million 10 acha uboya wewe dunia inatema fedha leo km asemavyo mtoa mada wale wa mbape tushawapoteza
 
Team Argentina odds zilikuwa 2.70...weka million 5 upate million 10 acha uboya wewe dunia inatema fedha leo km asemavyo mtoa mada wale wa mbape tushawapoteza
Walioliwa sasa hivi wanasaga meno
 
Back
Top Bottom