KERO Mifugo inagoma kunywa maji yanayotoka Bwawa la Swaswa (Dodoma) lakini yanatumika kumwagilia mbogamboga

KERO Mifugo inagoma kunywa maji yanayotoka Bwawa la Swaswa (Dodoma) lakini yanatumika kumwagilia mbogamboga

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Mzee wa Code

Member
Joined
Sep 23, 2024
Posts
61
Reaction score
91


Dodoma inazidi kukua kwa kasi, baadhi ya vinavyochangia ukuaji huo ni uwepo wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) tangu Mwaka 2007 na Serikali kufanya maamuzi ya kuwa Makao Makuu kwa vitendo.

Ukuaji huu wa kasi umesababisha ongezeko la mahitaji ya ardhi kwa ajili ya makazi na biashara, huku baadhi ya maeneo hatarishi yakitumika kama makazi na vyanzo vya uzalishaji wa chakula.

Moja ya changamoto kuu zinazotokana na hali hii ni uwepo wa mabwawa ya maji taka eneo la Swaswa, ambapo wakazi wa Dodoma wanakula mbogamboga zinazolimwa pembezoni mwa mabwawa hayo, hali inayoweka afya zao hatarini.

Mazingira ya Hatari kwa Afya ya Walaji
Eneo la Swaswa lina mabwawa ya maji taka yaliyotengenezwa ili kuhifadhi na kuchakata maji taka ya jiji.

Hata hivyo, kutokana na ongezeko la mahitaji ya mbogamboga, wakazi wa eneo hilo wamegeuza mabwawa hayo kuwa chanzo cha maji kwa kilimo cha bustani.

Maji hayo kutoka katika bwawa hilo hutumika kumwagilia mboga zinazouzwa katika masoko ya Dodoma, ikiwemo Soko la Sabasaba ambalo linahudumia wakazi wengi wa jiji.

Kilimo hiki kinachotegemea maji ya mabwawa ya maji taka kinaweka afya za walaji wa mbogamboga hizo katika hatari kubwa ya magonjwa mbalimbali.

Maji hayo yanayotumika kumwagilia inasemekana "yamewekewa dawa ya kuondoa uchafu," hali hiyo inawafanya Wakulima wanaoyatumia wahisi kuwa ni salama kwa matumizi ya kilimo, hivyo wanayatumia bila kinga yoyote.

Kutokuwepo kwa kinga na elimu ya kutosha kwa wakulima hao kunaongeza hatari ya kusambaza kemikali hatari, sumu, na bakteria kwa walaji wa mbogamboga.

Madhara kwa Afya
Kawaida Wadudu wengi wanavutiwa na maji taka lakini nhayo maji ya Bwawa sio kipenzi cha Wadudu kama nzi.

Nilipofika eneo la tukio, Mfugaji mmoja aliniambia kuwa hata mifugo, hasa ng’ombe, hawanywi maji hayo hata inapotokea wamelazimishwa.
Ishara hiyo pekee inatosha kutoa ishara kuwa kuna jambo halipo sawa.

Hivyo, kutumia maji haya kwa kilimo cha mboga, kuna uwezekano mkubwa wa kueneza kemikali hatarishi kama vile metali nzito na sumu nyingine kwenye mazao yanayoliwa na Wananchi wengi wa Dodoma.

Mimi sio mtaalam lakini inawezekana hali hiyo ya kutumia maji hayo kumwagilia mbogamboga ikawa na madhara katika mfumo wa mwili wa binadamu.


20241112_133314.jpg

20241112_133320.jpg

Usalama wa Watoto na Wakazi wa Swaswa
Mbali na hayo yote, mabwawa hayo pia yamekuwa kero kwa wakazi wa Swaswa kutokana na usalama kuwa mdogo.

Watoto ambao hawana uangalizi maalum wakati wa kucheza karibu na mabwawa hayo wameathirika, na baadhi yao wameripotiwa kuzama katika mabwawa hayo.

Wito kwa Mamlaka za Dodoma
Ni muhimu kwa Mamlaka za Jiji la Dodoma pamoja na Serikali, kuchukua hatua kali na za haraka katika kulinda afya za wakazi na walaji wa mbogamboga zinazolimwa pembezoni mwa mabwawa haya.

Mabwawa haya yanahitaji kuhamishwa au kuwekewa mfumo wa kisasa wa kuchakata maji taka ili kuhakikisha maji yanayotoka hapo yanakuwa salama kwa mazingira.

Hatua hizi ni muhimu ili kulinda afya za walaji wa mboga zinazotokana na maji ya mabwawa haya na kuhakikisha kuwa wakazi wa Dodoma wanapata chakula salama.

Kulinda afya na usalama wa jamii ya Dodoma inapaswa kuwa kipaumbele cha mamlaka zote husika.

20241112_134640.jpg

20241112_134651.jpg

20241112_135003.jpg

20241112_140401.jpg

 
magonjwa yasiyoambukiza yamekuwa mengi kwa sababu tunakula vitu vya ajabu sana
 
maini na figo yanakufa ovyo, saratani za kumwaga kumbe Serikali yetu inashiriki kutulisha kemikali
 
Maji taka ya maji Gani? Hapa Iringa kuna Maji taka toka machinjioni. Yanafaa kwa kumwagilia lakini si salama kwa mifugo.

Maji yanayotumika ndani kwenye machinjio ni maji yanayotoka kwenye kisima hivyo yana chumvi chumvi na mifugo haiyapendi.

Kwa ivo kipimo kuwa mifugo hainywi maji hayo ndiyo kuwa ni hatarishi kwa Afya za binadamu, siyo sahihi Sana.

Labda kama maji hayo yanatoka kwenye viwanda vinavyozalisha kemikali zenye sumu.
 
Back
Top Bottom